Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Ubovu wa mfumo anauogelea Dr. Slaa huu hapa:
Rais anamteua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi; na akishafanya hivyo hakuna chombo chochote huru kinachoweza kuhoji sababu za kumteua au vigezo alivyotumia kumteua! Hapa inaonekana wazi rais anamteua mtu kwa urafiki tu - na haipingiki mahakamani - period.
Uchaguzi ukishafanyika, mwenyekiti huyo wa tume akishatangaza kuwa fulani ndiye kashinda hakuna chombo chochote kinachoweza kuhoji uhalali wa matokeo hayo na hayawezi kupingwa hata mahakamani- period.
Ni wazi basi kuwa watu hawa wawili (au taasisi hizi mbili - serikali na tume ya uchaguzi) sheria imewatengenezea mazingira ya urafiki mbaya. Nakuteua uwe mwenyekiti wa tume na wewe baadaye nitangaze kuwa nimeshinda (na hakuna wa kuhoji hata mahakama).
Ni mazingira haya yaliyoifanya tume ishindwe kusikiliza hoja za Chadema.
Hivi kama kweli JK alikuwa na uhakika kuwa ameshinda, kwanini tume isingesikiliza malalamiko ya Chadema na kuiumbua kuwa inasema uongo.
Mazingira haya ya urafiki wa tume na rais ndiyo yalisababisha kenya ikaingia kwenye machafuko. Kumbuka Kibaki alivyotangazwa na haraha haraka akaapishwa!
Haijalishi wewe ni CCM au Chadema - tunapaswa kudai mfumo huru, siyo tung'ang'anie mfumo mbovu ati kwa sababu tu unatuhakikishia kuwa madarakani.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE