Dr Slaa atikisa Iramba Magharibi- Singida

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Katibu Mkuu CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameingia mkoani Singida kwa kishindo kikubwa ambapo amelakiwa na wabunge Tundu Lissu na Christina Mugwai tayari kuungana kulitikisa Jimbo la Iramba

Katibu Mkuu anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara eneo la Shelui, Jimbo la Iramba Magharibi.

Dr Slaa aliyetikisa vilivyo kanda ya Magaribi kwa zaidi ya wiki mbili anatarajiwa kuhitimisha ziara yake leo na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Update 1.....

Msafara wa Katibu Mkuu umeshawasili tayari. Wananchi wamejitokeza kwa wingi hapa Madukani, Mkwajuni. Mkiti wa Wilaya ameshafungua mkutano. Katibu wa Mkoa anatambulisha viongozi wa chama!

Diwani wa Mungaa Alex Mateo Kiondo kajitambulisha hapa akiwapatia wananchi pole kwa jua kali la miaka 52 ya utawala wa CCM. Sasa ni Imma Jingu Diwani wa Iseke aliyepatikana uchaguzi mdogo uliopita anasema CCM walikuja na hela kibao zikaliwa na wananchi wakachagua CHADEMA. Amewataka wananchi wajiandae kuchagua utawala wa haki mwaka 2014 na 2015.

Kamanda Selema naye kasalimia. Huyu ni yule mmoja wa wale wana CCM waliomfungulia kesi Lissu kwa shinikizo la CCM.

Baada ya Kaimu Mkiti wa Mkoa Shaaban, sasa kapanda Mbunge wa Viti Maalum, Christina. Anawapongeza kwa kujitokeza kwa wingi asubuhi hii pamoja na kuwa na shughuli nyingi.

Updates 2.....

Waitara Mratibu wa Msafara anaelezea summary ya ziara nzima ya Dkt. Slaa ambaye amefanya jumla ya mikutano ya hadhara 20 na kote amefanya vikao vya ndani, akikagua mafaili kujua chama kinavyoendeshwa! Akaomba akiwa njiani afanye mkutano mmoja Shelui.

Waitara anasema namna ambavyo Mbunge wa Iramba Magharibi anavyowaaibisha wananchi wa jimbo hili. Alivyotema mate bungeni wkt CCM wanasema ni mahali patakatifu. Anaelezea namna alivyopanga mpango wa kumwagia tindikali kijana wao wa CCM kisha sasa wamemgeuza bango ambapo Kinana anamtembeza mikutanoni!

Waitara anawaambia hapa jinsi ambavyo makosa ya kuchagua CCM inayoendekeza ufisadi na kulea utawala mbovu, imeugharimv mkoa huu. Amewaasa kuacha kuhongwa hadi miwa kama walivyofanyiwa na Mbunge wao. Anawaambia wamshukuru Kamanda Lissu ambaye amekuwa akiwapigania sana bungeni. Akishirikiana na Wabunge wa Viti Maalum, Christina na Christowaja!

Anawauliza kama kuna mtu anakubali kuwa CCM mwisho wake umekaribia, wote wamenyoosha. Na sasa wanapiga pipoz power ya nguvu kumkaribisha Lissu jukwaani.

Lissu amepanda. Anaanza kwa kumnukuu aliyekuwa Mkiti wa Mkoa wa Singida, Kitundu ambaye alisema Lissu huwa anafanya mikutano jimboni kwake tu. Kitu ambacho si kweli. Ukweli ni kwamba amefanya mikutano ktk majimbo yote isipokuwa Iramba Magharibi tu. Hivyo amewaomba samahani kwa hilo. Anazungumzia maamuzi wa CC.

Anasema Chadema imefanya maamuzi ambayo CCM hawawezi kufanya. Ni maamuzi magumu, sahihi na muhimu. Anasema wamewavua uongozi Zitto Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba

Anasema Chadema imefanya maamuzi ambayo CCM hawawezi kufanya. Ni maamuzi magumu, sahihi na muhimu. Anasema wamewavua uongozi Zitto Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba

Si suala la chuki binafsi kama watu wanavyotaka kuonesha kutafuta huruma na kuendeleza ulaghai. Wale wale wanaosemwa wanawachukia akina Zitto na Kitila ndiyo hao hao walikuwa mstari wa mbele kuwatetea waliposhtakiwa kwa kesi mbalimbali, kesi ya Ndago, kesi ya Manji dhidi ya Zitto na alipofukuzwa bungeni. Alipofukuzwa bungeni wale wale wanaompenda leo, walimtukana na kumbeza kwa kila neno na kashfa kibao. Waliosimama naye wima leo wanaonekana eti wanamchukia!

Anasema hapa hatazungumza Mwigulu Nchemba, bali atazungumza habari za Iramba ili wajue habari za kwao. Anawasomea mafungu ya bajeti ya kila mwaka tangu mwaka juzi akionesha namna wanavyostahili kupata fedha nyingi lkn wanachangishwa michango ya kufa mtu!

Anasema mambo haya anayowaambia anajua hakuna mtu wa CCM akiwemo mbunge wao anaweza kuwaambia maneno haya. Badala yake watawaambia mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na bajeti ni finyu, wakati kwa mujibu wa bajeti, kuna mafungu ya huduma mbalimbali, afya, elimu n.k, lkn matokeo yake zinaandikwa kwenye ripoti zimebaki. Kisha wananchi wanachangishwa na kuishia kuhongwa khanga.

Update 3....

Anasema habari za hoja ya ukombozi ni kwa kila mtu. Kila mtu kbs. Anasema chini ya utawala wa CCM kila mtu analiwa, askari polisi wanaliwa. Anasema namna wabunge wa CHADEMA walivyoibua hoja ya stahili za askari polisi rationing allowance ambayo inapaswa kuwa laki moja lkn wanapewa 50,000 pekee. Waziri Kagasheki alipokiri bungeni kuwa ni laki moja IGP akatuma waraka kwa RPCs wote akiwataka wote waliovujisha siri hiyo ya askari 'kuliwa' na wakubwa wao, wasakwe. Kila mtu analiwa, mkulima analiwa, wafugaji wanaliwa, madaktari wanaliwa, walimu wanaliwa, kila mtu...sasa anapanda Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa sasa anaelekea mkutano wa pili eneo la Kyengege ambako ni kijijini alipozaliwa mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

Update 4..

Msafara umeshafika eneo la mkutano hapa Kyengege. Pamoja na vitisho, watu wamejitokeza kwa wingi hapa karibu na madukani, mbele kbs ya ofc ya CCM.

Tundu Lissu ameshakaribishwa kuzungumza. Anaanza kwa kuonesha namna gani Mkoa wa Singida umekuwa nyuma miaka 52 tangu uhuru kwa sababu ya uongozi mbovu na siasa chafu za CCM. Anaonesha tofauti ya majimbo mengine yaliyo chini ya CCM na jimbo lake. Anasema mafanikio ya ustawi wa wana Singida utaonekana punde wakiiasi CCM!

Source:Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene
 
Last edited by a moderator:

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
250
Katibu Mkuu CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameingia mkoani Singida kwa kishindo kikubwa ambapo amelakiwa na wabunge Tundu Lissu na Christina Mugwai tayari kuungana kulitikisa Jimbo la Iramba

Source:Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

Kwa msio na ufahamu, Christina Mugwai ni Dada wa Mh. Tundu Lissu.
Christina Mugwai ni Mbunge wa Viti Maalum Chadema.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,360
2,000
Katibu Mkuu CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameingia mkoani Singida kwa kishindo kikubwa ambapo amelakiwa na wabunge Tundu Lissu na Christina Mugwai tayari kuungana kulitikisa Jimbo la Iramba

Katibu Mkuu anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara eneo la Shelui, Jimbo la Iramba Magharibi.

Dr Slaa aliyetikisa vilivyo kanda ya Magaribi kwa zaidi ya wiki mbili anatarajiwa kuhitimisha ziara yake leo na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Update 1.....

Msafara wa Katibu Mkuu umeshawasili tayari. Wananchi wamejitokeza kwa wingi hapa Madukani, Mkwajuni. Mkiti wa Wilaya ameshafungua mkutano. Katibu wa Mkoa anatambulisha viongozi wa chama!

Diwani wa Mungaa Alex Mateo Kiondo kajitambulisha hapa akiwapatia wananchi pole kwa jua kali la miaka 52 ya utawala wa CCM. Sasa ni Imma Jingu Diwani wa Iseke aliyepatikana uchaguzi mdogo uliopita anasema CCM walikuja na hela kibao zikaliwa na wananchi wakachagua CHADEMA. Amewataka wananchi wajiandae kuchagua utawala wa haki mwaka 2014 na 2015.

Source:Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

Mkuu Molemo naona mmeamua kutikisa: Juzi kati Dr. Slaa Katoka huko Kigoma nasikia hakutikisa, juzi Zitto naye kaenda Katikisa vilivyo. Ni mwendo wa kutikisa, huyu akitoka kutikisa huyu anaenda kutikisa zaidi! Mwisho mfanye tathimini kuona nani katikisa zaidi.

Naomba uniulizie kwa kamanda Tundu Lissu; vipi amemalizana na wale madiwani waliokuwa wakimshutumu kutaka kugawa pesa za mfuko wa maendeleo kama pesa zake binafsi?

Last edited by a moderator:

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,523
2,000
Kwa msio na ufahamu, Christina Mugwai ni Dada wa Mh. Tundu Lissu.
Christina Mugwai ni Mbunge wa Viti Maalum Chadema.
kwani tatizo ni nini? Mbona Abdala kigoda na dada ake Aisha kigoda wako bungeni? Pia vita kawawa na dada ake mbona wote wako bungeni?
 
AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,505
2,000
Timueni kwanza Zitto ndio tuje tuelewane vizuri maana wanachama mnatuchanganya hatujui tushike lipi na tuache lipi, Wanachama wengi tumeshaanza kukata tamaa kabisa sababu kunaonekana hakuna haki kabisa, Masaliwa walitumuliwa faster tena kwa ushahidi hasa wa JF lakin Zitto tuhuma kibao lakin bado mnachamchekea tu.

INAUMIZA SANA SIO SIRI.
 
Last edited by a moderator:

mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
kweli chadema majanga sikia hii slaa amelakiwa na tundu lisu na cristina lisu kwahiyo kalakiwa na ndugu tu basi.
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
Timueni kwanza Zitto ndio tuje tuelewane vizuri maana wanachama mnatuchanganya hatujui tushike lipi na tuache lipi, Wanachama wengi tumeshaanza kukata tamaa kabisa sababu kunaonekana hakuna haki kabisa, Masaliwa walitumuliwa faster tena kwa ushahidi hasa wa JF lakin Zitto tuhuma kibao lakin bado mnachamchekea tu.

INAUMIZA SANA SIO SIRI.

wewew unatuletea mambo gani wewe zito hafukuziki chadema.
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,523
2,000
Mkuu Molemo naona mmeamua kutikisa: Juzi kati Dr. Slaa Katoka huko Kigoma nasikia hakutikisa, juzi Zitto naye kaenda Katikisa vilivyo. Ni mwendo wa kutikisa, huyu akitoka kutikisa huyu anaenda kutikisa zaidi! Mwisho mfanye tathimini kuona nani katikisa zaidi.

Naomba uniulizie kwa kamanda Tundu Lissu; vipi amemalizana na wale madiwani waliokuwa wakimshutumu kutaka kugawa pesa za mfuko wa maendeleo kama pesa zake binafsi?

teh teh, pesa za mfuko wa jimbo ziko chini ya mbunge na si vinginevyo! Huo ndo utaratibu.
 
Last edited by a moderator:

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
1,195
Mkuu Molemo naona mmeamua kutikisa: Juzi kati Dr. Slaa Katoka huko Kigoma nasikia hakutikisa, juzi Zitto naye kaenda Katikisa vilivyo. Ni mwendo wa kutikisa, huyu akitoka kutikisa huyu anaenda kutikisa zaidi! Mwisho mfanye tathimini kuona nani katikisa zaidi.

Naomba uniulizie kwa kamanda Tundu Lissu; vipi amemalizana na wale madiwani waliokuwa wakimshutumu kutaka kugawa pesa za mfuko wa maendeleo kama pesa zake binafsi?

Ni vizuri hizi hoja tuchangie huku tukijua tunachochangia ni kitu gani, mgogoro wa fedha za mfuko wa jimbo ni upuuzi kuzungumzia, kwa ninaye jua naona utakuwa umtendei haki Lissu, ile fedha ikija nyingi sana mfano ilamba wanapata sii za idi ya milioni 40 hapo hakuna kigezo cha kitaalamu kinachotumika kugawa, kila diwani atataka apate mradi kwenye kata yake, million 40 kama jimbo lina kata 20 utaweza kweli kuendeleza miradi hiyo ? Serikali ya ccm imeendekeza siasa mno kuliko maendeleo
Kuna haja gani ya kuwepo mfugo wa jimbo ili hali fedha nyingine zote za maendelea zinapitia kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya /
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom