Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,876
- 2,744
Katika jambo lisilotarajiwa na wengi, Dr Slaa amepita katikati ya maduka hapa jijijini Mwanza huku akiamsha taharuki kwa mamia ya watu wakitaka kumwona. Dr Slaa akiwa ameambatana na mbunge wa Nyamagana mh Wenje alipata wakati mgumu baada ya kila mtu kutaka kumsalimia. Nimeshuhudia magari yakipiga honi na abiria walikuwa wanashuka kwenye daladala wakikimbilia eneo aliopo. Kesho kuna uchaguzi wa meya wa jiji la Mwanza, yawezekana ujio wa Dr ni mahususi kwa shughuli hiyo.
hii hali naifananisha na ndoto niliyoiota majuzi, kwamba nilifika maeneo ya Tabata Aroma nikamkuta amekaa na wadau kadhaa kando kidogo ya barabara kwenye viti wakiwa wanaabadilishana mawazo. Nikampa mkono (ila nilisalimiana nae kwa mkono wake wa kushoto. Kwa mujibu wa ndoto yangu bado una maummivu kiasi ila baadae tukasalimiana kikawaida). Sekunde zilivyokuwa zikisogea watu walionekana kuongezeka pale tulipokuwa na Dk. Watu wakawa wengi sana wakitaka kumpa mkono wa salam. Hali iliyokuwepo ilibidi wapambe wamtoe pale na kumwingiza nyumba iliyokuwa jirani kwa usalama wake. Nao watu bado wakawa wengi pale nje, na barabarani kukawa kumejaa sana na brass band ikawa inapita kwa ajili ya Dk