Dr. Ryoba bado unajipanga TBC?

Kwa uelewa Mkubwa na wa Kutukuka wa Mwalimu wangu Kipenzi Dkt. Ayub Rioba hana haja ya kukurupuka na kwa nimjuavyo sasa hivi anaandaa vitu ambavyo nina uhakika akiviwasilisha kwa Wafanyakazi wa TBC Redio na Tv Wengi wenu mtaacha rasmi kutizama Tv zingine na kusikiliza Redio zingine na muda wote mtakuwa glued TBC. Sina shaka na Mwalimu wangu na kitendo cha Rais Magufuli kumteua Rioba ni sawa sawa na Rais wa FIFA kumkabidhi TUZO ya World Best Footballer of the year Lionel Messi ( kifupi kipele kimempata mkunaji ). Dkt. Rioba achana na hawa Wanafiki tumia UELEDI wako.

Ukweli ni kwamba huyu Mura Ayoub Ryoba TBC(Radio&TV ) inaonekana ni Viatu OVERSIZE kwake! Tangu ateuliwa sijaona ubunifu wowote zaidi ya vipindi vyao vya ku-bore na visivyo na mvuto!
Nilitegemea baada ya uteuzi angeibadilisha TBC lakini kumbe siyo! Unaweza kuwa mwalimu mzuri darasani lakini ukipelekwa kusimamia au kuongoza Taasisi inakuwa sifuri kabisa!
 
Naskia mkuu wa kaya naye hutazama Cloud TB na kusikiliza Cloud FM tu....usitegemee mapya. Hata Makonda hahangaiki na ka TBC ...Ukweli na Uwazi
 
Naukubali weledi wa Dr. Rioba, ila nina wasiwasi kama anaweza kufanya kazi kwa kiwango chake hapo TBC. Anafanya kazi chini ya wizara na waziri ambaye ajenda yake kuu ni kueneza propaganda ya chama na serikali na kudhibiti upinzani.
 
Back
Top Bottom