Dr. Slaa aonekana kuufyata mkia na kumkubali JK...kimyakimya....................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Ni nani atasahau hizi picha.....................

pg17.jpg

Ni nani atasahau hoja hizi za Dr. Slaa.......................

Dk. Slaa apinga matokeo

*Asema Usalama wa Taifa wamechakachua kura
*Aeleza tofauti ya zinazotangazwa na za vituoni
*Sasa aiomba jumuiya ya kimataifa iingilie kati
*Ridhiwan asema ameshaona dalili za kushindwa

Na Maregesi Paul

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, ametoa tuhuma nzito za wizi wa kura akiihusisha Idara ya Usalama wa Taifa.

Amesema kuwa kitendo cha Idara hiyo kujiingiza katika siasa na kushiriki kubadili matokeo ya kura katika maeneo mbalimbali nchini ni cha hatari kwa kuwa viongozi wanaopatikana sio chaguo la wananchi.

Amesema kwamba kubadili matokeo kunaweza kuzua vurugu kwa kuwa wapigakura wanajua ukweli juu ya kinachofanywa.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana.Mmoja wa watuhumiwa wa "uchakachuaji kura", Ridhiwan Kikwete, amejitokeza haraka kujibu tuhuma hizo, akisema Dk. Slaa ametoa madai hewa baada ya kuona kuna dalili zote za yeye kuukosa urais.

Ridhiwan alisema Dk. Slaa anachofanya ni kutapatapa kutokana na imani yake kwamba watu wengi waliokuwa wakifika kwenye mikutano yake wangempa kura.

"Asidanganywe na umati aliokuwa akiupata, awaulize kina Augustine Mrema au Freeman Mbowe, asichukulie kuwa wote aliowaona walikuwa wapigakura wake, wengine walifika kumshangaa mambo aliyokuwa akizungumza," alisema Rishiwan.

Maudhui ya mkutano wa Dk. Slaa yalikuwa kueleza jinsi Chadema isivyoridhishwa na mwenendo wa utoaji matokeo ya kura zilizopigwa Oktoba 31.

"Tumewaiteni hapa ili kuzungumzia mwenendo wa kura za urais kwani kwa mujibu wa Katiba yetu, Rais akishaapishwa hakuna chombo chochote kinachoruhusiwa kuhoji ushindi wake.

"Kwa kuwa NEC inaendelea kutangaza matokeo yanayoonekana kuwa na dosari, naomba nisema yafuatayo kwa kuwa ni ya msingi kwa mustakabali wa nchi hii.

"Kama wote tunaitakia mema nchi hii, naiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifute matokeo yote ya urais na kura zirudiwe upya kwa kuwa hayo yanayotangazwa sio matokeo ya wananchi.

"Hatuwezi kukubali matokeo ya dola, hizo si kura za wananchi, ni kura za Usalama wa Taifa ambao wameshiriki kuchakachua matokeo haya.

"Vile vile matokeo ya ubunge yaliyochakachuliwa katika majimbo yote, NEC iyafute na uchaguzi urejewe upya ili haki iweze kutendeka.

"Lakini, kama tabia hii ya kuchakachua matokeo haitakoma, siku uzalendo utakapotushinda na tukawaamuru wananchi waingie mitaani, tusilaumiwe.

"Hivi wananchi wakiingia mitaani nani atabaki, siyo CCM wala Chadema, CCM wasitake kutupeleka huko tusikotaka.

"Katika haya, jumuiya ya kimataifa lazima itoe hadharani ripoti yake, TEMCO nao wasiogope kuitoa, waitoe ili wananchi wajue kilichofanywa na CCM," alisema Dk. Slaa.

Alimtaka Mkuu wa Usalama wa Taifa ajiuzulu wadhifa huo kwa maelezo kwamba ana hakika maofisa wa Idara yake wameshiriki kubadili matokeo ya kura zinazoelekea kumpa ushindi mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Katika mkutano huo, mgombea huyo wa urais alitumia muda mrefu kueleza jinsi matokeo yalivyobadilishwa.

Alisema kuwa matokeo ya urais yanayotangazwa na NEC kutoka katika majimbo nchini yanatofautiana na matokeo yaliyoko katika vituo vya kupigia kura.

Katika hatua nyingine, alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, aongoze Jeshi hilo kwa mujibu wa Kitabu cha Haki na Wajibu kwa Mpiga Kura kilichotungwa na Jeshi la Polisi.

Ama kweli kimya cha Dr. Slaa kina mshindo mkuu......................
 
Elizaa

Senior Member
Oct 19, 2010
136
225
Dr Slaa ni mtu mwenye busara, haina maana kuendeleza malumbano yasiyoleta tija. Kama katiba inasema rais akishatangazwa huwezi kupinga!!! ya nini aendelee kung'ang'ania kutokubali matokeo????
Kunyamaza ni busara na hekima.
Hongera Dr Slaa kwa kutumia busara kwa hili.
 
Lisa Rina

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
2,212
2,000
Ila ss km mambo yatakua ivivi kila wkt so inabidi wawe wananyamza tu?tutafka kweli?c 2tatawaliwa na hawa watu maisha?mana chances za katiba kubadilishwa
Naona ni ndogo mno.neways imjussaying
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,287
2,000
Dr. Slaa angeweza kabisa kufanya kama walivyofanya kule Ivory Coast; alikuwa na haki ya kulalamika hivyo na tuliona mwanzo lakini mwishowe hekima na mapenzi kwa nchi yake yalizidi kutaka kuingia madarakani. Kumbuka upande wa pili hawakuahidi hata mara moja kuwa wakishindwa watakubali matokeo. Maana yake ni kuwa badala ya kumuona kafyata mkia, ni muhimu kumuona kama shujaa aliyeliepushia taifa lake madhara makubwa. NInaamini si mtu mwenye kiu ya madaraka kwani wenye kiu tumewaona wamefikia hatua gani kuyachukua au kubakia nayo.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Kwa kifupi Ruta, unachosema hapa ni kwamba YOU and YOUR boss are very much worried about the forgoing silence. Kweni ni kama vile kivuli kinawakimbiza vile.

Tulieni Mle jamaa! Achebe anahoji kwamba 'ni nani hasa huyo menye uwezo wa kutema tonge la ugali na mnofu wa samaki ambalo BAHATI LIMETWALISHA mdomoni mwake kimiujiza tu???' Chamsingi hapa ni kuendelea kula kwa amani tu wala kusiwepo na mashaka.

Naamini kwamba tunapoangalia kapicha mathalan ya Dr Mvungi akikimbizwa na kicha pale Kariakoo sokoni wengi watamuonea huruma sana na hata kutamani kuonelea wamuokoe vipi na janga hilo. Lakini, pindi unapogeuza picha hii ya kwamba sasa ni huyu mwanafalsafa wa sheria ndie kweli kachukua fimbo na kuanza kumkimbiza kichaa kila mtu atashangaa sana na hata kuhamaki kutamani kumtia adabu kidogo.

Ratiba ya uchaguzi ilishakamilika hata kama uchaguzi haukufanyika sasa cha msingi ni kushugulikia visababishi vya hali hiyo na wala si mateo yatokanayo na hali hiyo. Hofu yangu ni kwamba endapo utakua unasubiri kuona watu wakijihangaisha kushughulikia matokeo basi kuna uwezekano ukasubiri sana hapa
.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Ila ss km mambo yatakua ivivi kila wkt so inabidi wawe wananyamza tu?tutafka kweli?c 2tatawaliwa na hawa watu maisha?mana chances za katiba kubadilishwa
Naona ni ndogo mno.neways imjussaying

Hapo kwenye katiba utanitonesha bureeeeee. Kwa madaraka wadandie salama lakini kwa katiba mzee hata Dr Slaa na wanaharakati wengine wengi waliokwishajitokeza kamwe hatutowaachia hata ka-mwanya wakameza mate nakuambia tena.

Hili la katiba, Dr Slaa na wengine ni wabeba ujumbe tu, lakini moto wote ni umma wa Tanzania.
 
Simple Mind

Member
Oct 27, 2010
9
20
Mijadala kama hii imepitwa na wakati. Vumbi la kisiasa limeshatulia na maisha yanatakiwa yaendelee. Nakubaliana na Mwanakijiji kwamba hapo ni busara imetumika kuliepusha taifa na vurugu na machafuko ambaye kawaida masikini ndiyo huwa wanaathirika sana kwani hupigania wasichokiweza. Slaa alisema hana dola wala mabomu hivyo hawezi kupigana wala kusababisha machafuko
 
Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,115

SIoni kama hoja ya Mwanakijiji ina msingi wowote. Ishu hapa sio Slaa kama individual kukataa matokeo, maana akifanya hivo atakuwa hajui maana na thamani ya dhamana ya watu waliochukua muda wao kushiriki mchakato wa kampeni na hatimaye kuhitimisha kwa kumpigia kura. Hapa na-assume kwamba kweli kura zake zimechakachuliwa.

Lakini kinyume chake mi naona kwamba huyu bwana akiendelea kukaa kimya bila kufanya lolote sisi wengine tutamchukulia kama ni mwongo,mzandiki na sore loser tu. Maana haiezekani wewe mtu uibiwe kura zako in plain sight halafu ukae kimya walau usioneshe kwa dunia (neutrals) vidhibiti kuonesha hoja yako. It simply does n't add up.
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
Mkuu Abdulhalim, heshima kwako. Umesema Dr Slaa hajaonyesha uthibitisho wa kuibwa kura. Je siku aliyoomba harakati za kuhesbu kura isimmishwe hakutoa ushahidi? Je si kweli kuwa tume ikakiri kuwa Geita 'walikosea' kutoa hesabu na kumnyima kura 18,000. Dr Slaa pia alitoa mifano mingine. Sasa unataka ushahidi gani zaidi? Dr Slaa hana vyombo vya dola kuchunguza kama polisi, ameleta mezani evidence alizo nazo. Kama wewe pamoja na hayo bado unaamini uchaguzi ulikuwa wa haki basi ni kwa kuwa umeamua na si kwa sababu Dr Slaa alikaa kimya. Mimi binafsi nasema the burden of proof haiko na dr Slaa yeye alshatoa evidence alicho nacho na hata baadhi ya magazeti kama Mwanahalisi wameonyesha. The burden of proof iko na serikali ikanushe na kutueleza wanawezaje ku'kosea' kur a 18,000 za mgombea, Geita, yale masanduku ya kura yaliyokamatwa Segerea yametoka wapi nk.
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,228
2,000
Ruta, personally sina matatizo sana na kimya cha Dr Slaa kwani kwa mazingira yaliyopo sasa hakuna hekima iliyo bora kama kukaa kimya.
Besides, kukaa kimya kunampa mtu space ya ku-contemplate objectively.

Kwa jinsi unavyojitambulisha kwenye signature yako nina uhakika kuna kitu umeki-analyse tayari - so mwaga nyanga zako hapa jamvini tukusikie!

Otherwise, tuambie wewe ungekuwa Dr Slaa ungefanyeje? Huna haki ya kumlaumu Dr kama wewe mwenyewe huna hata chembe ya idea...
 
Lisa Rina

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
2,212
2,000
Hapo kwenye katiba utanitonesha bureeeeee. Kwa madaraka wadandie salama lakini kwa katiba mzee hata Dr Slaa na wanaharakati wengine wengi waliokwishajitokeza kamwe hatutowaachia hata ka-mwanya wakameza mate nakuambia tena.

Hili la katiba, Dr Slaa na wengine ni wabeba ujumbe tu, lakini moto wote ni umma wa Tanzania.

Tuombe iwe ivo...kila kitu chawezekana!
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Ruta, personally sina matatizo sana na kimya cha Dr Slaa kwani kwa mazingira yaliyopo sasa hakuna hekima iliyo bora kama kukaa kimya.
Besides, kukaa kimya kunampa mtu space ya ku-contemplate objectively.

Kwa jinsi unavyojitambulisha kwenye signature yako nina uhakika kuna kitu umeki-analyse tayari - so mwaga nyanga zako hapa jamvini tukusikie!

Otherwise, tuambie wewe ungekuwa Dr Slaa ungefanyeje? Huna haki ya kumlaumu Dr kama wewe mwenyewe huna hata chembe ya idea...

Dr. Slaa's best weapon are the courts of law...................silence means poor leadership.................If Dr. Slaa can't stand the heat he has no reason to complain...................hence he has no business being in the kitchen...................He impresses upon me as a whiner.....but nothing else....
 
Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,703
2,000
Mkuu Abdulhalim, heshima kwako. Umesema Dr Slaa hajaonyesha uthibitisho wa kuibwa kura. Je siku aliyoomba harakati za kuhesbu kura isimmishwe hakutoa ushahidi? Je si kweli kuwa tume ikakiri kuwa Geita 'walikosea' kutoa hesabu na kumnyima kura 18,000. Dr Slaa pia alitoa mifano mingine. Sasa unataka ushahidi gani zaidi? Dr Slaa hana vyombo vya dola kuchunguza kama polisi, ameleta mezani evidence alizo nazo. Kama wewe pamoja na hayo bado unaamini uchaguzi ulikuwa wa haki basi ni kwa kuwa umeamua na si kwa sababu Dr Slaa alikaa kimya. Mimi binafsi nasema the burden of proof haiko na dr Slaa yeye alshatoa evidence alicho nacho na hata baadhi ya magazeti kama Mwanahalisi wameonyesha. The burden of proof iko na serikali ikanushe na kutueleza wanawezaje ku'kosea' kur a 18,000 za mgombea, Geita, yale masanduku ya kura yaliyokamatwa Segerea yametoka wapi nk.

Dr Slaa ametoa ushahidi mwingi tu, hata humu JF ilandikwa na mahesabu yakatolewa ni wajibu wa Serikali kukanusha.
Lakini kwa kuwa wao wameshikilia dola Dr kaamua kunyamaza, lakini kimya kingi kina mshindo mkuu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Dr. Slaa angeweza kabisa kufanya kama walivyofanya kule Ivory Coast; alikuwa na haki ya kulalamika hivyo na tuliona mwanzo lakini mwishowe hekima na mapenzi kwa nchi yake yalizidi kutaka kuingia madarakani. Kumbuka upande wa pili hawakuahidi hata mara moja kuwa wakishindwa watakubali matokeo. Maana yake ni kuwa badala ya kumuona kafyata mkia, ni muhimu kumuona kama shujaa aliyeliepushia taifa lake madhara makubwa. NInaamini si mtu mwenye kiu ya madaraka kwani wenye kiu tumewaona wamefikia hatua gani kuyachukua au kubakia nayo.
With all due respect Mzee Mwananakijiji.......................Nchi inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia na utawala bora......unapoona umeonewa unakimbilia mahakamani siyo kwenye mahakama za kisiasa....................au public opinion........................tatizo la Dr. Slaa ni kutoa tafsiri ya katiba yetu kuwa inamzuia kwenda mahakamani kuhoji matokeo ya kura ya Uraisi iliyotamkwa na NEC...........Huwezi ukawa na rundo la ushahidi halafu ukachelea kwenda mahakamani..........na hata mahakama kama itakudhulumu hiyo itakuwa ni hoja nyingie ya kudai mfumo mpya wa kikatiba kwa sababu mahakama zitaonekana zina muundo wa kulinda haki za watawala tu...........

Kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama tu.......................Dr. Slaa alifanya makosa kuingilia uhuru wa Mahakama wa kutafsiri sheria za nchi kazi ambayo ni ya mahakama........................................

Kuna msemo usemao............the greatest error in life is self-defeat.................and Dr. Slaa is slowly teetering to that nook.................
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
SIoni kama hoja ya Mwanakijiji ina msingi wowote. Ishu hapa sio Slaa kama individual kukataa matokeo, maana akifanya hivo atakuwa hajui maana na thamani ya dhamana ya watu waliochukua muda wao kushiriki mchakato wa kampeni na hatimaye kuhitimisha kwa kumpigia kura. Hapa na-assume kwamba kweli kura zake zimechakachuliwa.

Lakini kinyume chake mi naona kwamba huyu bwana akiendelea kukaa kimya bila kufanya lolote sisi wengine tutamchukulia kama ni mwongo,mzandiki na sore loser tu. Maana haiezekani wewe mtu uibiwe kura zako in plain sight halafu ukae kimya walau usioneshe kwa dunia (neutrals) vidhibiti kuonesha hoja yako. It simply does n't add up.

Hizi ndizo hoja za kimsingi hapa....................kama Dr. Slaa ana ushahidi kwa nini haendi mahakamani?............vinginevyo Dr. Slaa ni tapeli wa kimataifa.......................Aona hawezi kugeuza ukweli kuwa JK alimzidi kete..........za kuchakachua kiasi kwamba hawezi hata kujua JK alifanyeje hata kumbwaga..................
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
<p>
Dr. Slaa's best weapon are the courts of law...................silence means poor leadership.................If Dr. Slaa can't stand the heat he has no reason to complain...................hence he has no business being in the kitchen...................He impresses upon me as a whiner.....but nothing else....
</p>
<p>&nbsp;</p>
Mkuu I sense ur frustration but there are many ways to skin a cat. Running to courts when the options are limited will only result in Dr Slaa becoming another Rev Mtikila, best case scenario - "that batty uncle living in the attic."
If we want dr Slaa to remain a national leader, we need to give him room to act like a leader not a radical activist.
I would actually turn it around n say let others go to court on his behalf. Let Rev Mtikila do that (I believe he is doing that).
Remember it is not abt winning the battle (n wasting energy on it) but winning the war. That is the good signs of leadership. That is the strategy that I see dr Slaa using, n we need to patiently see where he wants to go.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,574
2,000
Dr Slaa ametoa ushahidi mwingi tu, hata humu JF ilandikwa na mahesabu yakatolewa ni wajibu wa Serikali kukanusha.
Lakini kwa kuwa wao wameshikilia dola Dr kaamua kunyamaza, lakini kimya kingi kina mshindo mkuu!!!!!!!!!!!!!!!

Unachofanya hapa unatetea uozo wa kukalia haki na hivyo kutoa mfano mbaya kwa jamii kuwa ukionea wewe jitulize kasuku.....................huo ni uzembe gani..........................Those are signatures of a poor leader.................
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
<p>
Hizi ndizo hoja za kimsingi hapa....................kama Dr. Slaa ana ushahidi kwa nini haendi mahakamani?............vinginevyo Dr. Slaa ni tapeli wa kimataifa.......................Aona hawezi kugeuza ukweli kuwa JK alimzidi kete..........za kuchakachua kiasi kwamba hawezi hata kujua JK alifanyeje hata kumbwaga..................
</p>
<p>&nbsp;</p>
Hapana tutakuwa tunarudiarudia hoja bila sababu; kama ingekuwa ni uchaguzi wa mbunge nina uhakika dr Slaa angekuwa mahakamani. Lkn katiba iko wazi kuwa ktk kura za Rais hakuna rufani.
Sasa kama unaelewa hayo kwa nini uanze kum-accuse dr Slaa kuwa tapeli kwa kuwa hatendi kama UNAVYOTAKA wewe. Hii haiko sawa kwani hatua unazotaka achukue ziko kinyume na sheria. Asante.
 
Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,115
2,000
Mkuu Abdulhalim, heshima kwako. Umesema Dr Slaa hajaonyesha uthibitisho wa kuibwa kura. Je siku aliyoomba harakati za kuhesbu kura isimmishwe hakutoa ushahidi? Je si kweli kuwa tume ikakiri kuwa Geita 'walikosea' kutoa hesabu na kumnyima kura 18,000. Dr Slaa pia alitoa mifano mingine. Sasa unataka ushahidi gani zaidi? Dr Slaa hana vyombo vya dola kuchunguza kama polisi, ameleta mezani evidence alizo nazo. Kama wewe pamoja na hayo bado unaamini uchaguzi ulikuwa wa haki basi ni kwa kuwa umeamua na si kwa sababu Dr Slaa alikaa kimya. Mimi binafsi nasema the burden of proof haiko na dr Slaa yeye alshatoa evidence alicho nacho na hata baadhi ya magazeti kama Mwanahalisi wameonyesha. The burden of proof iko na serikali ikanushe na kutueleza wanawezaje ku'kosea' kur a 18,000 za mgombea, Geita, yale masanduku ya kura yaliyokamatwa Segerea yametoka wapi nk.

Nimekusoma.

Binafsi sijaona huo ushahidi, na ningependa kuona kuna official documents kutoka kwa wahusika kuonesha vielelezo vyao..hotuba za mdomoni tu hazisaidii lolote.

Labda ishu nyingine ni significance ya discrepancy wanayoiongelea..kama kweli ni significant halafu Slaa anakaa kimya bila kutoa muongozo wowote anataka waliokusapoti wamueleweje? Kwamba their efforts were for nothing? Hata kama sio significant, kwamba makosa ni ya kibinadamu na sio ya kupangwa, lakini kuna mikakati gani kuhakikisha kwamba kuna mchakato huru kwene chaguzi zijazo, baada ya somo la uchaguzi ulioisha? Does it count kwamba kushiriki ni muhimu kuliko kujua process ya refereeing?

Haya ni mambo ambayo tulitegemea CDM waanze kuyavalia njuga, kabla hayajapoa, yaani ni top ktk 'to-do' list. IMO, ni ya muhimu maana yanahusika moja kwa moja na crop ya uongozi na maamuzi ya mustakabali wa taifa. Refereeing mbovu uongozi mbovu. Kama haina mikakati yoyote basi CDM iketi kitako na kujiunga na CUF...tujue moja.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom