Dr. Slaa Anafaa Kuwa Rais

Wakuu,
Ni siku chache zimebaki watanzania tutakapopiga kura kuchagua viongozi wetu ( wawe watu au chama!)
Ni wazi, kwa sasa kila mtanzania mwenye haki ya kupiga kura atakuwa ameshasikiliza sera za vyama mbali mbali katika kampeni zinazoendelea kwa sasa.
Baada ya kusikiliza kampeni za vyama mbali mbali, binafsi nimeona kwamba Dr Slaa anafaa kuwa rais wa nchi yetu.
Pengine mkuu yeyote anaweza kuniuliza ni kwanini. Majibu yako mengi lakini hasa; Dr Slaa-
  • Ni mjasiri anayetetea maslahi ya taifa (sote tumeshuhudia bungeni).
  • Anatoa matumaini kwa watanzania walio wengi kupitia sera ya elimu bure.
  • anaahidi vitu vinavyotekelezeka, mfano kupunguza kodi ya vifaa vya ujenzi.
  • Tunamuamini tunamhitaji.
  • Ongezea...!
Kutokana na hayo, Dr WS anafaa kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 31 oktoba, 2010.


Mungu ibariki Afrika! Mungu ibariki Tanzania!


nawasilisha!!!

Nilijua unataka kusema ANA VIGEZO au SIFA ZA KUWA RAIS kumbe ANAFAA?
 
tatizo umri umemtupa mkono

Umri si kigezo umri wake unatosha sana tena watu kama Dr slaa kwa umri wao ni dawa ya nchi hii. Dr slaa ni mti wa dawa uliokomaa kushimbwa dawa na kutibu magonjwa sugu. Karibu Dr slaa kipenzi cha watanzania.
 
Hana dhambi usimlinganishe na aliegeuza madhabau kuwa sehemu ya kugegeda amri 6

Hii imechuja kajipange upya Mingoi! Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyaona ndani ya ccm watayafafuta nje ya ccm (Mwalimu Nyerere)
 
Umri si kigezo umri wake unatosha sana tena watu kama Dr slaa kwa umri wao ni dawa ya nchi hii. Dr slaa ni mti wa dawa uliokomaa kushimbwa dawa na kutibu magonjwa sugu. Karibu Dr slaa kipenzi cha watanzania.

kuwa na umri mkubwa sio hekima ona jinsi mugabe pamoja na kuwa na umri mkbwa alivyoiharibu zimbabwe
 
kuwa na umri mkubwa sio hekima ona jinsi mugabe pamoja na kuwa na umri mkbwa alivyoiharibu zimbabwe

Ebu nikumbushe juzi Mugabe kachaguliwa kuwa kiongozi gani vile Africa? Dr slaa anatosha anayo dawa ya kutibu ufisadi na ccm mnamuogopa.
 
mkuu minda nakuunga mkono 101%. mh profesa dr slaa ndiye anafaa kuikomboa nchi hii kutoka kwenye lindi la ufisadi ulioasisiwa na ccm na kuipeleka kwenye ukombozi halisi na maendeleo endelevu. hongera prof slaa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom