Mkutano mkubwa wa hadhara wa kumtambulisha Katibu mkuu CHADEMA Dr Vicent Mashinji -Furahisha Mwanza

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,228
Ni Jumapili njema yenye kila aina ya shamrashamra hapa Mwanza.

Jumapili iliyoingia katika historia ambayo usiku wa kuamkia kwake Taifa limeshuhudia Msomi aliyebobea Dr Vicent Mashinji akiukwaa nafasi ya Katibu mkuu wa chama kinachopendwa zaidi nchini CHADEMA.

Freeman Mbowe gwiji wa siasa za Tanzania aliicha dunia mdomo wazi pale alipotamka jina ambalo halikutarajiwa kabisa kuvaa viatu vya Katibu Mkuu.Shangwe nderemo na hoihoi za wajumbe ziliashiria kukubalika kwa mteule huyo wa Mwenyekiti.

Kama ilivyotangazwa awali kijana huyo mwenye miaka 43 na msomi ambaye huenda ndiye msomi kuliko makatibu wakuu wa vyama vyote duniani atapanda jukwaani kutambulishwa kwa umma.

Mkutano wa kumtambulisha Dr Mashinji utafanyika katika viwanja vya Furahisha kuanzia saa 8 mchana na utahudhuriwa na viongozi wote wakuu.

Tutawaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya mikutano jijini Mwanza kwa miaka ya karibuni.

Updates....

Msafara mkubwa wa viongozi wakuu wa chama wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe,Waziri mkuu Mstaafu Edward Lowassa na Katibu mkuu Dr Vicent Mashinji umeshawasili hapa uwanjani na kupokelewa kwa shangwe hoihoi na nderemo.

Hotuba za Viongozi:

Halima Mdee

Anasalimia

1. Anasema mwanza waelewe kuwa uchaguzi uliopita ccm walipigwa chini.

2. Anasema ccm acha wabane daslam lakin wataachia. Anasema ccm watake wasitake ,maguful atake asitake lakin meya atatoka cdm.

3. Anawataka wakazi wa mwanza kwa nyomi hii wawe wanaenda mahakamni .

Wenje

1. Anasema sio mbunge tu alietangazwa pale jiji bali ni mbunge wa jimbo la nyamagana. Anasema kwasbab hata wao kuwa aliwashinda ccm.

Anasema hata akiwa peke yake, anafuraha kwasbabu anajua alishinda.

Anasema tuombeane tu,kwasbabu kesi ipo mahakamani.

Anasema haijalishi itachukua muda gani lakini haki itakuja.

Anasema kwa.miaka mitano iliyopita jiji la mwanza, lilijenga heshima.

Anasema ataanza ziara katika jimbo hili, na atakuwa anasimamia shughuli.

Anamshkuru mbowe kwa kuja kufanyia mkutano wa baraza kuu toka mwanza ni heshima ya kwa mwanza

Lissu

Anasema kamati kuu ilikuja mwanza kumsaidia mwekiti kupata katibu mkuu.

Mwenyekiti kafanya kazi yake.pia na baraza kuu limefanya kazi yake.

Salim mwalim

Anasalimia

1. Anasema hii ni mara ya 8 kuhutubia uwanja huu, anasema hazina kubwa ya vijana wa cdm ni hoja.

Anasema cdm imejaa kila.sehem ,ipo kwa tiss, makazini na popote pale.

Anasema ccm wasihangaikr na kununua watu wa cdm maana itakula hasara zaid kuliko faida.

2. Anasema usajili umekamilila.

Kushoto mwalimu, kulia mnyika.na kati mashinji.

Anasema makuful muda wa honeymoon kishaisha ajiandae kwa kazi.

Triple M ya barcelona ,ishaingia uwanjani.

Mnyika

Anashukuru kwa mbowe kumchangua Mashinji.

Anasema pia atampa ushirikiano katibu mkuu aliechaguliwa

Lowassa

1. Anasema na sherehe ya kumtambulisha km.

Anasema la kwanza mnanikumbuka ? Watu wanaanza kuimba Rais rais rais

2. Anasema anashukuru sana kwa kupewa kura nyingi sana toka mwanza.

Anawashukuru wote , anasema baada ya matokeo vijana atoe kauli. Vijana walitaka wakadai haki zao road. Anasema aliwatuliza vijana waliotaka kudai haki yao kwa kuandamana barabarani

Anasema 2020 anawahakikishia tutaingia ikulu
Anasema anajua tunampenda na yy anatupenda pia.

Anasema kwa wizi wa ccm wakaiba kura zake na za wenje.

Anampongeza KM na anasema ni kijana na ni kiboko kwa maccm.

Mbowe

Anasalimu

1. Anasema waandishi wa habri wa muhimu katoka kupoginia tz tuitakayo.

2. Anaungana na lowassa na wenje , na wagombea wote kwa namna ya kipekee sana ilituunga mkono wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Kanda ya ziwa ilikua ni eneo muhimu kuamua ni nani awe raisi na aweze kulisimamia bunge.

3. Anasema anawashukur woote akina mama na baba. Anasema mwanza imefanya diasa za amani.

4. Dunia inajua,ccm ,lubuva ya kwamba kanda ya ziwa ilichagua upinzani yaana UKAWA. Lakin kwa kujua hayo ccm wakawekeza hila kanda ya ziwa
5. Anasema mwanza ni jiji kubwa na la pili kwa ukubwa nchi hii.

Anasema dar ipo chini ya ukawa lakini magamba wanataka kuchakachua,lakini anasema ccm wakijaribu kugusa au kuchakachua dar kitanuka

Anasema jiji la arusha cdm ilishinda , na tulichukua jiji.

6. Anasema jiji la 4 kwa ukubwa , wanchi walisema mbunge wao ni sugu, rais wao ni lowassa na tukachukua jiji na kata nyingi.
Katika madiwani 34, cdm 29

7. Jiji la 5 kwa ukubwa, wakaamua raisi wao ni lowassa na mbunge wao ni ukawa....anasema leo hii mbunge wa tanga anatoka cuf

Anasema umeya walichakachua ,lakini ipo siku.

8. Manispaa ya moshi cdm inaongoza , kwa madiwani wa kutosha.

Iringa pia wakaamua mbungr ni msigwa , lowassa kuwa raisi wako. Katika madiwani
34, cdm 24 au ukawa

8. Ansema nimetaja majiji makusud kwasbabu majiji ndio yanaongoza mabadiliko.

Anaema kwangu pia nilipiga, madiwani 100%, ubunge 90%

Anasema kule kwake hai hana diwani wa ccm hata mmoja.

9. Anasema mwanza iliamua , lakini ccm na tume walitengeneza utatu wa dhambi.

10. Kumkosa mbunge ni aibu, anasema mabomu pia yalipigwa na risasi zilipigwa. Lakini walikomaaa mpk kura zikapatikana.

11. Anaasema.chama kinatambua umuhimu wa mwanza ,ndio maana kimeamua kuja kufanyia kikao mwanza.

Anasema tumekuja huku tuje tujiangalie na kuendeleza na vita.

Anasema hii vita hatujapoteza, anasema wapo kwaajili ya kupanga upya majeshi na kuendelea kuishambulia mwanza.

12. Anasema pamoja na kumuua mawazo lakin wamekuja na mawazo mpya KM, lakini anasema kuna mawazo wakutosha.

Anasema mashinje hajachaguliwa kuwa KM wa wasukuma bali wa watanzania.

Na pia amechaguliwa kwa kuwa na sifa. Anasema kila.mtu ananafasi endapo tu anauwezo.

Mashinji anashanagaa baba ake sio mwanasiasa, wala lowassa sio mjomba wake lakini amechaguliwa.

Anamuelezea mashinji.

1. Cdm kazi yao ni kuibua vipaji na ndicho walichokiona kwa mashinji.

2. Anasema ccm n watu wa propaganda.

3. Anasema watu wote wanauwezo wa kuwa KM , lakini KM lazima awe mmoja.

4. Ansema cdm lazima nafasi za kazi wasaidizane.

Anasema waliopo bubgeni watapambana bungeni

Akina mashinji watapambana nje ya bunge, hii ndio sababu ya kuchagua.mtu alie nje ya bunge ili apambane na wezi ccm.

Ansema

Wakaangalia elimu, akasema elimu pekee sio yakumfanya awe KM. Asije kuwa muoga lakini ana elimu.

Wakaangalia wakakuta ni kiongozi wa mgomo wa ma dk, kwaio huyu sio muoga. Mgomo ulifanya afukuzwe kazi.

Wajumbe wa kamati kuu walimpitisha kwa 100%

Mashinji anakazi kubwa ya kujenga cdm nchi nzima.

Dr Vicent Mashinji -Katibu Mkuu

Anasalmia

1. Anasema kuna mtu alimuuliza kuwa udokta na siasa wapi na wapi.

Akamwambia subiri ataona. Anaema 2020 tutakuwa pembeni ya bahari.

Anasema atakuwa katikati,mwalimu pemben mnyika pembe.

Mbowe nyuma anasoma mchezo

Anasema yy ni mzee wa mikakati ,kwio anakuja na mikakati.

Ansema mwanza ,walikuwa wanamtania kuwa ss nyie wasukuma kwamba hata akipigwa anasema tu ndoho tabu.

Anasema wanataka mabadiliko ya kimfumo, ndani na nje

Anasema atasimika chama kwa wananchi.

Anasema ni lazima kiimarishe misingi na mashina.

Anasema kwamba ujanja ujanja wa daslam utaisha kwasbab kaja kimkakati.

Anaema anahitaji viongozi kuheshimu maamuzi ya wananchi.

Anasema anahirimisha chama ,ili sio wtu waje waibe kura alaf tunawaangalia tu.

Anasema wanachi wanatoa maoni alaf kikundi cha watu wanachakachua.

Anasema kansa ya uoga lazima ife

Anasema

Hakuna jeshi lirashinda kwa kupigana na watu wasio na silaha.

Anasema dhamira yetu ndio itakuwa silaha yetu

Anasema tukikataa ni lazima dunia ione tumekataaa.

Anasema vurugu huwa ni jibu kama muda wa vurugu utafika.

Anasema wanasiasa kuwatumia vibaya polis, kunasbabisha wanachi kuchukiana na polisi.

Anasema watapambana kwa hoja, na kila namna. Ikishindikana mwishoni tutapambana kwa.mawe.

Amasema wamepanga mkakati na tusiogope.

Anasema kila kata atatengeneza kamati ya ufuatiliaji, hata kama hatuna hata diwani

Lakini lazima wafatilie wanachama na kila shguhuli ndani ya chama.

Anasema tukiwa na kamati mambi ya wenje yasingekwepo maana uchaguzi uliopita walipochelewesha tulitaka.kuvunja geti wakatangaza.

Anasema hii ni nchi yetu, tuaenda kuidai katiba yetu.

Ansema katiba mpya ni ajenda ya kudumu bungeni

Katibu Mkuu amemaliza na kushukuru kwa yote yaliyofanyika.Ameahidi utumishi uliotukuka.

MWISHO.
 
Kama ilivyotangazwa awali kijana huyo mwenye miaka 43 na msomi ambaye huenda ndiye msomi kuliko makatibu wakuu wa vyama vyote duniani atapanda jukwaani kutambulishwa kwa umma..

Kweli mapenzi ugonjwa, yaan huyo Daktari kwa kuwa na degree yake ya Medicine na Masters ya Business Administration basi anakuwa msomi kuliko makatibu wa vyama vyote duniani?seriously?kama huyo ni msomi kihivyo labda reference yako ilikuwa too weak.

Labda kama huko Chadema mtu kuwa na masters ni usomi mkubwa kiasi hicho, may be kwa sababu umemlinganisha na Mwenyekiti.
 
Ni Jumapili njema yenye kila aina ya shamrashamra hapa Mwanza.

Jumapili iliyoingia katika historia ambayo usiku wa kuamkia kwake Taifa limeshuhudia Msomi aliyebobea Dr Vicent Mashinji akiukwaa nafasi ya Katibu mkuu wa chama kinachopendwa zaidi nchini CHADEMA.

Freeman Mbowe gwiji wa siasa za Tanzania aliicha dunia mdomo wazi pale alipotamka jina ambalo halikutarajiwa kabisa kuvaa viatu vya Katibu Mkuu.Shangwe nderemo na hoihoi za wajumbe ziliashiria kukubalika kwa mteule huyo wa Mwenyekiti.

Kama ilivyotangazwa awali kijana huyo mwenye miaka 43 na msomi ambaye huenda ndiye msomi kuliko makatibu wakuu wa vyama vyote duniani atapanda jukwaani kutambulishwa kwa umma.

Mkutano wa kumtambulisha Dr Mashinji utafanyika katika viwanja vya Furahisha kuanzia saa 8 mchana na utahudhuriwa na viongozi wote wakuu.

Tutawaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya mikutano jijini Mwanza kwa miaka ya karibuni.
Umeandika kishabiki kupitiliza......
 
Itakua hewani kwa Tv na Redio ili tumsikie huyo mteule mpya ana dira gani? Maana uimara wa opposition ndiyo uimara wa State au Serikali iliyoko madarakani
 
Hakuna ushabiki hapo

Ebu tueleze huo usomi wake wa kuwa msomi wa kiwango cha Katibu Mkuu msomi kuliko wote duniani?hivi Masters huko Chadema ndio usomi wa ajabu hivyo?

Tambua anaitwa Dr kwa maana ya Daktari wa Hospital, kwa degree yake ya kwanza ya Medicine na sio kwa kuwa na PHD. Unless kama wenzetu huko mlikimbia umande.
 
Asante kwa Taarifa Mkuu Molemo, najua upo kwenye msafara huko Mwanza, tunakutegemea kwa updates...

Nina furaha ya aina yake kwa uteuzi uliofanywa wa nafasi ya KM.

Mbowe anastahili tuzo kwa kuibua watu wenye uwezo!!
 
Mbona haionyeshi kuwa kasajiliwa na chama cha madaktari? Tunamwitaje Dr? Bora tumwite tabibu tu.
 
Ebu tueleze huo usomi wake wa kuwa msomi wa kiwango cha Katibu Mkuu msomi kuliko wote duniani?hivi Masters huko Chadema ndio usomi wa ajabu hivyo?

Tambua anaitwa Dr kwa maana ya Daktari wa Hospital, kwa degree yake ya kwanza ya Medicine na sio kwa kuwa na PHD. Unless kama wenzetu huko mlikimbia umande.

Ficha upumbavu wako, soma vizuri CV ya jembe Mashinji uone nondo za ukweli... Jamaa ni mult-purpose

Huyo Kinana wenu zaidi ya cheti cha poaching ana nini la zaidi? Nakumbuka Kinana alipata zero O'level Arusha sec
 
Back
Top Bottom