Dr. Slaa AMKIMBIA Wilson Mukama katika mjadala?

Kafanya la maana yaani wewe Mbuni halafu uende kufanya mdahalo nyumbani kwa Nyani na unayefanya nae huo mdahalo ni Kima! Heri hata wangeenda ITV au STarTv KIDOOOGO! si mnakumbuka last time kila akitaka kuongea anakatizwa ila akiongea mwenzie aaaahh, ndio hakwenda sasa wajinyonge na TENDWA NA BANA wamekiri kuwa WAAJIRI wao wanaelekea shimoni. Full stop
Wakati mwingine kushiriki katika midahalo na watu kama Mukama au Nape ni kujishushia hadhi inakua ni sawa na" kumimbiza mwendawazimu ukiwa uchi baada ya kuchukua nguo zako wakati unaoga kisimani ambapo mwendawazimu huyo akiwa amevaa nguo"Watu watashindwa kuelewa nani mwendawazimu kati yako na huyo aliechukua nguo zako.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
A man bosts his *p... though its small.. The Beautyful are Not Yet Born, Miongoni mwa majitu majinga TZ ni Slaa.
 
Kiingereza chako tu kina matege, sasa utakuwaje na academic qualifications? Kama una ubavu weka credentials zako humu jamvini watu wakufanyie evaluation. Usipende kujisifia wacha watu wakusifie kama unastahili.
 
Naona unahangaika kujibu kila mtu dada........ we ulitakaje? Ahudhurie au asihudhurie? Ni vema hakuhudhuria na kwa hili imefichua upumbavu wako kwani umeishia kutukana matusi kila unayeona post yake. Pole..! words are wind but blows are unkind.
 
Wewe na wenzako manaomsifia ndiyo mnaotukana bila kutoa majibu.
 
Dk. Wilbroad Slaa ameingia mitini licha ya kuthibitisha kushiriki kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 ambacho kililenga kumkutanisha na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. Wote walithibitisha kushiriki lakini ghafla Dk. Slaa akaingia mitini.

Magwanda hoja yao kuu ni moja2''ufisadi''.Hoja ikiwa tofauti wanakua kama wamefilisiwa chakuongea.watz wana kero tofauti tofauti acheni kukariri!
 
pipoooooooooooooz!!!!!! kwanza tbc wangemchakachua dr.slaa2 mana wakiona anatachi kwenye ukweli wanajifanya kuvurugavuruga2!
 
Kamura tuliza munkari dogo ungefanya mashambulizi yako kwa staha kidoggo ingekusaidia hata wewe kuwa mwerevu. Tunu za mwanadamu ni mbili tu AKILI na HAYA. Tumia japo moja kti ya hizo vinginevyo utaendelea kudharaulika.......... Pole tena!!!!!!!!
 
Huyu mzee anako elekea ni kubaya, kila siku zinavyo kwenda anazidi kuwa punguani. Mi na wasi wasi kina Zitto wamempiga kipapai.
 
Mukama huyu huyu wa magamba?kama ni huyu hapana halingani DK,Pia ni vizuri DK hakwenda kwa sababu asingekuwa huru kuzungumza TBC1 angekuwa kama picha tu,nafasi angepewa bosi wa aliyechoka MUKAMA.Mdahalo wafanyie TV nyingine sio TBC,hicho chombo ni cha CCM,kwa taarifa yenu inteligensia imefanya kazi na kugundua walichopanga CCM na TBC1.
 
Mkuu kiswahili nacho ni lugha. Kwanini ujikakamue kuongea lugha ambayo haikupendi?
 
Hivi Mkama ndiyo nani? Ni CCM? Kama ni ndiyo basi yeye na wapambe wake wasome sahihi yangu.....
 
WanaJF,
Siamini kama kwa umaskini niliouona vijijini hii thread inastahili kuwapotezea watu makini muda wao. Ninaamini watanzania tuna sababu ya kubadili fikra zetu kutoka kwenye ushabiki usio na maana kuelekea ujengaji wa hoja yenye tija kwa manufaa ya Taifa letu. Ni ushabiki huu usio na maana leo miaka 50 baada ya uhuru wazazi wetu, wajomba zetu, marafiki zetu wengi vijijini hususan Igunga ambapo nimeshuhudia kwa macho yangu baada ya kupita vijiji vyote wanaishi kwenye maisha chini ya kiwango cha binadamu. Fikiria, takriban vijiji vyote 98 hakuna maji ya uhakika, safi wala salama. Mabwawa machache yaliyoko ndiyo maji ya binadamu, ng'ombe, fisi kwa matumizi yote unayoweza kufikiria. Vijiji takriban theluthio mbili haviko karibu na zahanati na hata vyenye zahanati hakuna dawa wala wataalamu, barabara sehemu kubwa ni mapalio ya ng'ombe, madarasa ya watoto wetu ni magofu yasiyotamanika wakati rasilimali za taifa zinachezewa na watu wachache. Pamoja na yote haya badala ya sisi tulioona mwanga tunaleta pumba kwenye Jamvi hili Tukufu linalopaswa kuwa mwanzo wa fikra ya ukombozi. Inanisikitisha sana. Huhitakji kwenda shule kuelewa hali halisi ya nchi yetu kwa mtu mwenye nia njema na dhamira safi ya iukombozi. Wakati umefika wa kuacha mawazo ya kufikirika na kuwa " concrete", time is Money, tungelitumia muda tunaotumia kwenye porojo za upupu kwenye mawazo ya kujenga Taifa tunmgelisogeza Taifa letu hatua mbele.

Kuhusiana na Mada Dr Slaa kumkimbia Mukama Facts ni hizi hapa, na mwenye busara atapata mang'amuzi sahihi:-
i) Tarehe 5 Oktoba 2011, siku ya Jumatano nilipokea SMS (moja kati ya sms takriban 800 nilizopokea siku hiyo), kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama mtangazaji wa TBC1 akiniomba nishiriki kipindi cha Jambo Tanzania kingerushwa tarehe 7 Oktoba, 2011. Kwa kuwa nilikuwa safari na kutokana na uwingi wa sms sikuweza kumjibu kama ambavyo siku jibu sms nyingine nyingi pia.
ii) Taree 6 Oktoba 2011, siku ya alhamisi alinipigia simu ya mkono mtu aliyejitambulisha kuwa ndiye aliyeniletea sms jana yake kuhusiana na kipindi cha Jambo Tanzania. Tulisalimiana vizuri. Nikamjibu kuwa sitaweza kushiriki kwa kuwa niko mbali na Dar-Es-Salaam. Ndipo aliponiambia kuwa kipindi kingemshirikisha pia Bwana Mukama, Katibu Mkuu wa CCM na kuwa tungelijadili maswala ya Uchaguzi wa Igunga uliomalizika punde na Tuhuma ya Chadema kuingiza nchini magaidi kama alivyotuhumu bwana Mukama. Nikamjibu kuwa "niko mbali hivyo sitaweza kushiriki hata angelishiriki nani". Swali ni kuwa "niko mbali na Dsm". Nikaeleza " hata hivyo Mukama niliisha kumjibu na jibu langu lilitolewa na TBC1 hivyo sidhani kama kuna sababu ya kujibu zaidi kwani Mukama hajatoa ushahidi, Polisi nao wamemtaka atoe ushahidi na hajatoa". Mtangazaji akaniambia ameelewa na tukaagana vizuri.
iii) Kwa bahati mbaya kipindi chenyewe sijakiona, lakini "Source" inayotajwa hapa ni Gazeti la Uhuru. Sasa hili naona linatia doa na kuzua maswali kadhaa ya msingi na ningelipenda maswala haya yapate majibu ili tusipoteze muda kwenye Propaganda na porojo zisizo na maana.
a) Gazeti la Uhuru lililosomwa tarehe 7/10 Asubuhi kwa vyovyote lilipaswa kuwa limeandikwa kabla ya saa 6 usiku Tarehe 6/10. Gazeti hilo lilijuaje kuwa Dr Slaa kakimbia mdahalo uliofanyika saa 1.15 asubuhi tarehe 7 Oktoba?
b) Je nani alipeleka habari kwa Gazeti la Uhuru kuwa Dr Slaa kamkimbia Mukama. Ni mtangazaji ambaye nilimweleza wazi kuwa sitashiriki kwa kuwa niko mbali na Dsm? Kama ni yeye alikuwa na lengo gani wakati anajua fika siko Dsm na tuliagana vizuri?
c) Kama ni Mtangazaji kapeleka taarifa hiyo Gazeti la Uhuru, ni kwanini kapeleka Gazeti la Uhuru tu, na siyo magazeti mengine hususan Daily News ambayo ni chombo cha serikali kama ilivyo TBC1. Kuna undugu gani kati ya TBC1 na Gazeti la Uhuru?
d) Kama siyo mtangazaji wa TBC1 ni nani na kwa lengo gani?

Ni vema WanaJF tutazame mambo kwa darubini sahihi kabla ya kupoteza muda kwenye non issues. Na hasa pale ambapo wahusika tuko kwenye Jamvi hili, hatufichi majina yetu, sina ninayemwogopa mbele ya ukweli, na wala hakuna litakalonitoa katika dhamira ya kuitetea nchi yangu na kutetea demokrasia ya kweli. Watu wanaweza kupiga propasganda na porojo kama wanavyotaka, lakini ndipo pia tunapata kigezo na kupima si tu IQ, lakini pia dhamira ya watu. Mungiu awabariki wale wote wenye nia njema.
 
Magwanda hoja yao kuu ni moja2''ufisadi''.Hoja ikiwa tofauti wanakua kama wamefilisiwa chakuongea.watz wana kero tofauti tofauti acheni kukariri!

ufisadi ndo janga linalo tafuna nchi, umeme bcuz of that, same to maji, ha2na means yoyote ya usafir iwe train kwishei, airway kwishneii... Thnk kuhusu Dowans mshtak na mshtakiwa ni ni m2 m1, anakula njama za kudhurumu kod za raia... Maandalz 2015, jimbo moja 3bn... M2 mzima anatoa lawama za makomandoo ana facts wala evidence...
 
Kamura tuliza munkari dogo ungefanya mashambulizi yako kwa staha kidoggo ingekusaidia hata wewe kuwa mwerevu. Tunu za mwanadamu ni mbili tu AKILI na HAYA. Tumia japo moja kti ya hizo vinginevyo utaendelea kudharaulika.......... Pole tena!!!!!!!!
Shangaa mkuu wangu,mtu mishipa imemsimama thread nzima yeye mwanzishaji anawajibika kujibu matokeo yake kapoteza mwelekeo na kuishia kuporomosha mitusi.
 
Kamura ndiyo wale CCM haswaaaa ninaomanisha kwenye SAHIHI yangu hapa chini.

Kamura, "........You're out of control. You're the hater and unattractive inside"

Mihasira kibao na uso wake unaona umetoka gazeti lisilouzika, gazeti baya kama uso wake.... UHURU.

images

WanaJF,
Siamini kama kwa umaskini niliouona vijijini hii thread inastahili kuwapotezea watu makini muda wao. Ninaamini watanzania tuna sababu ya kubadili fikra zetu kutoka kwenye ushabiki usio na maana kuelekea ujengaji wa hoja yenye tija kwa manufaa ya Taifa letu. Ni ushabiki huu usio na maana leo miaka 50 baada ya uhuru wazazi wetu, wajomba zetu, marafiki zetu wengi vijijini hususan Igunga ambapo nimeshuhudia kwa macho yangu baada ya kupita vijiji vyote wanaishi kwenye maisha chini ya kiwango cha binadamu. Fikiria, takriban vijiji vyote 98 hakuna maji ya uhakika, safi wala salama. Mabwawa machache yaliyoko ndiyo maji ya binadamu, ng'ombe, fisi kwa matumizi yote unayoweza kufikiria. Vijiji takriban theluthio mbili haviko karibu na zahanati na hata vyenye zahanati hakuna dawa wala wataalamu, barabara sehemu kubwa ni mapalio ya ng'ombe, madarasa ya watoto wetu ni magofu yasiyotamanika wakati rasilimali za taifa zinachezewa na watu wachache. Pamoja na yote haya badala ya sisi tulioona mwanga tunaleta pumba kwenye Jamvi hili Tukufu linalopaswa kuwa mwanzo wa fikra ya ukombozi. Inanisikitisha sana. Huhitakji kwenda shule kuelewa hali halisi ya nchi yetu kwa mtu mwenye nia njema na dhamira safi ya iukombozi. Wakati umefika wa kuacha mawazo ya kufikirika na kuwa " concrete", time is Money, tungelitumia muda tunaotumia kwenye porojo za upupu kwenye mawazo ya kujenga Taifa tunmgelisogeza Taifa letu hatua mbele.

Kuhusiana na Mada Dr Slaa kumkimbia Mukama Facts ni hizi hapa, na mwenye busara atapata mang'amuzi sahihi:-
i) Tarehe 5 Oktoba 2011, siku ya Jumatano nilipokea SMS (moja kati ya sms takriban 800 nilizopokea siku hiyo), kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama mtangazaji wa TBC1 akiniomba nishiriki kipindi cha Jambo Tanzania kingerushwa tarehe 7 Oktoba, 2011. Kwa kuwa nilikuwa safari na kutokana na uwingi wa sms sikuweza kumjibu kama ambavyo siku jibu sms nyingine nyingi pia.
ii) Taree 6 Oktoba 2011, siku ya alhamisi alinipigia simu ya mkono mtu aliyejitambulisha kuwa ndiye aliyeniletea sms jana yake kuhusiana na kipindi cha Jambo Tanzania. Tulisalimiana vizuri. Nikamjibu kuwa sitaweza kushiriki kwa kuwa niko mbali na Dar-Es-Salaam. Ndipo aliponiambia kuwa kipindi kingemshirikisha pia Bwana Mukama, Katibu Mkuu wa CCM na kuwa tungelijadili maswala ya Uchaguzi wa Igunga uliomalizika punde na Tuhuma ya Chadema kuingiza nchini magaidi kama alivyotuhumu bwana Mukama. Nikamjibu kuwa "niko mbali hivyo sitaweza kushiriki hata angelishiriki nani". Swali ni kuwa "niko mbali na Dsm". Nikaeleza " hata hivyo Mukama niliisha kumjibu na jibu langu lilitolewa na TBC1 hivyo sidhani kama kuna sababu ya kujibu zaidi kwani Mukama hajatoa ushahidi, Polisi nao wamemtaka atoe ushahidi na hajatoa". Mtangazaji akaniambia ameelewa na tukaagana vizuri.
iii) Kwa bahati mbaya kipindi chenyewe sijakiona, lakini "Source" inayotajwa hapa ni Gazeti la Uhuru. Sasa hili naona linatia doa na kuzua maswali kadhaa ya msingi na ningelipenda maswala haya yapate majibu ili tusipoteze muda kwenye Propaganda na porojo zisizo na maana.
a) Gazeti la Uhuru lililosomwa tarehe 7/10 Asubuhi kwa vyovyote lilipaswa kuwa limeandikwa kabla ya saa 6 usiku Tarehe 6/10. Gazeti hilo lilijuaje kuwa Dr Slaa kakimbia mdahalo uliofanyika saa 1.15 asubuhi tarehe 7 Oktoba?
b) Je nani alipeleka habari kwa Gazeti la Uhuru kuwa Dr Slaa kamkimbia Mukama. Ni mtangazaji ambaye nilimweleza wazi kuwa sitashiriki kwa kuwa niko mbali na Dsm? Kama ni yeye alikuwa na lengo gani wakati anajua fika siko Dsm na tuliagana vizuri?
c) Kama ni Mtangazaji kapeleka taarifa hiyo Gazeti la Uhuru, ni kwanini kapeleka Gazeti la Uhuru tu, na siyo magazeti mengine hususan Daily News ambayo ni chombo cha serikali kama ilivyo TBC1. Kuna undugu gani kati ya TBC1 na Gazeti la Uhuru?
d) Kama siyo mtangazaji wa TBC1 ni nani na kwa lengo gani?

Ni vema WanaJF tutazame mambo kwa darubini sahihi kabla ya kupoteza muda kwenye non issues. Na hasa pale ambapo wahusika tuko kwenye Jamvi hili, hatufichi majina yetu, sina ninayemwogopa mbele ya ukweli, na wala hakuna litakalonitoa katika dhamira ya kuitetea nchi yangu na kutetea demokrasia ya kweli. Watu wanaweza kupiga propasganda na porojo kama wanavyotaka, lakini ndipo pia tunapata kigezo na kupima si tu IQ, lakini pia dhamira ya watu. Mungiu awabariki wale wote wenye nia njema.

Je ulimpangia siku ambayo unaweza kuwa tayari kwa mjadala? akakataa kuweka ratiba ya mjadala siku hiyo?

Kwani wewe unaogopa gazeti la uhuru? vipi mkuu unaogopa wapinzani wako wa kisiasa?
 
Wewe unapoteza muda wako huyu mzee Slaa ni mnafiki mkubwa.
 
Back
Top Bottom