Dr Slaa atikisa Iramba Magharibi- Singida

Dr Slaa atikisa Iramba Magharibi- Singida

Status
Not open for further replies.
Kwa msio na ufahamu, Christina Mugwai ni Dada wa Mh. Tundu Lissu.
Christina Mugwai ni Mbunge wa Viti Maalum Chadema.

Na wasiojua January Makamba ni mtoto wa Mzee Yusuph Makamba aliyekuwa katibu mkuu wa CCM.
 
Peoples power hakuna chama kama Chadema,kama kweli watu wanataka kuotoka kwenye dimbwi la umaskini hawana budi kuwaamini na kuwachagua Chadema make ndio suluhisho lililobaki Tulianza na Mungu na bado tuko naye hadi kieleweke.Peoles Power
 
Hoja hiyo haina mshiko ulitaka amuweke dada yako ambaye ni kibaraka wa ccm
 
kwa msio na ufahamu, christina mugwai ni dada wa mh. Tundu lissu.
Christina mugwai ni mbunge wa viti maalum chadema.
hili ni jambo la ujinga kabisa to divert unnecessary attention. This is not the first for the folks to join hands in fighting against the malaise of the nation . There are several scores around the world where member from the same family are ruling democratically, we have comrade Raul Castro brother to former Cuban president Fidel Castro, even within ccm itself there are score of same family rullers; the first lady is the member of one of the ccm organs, the son of incumbent president is a very powerful icon behind the decisions of the ruling party and the government. The family of the president is suspected of taking party in assisting the president to make tough decisions. So we are worried by motive behind mentioned mugwai as having nominated her for a special set. After all CDM had no outstanding choice beside her. Please refrain yourselves from causing insinuation at this [point of time
 
Na wasiojua January Makamba ni mtoto wa Mzee Yusuph Makamba aliyekuwa katibu mkuu wa CCM.

Napia waziri Husein Mwinyi ni mtoto wa Rais mstaafu Ally Hasani Mwinyi na Mathayo David ni mtoto wa Waziri mkuu mstaafu David Msuya.
 
CCM ni destructive machine ambayo ni powerful sana. NCCR walipoihenyesha sana mwaka kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 hawakuweza tena kuhimiri mapigo ya CCM yaliyofuata hadi wapiganaji wakubwa akina Lamwai wakaishia kuisaliti NCCR yao na hivyo kuelekea kifo chake cha mende, mwisho wa yote makadi wengi wa NCCR-Mageuzi ya wakati huo kama vile Lamwai, Nsanzugwako na wengineo wakarudi CCM na kupata vyeo huo.

Baada ya mateso yaliyotolewa na CHADEMA kwa CCM mwaka 2010 na kuilazimisha kutumia njia chafu ili ipate ushindi, haya tunayoona leo ni matokeo ya hiyo destructive machinery process. Baadhi ya makada wakubwa wa CHADEMA watarudi CCM na kupata vyeo kama ilivyokuwa kwa akina Lamwai na Nsanzugwako,
 
Timueni kwanza Zitto ndio tuje tuelewane vizuri maana wanachama mnatuchanganya hatujui tushike lipi na tuache lipi, Wanachama wengi tumeshaanza kukata tamaa kabisa sababu kunaonekana hakuna haki kabisa, Masaliwa walitumuliwa faster tena kwa ushahidi hasa wa JF lakin Zitto tuhuma kibao lakin bado mnachamchekea tu.

INAUMIZA SANA SIO SIRI.

Aisee wewe jamaa huna hurima kabisa duh. Mtamuua huyo jamaa na presha walah
 
Last edited by a moderator:
Na wasiojua January Makamba ni mtoto wa Mzee Yusuph Makamba aliyekuwa katibu mkuu wa CCM.

Kweli sasa tunapo kipeleka chama(CDM) ni kubaya,
January Makamba sio mbunge wa viti maalum,hakuna conflict of interest hapo kwani January amechaguliwa kwa kupigiwa kura na wananchi,wakati huyu amepata ubunge coz ya lisu,na ndio maana chama kinachafuka kwakufanya mambo ya ajabu.
 
Timueni kwanza Zitto ndio tuje tuelewane vizuri maana wanachama mnatuchanganya hatujui tushike lipi na tuache lipi, Wanachama wengi tumeshaanza kukata tamaa kabisa sababu kunaonekana hakuna haki kabisa, Masaliwa walitumuliwa faster tena kwa ushahidi hasa wa JF lakin Zitto tuhuma kibao lakin bado mnachamchekea tu.

INAUMIZA SANA SIO SIRI.

Hata mimi inaniuma saaaaana
 
Last edited by a moderator:
Hoja hiyo haina mshiko ulitaka amuweke dada yako ambaye ni kibaraka wa ccm

Si kila jambo lakupinga,huku ni kujuana,na hapa ndipo kwenye walakini coz hapa ndio CDM haijashika dola akishika dola itakuaje,ni bora tubaki na CCM kwani Zimwi likuajalo halikuli ukakwisha.
 
pia ndesamburo ana mtoto wake pia na mkwe wake kiwhelu. Pia mbowe ana mzazi mwenzake ,same to dkt slaa,na wote ni s.seats.

Nafasi za ubunge wa viti maalumu zimetumiwa vibaya na vyama vyote - CCM na CHADEMA. Nafasi wamepewa maswahiba, wapenzi, ndugu wa damu nk. Yaani ni kama vile zilikuwa zinagawanywa kwa wanene ndani ya chama. Huu pia ni ufisadi. Kuna haja ya kuvifuta viti maalumu kwani havina tija yoyote
 
kwa hiyo wanapeana ubunge kiundugu siyo! Ina maana huko singida chadema wapo ukoo wa tundu lissu tu waliosoma??? Chadema genge la koo za watu

vp kuhusu ukoo karume,mwinyi,kikwete,makamba na wengineo kibao,hivi ni wao tu wanaofaa kuwa vingozi? Familia ya kikwete uchaguzi wa nec ilipitaje bila kupingwa? Una boga badala ya kichwa! Cdm ndilo tumaini pekee la wanyonge ndio maana hata sisi maskini tunapata fursa ya kugombea uongozi na hilo lipo wazi hata kwa misukule kama wewe mnatambua!
 
sema tu christina lisu, mbona kila moja anajua?
Katibu Mkuu CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameingia mkoani Singida kwa kishindo kikubwa ambapo amelakiwa na wabunge Tundu Lissu na Christina Mugwai tayari kuungana kulitikisa Jimbo la Iramba

Katibu Mkuu anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara eneo la Shelui, Jimbo la Iramba Magharibi.

Dr Slaa aliyetikisa vilivyo kanda ya Magaribi kwa zaidi ya wiki mbili anatarajiwa kuhitimisha ziara yake leo na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Update 1.....

Msafara wa Katibu Mkuu umeshawasili tayari. Wananchi wamejitokeza kwa wingi hapa Madukani, Mkwajuni. Mkiti wa Wilaya ameshafungua mkutano. Katibu wa Mkoa anatambulisha viongozi wa chama!

Diwani wa Mungaa Alex Mateo Kiondo kajitambulisha hapa akiwapatia wananchi pole kwa jua kali la miaka 52 ya utawala wa CCM. Sasa ni Imma Jingu Diwani wa Iseke aliyepatikana uchaguzi mdogo uliopita anasema CCM walikuja na hela kibao zikaliwa na wananchi wakachagua CHADEMA. Amewataka wananchi wajiandae kuchagua utawala wa haki mwaka 2014 na 2015.

Kamanda Selema naye kasalimia. Huyu ni yule mmoja wa wale wana CCM waliomfungulia kesi Lissu kwa shinikizo la CCM.

Baada ya Kaimu Mkiti wa Mkoa Shaaban, sasa kapanda Mbunge wa Viti Maalum, Christina. Anawapongeza kwa kujitokeza kwa wingi asubuhi hii pamoja na kuwa na shughuli nyingi.

Updates 2.....

Waitara Mratibu wa Msafara anaelezea summary ya ziara nzima ya Dkt. Slaa ambaye amefanya jumla ya mikutano ya hadhara 20 na kote amefanya vikao vya ndani, akikagua mafaili kujua chama kinavyoendeshwa! Akaomba akiwa njiani afanye mkutano mmoja Shelui.

Waitara anasema namna ambavyo Mbunge wa Iramba Magharibi anavyowaaibisha wananchi wa jimbo hili. Alivyotema mate bungeni wkt CCM wanasema ni mahali patakatifu. Anaelezea namna alivyopanga mpango wa kumwagia tindikali kijana wao wa CCM kisha sasa wamemgeuza bango ambapo Kinana anamtembeza mikutanoni!

Waitara anawaambia hapa jinsi ambavyo makosa ya kuchagua CCM inayoendekeza ufisadi na kulea utawala mbovu, imeugharimv mkoa huu. Amewaasa kuacha kuhongwa hadi miwa kama walivyofanyiwa na Mbunge wao. Anawaambia wamshukuru Kamanda Lissu ambaye amekuwa akiwapigania sana bungeni. Akishirikiana na Wabunge wa Viti Maalum, Christina na Christowaja!

Anawauliza kama kuna mtu anakubali kuwa CCM mwisho wake umekaribia, wote wamenyoosha. Na sasa wanapiga pipoz power ya nguvu kumkaribisha Lissu jukwaani.

Lissu amepanda. Anaanza kwa kumnukuu aliyekuwa Mkiti wa Mkoa wa Singida, Kitundu ambaye alisema Lissu huwa anafanya mikutano jimboni kwake tu. Kitu ambacho si kweli. Ukweli ni kwamba amefanya mikutano ktk majimbo yote isipokuwa Iramba Magharibi tu. Hivyo amewaomba samahani kwa hilo. Anazungumzia maamuzi wa CC.

Anasema Chadema imefanya maamuzi ambayo CCM hawawezi kufanya. Ni maamuzi magumu, sahihi na muhimu. Anasema wamewavua uongozi Zitto Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba

Anasema Chadema imefanya maamuzi ambayo CCM hawawezi kufanya. Ni maamuzi magumu, sahihi na muhimu. Anasema wamewavua uongozi Zitto Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba

Si suala la chuki binafsi kama watu wanavyotaka kuonesha kutafuta huruma na kuendeleza ulaghai. Wale wale wanaosemwa wanawachukia akina Zitto na Kitila ndiyo hao hao walikuwa mstari wa mbele kuwatetea waliposhtakiwa kwa kesi mbalimbali, kesi ya Ndago, kesi ya Manji dhidi ya Zitto na alipofukuzwa bungeni. Alipofukuzwa bungeni wale wale wanaompenda leo, walimtukana na kumbeza kwa kila neno na kashfa kibao. Waliosimama naye wima leo wanaonekana eti wanamchukia!

Anasema hapa hatazungumza Mwigulu Nchemba, bali atazungumza habari za Iramba ili wajue habari za kwao. Anawasomea mafungu ya bajeti ya kila mwaka tangu mwaka juzi akionesha namna wanavyostahili kupata fedha nyingi lkn wanachangishwa michango ya kufa mtu!

Anasema mambo haya anayowaambia anajua hakuna mtu wa CCM akiwemo mbunge wao anaweza kuwaambia maneno haya. Badala yake watawaambia mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na bajeti ni finyu, wakati kwa mujibu wa bajeti, kuna mafungu ya huduma mbalimbali, afya, elimu n.k, lkn matokeo yake zinaandikwa kwenye ripoti zimebaki. Kisha wananchi wanachangishwa na kuishia kuhongwa khanga.

Update 3....

Anasema habari za hoja ya ukombozi ni kwa kila mtu. Kila mtu kbs. Anasema chini ya utawala wa CCM kila mtu analiwa, askari polisi wanaliwa. Anasema namna wabunge wa CHADEMA walivyoibua hoja ya stahili za askari polisi rationing allowance ambayo inapaswa kuwa laki moja lkn wanapewa 50,000 pekee. Waziri Kagasheki alipokiri bungeni kuwa ni laki moja IGP akatuma waraka kwa RPCs wote akiwataka wote waliovujisha siri hiyo ya askari 'kuliwa' na wakubwa wao, wasakwe. Kila mtu analiwa, mkulima analiwa, wafugaji wanaliwa, madaktari wanaliwa, walimu wanaliwa, kila mtu...sasa anapanda Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa sasa anaelekea mkutano wa pili eneo la Kyengege ambako ni kijijini alipozaliwa mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

Update 4..

Msafara umeshafika eneo la mkutano hapa Kyengege. Pamoja na vitisho, watu wamejitokeza kwa wingi hapa karibu na madukani, mbele kbs ya ofc ya CCM.

Tundu Lissu ameshakaribishwa kuzungumza. Anaanza kwa kuonesha namna gani Mkoa wa Singida umekuwa nyuma miaka 52 tangu uhuru kwa sababu ya uongozi mbovu na siasa chafu za CCM. Anaonesha tofauti ya majimbo mengine yaliyo chini ya CCM na jimbo lake. Anasema mafanikio ya ustawi wa wana Singida utaonekana punde wakiiasi CCM!

Source:Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom