Dr.Slaa ajibu hoja mbalimbali na kueleza Sera za CHADEMA hapa JF

Mh Slaa,
Pole na kazi, ningependa fahamu kwani hamuwezi fanya maendeleo yoyote yenye kulenga kuwanufaisha watanzania?kwani ni lazima muingie ikulu ndo mtufanyie hayo maendeleo mnayosema?
Mkuu, swali lako ni zuri sana. Ila ninavyofahamu ni kuwa, vyama vyote vya siasa vimeundwa kwa ajili ya kushinda uchaguzi na kuunda serikali, kama mojawapo ya madhumuni makuu.

Ngoja tusikie majibu ya Mh. Dr. W. Slaa. Inawezekana CHADEMA ina malengo tofauti.
 
Mheshimiwa Slaa;

Nina maswali yangu mafupi tuu

1. Kama tunavyofahamu viongozi wa Tume ya uchaguzi wanachaguliwa na Rais, pia wako pale kwa discretion ya Rais. Je CHADEMA hamuoni ya kuwa kutokana na muundo wa hii tume ni vigumu kwa hii tume kuwa fair kwa vyama vya upinzani?

2. Mwezi wa kumi na moja mwaka jana, viongozi wa EAC walikubalina kwa kauli moja kuruhusu free movement of people na kuondoa maswala ya working permit kwa washirika wa hii jumuia. Ningependa kujua msimamo wa Chadema katika hili swala, je mnakubalina na huu ushirika ? na kama jibu ni ndiyo, je mnahisi nini kifanyike ile mwananchi wa pale Tanadaimba aweze kunufaika na huu umoja.

Natanguliza shukrani
 
Rufiji said:

Rufiji,

..kwanza nikuombe radhi kwa kutochangia posting yako iliyohusu suala la EAC.

..pili nakushukuru kwa kuuliza swali hili.

..labda na mimi niongeze kwamba ningependa kujua msimamo wa Chadema kuhusu suala hili ukizingatia msimamo halisi wa wananchi kama ulivyojidhihirisha wakati wa mikutano ya Tume ya Professor Wangwe.

..kwa kweli ningeomba Dr.Slaa aongee kwa kirefu kuhusu nafasi, mipango, na malengo ya Watanzania ktk jumuiya ya EAC.
 
Maana yake ni kuwa vingine vimeanzishwa au kuwa facilitated na Serikali kwa lengo la kulinda Serikali. Kuna sura pana ya vyama vya aina hiyo hapa kwetu. Haiingii kwenye akili ya yote, chama cha Upinzani kuwa kwenye Pay Roll ya Chama Tawala( Tunao ushahidi). Ni dhahiri huwezi kuungana na chama cha aina hiyo. Pili, huwezi kuungana na kiongozi wa chama ambaye mchana anacheka nawe lakini usiku anakupiga kisu. Tunaomfano hai.

Kauli ya Chadema na hata Katiba ya Chadema iko wazi kuhusu uwezekano wa kuungana na chama kingine "makini". I think that is the key word siyo mataka tu ya wananchi ambao hawajui details ya mambo tunayokumbana nayo kila siku. Kuna kupenda kitu, na kuna kuangalia kama kitu hicho realisitically kinawezekana. Chadema iliisha kuonyesha njia kwa kuunga vyama vya wenzetu, mara mbili. Nadhani nia na dhamira ya Chadema cannot be challenged practically with evidence.

Mheshimiwa ukiwa kama Katibu Mkuu wa chama chako na ambapo unapaswa kuwa kiungo muhimu cha kuwezesha kufikiwa kwa matamanio ya watanzania walio wengi ambao kwao wao hawako tayari kuamini kuwa vyama vya upinzani vina nia ya dhati na umakini wa wao kuweza kuwapa imani ya kutawala hadi pale watakapoungana ama hata kushirikiana kikamilifu, huoni kuwa matamshi kama haya yamekosa uluwa na yanajenga ukuta badala ya kujenga daraja?

Mheshimiwa unaweza kuona kuwa hayo ni matakwa tu ya wananchi ambao hawajui details ya mambo tu(m)nayokumbana nayo kila siku lakini ndio ukweli wa mambo. Watanzania walio wengi wangependa kuondokana na janga la CCM lakini kamwe hawako tayari kuona wanajaribisha utawala wa nchi yao kwa "WAPINZANI" wanaoamini wameshindwa kuthibitisha kuwa wao ni mbadala makini na wa kuaminika. Na moja ya vigezo vyao vya umakini na imani hiyo ni kwa vyama hivyo vya upinzani kuungana na ikishindikana basi angalau kuwa na ushirikiano wa dhati. Chonde chonde waheshimiwa jaribuni kuepuka huu USISI na UWAO kati yenu.

Kwa heshima na taadhima

omarilyas
 
d) Kwa mtu yeyote mwenye kutaka ukweli, angelienda TEC na kuomba in confidence, Handing Over notes zangu kwa Katibu Mkuu aliyenifuata, Mhe. Methodius Kilaini, kama alikwazik na jambo lolote katika Handing over yangu kwa maana ya fedha zilizotafunwa au dosari nyingine yeyote ya kifisadi. kupenda kujenga proganda bila utafiti wa kina inaonyesha dhahiri kutokuwepo kwa dhamira safi.

Nashukuru sana Dr. Slaa kwa majibu haya naona watu waliokuwa na dukuduku la kujua hasa uhusiano wako na Kanisa Katoliki watakuwa wamepata jibu, kama ulivyosema kama kuna mtu anataka ukweli zaidi basi aende TEC vinginevyo atuambie anachotafuta, asante sana.

Vilevile umejibu vizuri suala la muungano wa upinzani ni kweli huwezi kuungana na chama chenye Pay Roll ya CCM ni uendawazimu, ni bora waendelee kusema Chadema ina umimi kuliko kuungana na vyama mamuluki, hata ndoa huwa hailazimishwi, asante kwa haya majibu.

Ila lile la Zitto naomba Chadema iende nalo taratibu wasikurupuke ingawa inaonekana Zitto hana Collective responsibility lakini kumfukuza italeta mtafaruku zaidi ni bora apunguziwe majukumu kuliko kufukuzwa, mwacheni ajiondoe mwenyewe. Hata hivyo nakumbuka ulishalitolea majibu kuwa Chadema ni System hata akiondoka Mbowe, Dr Slaa, Zitto Chadema itabaki kuwa Chadema. Tunashukuru na nakutakia mafanikio mema katika harakati zako zote.
 
Pamoja na kuchelewa naomba kumuuliza Dr Slaa iwapo CHADEMA ina utaratibu wowote wa kuhakikisha kura hazitaibiwa na CCM wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu hasa maeneo ya vijijini.
 
Mayenga,
Asante sana kwa maswali mazuri sana. Ningependa kujibu tu kwa ufupi kama ifuatavyo:
a) Kuwa nilipokuwa Padre na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC) niliondolewa kwa Ufisadi na kutafuna michango ya Ziara ya Papa Yohane Paulo wa Pili. Ah, sijui nisemeje, anayetafuna michango na kufanya ufisadi hufikishwa kwanza mahakamani na akipatikana na hatia hufungwa gerezani kwa mujibu wa Sheria.
b) Kama hoja hii siyo ya Propaganda na kama mtoa hoja anaelewa Sheria za Kanisa Katoliki, au na wale wanaopigia debe hoja hii, basi ningelitegemea mambo kadhaa i) Wangeliweka hadharani "Hati"( Decree) ya kuondolewa kwa ufisadi. Kanisa Katoliki ina very elaborate procedure kwa mujibu wa Sheria zake, hivyo isingelimwondoa tu mtu aliyetafuna michango, na hata kumwondoa Upadre, ambao kama nilivyosema ni Sakramenti na haufutiki, isipokuwa kwa Taratibu elaborate za " Laiciztion", hati ambayo hutolewa na Papa peke yake kupitia Wizara ( Idara yake husika). Hati niliyonayo inayonirudishia hadhi ya Ulei (Laity) haitoe mahali popote process yoyote dhidi yangu, bali inajibu Maombi niliyowasilisha mwenyewe kwa mandishi yaliyosainiwa na mimi mwenyewe chini ya Kiapo, na kwa kuwa maombi yangu yalifikia viwango vinavyotakiwa nikapewa Decree husika.
c) Katika Kampeni ya 1995 ndiyo hoja kubwa iliyotumika na CCM na kwa bahati mbaya kila uchaguzi unapokuja hujaribu kufufua tena propaganda hiyo. Hata hivyo, iwapo si propaganda, basi ningeliwategemea kwenye Jamvi hili wangeliweka angalau Indicators ( viashiria) kuwa huyu bwana aliondolewa na Kanisa, aidha kwa document, au kwa kiashiria kuwa kuna chuki kati ya Dokta Slaa na Maaskofu au viongozi wa Kanisa Katoliki. Badala yake Dr. Slaa ameendelea ku enjoy uhusiano na Kanisa Katoliki katika ngazi zake zote, na hata siku wazee wa Karatu walipokuja kuniomba katika delegation kulikuwa na Mapadre wawili Fr. Reginald Barhe ( class mate wangu) na Fr. Dominick Rahhi aliyekuwa Parokia ya Karatu wakijua kuwa nikiwaona wenzangu,basi nitakubali kugombea. Nami kwa Historia yangu ndani ya ccm nikakubali na kuwaambia nitagombea kwa Tiket ya CCM kwa kuwa ndiyo chama nilichokijua hadi wakati huo. Hata ccm wenyewe katika hoja ya kuniengeua kuwa Mgombea kwa tiket ya ccm walieleza kuwa "nimesaidiwa na Kanisa Katoliki, japo hawakuweza kuonyesha uthibitisho wowote, wala sikuhojiwa kuhusu hoja hiyo) badala yake wakaamua kuniondoa kwa msingi wa "siyo mwenzetu". Hivyo sina zaidi ya kusema hiyo ni propaganda isiyo na mshiko kwa kuwa Wananchi wa Karatu ndio walionifanyia Sherehe ya Upadre, ndio walioshiriki siku ya Upadre wangu, ndio walioniomba kugombea na kunifanya nishinde kura za maoni ndani ya ccm( kabla ya kuondolewa kwa mizengwe) na ndio walioendelea kunichagua katika chaguzi zote 3 toka 1995.
d) Kwa mtu yeyote mwenye kutaka ukweli, angelienda TEC na kuomba in confidence, Handing Over notes zangu kwa Katibu Mkuu aliyenifuata, Mhe. Methodius Kilaini, kama alikwazik na jambo lolote katika Handing over yangu kwa maana ya fedha zilizotafunwa au dosari nyingine yeyote ya kifisadi. kupenda kujenga proganda bila utafiti wa kina inaonyesha dhahiri kutokuwepo kwa dhamira safi.

Nadhani kwa ujumla maelezo haya yametoa picha kamili ambayo imeendelea kurudiwa mara kwa mara na wana ccm katika jitihada zao mbalimbali, hasa wana ccm wanaotoka nje ya Karatu, kwa kuwa Karatu hadi leo majina yangu ni Willy, Dr. na Padre kwa maana ya ukaribu wa watu wa Karatu na Dr. Slaa

Asante sana Mh. Dr. Slaa kwa majibu mazuri. Tafadhali msituangushe ktk uchaguzi ujao tunataka wagombea makini hasa Kanda ya ziwa.
 
Ningependa turudi kwenye maswali na majibu na Mhe. Dr. W. Slaa. Tafadhali tusiharibu jamvi hili kwa kurushiana maneno. Hayasaidii, hayajengi na wala yanaonyeshi kuwa tuko serious na issues muhimu.

Mhe. Dr. Slaa amejitolea/amekubali kuja na kuzungumza na wanaJF. Hiyo ni jambo jema na bora sana. Hata kama unafikiria kuwa majibu yake si kama ulivyotegemea, nadhani ni busara kuuliza kwa mapana zaidi ili kuhakikisha anajibu kama unavyotarajia. Siamini kuwa hana majibu ya maswali yetu.

Mhe. Dr. Slaa, ningependa kukuuliza maswali machache.

1. Je Chadema inaonaje maandalizi yake kwa uchaguzi Mkuu ujao?

2. Je, Chadema inachukuliaje malumbano yanayoendelea kati ya viongozi wa CCM hasa kuelekea uchaguzi mkuu? Inaona malumbano hayo kutoa nafasi yoyote ya ushindi wa kishindo? Inategemea kuna baadhi ya wanasiasa wazuri kujiunga na chama chenu?

3. Mna mikakati gani ya kuhakikisha uratibishaji mzuri zaidi wa wagombea wa nafasi mbalimbali na kuhakikisha yaliyotokea Kyela hayajirudii tena katika uchaguzi mkuu ujao?

4. Je, mmechukua hatua gani kama chama na hasa wewe kama Mbunge kuhakikisha nchi inapata Katiba ya maana zaidi, yenye kuendana na maisha ya sasa ya waTanzania na yenye kulinda maslahi ya wadau wote wa siasa nchini?

Ni hayo tu, nitashukuru kama utapata nafasi ya kuyajibu.
 
Nsololi,
Nakushukuru sana kwa maswali mazuri kuhusu sera mbadala ya kilimo, pamoja na hali halisi ya ccm katika kilimo.
a) Ni kweli hampati nafasi ya kusikia Sera Mbadala ya Chadema katika Kilimo. Sera ya Chadema toka mwaka 1992, ni Soko huria na Biashara ya Soko. Mtu yeyote anayependa kufanya utafiti ataona sera hiyo ambayo haijabadilika hali leo. Kwa msing huo nikiisha kusema Soko huria sidhani kama ninahitaji ufafanuzi wa kina. Tatizo la msingi ni kuwa CCM ambayo hadi 1992 Sera yake ilikuwa ni kufuata siasa ya Ujamaa na kujitegemea, iliacha ghafla baada ya 1992 na kuchukua Sera ya Soko huria bila kuandaa wala mazingira wala kanuni zinazosimamia Soko na Biashara huria. Matokeo yake ni kuwa leo kuna Soko holela badala ya Soko huria. Wanaoishi Marekani, Canada na kwingineko wanafahamu kanuni nyingi zinazotawala soko huria hasa EU, smbako kwa bahati nzuri kwa miaka mitano nimekuwa mbunge wa Kuwakilisha Bunge letu kwenye Bunge la ACP-EU ( Joint Assembly pursuant to Lome Convention and later Cotenou Convention). Ni dhahiri Sera ya Chadema haisikiki kwa kuwa kipindi kisicho cha uchaguzi Sera siyo priority ya vyombo vya habari na tunalizungumza sana kwenye Operation Sangara na mikutano mbalimbali. Sera za Chadema ziko available na zilikuwepo hadi kwenye web page yetu. anayehitaji anaweza kutumiwa akiomba japo saa hizi tunafanya maandalizi ya kufanya riview kwa ajili ya uchaguzi.

Dr. napenda kuendeleza kidogo mjadala wa sera ya CHADEMA katika Kilimo. Nashukuru kujua kua umekuwa ukiwakilisha Bunge letu kwenye Bunge la ACP-EU na hapo ndipo ninataka kujua kwanini unaendelea kuiunga mkono policy hii ya soko huria hasa kwenye kilimo huku ukijua kwa dhati kabisa historia ya General Agreement on Tarrif and Trade (GATT) mpaka kuanzishawa kwa WTO ambayo hasa inakazia kuhusu soko huria. Kwamba tangu muda huo hadi leo imekua ngumu kwa EU kukubali sera za soko huria katika maswala ya kilimo na ndiyo maana katika majadiliano ya soko huria Agriculture ilikuwa haiguswi mpaka recently na bado wamekataa kuondoa baadhi ya vikwazo kama subsidies hata baada ya makubaliano ya Doha kuvunjika.

Sasa Maswali:
  • Je ni sababu zipi ziliifanya EU kuwa wagumu kiasi hicho ambazo sisi hazituhusu mpaka uendelee kuipigia debe sera hii ya soko huria huku ukijua kabisa umuhimu wa serikali kumlinda mkulima?
  • Je ni nini maoni ya CHADEMA kuhusu kilimo kwanza na vipi ingefanya tofauti na hii kauli mbiu ya CCM ya "kilimo kwanza" ambayo kwa maoni yangu inalenga kuwanufaisha elites wanaojua kinachoendelea katika WTO hasa kwa habari ya kilimo?
 
Dr. Slaa

tunashukuru kwa ufafanuzi wako makini.

SWALI: Katika ufuatiliaji wako wa lile sakata la CCM kuingiza magari na kukwepa kiasi kikubwa cha kodi, je walikwepa kiasi gani? na je, wamelipa kiasi walichokwepa?
Wana JF,
Kwanza naomba niwasalimie wote na kuwashukuruni sana kwa dhati kwa maswali mengi ambayo yameendela kuja pamoja na kuwa majibu yamechukua muda mrefu. Kutoa tarehe 12 Januari, nimekuwa na Kamati ndogo ya Kamati ya LAAC ambaye ilifanya ukaguzi wa mahesabu ya Halmashauri za Wilaya ya Bagamoyo (Pwani), Halmashauri ya Korogwe Vijijini (Tanga), Muheza (Tanga), Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro. Ukaguzi huo umeendana na kukagua miradi mbalimbali (site inspection-Value for Money Audit. Hivyo mnavyoona ilikuwa vigumu sana kuingia kwenye mtandao kwa kipindi chote hicho.
Kutokana na uwingi wa maswali, nitajaribu kuyaweka yale yote yanayofanana katika kundi mmoja, na mengine nitayajibu kwa mtiririko jinsi yalivyokuja. Iwapo kwa mtindo huu mtu hataridhika, bado anaweza kuomba afafanuliwe kwa kina zaidi, pale na nitafanya hivyo pale inapowezekana.
Pili, hakuna haja ya kutukanana ndugu zangu. Tulikubaliana kuwa na mtandao ambao wote tunaheshimiana, tunaelimishina pale ambapo mtu haelewi, na hata yule mwenye ajenda yake hakuna haja ya kumtukana. Uvumilivu ni jambo kubwa sana katika mtandao kama huu unaojumuisha watu wa itikadi mbalimbali, imani mbalimbali, falsafa zinazotofautiana na pengine hata tamaduni zinazotofautiana. Iwapo mtu anaona ametukanwa badala ya ku react, ni vema aka "Ignore"( puuza) hakuna kinachouma kama kumpuuza mtu kama ni mwelewa.

i) Wachangiaji kadhaa, akiwemo Mzitto Kabwella, Omarilyas, na wengine wamependa nitoe ufafanuzi zaidi kuhusu
a) Swala la Zitto kumpinga Katibu Mkuu wake hadharani. Niseme tu, kuwa swala hili nilikwisha kulitolea ufafanuzi, sidhani kama lina haja ya kuliendeleza zaidi. Zitto kwa sasa hivi yuko Ujerumani akimalizia masomo yake. Mara kadhaa amekuwa akifika Dar na kila mara amkuwa akiwasiliana nami, na kunipa picha ya majadiliano yanayoendelea kwenye vyombo vya Habari. Nadhani itoshe kusema tu kuwa sioni umuhimu wa kuendeleza swala hili kwani kinachoonekana migogoro wakati mwingine imepandikizwa kwa malengo, wakati mwingine inaweza kuwa na dalili za ndani lakini nilikwisha kulitolea maelekezo na ngazi za chama nazo zilikwisha kulitolea maamuzi. Nadhani muhmu zaidi ni kujenga utamaduni wa kuvumiliana pale ambapo kauli zinaweza kutofautiana, na hazina madhara kwa chama, mathalan chama kinachoamini katika misingi sahihi ya demokrasia ya kweli. Kama nilivyosema, Tafsiri ndani ya chama isitafsiriwe kwa mtu mmoja au wawili, bali kama ni vikundi ni lazima kuwe na utafiti wa kina kujua vikundi hivyo vinaathiri chama kiasi gani, viko vingi au vina wafuasi wengi kiasi gani, na kama vikundi hivyo havikutengenezwa mezani kama ilivyotokea wakati wa Kafulila ambapo ilitengenezwa mezani kuwa kuna wenye viti 11 wa Mkoa wanamwunga mkono Kafulila. Ukiwauliza wawataje, na hata Gazeti liliwachapisha linaposhindwa kuwathibitisha basi ni dhahiri kuna msingi wa umbeya, majungu na uchochozi wenye ajenda iliyojificha.
b) Mgogoro katika chama cha siasa unapimwa kwa vigezo muhimu kama vile je, vyombo vya maamuzi, Kamati Kuu, Baraza Kuu, Mkutano Mkuu vimegawanyika kwa kiwango gani. Iwapo vyombo vya maamuzi viko united, mtu mmoja mmoja anayetofautiana na kauli ya wengi ni dhahiri hawezi kuwa tishio na akishikilia msimamo wake hawezi dhahiri pia kuwa mwana demokrasia. Vigezo hivyo hivyo, ningelipenda tuvitumie pia kuipima CCM, hasa kwa wale wanaopenda nitoe kauli yangu kuhusu vikundi na mgogoro ndani ya CCM. Vigezo vyovyote vya kisayansi ni lazima kwanza vita "Establish" criteria/parameters zinazoweza kuwa proved "empirically". Vinginevyo inaweza kubaki kuwa propaganda. Hii haina maana ya kusema kuwa tahadhari na hatua ya kuziba ufa zisichukuliwe mapema. Lakini uchukuaji wa hatua hizi ni pamoja na kupima faida na hasara ya hatua hizo.
c) Swala la Zitto kumsaidia Kafulila nalo nilikwisha kulifunga. Iwapo Vyombo vya maamuzi vitaona kuwa hatua hiyo inavunja Katiba, Kanuni na Maadili ya Chadema, hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa Katiba na Taratibu za ndani ya Chadema. Huu ndio utaratibu sio kwa Zitto tu lakini kwa viongozi wote wa ngazi ya Kurugenzi ambao mamlaka yao ya Nidhamu ni vyombo vya Juu yaani Kamati Kuu/Baraza Kuu au Mkutano Mkuu kadiri itakavyokuwa.
d)Swala la Kufulila kuitwa "Sisimizi" kama alivyouliza Magezi nadhani, tukubali kuwa kuna lugha ya kuongea na lugha ya kuandika, na hasa inapotumika "analogy". Neno Sisimizi katika analogy hii ilionyesha level ya Kafulila inaishia wapi, kwa vile kama ilivyoripoti yeye mwenyewe na baadhi ya vyombo vya habari vikataka kujenga dhana kuwa mamlaka yake ya nidhamu ni au Kamati Kuu au hata juu ya hapo. Nashukuru kuwa neno sisimizi lilieleweka haraka na watanzania na wale wote wanaojua ngazi za mamlaka. Kauli zinapaswa kuchukuliwa ndani ya "context" iliyotumika kupata maana halisi ya kinachomaanishwa na msemaji.
e) Mzitto pia ameliongelea swala la ukabila ndani ya Chadema. Sina uhakika Mzitto ana background gani, na kwa bahati mbaya hatumii jina lake halisi. Sidhani kama kuna mwandishi yeyote makini, au mwanasiasa ambaye kweli ni mwanasiasa anaamini kuna ukabila ndani ya Chadema, hasa kwa maana inayojengwa sana, ya Uchagga. Nimelitolea ufafanuzi mara kadhaa swala hili, Tumetoa mpaka majina ya viongozi wakuu wa Chadema, Wakurugenzi wa Idara za Makao Makuu na Kamati Kuu. Tumeonyesha kabila la kila mhusika, mahali anapotoka. Wale wote wenye nia njema wameelewa, lakini ambao kwa makusudi "hawataki kuelewa" kwa sababu zao za kisiasa ni kipropaganda hatuna namna ya kuwasaidia. La muhimu umma mkubwa wa Tanzania umeisha kuelewa chadema hakina ukabila, wala udini. Kwa mara nyingine, ninatoa challenge, kwa yeyote wenye ushahidi wa ukabila Chadema auweke hadharani kwenye mtandao huu, ndiyo namna pekee ya kuondoa majungu na umbeya. Vinginevyo hatuwezi kuimba wimbo huo huo kila siku, hasa tunapojua ni uwongo wa wazi.
Ni imani yangu nimeweka wazi bila kuficha jambo lolote. Mtu asipotaka kuamini sasa hapo ni hiari yake, kwani waswahili husema, punda unaweza kumpeleka mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.Nawashukuru sana
 
Dr. Slaa

tunashukuru kwa ufafanuzi wako makini.

SWALI: Katika ufuatiliaji wako wa lile sakata la CCM kuingiza magari na kukwepa kiasi kikubwa cha kodi, je walikwepa kiasi gani? na je, wamelipa kiasi walichokwepa?
Mfwatiliaji,
i) Kama nilivyosema, kiasi kilichokwepwa ni zaidi 6 Billion. Wameanza kulipa sijapata taarifa ya mwisho kama wamemaliza kulipa zote.
2) Jambo baya zaidi, wakati ninazungumzia taarifa ya ccm kuagiza magari 200 hatukujua kuwa wanaleta Bungeni mswada wa sheria ambao unapiga marufuki uagizaji wa Magari, nyenzo, vifaa vya uenezi( bendera, kadi) na au uingizaji wa Helcopter. Sasa ndio tumejua kwanini waliagiza mapema hivyo, na kuna taratibu nyingine tunafuatilia ambazo nazo zimefanywa kwa hila hivyo hivyo. Tatizo ni kuwa wenzetu wanapewa Taarifa muhimu na Serikali, na hivyo kufanya uwanja wa Siasa usiwe Level play ground, kama tulivyodai siku zote.
3) Tunafuatilia hata fedha zilizotumika, watu waliotumika kuagiza magari hayo wako safi kiasi gani au ni EPA nyingine. Ndiyo maana niliposema waende mahakamani, tulitegemea kuna taarifa nyingi tutaziweka hadharani mahakamani lakini walifuta wenyewe kauli yao waliyoitoa kwa hiari yao kuwa watanipeleka mahakamani. viashiria hivi si vya kupuuza hata kidogo katika kulinda mali na rasilimali za Taifa. Taarifa tulizonazo japo tunaendelea na utafiti unaashiria ufisadi mkubwa unaendelea bado.
4) Kama nilivyosema, Kodi na ushuru tunaofuatilia sio wa Magari mia mbili tu, tumepata nyaraka nyingi zinazoashiria, hata Mahindra za 2005 na vifaa vingine vilivyotumika katika kampeni za uchaguzi wa 2005 nazo hazikuwa zimelipiwa ushuru na Kodi. Ndiyo maana tumepiga kelele kuhusu mchakato wa ukwepaji uliokuwa unaendelea katika uagizaji wa Magari 200. Ni dhahiri kama tusingelitoka hadharani, wala wasingeliweka hadharani na wangelipata mwanya kama ilivyo desturi zao( na ninaposema hivi ni kwa vile nimekwisha kutoa katika michango yangu mingine aina ya hujuma zilizofanyika mathalan katka uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2009.
 
Ni imani yangu nimeweka wazi bila kuficha jambo lolote. Mtu asipotaka kuamini sasa hapo ni hiari yake, kwani waswahili husema, punda unaweza kumpeleka mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.Nawashukuru sana

Asante kwa ufafanuzi Dr Slaa. I hope hili la 'punda' halitatolewa kwenye context yake kama ilivyokuwa kwa 'sisimizi'!.
 
Dr. Slaa hasante kwa kujibu baadhi ya maswali uliyo weza Ila utaratibu uliotumiwa umekuwa mbovu sana kiasi cha kuwa destracted na watu wanaoquote majibu yako na kukutoa kwenye maswali ya msingi yaliyoulizwa awali. Mfano maswali yangu hukujibu kabisa.

Ushauri kwa wakati mwingine. Watu wakiandika maswali yao yatafutie majibu yote kwanza na pembeni kwenye Word then anza ku-copy na kupaste kabla ya kuanza kujibu ya wale wanaochallenge majibu yako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umewatendea haki wale waliokuuliza in-advance badala ya kujibu wanaotaka ufafanuzi wa majibu yako.

Baada ya hapo ndiyo sasa ungeingia kwenye mjadala kwa kujibu hoja za majibu yako.
 
e) Mzitto pia ameliongelea swala la ukabila ndani ya Chadema. Sina uhakika Mzitto ana background gani, na kwa bahati mbaya hatumii jina lake halisi. Sidhani kama kuna mwandishi yeyote makini, au mwanasiasa ambaye kweli ni mwanasiasa anaamini kuna ukabila ndani ya Chadema, hasa kwa maana inayojengwa sana, ya Uchagga. Nimelitolea ufafanuzi mara kadhaa swala hili, Tumetoa mpaka majina ya viongozi wakuu wa Chadema, Wakurugenzi wa Idara za Makao Makuu na Kamati Kuu. Tumeonyesha kabila la kila mhusika, mahali anapotoka. Wale wote wenye nia njema wameelewa, lakini ambao kwa makusudi "hawataki kuelewa" kwa sababu zao za kisiasa ni kipropaganda hatuna namna ya kuwasaidia. La muhimu umma mkubwa wa Tanzania umeisha kuelewa chadema hakina ukabila, wala udini. Kwa mara nyingine, ninatoa challenge, kwa yeyote wenye ushahidi wa ukabila Chadema auweke hadharani kwenye mtandao huu, ndiyo namna pekee ya kuondoa majungu na umbeya. Vinginevyo hatuwezi kuimba wimbo huo huo kila siku, hasa tunapojua ni uwongo wa wazi.
Ni imani yangu nimeweka wazi bila kuficha jambo lolote. Mtu asipotaka kuamini sasa hapo ni hiari yake, kwani waswahili husema, punda unaweza kumpeleka mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.Nawashukuru sana

Dr. Slaa nadhani kwenye hili mnafanya makosa technically. Tukumbuke kwamba watanzania ni taifa la kipekee ambalo watu walio wengi source ya information ni vijiweeni na majungu majungu mitaani.

Case no.1
Rejea pre-elections za 2005. Prof Mwandosya akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi alituhumiwa na gazeti la rai kuhusu mtoto wake kufadhiliwa na kampuni ya MSI Detecon, mwekezaji wa TTCL wakati ule. Kwenda South Africa na kufanya field na kampuni hiyo fully paid. Prof emerged only once kuelezea facts in a learned manner and when the wind kept on blowing alikuwa akijibu lightly and simply kama mnavyofanya nyie hivi sasa. HILO NILIKWISHAELEZEA. In the end wananchi wakaaminishwa kwamba the rumors were true. Proof? Why is ths guy don't want to discuss the issue?

Case no 2.
Tukirejelea tena kwenye mchakato wa uchaguzi CCM 2005, Dr. Salim alituhumiwa kwamba alikuwa memba wa Hizbu. Since he knew that was a lie and a useless rumor aliamua kukaa kimya. The rumor kept on going and what happened,wananchi wakaaminishwa kwamba the rumors were true. Proof? Why is ths guy don't want to discuss the issue?

Case no 3.
In the same 2005 pre-elections michakato the current president, H.E J. Kikwete alituhumiwa kwamba ana Ukimwi na magonjwa mengine kadha wa kadha. What happenned tulionyeshwa kwenye vyomba vya habari ITV, TVT, magazeti kwamba the candidate was physicaly fit! Of which in fact ingekuwa nchi zilizoendelea hii ilitosha kumuangusha muheshimiwa. And ever since afya ya mkulu imewekwa hadharani more than 2 times. What happens. Wananchi walio wengi they don't doubt kuhusu afya ya muheshimiwa.

Case no 4.
In those pre-2005 elections CUF ilituhumiwa kwamba ni chama cha kidini na wao pia wakafanya the same mistake wakijua tuhuma hizo si kweli wakapuuza. What happened?

Case no 5.
In 2005 nyie Chadema mlituhumiwa hili suala la ukabila. Lakini kwa sababu mlijua sio kweli hamkuweka the necessary efforts kucountereffect hiyo rumor. What happened wananchi wengi hasa kanda ya ziwa (I was there by that time) waliaminishwa ujinga huo and is probably why Chadema ilipata kura chache kuliko ilvyotegemewa.

So in my opinion Chadema should not take this matter lightly. Hii hoja mnahitajika kuwa na majibu nayo anytime regardless as to how many times itaulizwa. Jingine hebu fanyeni just a research say in 3 regions kuhusiana na hii tuhuma. You will be surprised!!!!!!!!!! As we are just some 9 to 10 months b4 elections jaribuni kuweka sawa hii ishu. It is few of us who understand it is rubbish lakini the majority aidha wanaamini au wanakuwa na mashaka.

Hii ni Tanzania na ni zaidi ya tuijuavyo!!!!
 
Dr slaa

Karibu Jamiiforums and we call it the home of great thinkers

Napenda niweke maswali kadhaa hapa ili ukipata muda wa kuyasoma basi niweze kupata majibu muafaka,

1 ) Najua CHADEMA kinakua kwa kasi na viongozi wanajitahidi kueneza chama vizuri.Sasa naona mmejikita sana kama chama kushuhulikia mambo ya kisiasa tu,je huoni kama chadema ikianzisha miradi ya maendeleo maemeo fulani fulani kwa kutumia ushawishi wa kisiasa kuwavuta wananchi watumie nguvu zao kutaitofaitisha CHADEMA na vyama vingine?

2) Chama kilianza mkakati wa kuchangisha wananchi mkakati wa kuchangisha fedha ili kukisaidia chama katika chaguzi zijazo,je mkakati huo umepata mwitikio? Has there any internal checks put in place to insure correctness in revenue and expenditure of the said project?

3) Ni kwa nini tunachangisha fedha wananchi kwa ajili ya kampeni na kwa nini sio kwa ajili ya kuanzisha SACCOS maeneo mbalimbali kama jawabu kwa wananchi kukua kiuchumi?

4) Chadema ina mpango wa kusimamisha mgombea ubunge kigoma kusini?

Ni hayo tu kwa leo

Dr Slaa, pole sana na kazi na hongera kwa kukubali kutoa maelezo kwenye maswali mbalimbali.

Dr. Slaa ukiwa kama mtendaji mkuu wa chama, ni wazi sote tuna jua kuna ethics za uongozi hasa kwenye mambo nyeti na majadiliano ya vikao mbalimbali ndani ya chama chochote kile. Kukubaliana au kutokubaliana kunaweza kutokea ila haya yote yanakuwa kwa ajili ya kulinda katiba, taratibu na mwongozo wa chama husika.

Swali. Kumekuwa na msuguano mkubwa sana kati ya uongozi wa chadema na Zitto Kabwe naibu katibu wa chadema. Je humuoni huu msuguano unakiiangamiza chama?

Vile vile si kweli kwamba kuna watu wanautengeza huu msuguano, bali ni Zitto mwenyewe anayetoa kauli tata kila kukicha na kusababisha chama kionekane kwamba hakina watu makini wa kukanya hii tabia au kumwajibisha kwa kukiuka ethics za kazi yake.

Zitto amekuwa akikatisha watu tamaa kiasi kwamba haaminiki tena?
Je kiongozi anapokuwa hayuko tena na msimamo wa chama anachokiongoza huyo ni kiongozi wa chama hicho tena, Kwanini chama kisichukue maamuzi mazito?
 
Ningependa turudi kwenye maswali na majibu na Mhe. Dr. W. Slaa. Tafadhali tusiharibu jamvi hili kwa kurushiana maneno. Hayasaidii, hayajengi na wala yanaonyeshi kuwa tuko serious na issues muhimu.

Mhe. Dr. Slaa amejitolea/amekubali kuja na kuzungumza na wanaJF. Hiyo ni jambo jema na bora sana. Hata kama unafikiria kuwa majibu yake si kama ulivyotegemea, nadhani ni busara kuuliza kwa mapana zaidi ili kuhakikisha anajibu kama unavyotarajia. Siamini kuwa hana majibu ya maswali yetu.

Mhe. Dr. Slaa, ningependa kukuuliza maswali machache.

1. Je Chadema inaonaje maandalizi yake kwa uchaguzi Mkuu ujao?

2. Je, Chadema inachukuliaje malumbano yanayoendelea kati ya viongozi wa CCM hasa kuelekea uchaguzi mkuu? Inaona malumbano hayo kutoa nafasi yoyote ya ushindi wa kishindo? Inategemea kuna baadhi ya wanasiasa wazuri kujiunga na chama chenu?

3. Mna mikakati gani ya kuhakikisha uratibishaji mzuri zaidi wa wagombea wa nafasi mbalimbali na kuhakikisha yaliyotokea Kyela hayajirudii tena katika uchaguzi mkuu ujao?

4. Je, mmechukua hatua gani kama chama na hasa wewe kama Mbunge kuhakikisha nchi inapata Katiba ya maana zaidi, yenye kuendana na maisha ya sasa ya waTanzania na yenye kulinda maslahi ya wadau wote wa siasa nchini?

Ni hayo tu, nitashukuru kama utapata nafasi ya kuyajibu.
Recta,
Nashukuru sana kwa maswali yako mazuri.
i) Maandalizi kwa Uchaguzi Mkuu: Kwanza ni kiri kuwa swala la maandalizi ni la kimkakati zaidi. Hivyo kwa sababu zinazoeleweka sitapenda kuingia kwa undani. Naomba radhi kwa kutokupa details hapa hadharani. Hata hivyo,
a) Maandalizi ya Chadema yako dhahiri. Yalianza na marekebisho makubwa ya Katiba ya Chadema yaliyozaa Toleo la 2006. Marekebisho hayo yalipeleka Chama hadi ngazi ya Msingi (inafanana na Shina la CCM). Tunaenda kubanana huko huko, kwa vile ccm inatumia sana mabolozi wake, na safari hii Chadema pia itakuwa na mabolozi wake ndio viongozi katika ngazi ya Shina. Pamoja na Shina Mtandao wa chadema kuanzia Shina, Tawi ,Kata hadi Wilaya umeimarishwa na unaendelea kuimarishwa kupitia Operation Sangara na Taratibu zingine za kiuendeshaji za ndani ya Chama. Hii ni hatua muhimu sana katika maandalizi ya uchaguzi kuwa na mtandao wa Chama. Hii itaimarisha sana shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa shughuli za uchaguzi. Wenzetu bado wanaweza kutugandamiza kwa kutumia mfumo mzima wa Serikali kuanzia Mkuu wa Mkoa , Wilaya, Tarafa, Kata (WEO) na VEO. Ndiyo maana kila mara tunapiga kelele kuwa katika mfumo wa demokrasia ya kweli Serikali ni lazima itenganishe mfumo wa Serikali na chama ili kuwa na level play ground. Dhana hii imekuwa ngumu sana kwa wenzetu, na mara nyingi siyo tu inatumika kupata kura lakini huvuka mipaka na kuinga kwenye unyanyasa na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu, kama inavyothibitishwa hivi sasa wilaya ya Nkasi ambapo viongozi wa Chadema walioshinda katika ngazi ya Serikali za Mitaa wamekamatwa mara tu baada ya kushinda na kufunguliwa kesi za jinai za kubambikiza. Ni bahati mbaya hakuna anayefanya utatifi kuhusu kiwango cha unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za kibinadamu vijijini. Hali inatisha sana. Hata hivyo, hatua ya kuwa na uongozi wa Chadema katika ngazi ya chini kabisa umeanza kuonyesha matunda kwani hata haya manyanyaso yalikuwa hayawezi kubainika bila uongozi thabiti.
b) Katiba ya Chadema imeanzisha Mabaraza muhimu sana 3 yaani Baraza la Wanawake, Baraza la Vijana, na Baraza la Wazee kutoka ngazi ya chini kabisa hadi Taifa ( Baraza la Vijana halijafanya uchaguzi ngazi ya Taifa baada ya dalili za rushwa kujitokeza na vurugu). Maandalizi ya Uchaguzi huo sasa yako mbioni. Mabaraza haya ndiyo nguzo muhimu katika kuimarisha Chama, na bila shaka in put ya mabaraza si swala la kujadili. Hata kimahesabu, hizi ni kura za uhakika, na idadi ya watu hawa si ya kudharauliwa kwa maana ya kura, ukiwajumlisha na ngazi zote za uongozi za chama. Huu ni mkakati muhimu na endelevu wa chama kujiimarisha, kwani chama hakiwezi kujiimarisha tu jukwaani.
c) Kazi inayofanywa na Operation Sangara ni kazi muhimu sana katika kujenga, kufufua, kuimarisha matawi ya Chama katika ngazi zote, tangu Msingi. Chama ni Wananchama na wanachama hupatikana kupitia matawi yao mbalimbali. Aliyeshiriki au aliyefuatilia Operation Sangara, ambayo imefika hadi kijijini kwa Makamba na maelfu ya vijiji kwa njia ya Helcopter au magari ni hatua muhimu na kubwa sana. Kazi hii bado inaendelea na itaendelea hadi "Kieleweke".
d) Kazi ya Kuelimisha na kuwahamasisha Watanzania katika ujumla wao, na hata kazi tunayofanya sasa ya kutoa elimu kwa njia ya Mtandao ni mbinu ya kuwafikia watu wengi kadiri iwezekanavyo wa kada mbalimbali, kuwaeleza kuhusu Chadema, Sera zake, inasimamia mambo gani, na kadha wa kadha, na hata kujenga tu urafiki na watu wa kada mbalimbali ni mbinu ya kujiimarisha kwa chama.
Kwa ujumla mbinu na mikakati ni mingi nipende tu kuyaonyesha hayo ya msingi, na yale ya kimkakati yataonekana zaidi wakati tutakapoweka hadharani Ilani ( Election Manifesto/Platform) yetu kwa wakati mwafaka. Wakati huo tukikamilisha kazi ya ku update, sera zetu, kila mmoja atapata nafasi wazi kujua Sera za Chadema ni nini, nini Itikadi na Falsafa (Ukiacha broad guideliness zilizoko kwenye Katiba na nyaraka mbalimbali ambazo hata sasa zinapatikana kwa kila mwenye kuzihitaji kwenye Website ya Chadema.
Ni imani yangu Recta ufafanuzi huu unakidhi haja, iwapo utahitaji ufafanuzi unaweza kuuomba tu, na nitajitahidi kujibu bila hiyana.
 
Dr. napenda kuendeleza kidogo mjadala wa sera ya CHADEMA katika Kilimo. Nashukuru kujua kua umekuwa ukiwakilisha Bunge letu kwenye Bunge la ACP-EU na hapo ndipo ninataka kujua kwanini unaendelea kuiunga mkono policy hii ya soko huria hasa kwenye kilimo huku ukijua kwa dhati kabisa historia ya General Agreement on Tarrif and Trade (GATT) mpaka kuanzishawa kwa WTO ambayo hasa inakazia kuhusu soko huria. Kwamba tangu muda huo hadi leo imekua ngumu kwa EU kukubali sera za soko huria katika maswala ya kilimo na ndiyo maana katika majadiliano ya soko huria Agriculture ilikuwa haiguswi mpaka recently na bado wamekataa kuondoa baadhi ya vikwazo kama subsidies hata baada ya makubaliano ya Doha kuvunjika.

Sasa Maswali:
  • Je ni sababu zipi ziliifanya EU kuwa wagumu kiasi hicho ambazo sisi hazituhusu mpaka uendelee kuipigia debe sera hii ya soko huria huku ukijua kabisa umuhimu wa serikali kumlinda mkulima?
  • Je ni nini maoni ya CHADEMA kuhusu kilimo kwanza na vipi ingefanya tofauti na hii kauli mbiu ya CCM ya "kilimo kwanza" ambayo kwa maoni yangu inalenga kuwanufaisha elites wanaojua kinachoendelea katika WTO hasa kwa habari ya kilimo?
Felister,
Nakushukuru sana.
i) Kwanza niseme tu kuwa EU ina Soko huru lakini siyo huria. Regulations zote mathalan "Rules of Origin" zinalenga katika kulinda Soko lao, japo siyo kwa njia ya blatant planning. Kanuni daima zinaweka mipaka. Wote wanaofahama sakata la "Banana Conflict" kati ya USA na EU ni dalili ya wazi kuwa nchi hizo zote ambazo ni wafalme na waalimu wa Open Market Economy ziliweka mipaka katika Biashara hadi WTO ikaingilia. Nilichoeleza ni kuwa Sawa tuwe na Market Economy, lakini Market Economy inayotawaliwa na Objective Regulations, siyo kila kukicha kila kiongozi anatoa maagizo, maelekezo, amri, na wakati mwingine kuwaachia kabisa wakulima at the mercy of the middlemen. A good market Economy is one with clear, objective regulations that are accessible to all, and all are bound to obledge. Swala la Biashara ya Vitunguu ya Mang'ola( Wilaya ya Karatu) ambapo Mkuu wa Mkoa anatoa maagizo ya kuruhusu wafanyi biashara wa nchi jirani kununua kwa kipimo cha "net" over 130 kgs instead of the statutory 90 ni dalili ya wazi ya kutokuwa na kanuni zilizowazi na zinazotekelezwa au zinazokuwa na msimamizi madhubuti. Wakati tunaweka Sera zetu after review, position ya Chadema katika Kilimo itakuwa wazi.
2) Swala la Kilimo Kwanza is a hoax. Mosi hakuna mtu anayeelewa exactly Kilimo Kwanza ni nini, si Mawaziri, si Wabunge, si Watendaji. Huwezi kutegemea Tija kutokana na Policy ambayo haijulikani. Serikali inasisitiza "Kilimo Kwanza" ni Kauli Mbiu, nadhani ifike mahali tuchoke na kubadilisha Kauli mbiu. Wanaojua Historia ya Nchi yetu, tumetoka kwenye Kauli kama hizo na tumebaki pale pale au tumeshuka zaidi, mathalan, Kauli Mbiu ya "Kilimo ni Uhai", "Kilimo cha Kufa na Kupona", tukaja na Kauli ya Kipaumbele kuwa katika "Kilimo cha Umwagiliaji", lakini yote kumi tunazunguka hapo hapo kama "Pia". Takwimu zinaonyesha kuwa miaka ya 1980 tulikuwa na hekta nyingi zaidi ya umwagiliaji kuliko leo, kwa zaidi ya Hekta 150,000. Hivyo, Tuna cancer ya Kauli mbiu kama political catchwords, na kwa kuwa wengi hatufanyi "analysis" au tunavutwa na ushabiki kuliko Critical scientific analysis, tunapokea na kumeza kila kitu. Kwangu mimi niliyezunguka wilaya karibu zote, na hivi karibuni kupitia Kamati ya LAAC tena, ambapo tunaona asilima takriban 80 za fedha za ASDP( Agricultural Sector Development Program) kutumika katika Semina zisizo na Tija, tena zinazowahusu watendaji wa Halmashauri and in most cases hao hao, and in very extreme cases fabricated names, "Kilimo Kwanza" kitabaki theory. Utaratibu wa kutenga Fedha kwa ajili ya matrekta (au power Tillers) sio endelevu, kwanza haujafanyiwa utafiti, hakuna utaratibu ulioandaliwa au unaoonyesha kuwa trekta hizo zitatumika vipi. Ikumbukwe kuwa mpango wa matrekta si mgeni katika nchi yetu, tumekwisha kutoa mabilioni ya fedha kupitia "Mfuko wa Pembejeo", na hakuna hata mmoja anayejua mfuko huu unaendeshwa vipi, trekta zilizogawiwa ziko wapi ( nina mifano hai ya jinsi Serikali ilivyodanganywa kuhusu Trekta hizo lakini hakuna hatua thabiti inachukuliwa kwa wahusika). Tusipoangalia Kilimo Kwanza kitakuwa avenue nyingine ya Ufisadi Mkubwa. Dalili ziko wazi, kama tunapenda kuchukua hatua wakati ni huu kuokoa mabilioni hayo. Navipongeza sana Vyombo vya Habari vinajitahidi sana kutoa Taarifa mbalimbali, lakini inaishia katika kusomwa. Hakuna hatua na hakuna wa kuchukua hatua.
Hivyo Felister, nina mengi ya kusema na kwa mifano hai, lakini maelezo yatakuwa marefu sana na si busara kuwachosha wasomaji wetu. Thanks once again,
 
Dr. Slaa nadhani kwenye hili mnafanya makosa technically. Tukumbuke kwamba watanzania ni taifa la kipekee ambalo watu walio wengi source ya information ni vijiweeni na majungu majungu mitaani.

Case no.1
Rejea pre-elections za 2005. Prof Mwandosya akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi alituhumiwa na gazeti la rai kuhusu mtoto wake kufadhiliwa na kampuni ya MSI Detecon, mwekezaji wa TTCL wakati ule. Kwenda South Africa na kufanya field na kampuni hiyo fully paid. Prof emerged only once kuelezea facts in a learned manner and when the wind kept on blowing alikuwa akijibu lightly and simply kama mnavyofanya nyie hivi sasa. HILO NILIKWISHAELEZEA. In the end wananchi wakaaminishwa kwamba the rumors were true. Proof? Why is ths guy don't want to discuss the issue?

Case no 2.
Tukirejelea tena kwenye mchakato wa uchaguzi CCM 2005, Dr. Salim alituhumiwa kwamba alikuwa memba wa Hizbu. Since he knew that was a lie and a useless rumor aliamua kukaa kimya. The rumor kept on going and what happened,wananchi wakaaminishwa kwamba the rumors were true. Proof? Why is ths guy don't want to discuss the issue?

Case no 3.
In the same 2005 pre-elections michakato the current president, H.E J. Kikwete alituhumiwa kwamba ana Ukimwi na magonjwa mengine kadha wa kadha. What happenned tulionyeshwa kwenye vyomba vya habari ITV, TVT, magazeti kwamba the candidate was physicaly fit! Of which in fact ingekuwa nchi zilizoendelea hii ilitosha kumuangusha muheshimiwa. And ever since afya ya mkulu imewekwa hadharani more than 2 times. What happens. Wananchi walio wengi they don't doubt kuhusu afya ya muheshimiwa.

Case no 4.
In those pre-2005 elections CUF ilituhumiwa kwamba ni chama cha kidini na wao pia wakafanya the same mistake wakijua tuhuma hizo si kweli wakapuuza. What happened?

Case no 5.
In 2005 nyie Chadema mlituhumiwa hili suala la ukabila. Lakini kwa sababu mlijua sio kweli hamkuweka the necessary efforts kucountereffect hiyo rumor. What happened wananchi wengi hasa kanda ya ziwa (I was there by that time) waliaminishwa ujinga huo and is probably why Chadema ilipata kura chache kuliko ilvyotegemewa.

So in my opinion Chadema should not take this matter lightly. Hii hoja mnahitajika kuwa na majibu nayo anytime regardless as to how many times itaulizwa. Jingine hebu fanyeni just a research say in 3 regions kuhusiana na hii tuhuma. You will be surprised!!!!!!!!!! As we are just some 9 to 10 months b4 elections jaribuni kuweka sawa hii ishu. It is few of us who understand it is rubbish lakini the majority aidha wanaamini au wanakuwa na mashaka.

Hii ni Tanzania na ni zaidi ya tuijuavyo!!!!
Na hili la wabunge wa viti maalumu wasilidharau....
 
Tafadhali mniwie radhi niwe tofauti kidogo katika uulizaji /utoaji maoni yangu.

1. Mh. Dr.W. Slaa nakupa nafasi hapa ya kutoa ushauri kwa Mh. Zitto K. ili kuboresha uongozi na harakati zake katika siasa.

2. Mh. Zitto K. nakupa nafasi hapa ya kutoa ushauri kwa Mh. Dr. W.Slaa ili kuboresha uongozi na harakati zake katika siasa.
Kibunago,
Asante kwa ushauri wako. Swali linaashiria kuwa Dr. Slaa na Zitto hawazungumzi na hawashauriani. Napenda kuweka wazi kuwa taswira hiyo siyo sahihi. Dr. Slaa na Zitto tuna mfumo wa mawasiliano ndani ya Chama, tuna mahali pa kushauriana kuhusu uongozi na mengine yote, na ndivyo tunavyofanya siku zote. Itoshe kusema kuwa uongozi wa Chama huongozwa na Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki ya Chama ambayo yote yanapatikana katika Katiba ya Chadema Toleo la 2006, hivyo, ushauri huu pamoja na nia njema inayoweza kuwepo utakuwa kinyume na Taratibu zetu za ndani ya Chama. Nakushukuru sana.
 
Back
Top Bottom