Dr.Slaa ajibu hoja mbalimbali na kueleza Sera za CHADEMA hapa JF


Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,842
Likes
98
Points
145
Lunyungu

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,842 98 145
Ndugu wana JF,

Baada ya maongezi magumu ya kumuomba Mh. Dr.Slaa kukaa hapa na kujibu maswali ya aina yeyote ile yanayohusu Chadema na Upinzani, hatimaye amekubali rasmi kwamba atajibu kila swali litakalotolewa hapa. Yeye ameamua kuongea na Watanzania wa kada yetu kwa njia hii na ataendelea kuongea na wa kada nyingine kwa mazingira mengine yatakayofaa. Amekubali kuanza na sisi hapa.

Ameniomba niwaambie kuwa wavumilivu baada ya maswali yenu maana muda wake ni mchache na safari na kazi nyingi. Lakini amekubali kuendeleza mahojiano nasi. Ninaomba sasa kila mwenye swali lake, siku zote tumekuwa tunajiuliza na labda anakuja kuchangia na kuondoka lakini sasa atakuwa hapa kila anapoweza kujibu maswali yetu sote.

Karibuni tuweke maswali na Dr.Slaa asante in advance kwa kutukubalia kufanya hili.

UPDATED:

Majibu ya Dr. Slaa yanaanzia hapa na kuendelea
 
B

Bumbwini

Member
Joined
Dec 10, 2009
Messages
61
Likes
1
Points
0
B

Bumbwini

Member
Joined Dec 10, 2009
61 1 0
Ahsante sana kwa kumuweka Dr. Slaa aweze kujibu maswali yetu.

Swali la kwanza ni dogo tu:

Vp wao kama CHADEMA wana maoni gani au wana ushauri gani kuhusu mwelekeo wakisiasa wa sasa huko Zenj.

Je, amani na CCM yake wana nia ya kweli yakuleta maridhiano ya kisiasa na kuondoa chuki na mifarakano huko Zenj kila wakati wa uchaguzi au ni yaleyale ya unafiki na mtoto akililia mpe pipi kama ilivyozoeleka kama miaka yote.

HEBU NIPE MAJIBU DR. SLAA NAYASUBIRI KWA HAMU KUBWA
 
mayenga

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Messages
3,932
Likes
723
Points
280
mayenga

mayenga

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2009
3,932 723 280
Swali kwako Dk Slaa,

Je ni kweli kwamba ulipokuwa Padre wa kanisa katolilki na ukiwa kama katibu mkuu wa baraza la maaskofu uliondolewa kwa ufisadi wa kutafuna michango ya ziara ya Papa Yohane Paulo wa pili?
 
N

Nsololi

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2007
Messages
297
Likes
47
Points
45
N

Nsololi

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2007
297 47 45
Swali/maoni langu (yangu) kwako Dk. Slaa:

CCM na serikali yake hairuhusu mkulima kuuza mazao yake mahala anakotarajia kupata faida kubwa, hasa nje ya mipaka ya nchi yetu. Lakini suala la atalimaje, atavuna vipi hilo wamemwachia mkulima. Akivuna basi hapo ndio wanamuwekea masharti. Mara haruhusiwi kuuza mahindi mabichi, n.k.

Je, Chadema kama chama mbadala nini sera yenu tofauti na hii ya CCM na serikali yake. Mnakubaliana nalo, kama sivyo mbona mko kimya????
 
Exaud J. Makyao

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2008
Messages
1,523
Likes
13
Points
0
Exaud J. Makyao

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2008
1,523 13 0
CHADEMA IKIPEWA DHAMANA YA KUIONGOZA TZ, KUANZIA BAADA YA UCHAGUZI MKUU UJAO, imejipanga kuwafanyia nini watanzania?
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,768
Likes
2,014
Points
280
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,768 2,014 280
Nina maswali MAWILI katibu Dk Slaa.

1. Zitto anakupinga hadharani na kwenye vyombo vya habari na anasema kabisa HAKUBALIANI na wewe kwa yale uliyoyafanya juu ya SISIMIZI Kafulila. Ni msaidizi wako wa karibu.....

(a) Utafanyaje nae kazi?
(b) Kwa nini usijiuzulu?
(c) Kama ulifanya yanayostahili kwanini Zitto anaendelea na Wadhifa wake?

2. Unalizungumziaje suala la Ukabila ndani ya chama Chetu Kitukufu?
 
A

Amanikwenu

Senior Member
Joined
Dec 1, 2009
Messages
187
Likes
2
Points
0
A

Amanikwenu

Senior Member
Joined Dec 1, 2009
187 2 0
Dr Slaa,

Je utagombea Urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu?
 
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,874
Likes
314
Points
180
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,874 314 180
Swali kwako Dk Slaa,

Je ni kweli kwamba ulipokuwa Padre wa kanisa katolilki na ukiwa kama katibu mkuu wa baraza la maaskofu uliondolewa kwa ufisadi wa kutafuna michango ya ziara ya Papa Yohane Paulo wa pili?
Hili siyo swali, nafikiri hapa unaleta porojo, tuwe serious. Kama huwezi kuuliza swali acha wengine waulize maswali ya msingi chief.

Hatupo hapo kupoteza muda kama wengine mnavyofikiria....
 
Ng'wanza Madaso

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Messages
2,278
Likes
100
Points
160
Ng'wanza Madaso

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2008
2,278 100 160
Mh. Dr Slaa,

Kwanza, Kama Chadema sera za Mambo ya nje, je mna mpango gani wa kufungua matawi ya CHADEMA nje ya nchi? I mean kwa Watanzania waishio nje ya nchi hasa wanafunzi na Watanzania waishio nje?

Pili, Je kama CHADEMA mna mpango wowote wa kuwafungulia kesi mafisadi hasa ambao mna ushahidi wa kutosha?

Tatu, Je unaliongeleaje hili suala la Jeetu Patel kupewa tenda kubwa ya matrekta kwa pesa ya walipa kodi wakati ana kesi ya ufisadi mahakamani?

Nne na mwisho mbona kimya kuhusu TRL wakati mnaona ni kipi kinaendelea?
 
H

Hofstede

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2007
Messages
3,584
Likes
41
Points
0
H

Hofstede

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2007
3,584 41 0
Dr. Slaa maswali yangu:

1. Kwa kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu CHADEMA imejipanga vipi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani katika kuhakikisha mnakuwa na majority ya wabunge katika uchaguzi mkuu wa 2010?

2. Tatizo kubwa la demokrasia Tanzania ni kutokuwepo na Tume ya uchaguzi iliyo na mamlaka kamili(huru) ya kusimamia uchaguzi bila kuingiliwa na usalama wa taifa au makada wa CCM ili ku-influence outcome au kumtangaza mshindi ambaye si chaguo la wananchi practical lakini kwa ku-temper na takwimu wanamtangaza wanayemtaka wao. Je CHADEMA mpo tayari kususia uchaguzi wa 2010 mpaka Tume huru ya uchaguzi ipatikane ama kwa kuzuia uchaguzi mahakamani mpaka haki ipatikane au kwa kuanzisha maandamano ya kudai haki hiyo?

3. Je CHADEMA mmejipanga vipi kuhakikisha kuwa katiba ya nchi inabadilishwa ili iendane na matakwa ya wananchi katika demokrasia ya vyama vingi iwapo wananchi watawapatia ridhaa ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu wa 2010?

4. Je CHADEMA ina mpango wowote wa kuhakikisha mali zote za wananchi zilizochukuliwa na watawala wa sasa zinarejeshwa mikononi mwa wananchi pindi mtakapo kuwa mmechaguliwa kuiongoza nchi?. Kama ndiyo je hamuoni kuwa kwa kutangaza kurudisha mali kutafanya watawala wasiwatangaze washindi wa uchaguzi kwa kuhofia maslahi yao, Je mtakuwa na mpango wa kuwa na Tume ya Maridhiano ili tuanze upya kuijenga nchi na kusahau yaliyopita?
 
Shaycas

Shaycas

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2009
Messages
902
Likes
40
Points
45
Shaycas

Shaycas

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2009
902 40 45
Hili siyo swali, nafikiri hapa unaleta porojo, tuwe serious.
kama huwezi kuuliza swali acha wengine waulize maswali ya msingi chief.

Hatupo hapo kupoteza muda kama wengine mnavyofikiria....
MWACHE SLAA ASEME KAMA SIO SWALA AU VINGINEVYO.
Mtoa mada ameruhusu maswali yoyote,wewe unakataa.why?
Mtoa mada hakusema kama KATIBU MKUU WA CHADEMA anawajibika kujibu bali DR.SLAA wa CHADEMA.
So maswali binafsi na ya CHADEMA yanaweza kuulizwa.
SORRY
 
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
5,565
Likes
25
Points
135
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
5,565 25 135
Mkuu acha kupotosha

MWACHE SLAA ASEME KAMA SIO SWALA AU VINGINEVYO.
Mtoa mada ameruhusu maswali yoyote,wewe unakataa.why?
Mtoa mada hakusema kama KATIBU MKUU WA CHADEMA anawajibika kujibu bali DR.SLAA wa CHADEMA.
So maswali binafsi na ya CHADEMA yanaweza kuulizwa.
SORRY
Msome Lunyungu mkuu

Baada ya maongezi magumu ya kumuomba Mh.Dr.Slaa kukaa hapa na kujibu maswali ya aina yeyote ile yanayo husu Chadema na Upinzani
 
Facts1

Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Likes
5
Points
0
Facts1

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 5 0
Naomba kumuuliza Dr.Slaa swali moja:

Katika CHADEMA nimekuwa nikisikia sekta chache tu mada zake zikijibiwa na wakurugenzi wake kama sekta ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa inayoongozwa na Ndg. John Mnyika, Sekta ya Mambo ya Katiba (Tundu Lissu), Bunge na Halmashauri inayoongozwa na John Mrema.

Kuna sekta zingine muhimu kama vile Elimu, Afya, Kilimo nk wakurugenzi wao ni akina nani kama wapo mbona sisikii wakijibu hoja zao kwenye mikutano mbalimbali.

Samahani wanaJF mimi binafsi kweli siwasikii wala siwajui.
 
Tripo9

Tripo9

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2009
Messages
2,272
Likes
177
Points
160
Tripo9

Tripo9

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2009
2,272 177 160
Mimi si-intatein CCM kuendelea kutawala. Na wala si-intatein ulafi na ubinafsi aka umimi wa viongozi wa upinzani wa kutotaka kuungana na kuweza kuing'oa CCM.

Kama upinzani Kenya wameungana na kusimamisha mgombea mmoja wa uraisi na akashinda why not us? Mwishowe wagombea wetu wa upinzani wa nafasi ya urais wanaishia kugawana kura chache chache tu.

Huyo Dr Slaa na wengine wa upinzani they need to change. We people of Tanzania we need changes as well. We are tired of CCM monopoly.

Hivyo wana JF mi kwa mtazamo wangu kweli sijaona wa kum-supot ktk hivi vyama unless nione muungano wa wapinzani unafanyika.

Asanteni wakuu wote.
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Maswali kwa Slaa
1. Kulikuwa na wazo la vyama vyenu kuungana i.e. CUF na Chadema kwa faida ya wananchi wapenda mageuzi je wazo hili limeishiwa wapi? tatizo ni nini?. Inasemekana chadema walikataa ku-finance sehemu ya gharama za umoja huo vipi ukweli wa habari hizi? hamuoni kwamba wapinzani ni watu wanao hadaa watu kwa faida ya ccm. inakuwaje mnashindwa kuungana ikiwa mna malengo mema?

2. Wewe uliwahi kuwa katibu wa kanisa katoliki Tanzania, na inasemekana una matarajio ya kugombea urais. vipi uhusiano wako na kanisa lako mpaka sasa? je chama chako kinapata msaada wa maaskofu wa kikatoliki? ili kuwapa upendeleo? uhusiano wako na jamii ya kiislamu ukoje? kuna tetesi kwamba Zitto ni unwanted product huko chadema kwasababu ya dini yake na mnampango wa kumuweka lwakatare kwenye nafasi yake kwa hila ukweli uko vipi? au bado unaendeleza catholism kwenye national level?

3. Uliwahi kuasi upadre (uhusiano wako na Mungu), ukaasi CCM kwa kuwa walikataa kupitisha jina lako. hii inaweza kuwa tabia yako ya kuasi? tukikupa nchi utashindwa vipi kuwa tatizo badala ya tumaini? kama huogopi kumuasi mungu wako utashindwa kutuasi sisi?
 
S

Selungo

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2009
Messages
1,272
Likes
1
Points
0
S

Selungo

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2009
1,272 1 0
Mh. Dr. Slaa.

Kwanza nakupongeza kwa kukubali kwako kwamba kila ukipata muda utakuwa unaingia hapa na kujibu maswali yetu, licha ya muda wako kuwa finyu sana kwa sababu za kuwatumikia Watanzania.

Swali:

1. Kutokana na mahojiano kwenye kituo kimoja cha telivisheni hapa nchini, mmoja wa viongozi tuliowapa dhamana ya kiongoza CHADEMA (NAIBU KATIBU MKUU WAKO) kueleza waziwazi kwamba, yeye atakuwa tayari kusaidia watu walio nje ya CHADEMA kupigania ubunge badala ya kuhakikisha kwamba CHADEMA inapata mgombea anayekubalika na kupata ushindi. Wewe kama kiongozi na mwanachama nini maoni yako kuhusu hili?

2. Kulingana na majibu yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mahojiano katika telivisheni siku ile, Mtanzania yeyote yule ameweza kuelewa kwamba Mh. Zitto ni zaidi ya CHADEMA. Endapo tunakuwa na viongozi wa aina hii ndani ya CHADEMA nini mustakabali wa chama kwa siku za baadaye na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguza mkuu mwakani?

3. Mh. Zitto kwa kauli yake mwenyewe amesema siasa halikuwa chaguo lake la kwanza. Ki maantiki hii ni kauli ambayo wanachama wengi wa CHADEMA hawakutarajia itolewe na mtu kama Mh. Zitto. Je, chama hakioni kwamba Mh. Zitto anajenga hoja za kutaka kufukuzwa CHADEMA ili ionekane siasa za upinzani Tanzania zimeshindwa kutimiza malengo yaliyotarajiwa? Na nini kauli ya Kamati Kuu kuhusu hili?

MAONI YANGU:

HAKUNA MAHALI POPOTE DUNIANI KIONGOZI KUJIONA NI ZAIDI YA CHAMA AU TAASISI. IKISHAFIKIA HAPO AMA KIONGOZI HUYO HATA AWE MSOMI NA MAARUFU KUPITA KIASI "ATAKUWA NI MUFILISI KISIASA" NA NI VYEMA AKATOKA NA WALA ASINGOJE AIBU. HATA KAMA AMEZALIWA NDANI YA CHAMA AU TAASISI HIYO.

ALUTA NA MAPAMBANO YATAENDELEA DAIMA.
 
D

Dr Willibrod Slaa

Verified Member
Joined
Jul 1, 2008
Messages
675
Likes
107
Points
60
Age
70
D

Dr Willibrod Slaa

Verified Member
Joined Jul 1, 2008
675 107 60
Ahsante sana kwa kumuweka Dr. Slaa aweze kujibu maswali yetu.

Swali la kwanza ni dogo tu:

Vp wao kama CHADEMA wana maoni gani au wana ushauri gani kuhusu mwelekeo wakisiasa wa sasa huko Zenj.

Je, amani na CCM yake wana nia ya kweli yakuleta maridhiano ya kisiasa na kuondoa chuki na mifarakano huko Zenj kila wakati wa uchaguzi au ni yaleyale ya unafiki na mtoto akililia mpe pipi kama ilivyozoeleka kama miaka yote.

HEBU NIPE MAJIBU DR. SLAA NAYASUBIRI KWA HAMU KUBWA
Bumbwini,

Ahsante kwa swali zuri. Awali niseme kuwa sina uhakika kama ninaweza kulijibu swali hili. Kimsingi kama unavyojua hatuna details sana kuhusu maridhiano kati ya Mhe. Amani na Seif. Hata hivyo niseme tu ifuatavyo:

a) Jambo lolote linalowarudisha jamii pamoja ni jambo la kuungwa mkono na wote. Ningependa kuwapongeza wahusika kwa hatua yao nzuri na angalau kupunguza sana tension iliyokuwa inajijenga baada ya Mazungumzo ya mwafaka kuvunjika.

b) Ni imani yangu kuwa "wote wawili" wana nia njema ya kuleta amani katika jamii yetu

c) Tahadhari ni kuwa kama inavyojadiliwa sasa katika vyombo vya habari, ni imani yangu kuwa hawatajaribu wala kuthubutu kuchezea Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar ambazo zote mbili zinaweka wazi kuwa urais unaweza kugombewa tu kwa muda wa vipindi viwili, na baada ya hapo Rais anayemaliza kipindi chake hatakuwa "eligible", yaani hatakuwa na haki ya kugombea tena.

d) Nadhani ni busara kulijibu swala hili baada ya kiini na content hasa ya majadiliano kufahamika.

Nashukuru sana.
 
K

K4jolly

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Messages
366
Likes
0
Points
0
K

K4jolly

JF-Expert Member
Joined May 21, 2009
366 0 0
Mh. Tunashukuru kwa majibu kuhusu Zenj. Lakini tunaomba ukipata wasaa basi jaribu kuelezea hali ya kisiasa ya Chadema Kuhusu Zitto, haeleweki, na ndo hivyo tunajiandaa kuingia kwenye uchaguzi Mkuu. Elezea wanachama wako wa CHADEMA na Uongozi vipi kuhusu Zitto mbona anachafua hali ya hewa ya chama!!
 
NgomaNzito

NgomaNzito

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
562
Likes
6
Points
35
NgomaNzito

NgomaNzito

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2008
562 6 35
Thanks Dr Slaa

Maswali yangu mafupi mawili:

1. Bado Chadema Mnakubaliana na muundo wa tume ya uchaguzi kama hamkubaliani nao mna mpango gani wa muundo huo kabla ya uchaguzi kwani kuna chama kingine kimeenda mahakamani kuukataa muundo huo.

2.Mkiwa wabunge wachache wa upinzani mna mpango gani na muswada sheria mpya ya matumizi ya fedha kwenye uchaguzi baada ya kuonekana sheria hiyo inawabana nyie huku ikiwapendelea chama tawala pindi itakapoletwa kwenye bunge lijalo

Asante
 
D

Dr Willibrod Slaa

Verified Member
Joined
Jul 1, 2008
Messages
675
Likes
107
Points
60
Age
70
D

Dr Willibrod Slaa

Verified Member
Joined Jul 1, 2008
675 107 60
Swali kwako Dk Slaa,

Je ni kweli kwamba ulipokuwa Padre wa kanisa katolilki na ukiwa kama katibu mkuu wa baraza la maaskofu uliondolewa kwa ufisadi wa kutafuna michango ya ziara ya Papa Yohane Paulo wa pili?
Mayenga,

Asante sana kwa maswali mazuri sana. Ningependa kujibu tu kwa ufupi kama ifuatavyo:

a) Kuwa nilipokuwa Padre na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC) niliondolewa kwa Ufisadi na kutafuna michango ya Ziara ya Papa Yohane Paulo wa Pili. Ah, sijui nisemeje, anayetafuna michango na kufanya ufisadi hufikishwa kwanza mahakamani na akipatikana na hatia hufungwa gerezani kwa mujibu wa Sheria.

b) Kama hoja hii siyo ya Propaganda na kama mtoa hoja anaelewa Sheria za Kanisa Katoliki, au na wale wanaopigia debe hoja hii, basi ningelitegemea mambo kadhaa i) Wangeliweka hadharani "Hati"( Decree) ya kuondolewa kwa ufisadi. Kanisa Katoliki ina very elaborate procedure kwa mujibu wa Sheria zake, hivyo isingelimwondoa tu mtu aliyetafuna michango, na hata kumwondoa Upadre, ambao kama nilivyosema ni Sakramenti na haufutiki, isipokuwa kwa Taratibu elaborate za " Laiciztion", hati ambayo hutolewa na Papa peke yake kupitia Wizara ( Idara yake husika). Hati niliyonayo inayonirudishia hadhi ya Ulei (Laity) haitoe mahali popote process yoyote dhidi yangu, bali inajibu Maombi niliyowasilisha mwenyewe kwa mandishi yaliyosainiwa na mimi mwenyewe chini ya Kiapo, na kwa kuwa maombi yangu yalifikia viwango vinavyotakiwa nikapewa Decree husika.

c) Katika Kampeni ya 1995 ndiyo hoja kubwa iliyotumika na CCM na kwa bahati mbaya kila uchaguzi unapokuja hujaribu kufufua tena propaganda hiyo.

Hata hivyo, iwapo si propaganda, basi ningeliwategemea kwenye Jamvi hili wangeliweka angalau Indicators (viashiria) kuwa huyu bwana aliondolewa na Kanisa, aidha kwa document, au kwa kiashiria kuwa kuna chuki kati ya Dokta Slaa na Maaskofu au viongozi wa Kanisa Katoliki. Badala yake Dr. Slaa ameendelea ku enjoy uhusiano na Kanisa Katoliki katika ngazi zake zote, na hata siku wazee wa Karatu walipokuja kuniomba katika delegation kulikuwa na Mapadre wawili Fr. Reginald Barhe ( class mate wangu) na Fr. Dominick Rahhi aliyekuwa Parokia ya Karatu wakijua kuwa nikiwaona wenzangu, basi nitakubali kugombea. Nami kwa Historia yangu ndani ya CCM nikakubali na kuwaambia nitagombea kwa Tiket ya CCM kwa kuwa ndiyo chama nilichokijua hadi wakati huo. Hata ccm wenyewe katika hoja ya kuniengeua kuwa Mgombea kwa tiket ya CCM walieleza kuwa "nimesaidiwa na Kanisa Katoliki, japo hawakuweza kuonyesha uthibitisho wowote, wala sikuhojiwa kuhusu hoja hiyo) badala yake wakaamua kuniondoa kwa msingi wa "siyo mwenzetu".

Hivyo sina zaidi ya kusema hiyo ni propaganda isiyo na mshiko kwa kuwa Wananchi wa Karatu ndio walionifanyia Sherehe ya Upadre, ndio walioshiriki siku ya Upadre wangu, ndio walioniomba kugombea na kunifanya nishinde kura za maoni ndani ya CCM (kabla ya kuondolewa kwa mizengwe) na ndio walioendelea kunichagua katika chaguzi zote 3 toka 1995.

d) Kwa mtu yeyote mwenye kutaka ukweli, angelienda TEC na kuomba in confidence, Handing Over notes zangu kwa Katibu Mkuu aliyenifuata, Mhe. Methodius Kilaini, kama alikwazik na jambo lolote katika Handing over yangu kwa maana ya fedha zilizotafunwa au dosari nyingine yeyote ya kifisadi. kupenda kujenga proganda bila utafiti wa kina inaonyesha dhahiri kutokuwepo kwa dhamira safi.

Nadhani kwa ujumla maelezo haya yametoa picha kamili ambayo imeendelea kurudiwa mara kwa mara na wana CCM katika jitihada zao mbalimbali, hasa wana CCM wanaotoka nje ya Karatu, kwa kuwa Karatu hadi leo majina yangu ni Willy, Dr. na Padre kwa maana ya ukaribu wa watu wa Karatu na Dr. Slaa
 

Forum statistics

Threads 1,250,866
Members 481,514
Posts 29,748,754