Kama ilivyo kwa kila mtanzania anayelilia mabadiliko ya nchi hii (isipokuwa magamba), nimezipokea taarifa za kutimuliwa kwa dr. Slaa katika hoteli ya Veta huko Mikumi-Morogoro kwa masikitiko makubwa. Nikiwa kama mzalendo wa nchi hii, tukio hili linatoa tafsiri nyingi sana katika tasnia ya siasa za nchi hii na mustakabali wa Taifa letu.zifuatazo ni baadhi ya tafsiri za tukio hili;
1. Ni Udhalilishaji mkubwa kwa 'rais' wa nchi. Itakumbukwa kwamba, Hadhi ya Dr. Slaa katika nchi hii kwa sasa ni adimu sana, kwani, kama si sababu kadhaa ikiwamo na uchakachuaji wa matokeo (kama ilivyokuwa imeripotiwa sana mara baada ya uchaguzi mkuu 2010), sina shaka Dr. Slaa angekuwa ndiye Rais wa nchi hii kwa sasa.Lakini pia, nani ajuaye ya 2015 endapo chama chake kikimpitisha kugombea tena? kitendo alichofanyiwa ni unyama mkubwa wenye lengo la kudhoofisha jitihada anazozifanya yeye na chama chake ambazo ni vigumu kwa sasa kufanikiwa.
2. Meneja wa hoteli aliyemzui Dr. Slaa ni kada na au kuwadi wa chama tawala-CCM. Tulio lililotokea ni dhahili kuwa ni la kisiasa. Na kama ni la kisiasa, basi sababu iliyotolewa na Meneja huyo kuwa eti 'chumba alichokuwa akitumie Dr. Slaa kilishakuwa na mtu) ni sababu dhaifu mno. ni sawa na zile ambazo zinachosha masikio yetu kutoka kwa jeshi la polisi kama sababu za kuzuia mikutano ya CHADEMA -uwanja mnaotaka kuutumia utatumiwa na watu wengine (ccm) siku hiyo hiyo. UPUUZI!!!!!!
3. Kuzima umeme kwa sababu ya mtu mmoja (Dk. Slaa) na kuwakosesha huduma hiyo muhimu maelfu ya wakazi wa Mikumi ni uonevu kwa wananchi hao. kulikuwa na sababu zipi hasa zenye mashiko za kuwaadhibu wananchi wale kwa kuukosa umeme, huku ikielezwa kuwa haikuwa desturi kwa muda kidogo kukatika umeme maeneo hayo.
4. Meneja/msimamizi wa huduma za umeme (Tanesco hapo mikumi/Morogoro ana kesi ya kujibu; iweje atumike kisiasa kwa maslahi ya chama fulani? hivi yeye hayuko ofisini kwa maslahi mapana ya watanzania wote? ni kwanini ameruhusu wanasiasa kuharibu /kuingilia wajibu wake? Kwanini afanye kazi kwa maslahi ya chama kilicho madarakani? kwa hakika ANASTAHILI KUJIUZU KWA MATUMIZI MABAYA YA OFISI.
5. HASARA ambayo TANESCO imeipata kwa kuzimwa umeme kwa zaidi ya saa 12 pasi na sababu za msingi ni kubwa. Hivi ni iunit' ngapi za umeme zingekuwa zimetumiwa na wananchi wa mji huo kwa saa hizo? ni pesa ngapi tanesco ingeliingiza kwa umeme kuwepo kwa saa hizo? Hasara hiyo itafidiwa vipi? nani ataifidia?
KIMSINGI KABISA, KUMPIGA TEKE CHURA SIO KUMWUMIZA, BALI NI KUMWONGEZEA MWENDO.TAFAKARI.