Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

kwanza hoja ya ufisadi imefikia mwisho utambue hilo. na ACT ndo chama makini cha upinzani kwa sasa.
 
Kama unataka uthibitisho kwamba sisi wengine ni CDM basi sema tukutumie namba za kadi zetu ukaprove ..usiwasakizie CCM kila jambo kwa ujinga wenu wenyewe kwani ndo waliowatuma mkauze chama chetu?

Nyie wapuuzi hamtakiwi hata kupewa uwezo wa kumiliki simu sa we unasema chama kimeuzwa we unaushahidi wowote wa mauzo na manunuzi cha chama au unaongea kwakuwa unamdomo na hulipii
 

Hata ww unastahili kuheshimiwa..ni haki ya kila mtanzania kikatiba
 
Leo lowasa awe mgombea kupitia chadema chama ilimwandaa lini?kwanini mwonzoni lowasa hakufunguka na aje chadema mpaka akatwe ccm kama siyo uroho wa madaraka?

Mkuu, Lowassa alifunguka kuhusu hili suala la Richmond hata alivyokuwa bado yuko ndani ya CCM. Kuna kipindi CCM walikuwa na mkutano mkuu, Edward Lowassa alikuwa analalamika jinsi Nape anavyomchafua na CCM imekaa kimya bila kumnyamazisha Nape. Edward Lowassa akaendelea kusema kwamba kama suala lenyewe analolitumia Nape kumchafua ni la Richmond, "kuna kitu gani nilichofanya katika Richmond ambacho Mh Raisi na mwenyekiti wa Chama hukukijua", Lowassa aliuliza. Mh Mkapa aliingilia kati haraka sana na kuomba mkutano uishe ili kumkinga mwenekiti.


Lowassa kuja Chadema na kupewa nafasi ya kugombea Uraisi hii imetoka na kimkakati zaidi. Lowassa ana watu wengi sana nyuma yake wanaomkubali, hilo tumeshuhudia wakati anazunguka mikoani kuomba wadhamini kwa tiketi ya CCM.
Watu wote wanaomkubali Lowassa ndani ya CCM watampa kura Lowassa na sisi tulio nje ya CCM tutampa kura Lowassa kwa lengo la kuiondoa CCM madarakani. Kuja kwa Lowassa Chadema amekuja na wanachama wengi sana, ushahidi ni kwamba kwa sasa tumeishiwa kadi za chama karibu katika ofisi zetu zote, watu wanajiunga Chadema kwa speed ya roketi. Naomba mkuu usitishike kwa hili la Lowassa kupeperusha bendera yetu, naomba tushikamane pamoja ili tushinde vita hii. "Sisi sote ni ndugu, adui yetu ni CCM"
 

Kiuhalisia ni kwamba CHADEMA na UKAWA wamejiunga na Lowassa na Lowassa hajajiunga na CHADEMA na UKAWA. Lowassa ana nguvu kubwa kuliko CHADEMA.

Mbowe ni bonge la mjasiria Mali, ana akili ya biashara. Katika hili mmachame huyu nampa big up. Hivyo ndivyo walivyo hasa linapokuja suala la kupiga hela hawaachi fursa ipite. Mbowe alishasema hawezi kuacha kumpokea Lowassa mtu anayekuja na wafuasi zaidi ya 1bill. Vinginevyo mtamuona kichaa kwa sababu maisha ya chama yanategemea watu. Kadi CDM inapatikana kwa Tshs 1,500/=, kwa watu zaidi ya 1 bill CDM wataingiza zaidi ya 1.5 bill za haraka. Ila ni kama kweli hao watu watajiunga CDM.

Tanzania ina fursa nyingi na Mbowe amegundua fursa, ambayo ni kutumia wananchi kupata ajira na fedha za kula bata duniani.
 

Ushahidi upo na anao Dr. Slaa kwani ndie aliyekuwa anamtangaza Lowasa Fisadi sasa tazameni mlipoweka ushahidi.
 

Ushahidi wanao Dk Slaa na Mbowe....waliomtangaza pale mwembeyanga.....
Au waliposema kuwa wana ushahidi kuwa Lowasa ni fisadi walikuwa wanatuongopea wananchi.....
 
Kwenye list of shame mlimleta ya nini kama mnamsimamisha Leo kama sio uwehu,hivi unajua hata unachosimamia?

Viongozi wa CHADEMA sio watu wa kuwaamini tena....bora nisipige kura tu nijipumzikie nyumbani....
Wao wenyewe kwa vinywa chao walituambia kuwa ushahidi wanao wa kuthibitisha kuwa Lowasa ni fisadi na kama anaona anaonewa awahi mahakamani... .leo wanatuambia kuwa ushahidi hawana na Lowasa ni msafi na kama kuna mtu mwenye ushahidi apeleke mahakamani.....sasa je ule ushahidi waliotuambia kuwa wanao ulikuwa ni wa uongo....??
Na kama ni uongo je hii inajenga picha gani kwa wapiga kama sio unafiki....???
SINA IMANI NA CHADEMA....
 
Kwa hili niko na wewe mkuu .
Bora CCM ichukue tena nchi kuliko
UKAWAna Lowasa .

Kumbukukeni Lowasa anapata fedha za kampeni
kutoka kwa watu wake ye anasema " marafiki" wa Lowasa .

Na hao marafiki watataka kurudishiwa fadhila
Lowasa akichukua ofisi . Ndo haposasa.
Hakuna cha bure siku hizi .
Bora Magufuli na CCM kuliko Lowasa UKAWA.
 

Mkuu nina kila sababu ya kuwaita viongozi wangu wa CHADEMA ni wanafki.....na sijui hao wanaowaunga mkono wanatumia kiungo gani cha mwili kufikiri....
Katika hali ya kawaida hata kama Lowasa ni msafi kama wanavyodai ingawa walituambia kuwa ni mchafu na ushahidi wanao.....lakini si kwa kutuaminisha kwa kauli nyepesi kama hizi eti systerm ndio mbovu na sio Lowasa.....ina maaana vibaka wote wakihamia CDM wanakuwa wasafi kwa kuwa kinachotakiwa ni kuiangusha CCM tu.....
Ukombozi wa kweli hauishii kwenye kuitoa tu CCM madarakani pekeeem..bali tunatakiwa tuweke watu makini wenye nia ya dhati ya kutufikisha kwenye nchi ya ahadi...na sio mamluki walio tayari kufanya lolote kwa ajili kupata uongozi kwa manufaa yao na vibaraka wao.....
 
Kwenye list of shame mlimleta ya nini kama mnamsimamisha Leo kama sio uwehu,hivi unajua hata unachosimamia?

Kwenye list of shame ata mkuu Wa kaya yupo kwa hiyo mwenyekiti wako ni fisadi ccm ni chama cha mafisadi ndio maana adi mwenyekiti fisadi
 
Kama kila ambaye hakubaliani na kamati kuu akifanya hivyo itakuwaje?Ni wangapi ambao huko nyuma waliwahi kutofautiana na kamati kuuvkatika maamuzi?je,nao walizira na kususia chama kama alivyofanya yeye?
 
Napenda kutoa rai kwa makamanda wenzangu, wanaharakati, na watanzania wote.

Uamuzi wa Dr . Slaa uheshimiwe..amefanya uamuzi sahihi kwa nafsi yake, na amesema hajaondoka kwenye chama..tumpe muda atafakari zaidi, atajoin nasi mbele ya safari.

Mchango wake kwenye chama chetu ni mkubwa sana..tuuheshimu kwa kufunga midomo yetu kumjadili, tufocus zaid kwenye uchaguzi mkuu wa oct 25.

Na uamuzi wa Mbowe kumruhusu Lowassa aingie kwenye chama nao ni sahihi kutokana na hali ya kisiasa ya wakati huu. Kila mtu aheshimu mawazo ya mwenzake.

Maccm yanaendeleza propaganda nyingi kana kwamba kuna mpasuko mkubwa, na chimvi nyingi juu ya Dr Slaa na juu ya Lowassa, na juu ya Mbowe na uamuzi wa Chama..tuwapuuze, tusiwape nafasi.

ALUTA KONTINUA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…