Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 42,558
- 35,261
Ni obvious, upinzani Tanzania kuhusu urais, watausikia tu kwenye bomba tu, kwasababu, kwanza hawana mgombea mwenye kaliba ya urais, lakini pia, hawana agenda zenye kugusa maisha halisi ya wa wananchi wote wa Tanzania, bali wao, wamejikita zaidi katika kuwatukuza viongozi wao, kwa kampeni za kuchangisha pesa kwaajili ya kuwasitiri viongozi wao, dhidi ya hali ngumu za kimaisha hususani kiuchumi wanazopitia huko mitaani wanakoishi.
Wapinzania hawana sera zenye ushawishi kwa wanachama wao wenyewe, na kwenye vyama vingine vya siasa nchini kitu ambacho kinathibitisha uwezo wao mdogo wa kuliunganisha taifa kisera. Na mbaya zaidi wapinzani Tanzania wana chuki na uhasama mkubwa sana baina yao, na kuwafanya kuko kabisa hoja zenye mashiko au muendelezo, walau za kuwavutia wapiga kura wa nchi hii.
Kubwa wanalolifanya zaidi wapinzani Tanzania kwa sasa, ni kuendekeza chuki na kuchochea uhasama, migawanyiko na ghasia miongoni mwa waTanzania, kwa kisingizio cha kudai au kutetea haki ambazo tayari kila mTanzanai anazo na yuko huru kuzitumia kadiri apendavyo.
Kama mdau wa siasa za Tanzania, una maoni gani kuhusu jambo hili la kisiasa kwa upinzani nchini, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2030, ukiachilia mbali uchaguzi wa serikali za mitaa 2029?
Mungu Ibariki Tanzania.