masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,847
- 15,023
hayo yao wenyewe , mimi mtanganyika wa katumbasongwe wala hayanihusu !
Hayo yao wenyewe , mimi Mtanganyika wa Katumbasongwe wala hayanihusu ![/ QUOTE]
Ewe Mtanganyika wa huko Ziwa Nyasa, kumbuka kodi unayolipa kwa biashara zako za Kasumulu ndizo zinazobeba gharama za kuuendesha matumizi na matanuzi ya serikali ya Zenj! Waache waendelee kushoboana huko visiwani hadi wajitoe tupate nafuu yetu!
Ukweli ukoje? Hao viongozi wa Zanzibar waliomtangulia Shein walipokuwa madarakani walishindwa kutoa mawazo yao ya ndani kuhusu muungano kutokana na mazingira ya kisiasa yenye hofu na woga ulioasisiwa na Nyerere kwa misingi aliyokuwa akiitetea! Kuanzia Karume ambaye alimsumbua sana Nyerere kuhusu Muungano hewa, kisha Abood Jumbe aliyetoswa kwa kujifanya jasiri, njoo kwa Salmin Amour aliyewaambia wazi Watz msiingilie mambo ya Zanzibar na OIC, hakuna aliyekuwa anaukubali muungano moyoni mwake! Na Shein akiondoka madarakani huenda akawa wa kwanza kuipokea Zanzibar "mpya na huru"
Hawa viongozi wa zenji ni vigeu geu sana!
Sita shangaa hata na yeye Shein kuupiga vita muungano baada ya kumaliza kipindi chake cha uraisi!
Karume yuko sawa hata sisi Watanganyika tunataka Tanganyika yetu, alafu tufanye muungano wa mkataba ikishindikana tuwe majirani wema kama tulivyo majirani na Kenya,Uganda, Malawi,Zambia,Burundi,Rwanda,Comoro na KongoKatika hali isiyo ya kawaida na kuonyesha kuwa uvumilivu unaenda kufikia kikomo,Dr Shein ameanza kufunguka kuonyesha asivyoridhika na mambo anayofanya Rais Msaafu Amani Karume katika masuala ya kisiasa, hususan Muungano.
Amani karume inaelekea ameingia ubia wa kisiasa na Maalim Seif Sharrif Hamad katika kudai Muungano wa mkataba, sera ambayo si ya chama chake cha CCM.
Katika gazeti la leo Nipashe ,9/07/2013 nanukuu:
"Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Katika hali inayoelekea kumlenga mtangulizi wake katika Ikule ya Zanzibar, Rais Ali Mohammed Shein , amesema hawezi kumzunguka Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Mrisho Kikwete kwa kupigia debe Muungano wa mkatabakama mwanavyotaka baadhi ya Wazanzibari
......
Akizungumza huku akionyesha kuchukizwa na kamati hiyo( ya akina Sef Sharrif Hamad na Karume),Dk Shein alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ), haina mawazo wala msimamo bali inachokingojan ni ni mawazo ya wananchi wenyewe kwa vile katiba ni chombo cha umma wenye maamuzi kuhusu Muungano wanao utaka."
Alimaliza
...
Wasiniingize mimi katika mpango wao wala wasitake kufika waendako kwa kutumia mabega yangu,wamelipika sasa walinywe wenyewe"
Huko Zenji mbichi na mbovu za Malim na swahiba wake Amani Karume zinaanza kujitokeza.
Karume yuko sawa hata sisi Watanganyika tunataka Tanganyika yetu, alafu tufanye muungano wa mkataba ikishindikana tuwe majirani wema kama tulivyo majirani na Kenya,Uganda, Malawi,Zambia,Burundi,Rwanda,Comoro na Kongo
namkubali sana Karume hapendi unafiki.
Naona wewe hujui chimbuko la siasa za muungano.Ukweli ukoje? Hao viongozi wa Zanzibar waliomtangulia Shein walipokuwa madarakani walishindwa kutoa mawazo yao ya ndani kuhusu muungano kutokana na mazingira ya kisiasa yenye hofu na woga ulioasisiwa na Nyerere kwa misingi aliyokuwa akiitetea! Kuanzia Karume ambaye alimsumbua sana Nyerere kuhusu Muungano hewa, kisha Abood Jumbe aliyetoswa kwa kujifanya jasiri, njoo kwa Salmin Amour aliyewaambia wazi Watz msiingilie mambo ya Zanzibar na OIC, hakuna aliyekuwa anaukubali muungano moyoni mwake! Na Shein akiondoka madarakani huenda akawa wa kwanza kuipokea Zanzibar "mpya na huru"