SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 50,080
- 75,445
Hata sisi watanganyika tunaitaka saaaaaaaaaaaaaaaaaana Tanganyika yetu, adui wa watanganyika ni CCM inayokataa kurudishwa kwa nchi yetu pendwa TANGANYIKA.
Acha chokochoko bora useme kilichosemwa siyo unapotosha ukweli humu, nani amesema Karume ameingia ubia na Maalim seif kisiasa na muungano wa mkataba? 66% wazanziabari walitowa maoni muungano wa Mkataba nani alilazimishwa? au ndo nyie mke si dumeKatika hali isiyo ya kawaida na kuonyesha kuwa uvumilivu unaenda kufikia kikomo,Dr Shein ameanza kufunguka kuonyesha asivyoridhika na mambo anayofanya Rais Msaafu Amani Karume katika masuala ya kisiasa, hususan Muungano.
Amani karume inaelekea ameingia ubia wa kisiasa na Maalim Seif Sharrif Hamad katika kudai Muungano wa mkataba, sera ambayo si ya chama chake cha CCM.
Katika gazeti la leo Nipashe ,9/07/2013 nanukuu:
"Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Katika hali inayoelekea kumlenga mtangulizi wake katika Ikule ya Zanzibar, Rais Ali Mohammed Shein , amesema hawezi kumzunguka Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Mrisho Kikwete kwa kupigia debe Muungano wa mkatabakama mwanavyotaka baadhi ya Wazanzibari
......
Akizungumza huku akionyesha kuchukizwa na kamati hiyo( ya akina Sef Sharrif Hamad na Karume),Dk Shein alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ), haina mawazo wala msimamo bali inachokingojan ni ni mawazo ya wananchi wenyewe kwa vile katiba ni chombo cha umma wenye maamuzi kuhusu Muungano wanao utaka."
Alimaliza
...
Wasiniingize mimi katika mpango wao wala wasitake kufika waendako kwa kutumia mabega yangu,wamelipika sasa walinywe wenyewe"
Huko Zenji mbichi na mbovu za Malim na swahiba wake Amani Karume zinaanza kujitokeza.
Kwa maoni hayo inaelekea ni mliberali weye!Acha chokochoko bora useme kilichosemwa siyo unapotosha ukweli humu, nani amesema Karume ameingia ubia na Maalim seif kisiasa na muungano wa mkataba? 66% wazanziabari walitowa maoni muungano wa Mkataba nani alilazimishwa? au ndo nyie mke si dume
Muungano wa mkataba kwani huu wa sasa hauna mkataba?
Dr Shein ni kichwa kilichokwenda shule, Karume hajasoma japo anasingizia hivyo ila ukweli ni kwamba hajasoma na hajuwi akifanyacho zaidi ya kubwia unga na kulewa. Na ndiyo maana hana msimamo.
Unaonaje muungano na Oman?Zanzibar kwanza
shein km unataka muungano huu uliopo sasa kajenge ikulu dodoma tuachie zenj yetu ww ni kibaraka wa watu wasio na utaifa
Dr Shein ni kichwa kilichokwenda shule, Karume hajasoma japo anasingizia hivyo ila ukweli ni kwamba hajasoma na hajuwi akifanyacho zaidi ya kubwia unga na kulewa. Na ndiyo maana hana msimamo.
Mkuu ulikuwa umesafiri nini hii mada tumejadili humu jf zaidi ya malambili,![]()
Ali Mohamed Shein
Katika kauli inayoekelea kumlenga mtangulizi wake katika Ikulu ya Zanzibar, Rais Ali Mohamed Shein, amesema hawezi kumzunguka Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete kwa kupigia debe Muungano wa mkataba kama wanavyotaka baadhi ya Wazanzibari.
Vile vile, Dk. Shein ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, alisema kamati ya maridhiano inayopinga muundo wa muungano wa serikali mbili, ilikusudia kumgombanisha, kumzulia na kumdhalilisha kwa wananchi na wanachama wa CCM kwa kumhusisha na harakati zao.
Ingawa hakutaja jina la kiongozi yeyote wa Zanzibar mbali tu ya kusema ni Wazanzibari, miongoni mwa viongozi waandamizi wa Zanzibar ambao wanatajwa kuupigia chapua Muungano wa Mkataba ni pamoja na Rais Mstaafu, Amani Karume ambaye anadaiwa kushirikiana vilivyo na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, kushikiza Muungano wa Mkataba.
Dk. Shein aliyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara wa CCM uliofanyika jana kwenye viwanja vya Kibandamaiti Mkoa wa Magharibi Kisiwani Unguja.
Alisema kamati hiyo imepotosha ukweli kwa kutaka kuuaminisha umma kwamba Wazanzibari wengi wanataka Muungano wa Mkataba hali ambayo ingeweza kusababisha mgongano baina ya wananchi, wanachama wa CCM na serikali yao.
"Nilisikia kwa mara ya kwanza kuwapo kwa kamati ya maridhiano na hasa baada ya kusikia Dk. Amani Karume na Maalim Seif wamekutana Ikulu, sikuwa na hofu kwa kuwa natambua umuhimu wa maridhiano, sikujua kama kulikuwa na kamati ya maridhiano ya kudai Muungano wa Mkataba,"alisema Dk. Shein.
Aidha, alisema wakati fulani mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar mwaka 2010, aliombwa na mtu mmoja akutane naye na alipomkubalia mtu huyo alikwenda Ikulu akiwa na watu wengine watano kati yao wakiwamo mawaziri wake wawili.
Alisema walipokutana naye walimweleza kuwa walikwenda kumpongeza kwa ushindi alioupata na kumjulisha kuwa wao ndiyo walioshiriki kuleta maridhiano ya kisiasa na kumkutanisha Dk. Karume na Maalim Seif Sharif Hamad, Novemba 5 mwaka 2009 katika mazungumzo ya faragha kwenye Ikulu ya Zanzibar.
Akifafanua zaidi, alisema kwa mara ya pili walimwendea na kumpa pole kwa ajali ya kuzama meli ya MV Spice Islander, lakini mara ya tatu walikwenda wakiwa na ajenda ya kutaka serikali ya Muungano wa Mkataba na kumweleza kuwa wanamtegemea awasaidie katika madai hayo.
"Niliwaambia wasubiri kuyatoa mawazo waliyonayo kwenye tume ya mabadiliko ya katiba mpya, niliwaambia kwamba mawazo hayo si yangu ila ni yenu na msinitegemee katika hilo, mimi ni Rais wa Zanzibar, nina chama changu na serikali haina mawazo kama mliyo nayo nyinyi hivyo msinichonganishe,"alisema na kushangiliwa.
Dk. Shein ambaye pia aliwahi kuwa Makamu wa Rais katika serikali ya awamu ya tatu, alisema baadaye watu hao walimpa kitabu chenye maoni yao na utetezi wa ajenda wanayoikusudia, lakini aliwaambia kuwa mawazo hayo ni yao na wanapaswa kwenda kuyasema wenyewe.
Akizungumza huku akionyesha kuchukizwa na kamati hiyo, Dk. Shein alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), haina mawazo wala msimamo bali inachokingoja ni mawazo ya wananchi wenyewe kwa vile katiba ni chombo cha umma ndiyo wenye maamuzi kuhusu Muungano wanaoutaka.
Alisema kwa bahati mbaya kamati hiyo ilianza kubeba jukumu la kuwasemea Wazanzibari kuhusu msimamo katika Muungano na kuwataka wakubali mfumo wanaoutaka wao na kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wananchi.
" Wasiniingize mimi katika mpango wao wala wasitake kufika waendako kwa kutumia mabega yangu, wamelipika sasa waacheni walinywe wenyewe,"alisema Dk Shein huku akishangiliwa na wanaCCM.
Alisema yeye amewahi kufanya kazi na kushika nyadhifa za juu katika serikali ya Mungano akimsaidia Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na awamu ya nne, Jakaya Kikwete, hivyo hawezi kuwasaliti na kuwazunguka viongozi wenzake.
"Sitamuogopa mtu yeyote atakaechezea amani ya nchi yetu, hakuna utani katika uongozi wa nchi na amani ya watu wake, tunafanya maamuzi ya pamoja kupitia Baraza la Mapinduzi, asiyeweza aninong'oneze kuwa ameshindwa kunisaidia, mwenye mushkel asisite kuniambia,"alisisitiza Dk. Shein.
Mkutano huo wa vunja jungu kabla ya kuingia kwa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani pia ulihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar Dk. Salmin Amour, Mke wa rais wa kwanza Fatma Karume, mwanasiasa mkongwe Abdulrazaq Simai Kwacha na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ali Ameir Mohamed, ambaye aliposimama kusalimia wananchi alikumbusha haja ya kuyalinda Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Kamati ya maridhainao inayoongozwa na Waziri wa zamani wa SMZ, Mzee Hassan Nassor Moyo, inalenga kutetea Zanzibar kupata mamlaka kamili na kiti Umoja wa Mataifa na kuungwa mkono harakati za Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kiislam wanaotetea Zanzibar ijitenge katika Muungano.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Aboubakar Khamis Bakari, Waziri wa zamani wa Kilimo na Maliasili, Masour Yussuf Himid, Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, Mkurugenzi wa Uenezi na Mwalisilianio ya Umma wa CUF, Salum Biman na mjasiriamali, Eddy Riyami.
CHANZO: NIPASHE