Habari za uhakika na zimethibitishwa na Mwigulu Nchemba mbele ya mkutano wa hadhara Nkinga leo jioni.
Kuwa Dr Dalaly Kafumu amepata ajali mbaya maeneo ya kijiji cha Mwisi, amelazwa hapa Nkinga hospital ameumia kichwani.
Nchemba amehusisha ajali hiyo na imani za kishirikina kuwa ni uchawi wa Cdm uliosababisha ajali hiyo.
-------
Kutoka kwa Kigwangalla:
Dr. Dalaly Kafumu amepata ajali ya kupinduka na gari akielekea kwenye kijiji kimoja kilichopo kata ya Mwisi ambako alikuwa anaelekea kushiriki mazishi ya Mama mmoja maarufu. Ajali hiyo ilitokea jana ambapo gari ilipoteza uelekeo kutokana na hitilafu ya barabara na hivyo kuvutwa, kugonga gema na kupinduka mara moja na gari kukaa matairi juu.
Gari iko nyang'anyang'a huwezi amini kama kuna mtu ametoka salama, lakini tunavyoongea hapa Dr. Kafumu na kijana wake ambaye alikuwa akiendesha walitoka salama. Dk. Alibanwa na Airbags na walilazimika ili kumtoa kuvunja mavyuma kwa shooka na kumkuta amezimia na alizinduka baada ya muda kidogo, pia alikuwa na bruises zilizokuwa zinavuja damu sana kichwani na alilazwa hospitali ya Nkinga na asbh hii atapewa ruhusa arudi nyumbani.
Amekuwa jimboni humo toka Jumatatu akifanya ziara ya kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoianzisha, pia kuwaondoa mashaka wananchi kuwa hatowatelekeza kwa kuwa ametolewa Ubunge, na kwamba bado yuko nao pamoja tu.