Dr. Shein kuelekea 2015... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Shein kuelekea 2015...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 21, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Inaelekea Shein ni mkimya sana. Makamo wetu wa raisi huyu kwangu mimi ndiye ninayeona anayefaa kuongoza nchi 2015. Hayupo kwenye spotlight sana kama viongozi wengine wakuu. Katika viongozi tulionao mimi naona huyu mzee ni moja kati ya waliyo bora maana haendekezi siasa za jukwaani. Sijui kwa nini yeye hatajwi kati ya moja ya watu wanaoweza kumrithi JK, labda mwenyewe hautaki uraisi. Ukilinganisha na viongozi wengine wanao tajwa tajwa sasa mimi naona so far namsupport Shein for 2015.

  Sababu zangu ni zifuatazo.
  1.Hajaonyesha tamaa wala uchu wa madaraka.

  2.Hana skendo yoyote kubwa anayo tajwa kuhusika.

  3.Haelekei kuwa na makundi

  4.Ni mpole na hapendi spotlight kitu ambacho kinaweza kuashiria he is all action and no talk.

  5.Tetesi niliyo sikiaga ni kwamba 2005 Kikwete alikua na mgombea mwenza wake mwenyewe lakini baada ya majadiliano wakaona kwamba Shein ndiyo anafaa kuwa kwenye tiketi ya chama.

  Sijui kama mwenyewe ana ndoto za 2015 lakini kwenye kundi la sasa yeye anaonekana kufaa kuliko wenzie. Wanaweza kutokea wengine wanaofaa kabla ya 2015 ila kwa sasa nimemuona huyu. Haya ni maoni yangu tu wakuu sijui nyie mna semaje.
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  ..hata ziara zake za mikoani viongozi wa huko wanamuogopa yeye kuliko wengine wote, heshima yake iko juu.
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yes mzee yuko vizuri sasa sijui kama yeye mwenyewe anataka kuwa au ana nia...si lazima uwe na nia kwanza..harafu ukiwa raisi inabidi kwenye kampeni uanze kuongea sana....na yeye ni mzee wa mkasi wake pale anafanya mambo.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini asiingie mwakani?
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Hivi kuna jambo gani ambaye amelifanya huyu mzee mpaka mkadhani anafaa kuchukua uongozi wa nchi? binafsi naona kama ni mtu ambaye ana kosa ushupavu wa kubeba mzigo mzito huu wa nchi masikini na iliyojaa ufisadi. Samahani lakini...mimi naona kama yupo yupo tu.....nielimisheni
   
 6. L

  Limbukeni Senior Member

  #6
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakupendekeza wewe naona unafaa zaidi
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Heshima mbele mkuu. Makamu wa raisi kazi yake ni kumsaidia raisi. Kuna kazi ambazo raisi hawezi kuzifanya zote yeye atapewa na makamu wa raisi. Pia kuna wizara ambazo zipo chini yake. Wewe kwa nini unadhani anakosa ushupavu? Kwa sababu siyo muongeaji au haongei sana kwenye vyombo vya habari? Kumbuka ni makamo wa raisi na kuna mambo ambayo yana takiwa yashikiwe kidete na raisi mwenyewe kama hilo swala la ufisadi. Mimi jamaa naona ni all action and no talk siyo kama hawa wanasiasa wetu wengine ambao huongea sana lakini hauoni chochote.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwa sifa zipi mkuu?
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu. Lakini bado sijapata kitu cha kushika hapo. Kama yeye ndiye anayemsaidia rais, anatakiwa anakolegea rais yeye apakazie. Sawa jamaa sio muongeaje, hiyo siyo sifa ya kuwa rais. Ni kipi hasa ambacho mtu anaweza akasema Shein alikisimamia kikaa vizuri? Huyu mzee ni kama Sumaye, japo yy anaweza akawa sio fisadi lakini hana ile drive na determination ya ku-dare mambo kwa maslahi ya taifa. Huyu alikuwa picked na Mzee Mkapa kwa maslahi binafsi kama alivyofanya kwa Sumaye.
  Tatizo anaweza akawa kondoo kabisa mafisadi wakatamalaki...bado nahitaji kuelimishwa tafadhali.
   
 10. Zwangedaba

  Zwangedaba Member

  #10
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 1, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Mkuu hii kama ni hoja mimi naunga mikono! Aingie mwakani kabsa.
   
 11. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Inaonekana wengi mnaona anafaa! jamani toeni elimu kwa wengine kama kweli ana mshiko....maana wengine tunamuona yupo yupo tu.
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Shein is a good guy.
  Anafaa kuongoza Tanzania.
  Shein 2015!
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu heshima mbele tena. Mimi naona kikubwa ni kwamba as far as we no huyu mzee ni msafi. hajawahi kutajwa kuwa na mambo yoyote ya kifisadi kwa hiyo hamna hata circumstantial proof kuhusu hilo. Katika wakati ambao karibia serikali nzima kila mtu ana skendo inafaa nchi iongozwe na mtu safi.

  Pili hana makundi na haelekei kuwa katika moja ya makundi yanayo gombana ndani ya CCM. Nadhani hili lita saidia kama akipata uraisi haitakuwa rahisi kwake kupachika tu watu kujaza marafiki na kwa ajili haelekei kuwa na mkono au ushirikiano na mafisadi siyo rahisi kutuingizia mafisadi baraza la mawaziri.

  Najua upole si sifa ya uraisi lakini hata uongeaji nao si sifa ya kuwa raisi mzuri na mfano tunao hapo ni JK.

  Lakini again haya ni maoni yangu tu labda wadau watani sahihisha.
   
 14. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MWANAFALSAFA,
  Mkuu, Hizo ndo sifa za Rais anaye faa Tanzania?

  Mbona umerahisisha sana wadhifa huu?

  Rais tunaye anayeifaa Tanzania ni yule mwenye mawazo ya kuibadilisha Tanzania kutoka katika uozo uliopo kuilekea katika maendeleo, na ambaye amejitokeza kuisemea Tanzania na serikali iliyoko madarakani.

  Shein yuko katika serikali iliyoko madarakani, na anakubaliana nayo ndo maana bado yuko madarakani.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ok mkuu kwa hiyo unaona anayefaa yuko nje ya serikali mkuu? Na kama siyo Shein kwa sasa unaona nani mwenye muelekeo wa kufaa kumpokea JK? Kwa sasa mimi naona upinzani kuchukua ni ndoto labda yatokee mabadiliko ya ghafla na ya uhakika otherwise yoyote tutake ishia kumchagua atakuwa ndani ya serikali au CCM. Hapa tuna badilishana mawazo tu ndiyo niya ya thread.
   
 16. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  Mkuu, sijui una maana gani haswa kusema Shein is a good guy...so, anafaa kuongoza Tanzania.

  Nadhani Tanzania inahitaji Rais shupavu, mwenye vision, anayejua tatizo letu hasa ni nini, mwenye ushujaa wa kuchagua watu makini wa kumsaidia katika vita ya kuondoa umaskini na ufisadi na mwenye nguvu na uwezo wa kufanya maamuzi mazito wakati wowote bila kumuogopa mtu yeyote.

  Shein, kwa mtazamo wangu, hana sifa hizo.

  Hana mvuto na kama vile yupo yupo tu. Kwa uelewa wangu mdogo, naona tungekuwa fine tu hata kama cheo cha makamu wa rais kingefutwa. Sasa sijui ni kutokana na udhaifu wa mzee huyu au system iliyopo imemfanya mzee kufichwa
   
 17. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,049
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  PUMBA!!!!Mwinyi,Kikwete na Mkapa walifanya nini mpaka wakaweza kuchukua uongozi wa nchi.Fikiria kwanza kabla ya kuteremsha pumba zako hapa.
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kiongozi Sinyolita,

  Matatizo ya utawala, sio kwa Tanzania tu bali kwa dunia nzima, hayasababishwi na kukosa viongozi wenye vision au lack of good ideas. Matatizo ya uongozi ni kukosekana kwa maadili. Rais hafanyi kazi peke yake, yuko kwenye timu inayounda taasisi ya urais ambayo ndio inayomuwezesha Rais kufanya maamuzi. Mara nyingi (au mara zote) Rais hupata ushauri mzuri wa kitaalam wa jinsi ya kushughulikia mambo, na huwa juu ya Rais na wanasiasa wenzake kama wafuate ushauri huo au lah. Kumbuka mfano wa white paper na mchakato wa serikali tatu.
  Iwapo tutapata kiongozi mwenye maadili yanayomuwezesha kuwa muaminifu kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kuliko kwa ''comrades'' then tutataua sehemu kubwa ya umasikini unaotusumbua.
  Shein mpaka sasa ameonekana kuwa na maadili na uaminifu. Ndio maana naunga mkono wazo la kumpendekeza kuwa kiongozi wa Tanzania.
  Swala kutokuwa na mvuto ni mapema mno kulitolea uamuzi, nafasi aliyo nayo haimuhitaji kujiweka mbelembele, ila kitu ambacho ninaweza kusema ni kwamba watu wanaomfahamu wanajua kuwa ana mvuto ndio maana amefika pale alipo hivi sasa.
   
 19. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  Kamanda ZeM, nina imani watu wengi tunahisi amefika hapo alipo kwa sababu waheshimiwa walitaka mtu asiye na uwezo wa kuwa-challenge, mtu wa 'yes' 'yes' na mtu wasiyemuhofia kwa lolote....

  Frankly, sioni huyu Dr. Chein akipewa nafasi ya kugombea urais whether 2010, 2015 au muda wowote ule!
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tupatie data za hiyo kauli yako
   
Loading...