Dr Willibrod Slaa
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,523
Nsololi,Swali/maoni langu (yangu) kwako Dk. Slaa:
CCM na serikali yake hairuhusu mkulima kuuza mazao yake mahala anakotarajia kupata faida kubwa, hasa nje ya mipaka ya nchi yetu. Lakini suala la atalimaje, atavuna vipi hilo wamemwachia mkulima. Akivuna basi hapo ndio wanamuwekea masharti. Mara haruhusiwi kuuza mahindi mabichi, n.k.
Je, Chadema kama chama mbadala nini sera yenu tofauti na hii ya CCM na serikali yake. Mnakubaliana nalo, kama sivyo mbona mko kimya????
Nakushukuru sana kwa maswali mazuri kuhusu sera mbadala ya kilimo, pamoja na hali halisi ya CCM katika kilimo.
Ni kweli hampati nafasi ya kusikia Sera Mbadala ya Chadema katika Kilimo. Sera ya Chadema toka mwaka 1992, ni Soko huria na Biashara ya Soko. Mtu yeyote anayependa kufanya utafiti ataona sera hiyo ambayo haijabadilika hali leo. Kwa msingi huo nikiisha kusema Soko huria sidhani kama ninahitaji ufafanuzi wa kina.
Tatizo la msingi ni kuwa CCM ambayo hadi 1992 Sera yake ilikuwa ni kufuata siasa ya Ujamaa na kujitegemea, iliacha ghafla baada ya 1992 na kuchukua Sera ya Soko huria bila kuandaa wala mazingira wala kanuni zinazosimamia Soko na Biashara huria. Matokeo yake ni kuwa leo kuna Soko holela badala ya Soko huria. Wanaoishi Marekani, Canada na kwingineko wanafahamu kanuni nyingi zinazotawala soko huria hasa EU, smbako kwa bahati nzuri kwa miaka mitano nimekuwa mbunge wa Kuwakilisha Bunge letu kwenye Bunge la ACP-EU ( Joint Assembly pursuant to Lome Convention and later Cotenou Convention).
Ni dhahiri Sera ya Chadema haisikiki kwa kuwa kipindi kisicho cha uchaguzi Sera siyo priority ya vyombo vya habari na tunalizungumza sana kwenye Operation Sangara na mikutano mbalimbali. Sera za Chadema ziko available na zilikuwepo hadi kwenye web page yetu. Anayehitaji anaweza kutumiwa akiomba japo saa hizi tunafanya maandalizi ya kufanya riview kwa ajili ya uchaguzi.