Dr Peter Dalaly Kafumu apata ajali

Too low wamloge hili nini?always anayekuwa wakwanza kufikiria imani za kishirikina na yeye ni mshiriki katika hayo mambo kwahiyo anajua mpangilio wake.
 
Tuombeane kheri, suala la ubinadamu libaki kuwa nembo ya Taifa. Poleni wote mliopata Ajali hii, Mungu awape nafuu mapema mrudi kulitumikia Taifa.
 
Huyu jamaa Mwigulu Mchemba ni wa aina gani huyu mtu lile domo lake kubwa linaropoka tu kila leo,huyu jamaa ni mshirikina sana na hawa ndio wanaouwa vikongwe kule kwao huyu t..i...g....o kwao si ndo Singitaa atakuwa na laana ya kuua vikongwe so ile damu ndio inamtafuta na bado we shall see

Kama mganga wa kienyeji ambae elimu ya kawaida hajaenda alafu watu na elimu zao na wengine ni wachumi waandamizi wanashika kile wanachoambiwa na kukisambaza hata kama sio cha ukweli basi usomi wao una shida. Pongezi kwa waganga wa kienyeji kwa kujenga uaminifu kwa wasomi ka Nchemba maana nyie ndi wasomi kuliko wao
 
Barabara bovu limemwangusha mbunge eliyeahidi kulijenga.igunga kaeni macho na wake zenu kama chemba yuko huko.
 
habari za uhakika na zimethibitishwa na mwigulu nchemba mbele ya mkutano wa hadhara nkinga leo jioni.

Kuwa dr dalaly kafumu amepata ajali mbaya maeneo ya kijiji cha mwisi, amelazwa hapa nkinga hospital ameumia kichwani.

Nchemba amehusisha ajali hiyo na imani za kishirikina kuwa ni uchawi wa cdm uliosababisha ajali hiyo.

-------
kutoka kwa kigwangalla:

Dr. Dalaly kafumu amepata ajali ya kupinduka na gari akielekea kwenye kijiji kimoja kilichopo kata ya mwisi ambako alikuwa anaelekea kushiriki mazishi ya mama mmoja maarufu. Ajali hiyo ilitokea jana ambapo gari ilipoteza uelekeo kutokana na hitilafu ya barabara na hivyo kuvutwa, kugonga gema na kupinduka mara moja na gari kukaa matairi juu.

Gari iko nyang'anyang'a huwezi amini kama kuna mtu ametoka salama, lakini tunavyoongea hapa dr. Kafumu na kijana wake ambaye alikuwa akiendesha walitoka salama. Dk. Alibanwa na airbags na walilazimika ili kumtoa kuvunja mavyuma kwa shooka na kumkuta amezimia na alizinduka baada ya muda kidogo, pia alikuwa na bruises zilizokuwa zinavuja damu sana kichwani na alilazwa hospitali ya nkinga na asbh hii atapewa ruhusa arudi nyumbani.

Amekuwa jimboni humo toka jumatatu akifanya ziara ya kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoianzisha, pia kuwaondoa mashaka wananchi kuwa hatowatelekeza kwa kuwa ametolewa ubunge, na kwamba bado yuko nao pamoja tu.

nampa pole sana mtanzani a mwenzetu huyo, na tunamwombea apone haraka. Isipokuwa comment ya mh. Mchemba... That's a very low level of thinking, he has to distinguish himself with a mere layman.

La pili; hiyo comment ya dr. Kigwangala , je mleta habari umemnukuu au umemtafsiri kwa maneno yako? Kwasababu kwa level yake asingeweza kusema " bruises zinazavuja damu sana" kitaalam.. Bruises ni michubuko tu na haiwezi kuwa inavuja damu sana (active bleeding) au la isingekuwa michubuko bali neno lililotakiwa kutumika ni lacerations na sio bruises. Naomba kuwasilisha.
 
Ccm ni kama wameambiwa waongee lolote saa yoyote,mahali popte...yani chochote haijalishi liwalo na liwe.
 
Basi kama CDM wameweza kusababisha ajali kwa dumba ipo siku JK atapata ajali aliyoandikwa na Mungu mtaihusisha na CDM. Jamani tukue tuache ujinga.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hapo kwenye bold ni kweli mkuu au unanogesha story tu ili ipate wachangiaji wengi?

Mkuu ni kweli uchawi umesemwa tena wazi kabisa. na matusi mengine mpaka Jaji aliyehukumu kesi ya Dr kafumu. Kwa mwendo huu na kutumia watu wa aina hii ni kuidhalilisha CCM na Kafumu zitaendelea kumgharimu sana kauli hizi za kina Nchemba.
 
Alienda kukata rufaa yaani haamini kwamba Matusi, Vitisho na Mabaya mengi yaliyo fanyika katika kipindi cha kampen kule ndio chanzo haamini? Basi kama ndio hivyo atakuwa na matatizo ya kuelewa mambo au anataka kufa na ubunge kichwani?
 
Mungu akuponye Dr. Kafumu and may holyspirit's comfort be with you in this difficult and painful moment!
 
Back
Top Bottom