Dr Slaa afunga barabara Mwanza

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Katika jambo lisilotarajiwa na wengi, Dr Slaa amepita katikati ya maduka hapa jijijini Mwanza huku akiamsha taharuki kwa mamia ya watu wakitaka kumwona.

Dr Slaa akiwa ameambatana na mbunge wa Nyamagana mh Wenje alipata wakati mgumu baada ya kila mtu kutaka kumsalimia.

Nimeshuhudia magari yakipiga honi na abiria walikuwa wanashuka kwenye daladala wakikimbilia eneo alilopo.

Kesho kuna uchaguzi wa meya wa jiji la Mwanza, yawezekana ujio wa Dr ni mahususi kwa shughuli hiyo.
 
Katika jambo lisilotarajiwa na wengi, Dr Slaa amepita katikati ya maduka hapa jijijini Mwanza huku akiamsha taharuki kwa mamia ya watu wakitaka kumwona. Dr Slaa akiwa ameambatana na mbunge wa Nyamagana mh Wenje alipata wakati mgumu baada ya kila mtu kutaka kumsalimia. Nimeshuhudia magari yakipiga honi na abiria walikuwa wanashuka kwenye daladala wakikimbilia eneo aliopo. Kesho kuna uchaguzi wa meya wa jiji la Mwanza, yawezekana ujio wa Dr ni mahususi kwa shughuli hiyo.

Ni dalili njema!!! Nape upo? Ritz, Rejao, Zomba et al mmesikia marafiki zangu. Heri mimi mshabiki sina kadi!!! Ninachoangalia ni mateso ya watanzania walio wengi ambao 67.9% wanaishi chini ya dola 1.25 kwa siku!!! Wengine hata mia hawana na ardhi walishanyang'anywa na wachimba madini.
 
Nimefurahi sana kufika kwa Dr. Slaa Mwanza.Ni muhimu sana ili kurekebisha hali ya hewa.
 
sasa hapa tujadili nini?
Hujaona cha kujadili mkuu?? Ngoja wenye cha kujadili waje thread itajaa kama kifusi. Kwa sada hivi wako hawa tu kwa dakika hizi chache thread imetua hapa. There are currently 15 users browsing this thread. (9 members and 6 guests).
 
Viongozi wa Chadema ndio pekee wanaonekana kuwa ni tegemeo la wanyonge Tanzania,

Mapambanop yaendelee Makamanda hadi tutakapoikomboa chi yetu hii pendwa
 
Back
Top Bottom