DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa

Naunga mkono hoja. Kieleweke kwamba, si Kikwete anayepingwa na kususiwa, ila ni mfumo mbovu wa utawala dhalili, usiojali misingi ya usawa, haki na demokrasia, bali unaotetea na kuendeleza maslahi ya watu wachache! Katika hili, tukikumbuka kwamba TANZANIA NI YA WATANZANIA WOTE, hatuwezi kuwa vipofu au kujifanya kama mbuni, akifukia kichwa chake ardhini na kuacha mwili wake nje, akidhani yuko salama. Kuendelea kufanya hivi ni kukaribisha vita na upotevu wa amani hapa nchini. Bado HATUJAJIFUNZA kutoka kwa majirani zetu wa karibu na wa mbali?

Sasa tuelekeze nguvu zetu katika mabadiliko yatakayoleta uwiano sawia, kwa Watanzania wote, bila kujali itikadi, dini, rangi wala kabila, kwani hii ndiyo misingi aliyoijenga Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alipotuasia kwamba Umoja ni Nguvu!

Tunapoteza umoja, tunapoteza uzalendo. Ni wangapi kati yenu wanaofikiria, hata kwa siku moja tu, suala lolote la kutatua matatizo ya nchi? Kwa mfano, Jijini Dar es Salaam, asilimia 70 ya wakazi wanaishi kwenye asilimia 70 hadi 80 ya maeneo ambayo YAMETHIBITIKA kuwa HAYAFAI KWA MAKAZI NA MATUMIZI ya binadam! Lakini bado tunasema CCM imetuletea maendeleo, na inapaswa kuungwa mkono! Ndani ya Jiji la Dar bado kuna maeneo - HATA KARIAKOO - ambapo kuna zile nyumba za tembe, yaani, "nyumba za mbavu za mbwa", ambazo watu wamejenga kwa miti na kukandika kwa udongo! Katika Karne Hii, hiki ni sawa kweli? Kwa nini tuwe na umaskini wa kutisha namna hii, ilhali Tanzania inahesabika kuwa NCHI YA TANO DUNIANI kwa uzalishaji wa DHAHABU?

Panapofuka moshi, pana moto. Lisemwalo lipo, kama halipo, LAJA! Anayekutahadharisha anakusaidia kutambua lililopo mbele yako, au linalokunyemelea. Na ukiona mwenzio ananyolewa, tia maji kichwani.

KANU ilitamka kwa kibri kikubwa, kwamba ingeitawala Kenya milele! Leo hii, KANU ni chama cha UPINZANI! Wananchi wakielimishwa, wanao uwezo wa KUIONDOA CCM MADARAKANI! Sisi wa CHADEMA tutawaelimisha ili kuwaamsha usingizini. Kama imeshindikana leo, 2015 tutaweza!

Mpaka Kieleweke!

A Luta Continua!

-> Mwana wa Haki

P.S. Nieleweke kwamba namtambua Rais Kikwete kama rafiki yangu, ndugu yangu na KAKA yangu. Ninamfahamu, ninamheshimu, yeye kama yeye, lakini sikubali misingi ya utawala anayoitetea na kuilinda. Sina chuki naye, ni ndugu yangu. Tukubali kutofautiana. Siwezi kumchukia binadam yeyote hapa duniani, lakini nina haki ya KUPINGA na kutofautiana na yale anayoyasimamia na kuyatetea. Haki ya Kupinga bila Kufanya Vurugu (Non-Violent Protest) ni haki ya msingi kabisa ya kila binadam. Wabunge wa CHADEMA wasilaumiwe kwa yale waliyoyafanya! Wanawawakilisha WATANZANIA WOTE, walio wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA au wa chama chochote kile cha siasa. Ukishakuwa Mbunge, wewe ni mwakilishi wa Watanzania wote, bila kujali kama alikupigia kura au la, na bila kujali chama chake, itikadi yake, dini yake, rangi wala kabila, na bila kujali iwapo ni mkazi wa jimbo lako ama la! HIYO NDIYO MAANA SAHIHI ya kuwa Mbunge!
 
Huyu jamaa anayesema upuuzi.... tunamjua ni shamba boy wa nyumbani kwa jamaa kule bwagamo........
 
haaa! Usiniambie hujaelewa sababu hapo.
Au ulitaka aandike;
sababu ya kwanza.....
Sababu ya pili.......

Sababu ya mwisho......
Nimemaliza.

inawezekana hajaelewa. Si ni wale wale wanaopewa mikataba ya madini wakasaini wanaanza kuulizana kuwa mbona insha haina paragraphs? Si kila kitu kina first,second etc. Hapa tunaamini wee ni Great Thinker unatakiwa kudadavua wala si kumezeshwa!
 
haaa! Usiniambie hujaelewa sababu hapo.
Au ulitaka aandike;
sababu ya kwanza.....
Sababu ya pili.......

Sababu ya mwisho......
Nimemaliza.

....inawezekana hajaelewa. Si ni wale wale wanaopewa mikataba ya madini wakasaini wanaanza kuulizana kuwa mbona insha haina paragraphs? Si kila kitu kina first,second etc. Hapa tunaamini wee ni Great Thinker unatakiwa kudadavua wala si kumezeshwa!
 
Walipogoma CUF zenji mlisema hivyo hivyo subirini 2000 kama watapata seats,wakaendelea kuvipata mpaka mkaamua kuyagawa majimbo,na bado ngoma iko vivi!.2010 wakachukua mkachakachua ili mradi chechemea ibaki madarakani bara na visiwani.
hapo unanyesha jinsi ulivyo mvivu wa kuchambua mambo.
endelea kuamini hivyo kwani ndo mwisho wa upeo wako!

Katiba mpya hailetwi kwa CHADEMA kutoka Bungeni , na hilo lililofanyika la kumkataa RAIS wataalamu wote wa mambo ya siasa wanasema halina athari yoyote kwani Rais na Serikali yake wataendelea na wajibu wao kama kawaida. Nyie Mkisusa wenzenu wala na mwisho wa yote mtarudi kwa huyo huyo JK ili mambo yenu yatengemae.
 
Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.

Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.

Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.

Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.

Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.

Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.

Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.

Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke!



from: - Habari


Hukubali?!. Lazima ukubali kuwa ndiyo hivyo hivyo hakuna tofauti na hivyo.
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?
Kama yupo mpuuzi duniani ni wewe, kuna uhaini gani zaidi ya kuiba kura na kuwafunga wananchi mdomo??wee **** kweli watanzania wengi ndio wanaokataa udhalimu wa jk na sisiem yake iliyochakaa inaongoza kidikteta.
Ni kuulize swali moja wewe uliye mpuuzi wakutupwa...magari ya jk unayosema kayatoa wapi...ni ya watanzania na jk hana lolote, asipokuwepo hayo magari yapo na suala la muda na mtu au chama chochote kikiongoza nchi vitu vyote vinakuwepo.. vipi wewe lofa wa namna gani tena mbumbu wa mwisho.

Nakushauri hapa sio mahali pako nenda kwenye midundiko kama mwenzio jk
 
katiba mpya hailetwi kwa chadema kutoka bungeni , na hilo lililofanyika la kumkataa rais wataalamu wote wa mambo ya siasa wanasema halina athari yoyote kwani rais na serikali yake wataendelea na wajibu wao kama kawaida. Nyie mkisusa wenzenu wala na mwisho wa yote mtarudi kwa huyo huyo jk ili mambo yenu yatengemae.
wewe umekula au unaliwa tuu! Ukiona umekula ujue umeliwa!!
 
Wabunge wa CHADEMA wanapaswa kupongezwa kwa ujasiri wao uliomfanya JK abakie kusema Heee!!!!! na kufuatiwa na smile la kujilazimisha
 
wabunge wa chadema wanapaswa kupongezwa kwa ujasiri wao uliomfanya jk abakie kusema heee!!!!! Na kufuatiwa na smile la kujilazimisha
na heshima itakuwepo tuuu! Uwizi utafanyika lakini kwa wooga! Majambazi wakubwa checheme
 
hivi kwa nini watz waoga namna hii
kilichofanyika jana ni kitendo cha amani na wala hakuna shidA
wametumia haki yao ya msing kabisa

argentina jana bungeni wametwangana makofi huku kwetu watu wametoka kwa amani tu
 
Upuuzi mtupu!

Upuuzi uko wapi, alichosema ni upuuzi au jamii forums ni upuuzi, au Slaa ni upuuzi? Mbona sijakuelewa?

Kama una maanisha upuuzi kwa alichokisema Slaa then nadhani ule mshipa wako wa maji taka umeingilia mishipa ya utambuzi, na in a very plain language wewe ndio mpuuzi. Watu wengine bana, utadhani sio watanzania!!! akha

The message is clear and simple!! sasa kama umeona upuuzi, just keep quite dude, loh
 
Katiba mpya hailetwi kwa CHADEMA kutoka Bungeni , na hilo lililofanyika la kumkataa RAIS wataalamu wote wa mambo ya siasa wanasema halina athari yoyote kwani Rais na Serikali yake wataendelea na wajibu wao kama kawaida. Nyie Mkisusa wenzenu wala na mwisho wa yote mtarudi kwa huyo huyo JK ili mambo yenu yatengemae.


Una utapia-akili. Kama haina athari ya nini mnaumia hivyo. Lakini nataka nielimishwe kama kuabishwa siyo athari. Pia nijue kama atakapokutana na wafadhili (remember umatonyalism uliokithiri) wakamuuliza juu ya demokrasia hakutakuwepo athari. lakini muhimu ujue kwamba CHADEMA wanajua wazi marais dikteta hawajali malalamiko ya watu wao kwa hiyo hakuna jipya kwenye madai yako. Kuhusu kususa na nyie mkala, sioni mantiki hapo. Wasuse wasisuse mafisadi kazi yao ni moja...kumaskinisha nchi.

Finally...move ya chadema ndiyo the best ever au mlitaka wahamasishe vijana kuuana mitaani. All we need is a new katiba na huu ni mwanzo mzuri
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?


NIME KUKUBALI ''STEIN'' HUYU 1954 NIKIMEO KINACHO CHAMBUA MAMBO KWAAKILI YA KUFUATA MKUMBO....HII NISIASA AMBOYO HUENDA SAMBAMBA NA HALI NZIMAYA UCHUMI, SIASA BOM VIONGOZI BOM BASI RAIA NI HOHE HAHE MILELE..HAPA TUNATAKA KUJENGA TANZANIA BORA SIO USHABIKI bana..ETILIJAMAA LINASEMA POSHO YA JK...MASHANGINGI YA JK...HIZI NI KODI ZETU BANA AU WEWE MISHEN TOWN NINI HULIPI KODI....HEBU FIKIRIA 30% PAYEE UNAFIKIRI MCHEZO...BIG UP CHADEMA MPS...UJUMBE UMEFIKA WATAKEWASITAKE.... JUST IMAGINE ATTORNEY GENERAL ANATEULIWA NA RAIS...HAKUNA WAKUPINGA WALA KU COMENT...MWENYELKITI WA TUME YAUCHAGUZI HIVYO HIVYO...HIVI KESI YA KIMA JAJI AKIWA NYANI UNATEGEMEA NINI...TUJENGE TAIFA LILILO BORA TUNA TAKA TUME HURU..KATIBA MPYAAAAA...WANANCHI WANALIPA KODI WEWE UMEJENGA MADARASA YASIONA WALIMU WALA VIFAA UNASEMA ETIUMEJENGA SHULE ALAFU UNASEMA TUKUSIFU KWA MAZURI ULIOFANYA BADALA YA WEWE UWASIFURAIA KWA KUWAKAMUA KODI NA BARA BARA MBOVU NA FOLENI MWANZAO MWISHO...HIZI KODI MNAGAWANA TU....NAKUKUMBUSHA WEWE 1954....BADILI ID YAKO,,, TUPO MWISHO WA 2010...TUNAZIDI KUKUACHA NYUMA...IN 2015 SISI 'M' MTAKUA 'M'TAANI KWELI LAZIMA TUWA PIGE CHINI..NANI KAWADANGANYA ETI VIJANA TAIFA LA KESHO ACHENI METHALIZILIZO PITWA NA WAKATI..VIJANA TAIFA LA LEO..WAZEE TAIFA LA MAPUMZIKO....MUNGU WABARIKI WANA MADIRIKO(WANA HARAKATI) MUNGU IBARIKI CHADEMA.....
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?

JK ni nani mpaka awe na uwezo wa kumlipa mtu yeyote hapa Tanzania. Tafadhali pesa ya Tanzania ni ya walipa kodi. Tatizo ili mnalo nyie watu mliozaliwa miaka ya 57 au kabla. Tanzania ya sasa Rais ni mwajiriwa. Tofauti yeye ana madaraka ya kuwa mwangalizi wa mali ya UMMA. Kwa hiyo hakuna hata wakati mmoja mtanzania yeyote (zaidi ya familia yake JK) atatumia gari au mali ya JK. Na CHADEMA inataka misingi hii ieleweke. Na nyie watu wa karne ya mawe inabidi muelewe Rais siyo mmiliki wa Benki Kuu. Ni mwangalizi!
 
Mwaka ule ambao Rais Keneth Kaunda alishindwa uraisi hakuamini kwamba anaweza kushindwa. Tume ilipotangazwa kushindwa kwake, aliondoka ikulu bila ya kujiandaa na kwa aibu kubwa. Baada ya wiki moja alipanda ndege kuja Tanzania na alipewa nafasi ya kuhutubia NEC-CCM na kuwaeleza kuwa "msiombe kushindwa uchaguzi, ni adha kubwa katika maisha ya kisiasa" na ndio maana ndani ya kiini cha CCM (CCM york) hiyo fikra bado ipo. Unashangaa hata kanuni za uchaguzi zilizoundwa zinaisaidia CCM kushinda hasa katika ngazi ya uraisi. Je ni kwanini kura za uchaguzi wa raisi zisitangazwe majimboni? je ni kwanini matokeo ya uraisi yasipingwe? n.k.

Yaani ili CCM ishindwe ni ile hali ambayo ifanyike ndani yao (inside job) kama walivyofanya akina Mwanawasa kwa Kaunda.

Kususia JK ni haki na pia itafika wakati CCM itakosa njia na lazima itaongea nao. CUF walisusia ikaonekana ni kawaida, CHADEMA wamesusia sasa imekuwa si kawaida. CCM ni wanafiki wakubwa.
 
Back
Top Bottom