Dr Slaa afanyiwa hujuma Morogoro

Dr Slaa afanyiwa hujuma Morogoro

Msiyashangae haya mambo yanayoratibiwa na kufanywa na CCM dhidi ya CHADEMA au dhidi WANANCHI WANYONGE NA MASIKINI.
Ni kwamba hali waliyonayo kwa sasa hawa ccm hawafai hata kufuga bali ni kuwasaka kokote walipo na kuwaangamiza kabisa. cheki evolution yao;
ccm evap.jpg
TUSHIRIKIANE KWAPAMOJA WAPENDA MABADILIKO NA WANACHADEMA KWA UJUMLA KUMUANGAMIZA HUYU MNYAMA MBAYA KABISA CCM IFIKAPAO 2015.

Pipoooooooooooooooooooooooooooooooooooz?????????????????????
 
images


Meneja wa hoteli amnyang�anya chumba
Umeme wakatika, Tanesco wakana hujuma

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amefukuzwa katika nyumba ya kulala wageni ndani ya Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) Mikumi, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kisiasa ikiambatana na kuzimwa kwa umeme kwa mji mzima kwa saa zaidi ya 12 ili kudhibiti mikutano yake ya hadhara anayoifanya.

Dk. Slaa ambaye aliwasili majira ya saa 8.00 mchana mjini Mikumi akitokea tarafa ya Malinyi, wilayani Ulanga, Morogoro, katika Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni Sangara, alifikwa na udhalilishaji huo baada kuonyeshwa chumba chake lakini baadaye akanyang’anywa.

Baada ya kuwasili hotelini hapo, Dk. Slaa alikabidhiwa funguo ya sehemu ya kufikia kutoka kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, na kuingia chumbani, muda mfupi baada ya kuingia katika chumba hicho alitokea meneja wa hoteli hiyo, Jacob Sumary, na kumueleza kuwa sehemu hiyo imeshawekewa ‘oda’ na wateja wengine na hivyo kutakiwa kuondoka katika eneo hilo mara moja.

Hata hivyo, Dk. Slaa alihoji sababu za mmoja wa walimu wa Veta kuacha majukumu yake na kujipa jukumu la kuhudumia hoteli kwa kumhudumia eneo lenye vyumba vitatu lenye thamani ya Sh. 75,000 kwa kila chumba kimoja Sh. 25,000.

Meneja huyo alishikilia kumtaka Dk. Slaa aondeke hotelini hapo kwa kuwa yeye hakuwa na taarifa za ujio wake. Dk. Slaa alitii na kuondoka.

Naye Sumary alipofuatwa na NIPASHE jana kwenye hoteli hiyo kuzungumzia kitendo cha kumnyang’anya Dk. Slaa malazi, alikataa kuzngumzia suala hilo.

Awali alisikiliza NIPASHE ikimuuliza juu ya hatua alizochukua na kutaka kujua ni kwa nini, lakini alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na kukata simu yake.

Akizungumzia hali hiyo katika mkutano wa hadhara, Dk. Slaa alisema kuna mipango imefanywa kwa nia ya kumdhoofisha katika kampeni za kuwakomboa Watanzania.

“Kama mimi nafanyiwa mambo hayo kwa suala dogo la malazi tu na serikali ya CCM, je nyinyi wengine mtafanyiwaje? Mnapaswa kujifikiria mara mbili,” alisema Dk. Slaa.

Ghafla umeme ulizimwa katika mji wa Mikumi hali iliyotafsiriwa kuwa ni muendelezo wa hujuma zinazofanywa dhidi ya Chadema, kwani wananchi walidai mji huo haukuwa na tatizo la umeme.

“Watanzania wa leo siyo wa jana. Zimeni umeme. Hata mfanye nini tutaendelea na mkutano na wananchi watatusikiliza tu. Lakini nitakula nao sahani moja waliofanya hivi,” alisema Dk. Slaa.

Hata hivyo, kukatika kwa umeme huo kuliongeza mori kwa wakazi wa Mikumi kutokana na kuongezeka kwa wingi katika mkutano huo na kukemea vitendo vilivyofanywa na serikali dhidi ya Dk. Slaa.

Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Morogoro, Deogratius Ndamugaba, alisema kukatika kwa umeme kulitokana na hitilafu za kawaida na siyo hujuma au msukumo wa kisiasa.

“Kukatika kwa umeme Mikumi siyo kwa sababu ya Chadema ila ni feeder ya Mikumi iko nje tangu saa 12.45 jioni. Nguzo imeanguka na inapaswa kubadilishwa na sehemu yenyewe ni porini. Kuna giza na Chui,” alisema Ndamugaba.

Alisema amekuwa akijaribu kuwasiliana na vyombo vya habari ili kuwapa taarifa wananchi wa Mikumi.

Alisema utendaji kazi wa eneo hilo kwa muda huo ulionekana kuwa mgumu na kwamba, tayari mafundi wa Tanesco walikuwa katika eneo la tukio kufanya marekebisho.
 
Kuna jambo watu hawalisemi.
Kuna sababu tena ya msingi sana.
uamuzi wa kumfukuza ulikuwa sahihi.
Tukiweka siasa pembeni; mteja siku zote hafukuzwi; anatafutiwa alternative hata kama ni kosa la mteja, unless kama ameiba.

Huyu mwenye hotel/guest ame-risk sana business yake kufanya kitu kama hiki (kama ni kweli amesukumwa na siasa). Unaweza kumnyanyasa mtega mmoja lakini akawa na influence ya-kukufanya ukose wateja 100.

Only in Tanzania mteja sio mfalme. Pamoja na kuwa guest na hotel nyingi bado owner anakuwa na kiburi? Daah! Kaazi ipo.
 
Hayakuhusu. Nyie mmefanya hila zenu, subirini umma uwahukumu kwa maovu

Mimi nashangaa kama huyu Slaa sio tishio kwao kwanini wanaangaika naye hivyo? Wamwache tu aongee kwenye hiyo mikutano wananchi wataamua wenyewe. Hizi dalili sio nzuri kwakweli kwa CCM in a long run; it is just a short pleasure.
 
Kama inafikia hatua ya kuzimiana umeme, thats too much!
It's unbelievable kwamba mambo yote muhimu yanasimama kwasababu tu ya ubabe/ushindani wa kisiasa. Sijui priorities zetu watanzania zikoje. Aah! inachosha.
 
Huyo hotel meneja angeonekana wa maana kama angepandisha bei ya chumba ili apate Presidential price. Ndio maana bongo ni vigumu sana kutofautisha meneja wa hotel, mhudumu wa hotel, mhudumu wa bar na meneja wa bar; wote akili zao sawa tu.

Well said. Ndio maana watu wengi wanapoteza opportunity zaku-make profit/business hivi hivi bila kufikiri. Wakati wengine tukiwa kwenye business tunawaza how to maximize profit; wengine wanawaza kwingine kabisa. Huyu mtu ajue tu kwakumfukuza Slaa hajamkomoa, bali amewasaidia business competitors wake kwakuwapa business ya Slaa & Co. Inawezekana asijali sana kwasababu sio owner wa VETA; na uzalendo wake nao ni zero hivyo haoni pride yoyote VETA ikifanikiwa. Kweli mwenye macho haambiwi tazama!
 
Mimi nashangaa kama huyu Slaa sio tishio kwao kwanini wanaangaika naye hivyo? Wamwache tu aongee kwenye hiyo mikutano wananchi wataamua wenyewe. Hizi dalili sio nzuri kwakweli kwa CCM in a long run; it is just a short pleasure.

Kwa kweli hiki kitendo walichofanya CCM kimewadhalilisha sana.
 
Yaani kweli viongozi wa Tanzania hawako responsible. Inawezekanaje kutesa raia wengine kuwakosesha huduma ya umeme kwa ajili ya kumkomoa mtu mmoja Dr. Slaa?? Grrrhh.....Sioni kama wamemkoa Slaa hapo, kama ni kulala si angeweza kujiegesha kwenye kiti chake ndani ya gari yake!!!

Hii inaonyesha watu waliopewa dhamana ya uongozi hawako ethical. Hasira za wananchi zaweza kuwasulubu kama hawatakuwa makini na majukumu yao.
 
Hakika mambo haya yanaumiza sana,ila Mungu alimpa Mfalme Daudi nguvu hata akampiga Farao kwa jiwe na Kombeo. Ipo siku ccm watashangaa,wananchi wanaona! Wameona msitu wa mabwepande,vifo vya watu mbalimbali,manyanyaso ya walimu na madaktari,na wafanyakazi. Mungu atawasimamia wote wanaopigania haki. Mtawaliwa wa leo ndiye mtawala wa kesho.
 
Vitendo kama hivi vinazidi kukipa umaarufu CHDEMA na kukidhoofisha CCM bila kujua. Aliye nyuma ya mpango kama huu hana uwezo mkubwa wa kufikiri
 
Huyo meneja anapaswa kushikwa jina na sura yake...baada ya ukombozi 2015 atashughulikiwa kulinga na matendo yake.

Hakuna sababu ya kuwa na visasi kwa wapuuzi kama hawa wenye akili za kitoto. Kutakuwa na mambo mengi mno ya kimsingi ya kushughulikia. CCM ikiondoka madarakani ni kama ndiyo taifa limepata uhuru kwanza kwa maana ya kujipanga upya karibu katika kila sekta. Hebu angalia sheria, utumishi wa umma, polisi, usalama wa taifa, elimu, afya, maji, kilimo, nishati, miundombinu, nk shida tupu
 
Nafikiri ni wakati sahihi sana kufikiria swala la camping facilities na generator kwenye mikutano kama hii.

Tatizo kama kuna kitu chochote unakitegemea kutoka kwenye current system kufanikisha kazi ya kisiasa, watakitumia kama strategy ya kukukomoa.

Mara nyingi tunashuhudia mikutano ya cdm inaporushwa live kwenye tv, umeme unakatwa etc,

Camping vogn ambayo inaungwa kwenye gari kwa nyuma ni bei rahisi sana na inakuwa na facilities zote za nyumba. Its just an advice maana as we approach 2015 there will be alot of gorrilla tactics

Ninakubaliana na wewe umetoa ushauri mzuri sana. Na kwa kuongezea wakiwa na facility kama hiyo, wajipange kiulizi kwa kuwa hawa magamba ni hatari sana
 
Magamba kuwa wajanja basi,mbona mmeishiwa technic kiasi hicho duh poleni sana.
 
Huyo meneja anapaswa kushikwa jina na sura yake...baada ya ukombozi 2015 atashughulikiwa kulinga na matendo yake.

mtamfanyaje? Sidhani kama cdm ni chama cha kulipa visasi. Ila hotel ya kizembe hiyo, si sehemu nzuri ya kufikia. Kama dk slaa wameweza mnyan'ganya funguo sie wengine kajamba nani hata makofi tutapigwa na huyo manager.
 
Back
Top Bottom