Dr. Salim Ahmed Salim kuwa Obama wa Tanzania 2015?

Nianze na mstari wa chini kabisa, hilo la Autobiography! Hakika wazee wetu katika hili wanatuangusha sana na ndio maana unakuta mambo yaliyotokea kiasi cha miaka 50 tu iliyopita, bado yanakinzana kutoka kwa msimulizi mmoja hadi mwingine!

Tukirudi kwenye suala la ZNZ kubakizwa kwenye utawala wa Sultani na uwezekano wake wa kuwemo kwenye Commonwealth, binafsi nazani dhima kuu ya Mwingireza awali ilikuwa tu kutaka kumwacha Mwarabu aendelee kuwapo pale! Labda inawezekana kv walimuona tayari ameshakaa muda mrefu na ameshaji-establish kama kwake au labda walikuwa na agenda yao! Tusisahau kwamba, hata baada ya Sultan kutimuliwa ZNZ, familia yao walianza kukimbilia Uingereza badala ya Oman walikotkea!

Suala la SAS kwamba ndo alikuwa achukue nafasi ya Mwinyi; sina hakika nalo sana ingawaje ninavyohisi ni kwamba wengi walimtarajia sana SAS kuliko Mwinyi! Na hoja uliyoileta kuhusu Mwinyi kuingiliwa sana na Nyerere nazani ina-prove kwamba Mwinyi hakuwa first choice ya Baba wa Taifa! Wengine wanasema Baba wa Taifa alitamani sana amwachie mtu wake Kawawa lakini bila shaka aliona si busara....akaona ni bora kama uongozi ungeenda ZNZ! Lakini vyovyote iwavyo, hata kama Baba wa Taifa angependa Kawawa ndo awe mrithi wake, bado wananchi wengi walimpenda SAS! Na am very certain kwamba hata Baba wa Taifa mwenyewe nae hakuwa na tatizo na SAS! Kwamba, kama ingekuwa ni kwa matakwa yake, basi SAS kwake angekuwa ni best candidate kuliko Mwinyi! Hata hivyo, alifahamu hali tete ambayo ilikuwapo ZNZ....alifahamu kwamba wanazi wa Mapinduzi hawamtaki SAS!

Suala la Mwalimu kumuingilia Mwinyi siwezi kushangaa hata kidogo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, nazani Mwalimu alishitushwa na kasi ya mabadiliko iliyokuwa inafanywa na Mwinyi. Hii ni sawa na mtu anakuja nyumbani kwako kwa mara ya kwanza na kuanza kupangua pangua mpangilio mzima wa nyumba! Lakini pili, vile vile alikuwa ni mtu ambae hakuwaamini sana wenzake kama wangeweza kuendesha mambo vizuri! Na ndio maana hata kwenye mchakato wa uchaguzi wa CCM 1995, Mwalimu alipigana kufa na kupona kuhakikisha yule aliyemtaka si tu anapata nafasi ya kugombea kupitia CCM, bali pia alihakikisha anaingia Ikulu! Bado taswira ya katuni kwenye gazeti la Majira haijafutika kichwani mwangu ikimuonesha Mwalimu amembeba (kwa mbeleko) Mkapa huku Mkapa nae akiuchapa usingizi mgongoni!! Very funny cartoon!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…