Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amefanyiwa hujuma kubwa mkoani Morogoro kwa kufukuzwa chumba cha kulala wageni ndani ya chuo cha ufundi VETA, Mikumi Kilosa.
Kiongozi huyo ambaye alikabidhiwa chumba hicho na viongozi wa CHADEMA kikiwa kimelipiwa kila kitu na akaingia lakini ghafla akaja Meneja wa hoteli hiyo Jacob Sumary na kumtaka Kiongozi huyo wa upinzani nchini kuondoka mara moja kwenye hoteli hiyo kwa sababu tayari ilishalipiwa na mtu mwingine.
Kwa ustaarabu mkubwa na kutokutaka mabishano Dr Slaa aliondoka.
Pia katika hatua nyingine umeme ulizimwa mji mzima wa Mikumi jana kuanzia asubuhi hadi usiku katika kile kilichoonekana ni hujuma ya Tanesco ili Dr Slaa ashindwe kuhutubia,hata hivyo mbali na kukosekana umeme mikutano ya Dr Slaa ilifurika umati mkubwa wa watu huku kiongozi huyo akiwaambia maelfu ya watu atawahutubia hata bila vipaza sauti.
Vitendo hivyo vya kihuni alivyofanyiwa Dr Slaa viliwachukiza wananchi wengi wa Mikumi na kusema watalipa kisasi kwa kuindoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura.
Source: Nipashe/Mwananchi