Dr Slaa atikisa Iramba Magharibi- Singida

Dr Slaa atikisa Iramba Magharibi- Singida

Status
Not open for further replies.
Karibu nyumbani,karibu ugali wa uwele na mlenda saaafi.
Tahadhari.Bado tunaishi kwenye matembe maana tumeshindwa kununua vifaa vya ujenzi kama saruji na mabati ila mchanga na mawe yapo yakutosha,Hivyo ukiingia kuwa makini makaratasi yako yaweza vujiwa
 
Mkuu uongo huo uko wapi? mbona post ipo clear kabisa. Nimeisoma tena naona haina shida. Magazeti yaliripoti kama ambavyo niliandika.
Nyie wenyewe mnatengeneza majungu ya kubumba mnapeleka Habarileo, Uhuru na Jamboleo yachapishe ili kesho yake mnawahi kuyaposti JF na kuanza kujijibu wenyewe, hatari.
 
wewew unatuletea mambo gani wewe zito hafukuziki chadema.
Zito yuko chadema lakini shughuli zake anafanyia ccm.Na wanao muunga mkono humuJF ni wanaccm,hata ukitaka gazeti lililo cover vizuri habari za ZITO nunua la UHURU,HABARILEOnaJAMBOLEO.sijui unataka ushaidi gani?
 
Mkuu uongo huo uko wapi? mbona post ipo clear kabisa. Nimeisoma tena naona haina shida. Magazeti yaliripoti kama ambavyo niliandika.




Magazeti yaliripoti tofauti na ulivyoandika, ushabiki wako ulipitiliza, kwa kutaka sifa mpaka ukatunga uongo wako mwenyewe.
Mjane wa Mwangosi alikuja kukanusha na kuwaumbua ninyi nyote.
Ninyi watu ni waongo mpaka mwenye maswala mazito ya msiba..!!
Soma pages 09 hadi 11 za thread hiyo utajiona jinsi ulivyo muongo..!!
 
Swala la picha ofisi yetu ya propaganda bado inazishughulikia...endeleeni kusubiri na asanteni kwa utulivu.
 
Tupeni updates za kutosha na msisahau kutupia picha! Kila la heri makamanda!
Picha bado kitengo cha uenezi na propaganda kinaziandaa, tumemaliza maktaba nzima kukava matukio ya Tabora na Kigoma ndio maana kazi imekuwa ngumu kidogo.
 
Magazeti yaliripoti tofauti na ulivyoandika, ushabiki wako ulipitiliza, kwa kutaka sifa mpaka ukatunga uongo wako mwenyewe.
Mjane wa Mwangosi alikuja kukanusha na kuwaumbua ninyi nyote.
Ninyi watu ni waongo mpaka mwenye maswala mazito ya msiba..!!
Soma pages 09 hadi 11 za thread hiyo utajiona jinsi ulivyo muongo..!!

By Kimbunga Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!


============

Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa

HabariLeo | Oktoba 05, 2012

UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.
.
.
.
"Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake," alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

.

Hapo kwenye red,
Mwandishi wa mada hii (Kimbunga) kashindwa kabisa kusoma makala yake mwenyewe na kuona kuwa ina kasoro kubwa sana.
Kakurupuka, kaiweka hapa JF, na sasa anaumbuka kwa kuonyesha udhaifu wa hali ya juu sana wa kufikiri.
Yaani hakuweza kutofautisha kati ya ahadi ya rambi-rambi na ahadi ya kusomesha mtoto !!
Makala inajipinga yenyewe, halafu mwandishi wa mada anaiweka na kuiunga mkono moyoni mwake na kutoa hitimisho (conclusion) la mawazo yake !!
Huyu mwandishi wa mada hii (Kimbunga) naye ni 'Great Thinker' wa JF !! ??
CCM na vijibaraka wake wana kaazi kweli - kweli !!!

Mkuu naona hii kitu ilikuingia machoni! Mimi nimeandika makala hii wapi? Nilipoandika ni hapo kwenye wekundu na kisha habari yenyewe ikapachikwa kama ilivyokuwa imeandikwa kwenye Gazeti hapo chini ya bandiko langu.
 
Sasa Mwigulu anashikwa pabaya nyumbani kwao.Anatamani anyofoe kucha mtu
 
kwa kweli watu wamehamasika hapo Shelui,nimeonana na Kamanda Waitara maeneo ya stend nikiwa safarini,amenitia nguvu kuwa Dr.Slaa yupo fiti sana
 
katibu mkuu chadema dr wilbroad slaa ameingia mkoani singida kwa kishindo kikubwa ambapo amelakiwa na wabunge tundu lissu na christina mugwai tayari kuungana kulitikisa jimbo la iramba

katibu mkuu anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara eneo la shelui, jimbo la iramba magharibi.

Dr slaa aliyetikisa vilivyo kanda ya magaribi kwa zaidi ya wiki mbili anatarajiwa kuhitimisha ziara yake leo na kurejea jijini dar es salaam.

Update 1.....

Msafara wa katibu mkuu umeshawasili tayari. Wananchi wamejitokeza kwa wingi hapa madukani, mkwajuni. Mkiti wa wilaya ameshafungua mkutano. Katibu wa mkoa anatambulisha viongozi wa chama!

Diwani wa mungaa alex mateo kiondo kajitambulisha hapa akiwapatia wananchi pole kwa jua kali la miaka 52 ya utawala wa ccm. Sasa ni imma jingu diwani wa iseke aliyepatikana uchaguzi mdogo uliopita anasema ccm walikuja na hela kibao zikaliwa na wananchi wakachagua chadema. Amewataka wananchi wajiandae kuchagua utawala wa haki mwaka 2014 na 2015.

Kamanda selema naye kasalimia. Huyu ni yule mmoja wa wale wana ccm waliomfungulia kesi lissu kwa shinikizo la ccm.

Baada ya kaimu mkiti wa mkoa shaaban, sasa kapanda mbunge wa viti maalum, christina. Anawapongeza kwa kujitokeza kwa wingi asubuhi hii pamoja na kuwa na shughuli nyingi.

Updates 2.....

Waitara mratibu wa msafara anaelezea summary ya ziara nzima ya dkt. Slaa ambaye amefanya jumla ya mikutano ya hadhara 20 na kote amefanya vikao vya ndani, akikagua mafaili kujua chama kinavyoendeshwa! Akaomba akiwa njiani afanye mkutano mmoja shelui.

Waitara anasema namna ambavyo mbunge wa iramba magharibi anavyowaaibisha wananchi wa jimbo hili. Alivyotema mate bungeni wkt ccm wanasema ni mahali patakatifu. Anaelezea namna alivyopanga mpango wa kumwagia tindikali kijana wao wa ccm kisha sasa wamemgeuza bango ambapo kinana anamtembeza mikutanoni!

Waitara anawaambia hapa jinsi ambavyo makosa ya kuchagua ccm inayoendekeza ufisadi na kulea utawala mbovu, imeugharimv mkoa huu. Amewaasa kuacha kuhongwa hadi miwa kama walivyofanyiwa na mbunge wao. Anawaambia wamshukuru kamanda lissu ambaye amekuwa akiwapigania sana bungeni. Akishirikiana na wabunge wa viti maalum, christina na christowaja!

Anawauliza kama kuna mtu anakubali kuwa ccm mwisho wake umekaribia, wote wamenyoosha. Na sasa wanapiga pipoz power ya nguvu kumkaribisha lissu jukwaani.

Lissu amepanda. Anaanza kwa kumnukuu aliyekuwa mkiti wa mkoa wa singida, kitundu ambaye alisema lissu huwa anafanya mikutano jimboni kwake tu. Kitu ambacho si kweli. Ukweli ni kwamba amefanya mikutano ktk majimbo yote isipokuwa iramba magharibi tu. Hivyo amewaomba samahani kwa hilo. Anazungumzia maamuzi wa cc.

Anasema chadema imefanya maamuzi ambayo ccm hawawezi kufanya. Ni maamuzi magumu, sahihi na muhimu. Anasema wamewavua uongozi zitto kabwe, dkt. Kitila mkumbo na samson mwigamba

anasema chadema imefanya maamuzi ambayo ccm hawawezi kufanya. Ni maamuzi magumu, sahihi na muhimu. Anasema wamewavua uongozi zitto kabwe, dkt. Kitila mkumbo na samson mwigamba

si suala la chuki binafsi kama watu wanavyotaka kuonesha kutafuta huruma na kuendeleza ulaghai. Wale wale wanaosemwa wanawachukia akina zitto na kitila ndiyo hao hao walikuwa mstari wa mbele kuwatetea waliposhtakiwa kwa kesi mbalimbali, kesi ya ndago, kesi ya manji dhidi ya zitto na alipofukuzwa bungeni. Alipofukuzwa bungeni wale wale wanaompenda leo, walimtukana na kumbeza kwa kila neno na kashfa kibao. Waliosimama naye wima leo wanaonekana eti wanamchukia!

Anasema hapa hatazungumza mwigulu nchemba, bali atazungumza habari za iramba ili wajue habari za kwao. Anawasomea mafungu ya bajeti ya kila mwaka tangu mwaka juzi akionesha namna wanavyostahili kupata fedha nyingi lkn wanachangishwa michango ya kufa mtu!

Anasema mambo haya anayowaambia anajua hakuna mtu wa ccm akiwemo mbunge wao anaweza kuwaambia maneno haya. Badala yake watawaambia mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na bajeti ni finyu, wakati kwa mujibu wa bajeti, kuna mafungu ya huduma mbalimbali, afya, elimu n.k, lkn matokeo yake zinaandikwa kwenye ripoti zimebaki. Kisha wananchi wanachangishwa na kuishia kuhongwa khanga.

Update 3....

Anasema habari za hoja ya ukombozi ni kwa kila mtu. Kila mtu kbs. Anasema chini ya utawala wa ccm kila mtu analiwa, askari polisi wanaliwa. Anasema namna wabunge wa chadema walivyoibua hoja ya stahili za askari polisi rationing allowance ambayo inapaswa kuwa laki moja lkn wanapewa 50,000 pekee. Waziri kagasheki alipokiri bungeni kuwa ni laki moja igp akatuma waraka kwa rpcs wote akiwataka wote waliovujisha siri hiyo ya askari 'kuliwa' na wakubwa wao, wasakwe. Kila mtu analiwa, mkulima analiwa, wafugaji wanaliwa, madaktari wanaliwa, walimu wanaliwa, kila mtu...sasa anapanda dkt. Slaa.

Dkt. Slaa sasa anaelekea mkutano wa pili eneo la kyengege ambako ni kijijini alipozaliwa mbunge wa jimbo la iramba magharibi.

Update 4..

Msafara umeshafika eneo la mkutano hapa kyengege. Pamoja na vitisho, watu wamejitokeza kwa wingi hapa karibu na madukani, mbele kbs ya ofc ya ccm.

Tundu lissu ameshakaribishwa kuzungumza. Anaanza kwa kuonesha namna gani mkoa wa singida umekuwa nyuma miaka 52 tangu uhuru kwa sababu ya uongozi mbovu na siasa chafu za ccm. Anaonesha tofauti ya majimbo mengine yaliyo chini ya ccm na jimbo lake. Anasema mafanikio ya ustawi wa wana singida utaonekana punde wakiiasi ccm!

Source:afisa habari mkuu chadema tumaini makene

wacha waendelee na majungu sisi kazi tu,ni bora askari 10 wenye nidhamu kuliko 1000 wasiona nidhamu,na kwa tafsiri hiyohiyo tutasonga
 
Last edited by a moderator:
Dr usisahau kuwafahamisha yafanywayo na serikali ya CCM kwenye operation zao
View attachment 128351

Maana hata kaburu wa South Africa akiona haya mwenyewe ananywea maana hakupata kuyafanya huko Soweto
 
asante kwa taarifa nzuri iliyozingatia taaluma ya upashaji habari,,,tumepata yaliyojiri huko kama vile nasi tulikuwepo,,,safi sana kamanda,,,muendeleee kutupa hizo taarifa zenye kutia moyo na kutusogeza hapa tulipo, kikubwa ni kushinda lkn pili kupunguza kero za watanzania, mungu ibariki chadema na viongozi wake.
 
Kitengo cha uenezi cha chama kimepwaya sana siku hizi, yaani hatupati updates za kutosha kwa wakati, na picha ndo kabisaaa! Tunaomba makamanda au wana jf walioko huko iramba watupe yanayojiri huko!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom