Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 724
- 242
Naamini Watanzania wengi hawaridhishwi na utangazaji wa TBC, na baadhi yetu tuliposikia kuwa Dr Ayoub Ryoba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika hili tukafufua matumaini yetu kwa chombo hiki. Sasa ni muda umepita...je Dr Ryoba bado unajipanga?
Ningependa kuona TBC (hasa televisheni) inakuwa ya kisasa, vipindi vya kusisimua, watangazaji walio makini na kuvutia watazamaji; kushirikisha watazamaji kwa njia ya mtandao wa kijamii wakati wa habari; kuita wataalam au vyanzo vya habari studio wakati wa habari muhimu; kuwa na usikivu mzuri wa sauti; picha kutokwama kwama na kumuacha mtangazaji au msomaji akiwa anatahayari peke yake...
Ikiwezekana studio na au watangazaji wawe na mavazi nadhifu ya kufanana (unifomu) yanayotoa taswira ya taifa letu na utamaduni wetu kiasi kwamba hata mgeni akikuta habari inatangazwa au akifungulia TBC anaweza akagundua kuwa kituo ni cha Tanzania...
Ninakusubiri kwa hamu Mwalimu Ryoba!