Dr. Ramadhani K. Dau amlilia Alhajj Mzee Kitwana Kondo

Dr. Ramadhani K. Dau amlilia Alhajj Mzee Kitwana Kondo

Waislamu Wa nchi hii huwa siwaelewi .

Naona ni dizaini ya watu waishio na chuki mioyoni mwao.

Hasa Wa 'itikadi" Kali ubaguzi Wa wazi wazi ndio utamaduni wao.

Ni jambo la kusikitisha sana .

Angalia wanachoandika ama kukisema kwa mdomo utagundua tu kuna ka harufu ka udini ndani yake .

Wanaji-victimiZe.

Waonekane wanaonewa na kunyanyasa .

Wanataka historia iwabebe .

Wanapenda dezo .

Mbadilike wandugu .
Mkuu nafikiri isome tena hii makala ya Dr. DAU then uyapime maneno yako kama muwala unapatikana
 
Mkuu nafikiri isome tena hii makala ya Dr. DAU then uyapime maneno yako kama muwala unapatikana
Kuna kaharufu hako ndio, tusijifanye vipofu ubongoni. Wenyewe mi ni Mpwani, najivunia hii storia na mzee wetu, ila kulialia na kujiona mtengwa na dhaifu, unanyasisika si falsafa nzuri ktk maisha. Haswa inapoletwa na mtu msomi. Je wa Mzenga wafanyaje?

Mleta mada amejitaidi kuiumba kisomi kuficha udhaifu huu wa kulialia, kwa kutaja Tanzia za mjamaika, ila bado content ya stori nzima si tanzia.
 
Naona mzee ukikosa jibu unamkimbilia sykes aliyekuwa mkristo by nature na Muslim by artificially hapa habari ni za Dau na ukweli kutoka kwa Marehemu KK Kubali tu umeumbuliwa sasa Sykes sijui machado akusaidie kwa lipi hapa? Kk aligoma kuandikwa kihistoria yawezekana hata wazee wengine ndio walivyokuwa maana wanajua mabaya yao ni mengi kuliko mazuri hivyo walipatwa na khofu kuu... ni sawa na kina Mkapa n.k ukiwaweka kwenye mizani ni aibu tupu.

Na uongo mpya tena umeleta hapo juu ati kuwa wengi waliamini TANU haikuwepo hadi alipokuja Nyerere... huo ni uzandiki. Vitabu vya Siasa shuleni vilielezea kila kitu TAA na TANU sababu wahusika karibu wote walikuwapo.. miaka hadi ya 80s huwezi change the history. Utakuwa pekeyako ndio uliamini kuwa TANU haikuwepo hadi Nyerere...
Duduwasha,
Mzee Kondo tukimshawishi sana kuandika kumbukumbu zake na tuliyotaka aandike ni yale
aliyopata kuyajua wakati akiwa katika Special Branch wakati wa ukoloni hadi Tanganyika
ilipokuwa huru na baada ya hapo.

Haya ndiyo tuliyokuwa tukiyataka ayaandike lakini alikataa katakata.

Hicho ambacho wewe unashikilia kuwa nimeumbuka havifanani hata kwa mbali na hii ya
Mzee Kondo kunipa jina la ''mole,'' wa Waingereza aliyekuwa ndani ya TANU.

Lakini ukiwa wewe unaona mimi nimeumbuka hapana neno binadamu lazima tughitilafiane
katika fikra, hatuwezi sote tukaliona jambo kwa mtazamo unaofanana kwani ingekuwa
hivyo hii dunia yenyewe ingechusha.

Sykes Mbuwane aliingia Tanganyika kama askari mamluki akiongozana na Von Wissman
akiwa ni Muislam na alikuja na ndugu yake anaitwa Ali Katini.

Jina hili la Ali ndilo alilopewa Ally Sykes alipozaliwa kwa kumbukumbu ya baba yake huyu.

Hivyo vitabu vya shule na vinginevyo vilivyoandikwa kuhusu TAA na TANU hakuna hata kimoja
kilichaondikwa kwa usahihi.

Huwezi kutafiti historia ya TANU ukaanza na Nyerere 1954.
Inakubidi urudi nyuma kabla yake.

TANU imetokana na African Association ambayo ilibadilishwa jina na kuwa TAA mwaka wa 1948.
African Association iliasisiwa Kleist Sykes mwaka wa 1929 akiwa katibu na historia yake mimi
naifahamu vyema na nimeiandika kwa hiyo imehifadhiwa haitootoa tena na anaeitaka ataipata.

Mwanae Abdul 1950 akaja kushika nafasi ile ile ya katibu aliyokuwanayo baba yake katika miaka
ya 1930 hadi 1940.

Abdul alikuwa na fikra ya TANU toka alipokuwa Burma wakati wa Vita ya Pili ya Dunia na aliporudi
kutoka vitani alihangaika kutaka ndoto yake ile iwe kweli.

Ndiyo maana kuanzia 1950 hadi 1952 alijaribu sana kumshawishi Chief Kidaha Makwaia ajiunge
na TAA ili wamchague awe rais na waunde TANU.

Ikiwa ipo ''version,'' nyingine ya kuundwa kwa TANU mathalan kuwa Nyerere na yeye alikuwa na
mipango ambayo alijadiliana na watu wengine nje ya TAA kuanzisha TANU labda Musoma au
kwengineko na ielezwe ipate kuboresha historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini mimi kwa kauli ya baba yangu amenieleza kuwa yeye mara ya kwanza kumuona Nyerere
ilikuwa nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Abdul akamgusia baba yangu kuhusu
TANU ingawa kwa wakati ule TANU ilikuwa bado haijaundwa.

Kwa kuhitimisha ningependa kukufahamisha kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia ya
TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nimeieleza historia hii kwa mwaliko wa vyuo vikuu viwili Marekani, Chuo Kikuu Cha Iowa na Chuo
Kikuu cha Northwestern University, Evanston Chicago pia na Zentrum Moderner Orient, Berlin na
kwengine kwingi duniani.

Hakutokea hata mtu mmoja katika wajuzi wa historia ya Afrika kunipinga.
Kitabu sasa kina miaka 20 toka kichapwe na hakuna yeyote aliyekuja na historia mbadala.

Chembelecho, nimewafungua watu wengi kamba walizofungwa kwa miaka mingi.

Hii ndiyo sababu katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika mwaka wa 2011 Abdul na
Ally Sykes walitunukiwa nishani ya Mwenge wa Uhuru kama alama ya kuthamini mchango wao
katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Na Wewe tuletee Historia ya Wazee wako wa Nanging'ombe tutaijadili kuitetea na kushikamana!
Mimi najiamini na niko juu ya wastani, sihitaji umoja wa kuabudiana kama kwenye cult ili nitoboe maishani.
 
It wasn't me. Myself nimemuelewa Dr. Dau vizuri. But the old man mohamed said he is always involved in all kind of history of the people's in this country who are in the book of history of the independence of Tanganyika''s after their death he took all response kuwa he kept the secrets of the dead person... thanks to Dr. Dau he knows very well about the dead man... so Mr plod ha's no chance to spread his lies...... we need to stop him because no one has right to change the history
Punctuation
 
May all beings attain enlightenment.

Pole kwa Saku, pole kwa Kibibi, pole kwa familia.

Story za Mzee KK ni ndefu na nyingi. Nakumbuka Rais Mwinyi alivyohadithia kwamba alivyojiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani miaka ya mwanzo ya sabini kutokana na wazee kuuawa kwa kashfa za uchawi Shinyanga (Mwigulu kwa nini hajafuata mfano na kujiuzulu juu ya Kibiti?), basi Mzee Mwinyi akaondolewa kwenye nyumba ya serikali na kuwa na fadhaa kubwa.

Katika marafiki waliomsitiri vizuri sana wakati ule, nafikiri Mzee KK alikuwa wa kwanza. Kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Siku moja nilikuwa na Ndama mutoto ya Ng'ombe "Pedeshee" (wakati huo Ndama tu) mizungukoni Upanga baada ya shule chama kubwa Tambaza, basi Ndama kanishika mkono twende huku twende kule, safari kibao, Mi namdai Ndama hapo na yeye anazunguka mishemishe zake kutafuta hela, nikamwambia twende.

Tukaishia kwa Mzee KK mitaa miwili kutoka shule, Mtaa wa Mtitu kama sijakosea. Basi tumekaa ndani tunaongea nini, Mzee KK kaja nje huko na Benzi lake, amechakarika kafungia funguo za gari ndani ya Benzi. Ndama kutoka ndani na ujanja ujanja wake ule akatafuta waya wa kutundika nguo kujaribu kufungua kioo cha dirisha, lakini lile Benzi lilikuwa na kioo madhubuti. Mzee KK akawa na haraka zake akawa kukivunjilia mbali kile kioo cha Benzi.

Nikaona huyu Mzee mwisho.

May all beings attain enlightenment.

Ha haa..seems to be the good memories from the old good dayz..good for you man!!
 
It wasn't me. Myself nimemuelewa Dr. Dau vizuri. But the old man mohamed said he is always involved in all kind of history of the people's in this country who are in the book of history of the independence of Tanganyika''s after their death he took all response kuwa he kept the secrets of the dead person... thanks to Dr. Dau he knows very well about the dead man... so Mr plod ha's no chance to spread his lies...... we need to stop him because no one has right to change the history

Mzee ulitaka kuonyesha ufundi wa lugha lkn ndo hivyo tena hii kitu ya malkia huwa hainaga urafiki ki hivyo..
 
Naona mzee ukikosa jibu unamkimbilia sykes aliyekuwa mkristo by nature na Muslim by artificially hapa habari ni za Dau na ukweli kutoka kwa Marehemu KK Kubali tu umeumbuliwa sasa Sykes sijui machado akusaidie kwa lipi hapa? Kk aligoma kuandikwa kihistoria yawezekana hata wazee wengine ndio walivyokuwa maana wanajua mabaya yao ni mengi kuliko mazuri hivyo walipatwa na khofu kuu... ni sawa na kina Mkapa n.k ukiwaweka kwenye mizani ni aibu tupu.

Na uongo mpya tena umeleta hapo juu ati kuwa wengi waliamini TANU haikuwepo hadi alipokuja Nyerere... huo ni uzandiki. Vitabu vya Siasa shuleni vilielezea kila kitu TAA na TANU sababu wahusika karibu wote walikuwapo.. miaka hadi ya 80s huwezi change the history. Utakuwa pekeyako ndio uliamini kuwa TANU haikuwepo hadi Nyerere...

Muslim by artificially..haa haaa..bro una mbwembwe!!
 
Kuna watoto Dau kawaonea kwa kuandika habari za "Mwembetogwa" Faya.

Kuna watoto hawajui "Mchafukoge" wapi.

Kuna watoto hawajui Misheni Kota wapi na historia yake.

Ni vizuri ikiandikwa.

Hilo jina la Mwembetogwa limenikumbusha Mchizi mmoja alijilipua ukimbizi Sweden miaka ya tisini. Mtoto wa Upanga tu alikuwa anatafuta kusafiri nakutafuta maisha. Basi kajilipua Sweden ukimbizi. Serikali ya Sweden ikawatafutia sehemu wakae.

Mara Nyerere katika safari safari zake akawa kafika Sweden. Watu wa serikali ya Sweden wakamuuliza, Mwalimu Tanzania inaendaje siku hizi, tunaanza kuona mnatuletea wakimbizi wa kisiasa wanasema kuna mchafuko huko, habari gani hizi?

Nyerere akauliza wako wapi hao wakimbizi? Akaambiwa tulia, tutakupeleka. Nyerere akapelekwa mpaka kuwaona wakimbizi.

Kafanya nao mkutano anawauliza, wewe unatoka wapi? Wewe? Wewe? Alipofika kwa mchizi wangu akamuuliza wewe, jamaa akamjibu Faya.

Nyerere akamaka. Akasema "Faya hapa Mwembetogwa hapa? Hamna wakimbizi hapa".

Akaenda kuiambia serikali ya Sweden hawa vijana wanatafuta maisha tu, hakuna mkimbizi wa siasa hapa.

Serikali ya Sweden ikawapandisha ndege na kuwarudisha Tanzania.

Tangu siku hiyo mchizi ukimtajia Nyerere mnagombana naye.

Nikisikia jina la "Mwembetogwa" siishi kukumbuka hiyo story.
Ila wewe jamaa una mastore sana. Si kujua kuwa Mchafukoge ni mjini kabisa kama ilivyo Mwembetogwa. Nilijua ni huko uzaramoni kwa maana ya nje ya jiji
 
Mji wetu huu. Mjerumani kaja katukuta. Mpaka kanisa la Azania familia imejenga 1903. Kwa hiyo si ajabu kuujua.

Ila nikirudi leo mimi ndiye naonekana mgeni.
Wamejaa wakinga na warombo😀😀😀
 
Wamejaa wakinga na warombo😀😀😀
Ndugu zetu wote hao pia.

Ukiwa na elimu ya watu wa Afrika walivyotawanyika utajua hilo.

Pia, hakuna mji mkubwa unaojengeka kwa kuoana ndugu wa karibu tu na kufungia wageni.

Kuanzia Roma ya Kaizari mpaka New York ya Trump.

Mji mkubwa kuvutia watu mbalimbali ni sifa nzuri. Kiingereza wanasema "diversity".
 
Ndugu zetu wote hao pia.

Ukiwa na elimu ya watu wa Afrika walivyotawanyika utajua hilo.

Pia, hakuna mji mkubwa unaojengeka kwa kuoana ndugu wa karibu tu na kufungia ageni.

Kuanzia Roma ya Kaizari mpaka New York ya Trump.

Mji mkubwa kuvutia watu mbalimbali ni sifa nzuri. Kiingereza wanasema "diversity".
Mkuu nisiwe mchoyo wa fadhira michango yako inautofauti sana hasa ktk mada zenye kugusa hisia kama hizi uko subjective sana. Mkuu hongera sana.
 
Mzee ulitaka kuonyesha ufundi wa lugha lkn ndo hivyo tena hii kitu ya malkia huwa hainaga urafiki ki hivyo..
Kalagabaho mie siku zote husema simlazimishi mtu kuniamini. Ukweli ni kuwa huyo kachero alikuwapo na alikuja kuhusika sana katika matayarisho ya mapinduzi ya Zanzibar na ukipenda naweza nikakupa kisa chake kizima.
 
Kalagabaho mie siku zote husema simlazimishi mtu kuniamini. Ukweli ni kuwa huyo kachero alikuwapo na alikuja kuhusika sana katika matayarisho ya mapinduzi ya Zanzibar na ukipenda naweza nikakupa kisa chake kizima.

Mi nakuelewa sana mzee wangu tena hapa nyumbani nina vitabu vyako kwenye library yangu..wala.sina shaka na wewe
 
Shukran sana kwa Balozi Dafu kutuandikia wasifu wa KK. Mimi sifahamiani na Balozi Dafu pia siyo Muislam wala Mzaramo lakini tulifahamiana na KK na alikuwa mtu mwema kwa ujumla.
Akiwa ameanza kushindwa kutembea bila msaada niliwahi kukutana naye akaniambia maneno ya mwisho vile ingawa sikutambua wakati ule; na ushauri wake ulikuwa: nifanye mambo ambayo moyo wangu unatamani nisije nikafikia umri wake nikawa natamani kuwa ningekuwa kijana ningefanya lile na lile, jambo ambalo yeye halikumsumbua wakati ule akiwa mzee. Ushauri huu pia Steve Jobs yule mwanzilishi wa APPLE computer aliwahi kuutoa wakati wa uhai wake! KK alikuwa akitoa mafundisho ambayo ameyapata katika maisha yake kwa yeyote yote ambaye alipenda kumsikiliza.
KK alikuwa "king maker" kwa watu wengi sana hapa Tanzania. Kwa sababu wenyewe aliowasaidia kupanda hawapendi kusema sipendi kuwaumbua, lakini wengi sana wanatakiwa wamshukuru KK, hata kama vyeo vyao hawakuvitumia ipasavyo.
Pia binafsi sidhani kama kuna mtu anaweza kuandika historia kamili ya KK. Kila mtu alimfahamu KK kiasi kile ambacho KK alimshirikisha au alipata bahati ya kusimuliwa.
Bwana Muhamed Said anasema kweli kuwa KK alikuwa polisi hapo mwanzoni na nadhani ndiyo fani ilimsaidia kujua mambo mengi sana katika jamii, chama cha TANU/CCM na serikali.
Binadamu ye yote hakosi lawama maana hatukuumbwa malaika lakini KK aliwasaidia watu wengi na tena bila ubaguzi. Mwenyezi Mungu ampe faraja katika hali yake ya sasa hapo alipo.
Shukran tena Balozi Dafu.
 
huyu dau ni yupi? ni yule aliyepigiwia kelele sana hapa? au ni mwingine?
 
Back
Top Bottom