Dr. Ngoma na Ocean Road Hospital | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Ngoma na Ocean Road Hospital

Discussion in 'JF Doctor' started by Bulesi, Oct 31, 2009.

 1. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Dr. Ngoma ni mkurugenzi wa hospitali pekee nchini inayoshuhulikia tiba ya maradhi mbalilmbali ya cancer[ saratani] wakati huo huo anaendesha hospitali yake binafsi pia inayoshuhulikia pia tiba ya saratani iliyopo Mwenge ; Je wanajanvi hamuoni kuwa hapa pana conflict of interest? Je dawa zinazotakiwa ziwatibu wagonjwa Ocean Road haziwezi kuishia Mwenge? Mama Blandina Nyoni hana budi kulifanyia kazi swala hili!!
   
 2. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Madaktari wate bingwa wa hospitali za serikali wanatibu pia katika hospitali binafsi, hivyo si vizuri kutoa shutuma kwa Dr. ngoma pekee. Sina hakika kama una ushahidi kuwa Dr. Ngoma anachukuwa madawa pale Ocean Road!!
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ushahidi kama kuna hujuma inafanyika pale Ocean Road utapatikana tu pale uchunguzi wa kina utakapofanyika!! Ikumbukwe kuwa hivi karibuni kifaa muhimu sana cha kutibia wagonjwa wa Saratini kilipotea pale ocean road katika mazingira ya kutatanisha na kwavile kifaa kile kinagharimu mamilioni ya shilingi, ni lazima mtu aliyefanikisha wizi huu anafahamu jinsi ya kukitumia na si hivyo tu fedha nyingi za serikali na wafadhili zinapelekwa pale lakini maendeleo ya hospitali hayalingani na mapesa yanayopelekwa pale!! If a special audit was conducted the truth would come out.
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  There is a clear conflict of interest, sio kwa Dr. Ngoma tu, bali kwa madaktari wote wanaofanya hivi.

  Kwa mfano, Dk. Ngoma akiwa katika position ya ku-recommend ( even with very good reasons) mgonjwa atoke Ocean Road na aende kwenye hospitali yake binafsi Mwenge na watu wakisema kafanya hivyo kwa kujipendelea ili apate biashara atafanyaje?

  Kwa Daktari mkubwa kama huyu kufanya serikalini na wakati huo huo anafanya biashara zake hapo kuna a clear conflict of interest.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Madaktari wengi sana tu na hata Manesi wana hospitali zao, huko unapata madawa ambayo yana LEBO kabisa za Hospitali na Wards za serikali!

  Jana nimemtiBu mwanangu na kichupa cha dawa nilichonunua kwenye duka la dawa la Nesi mmoja kimeandikwa PB/MMH (Paedriatic Block-MOUNT MERU hOSPITAL). sA UTAJIULIZA, DAWA YA WADINI IMEFIKAJE DUKA LA DAWA USWAHILINI-Nikaja kugundua mwenye duka hilo ni Nesi wa M/Meru!
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Nadhani ukiona watu wanalalamika, ujue kuna jambo... Let's wait n see
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is a serious matter, na inawakwaza sana wagonjwa masikini kwasababu there is a clear difference ya service level kati ya hospitali za binafsi na zile za serikali ingawaje watabibu ni walewale... Na utakapojaribu kuliondoa hilo, utaona jinsi huduma za afya zitakavyoyumba

  ...lakini jiulize unategemea nini wakati spika wa nchi anasema posho mbili ni poa tu mbona hata waandishi wanachukua?
   
 8. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mimi mzazi wangu alnaugua cancer sasa tulipoenda ocean road huwezi amini tulilazimishiwa kweli akalazwwe mama ngoma kwani pale wana uangalizi mzuri na per day ni 190k kama sikosei japo sikukubaliana na hilo,yani alale mama Ngoma matibabu ORCI?Hii ni kwa watagonjwa wengi especialy wale ambao hawajui why upelekwe mama ngoma na sio aghakan etc!Conflict of int itakuwepo kama uchunguzi ukifanywa,pia mda wa kufanya kazi za public Daktari ataupunje aende za kwake! well hili linatakiwa kuwa defined tharaly katika ajira za govt
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama uongozi wa Ocean Road cancer centre utaimalishwa nchi yetu haitalazimika kutumia fedha nyingi tunazotumia sasa kuwapeleka viongozi wengi kwenda kutibiwa Apollo India; kwani sio siri kuwa viongozi wengi hasa wabunge wenye umri mkubwa wana matatizo ya prostate na wakina mama wengi wanamatatizo ya saratani ya matiti na kizazi; wakati wabunge na wakubwa wengine wanatibiwa nje wananchi wengi masikini hawana fursa hiyo na wanakufa sana especially sasa wakati imegundulika kuwa wakina mama wengi vijijini wana matatizo ya saratani ya matiti!! Tukiimalisha uongozi na vitendea kazi pale ocean road kazi ya Mewata itazaa matunda makubwa ya kuwasaidia mama na dada zetu wenye matatizo ya vizazi na matiti. Ocean road hospital inahitaji uongozi mpya wenye upeo zaidi ukweli ndio huo tusioneane haya!!
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Dr. Ngoma amekuwa na hiyo hospital kwa muda sasa akiwa na marehemu mke wake (ambaye alifariki kwa maradhi ya kansa).

  Kwa suala la madaktari Bingwa kuwa na hospital au Dispensary zao si ngeni!! Wengi wao wana private consultation in private hospitals na walio na uwezo wana zao.

  Ni mapema mno kusema kuwa huenda wanapata madawa na vifaa vungine ndani ya mahospital wanaotumikia.

  Hili la wao kuwa na private activity, lilitolewa rasmi pale ambapo serikali iliwaruhusu kama njia ya kujipatia kipato zaidi baada ya serikali kushindwa kuwalipa descent remuneration in relation to their expertism.

  Tufanye utafiti wa kina bila kuwatuhumu vinginevyo.
   
 11. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Serikali iwalipe mishahara inayoendana na kazi yao, sisemi wote wataacha but atleast wale rational wataridhika na kipato kimoja.

  Jamani jaribuni kuangalia kazi wanayofanya na mishahara, totally different.
   
 12. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,501
  Trophy Points: 280
  Eh kazi ipo,hapa hatuongelei mshahara kuwa mdogo au mkubwa kilichoulizwa ni mgongano wa kimaslahi,kwani katika kazi zote ukiajiriwa unatakiwa usiwe na mgongano wa kimaslahi na shughuli zako binafsi,hata mimi naona Dr ngoma anafanya sivyo kwani anatumikia vinavyofanana,si ajabu kushawishi wagonjwa wakatibiwe kwake mwenge kuliko ocean road na hata kuutumia muda wa kazi kwa shughuli zake binafsi,je anaposafiri kwenda nje kikazi tuna uhakika gani kama pia hafanyi shughuli zake za kwa mfano kuomba misaada au kununua vifaa kwa ajili ya hospitali yake?ama kwa hakika mama blandina atupie macho hilo
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani kuna mtu au watu wanaochunguza suala la Ngoma? Au wachangiaji wanapendekeza?

  Haiwezekani Dr Ngoma akalaumiwa kuwa na private hospital inayofanya mambo yaleyale anayoyasimamia kwenye umma, kwani ni ruksa serikali ilitoa. Lakini kama anaua ORTC ili ya kwake inyenyuke hapo ni ufisadi. Mlitaka Ngoma ang'oe meno wakati sio fani yake? Mbona mwalimu anafanya tuition na makenika wa Ujenzi serikalini ana gereji yake? Mkulima wa shamba la bwenyenye anaruhusiwa pia kuwa na bustani yake, tumlaumu pia? Secretary wa umma anaweza kuwa na kijiwe cha typing ili mradi haendi kijiweni kwake wakati anatakiwa kuwa kwenye shughuli za umma.

  Madaktari walilalishwa waweke vijiwe vyao ili wasitoroke kwenda nje wakalipwe vizuri zaidi. Nchi zingine serikali haijali kama imekusomesha na unaenda kufungua clinik yako humohumo nchini, sababu unawahudumia wazalendo walewale, tena pengine kwa ubora na kujituma zaidi.

  Leka
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna tuhuma za jumla kwa madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali binafsi; hapa tunazungumzia specifically hospital maalum ya Ocean Road ambayo in spite of fedha nyingi za wafadhili na serikali huduma zake kwa wagonjwa wetu haziridhishi!! Je inakuwaje hospitali ya mwenge inayotibu kwa fedha maradhi yale yale na inaendeshshwa na kiongozi huyo huyo mmoja iwe na tofauti ya huduma? Kuwa Dr. Ngoma alianzisha hiyo hospital zamamni sio issue, tatizo ni conflict of interest ambayo inaweza kumfanya Ngoma akawa mbunifu zaidi katika kuendesha hospitali yake kuliko ile ya serikali na hilo ndio tatizo!! Ndio maana hata wanasiasa sasa inabidi wachague biashara au siasa ili kuepusha conflict ya interest zao. Hakuna ubishi kuwa kwa Dr. Ngoma kuwa Director wa Ocean Road halafu pia kuwa na hospitali inayoshindana na hiyo hapo kuna tatizo ambalo linabidi kutatuliwa haraka ili wananchi wapate huduma stahili. Kwa vile nchi yetu ina utamaduni wa viongozi kuwa mafisadi inawezekana kabisa kuwa dawa za Ocean Road zinaishia Mwenge kwa mkurugenzi!!
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bulesi,
  Huyu Dr. ni Bingwa wa magonjwa ya Cancer. Sasa angefungua Cardiac hospital au vipi?

  Pale Mwenge wakati mke wake akiwa hai walikuwa na maternity home/ward pia (sijui kama bado ipo) na ni kwa kuwa mkewe alikuwa na field hiyo. Kwa Dr, Ngoma atakuwa na cooperative advantage kwa kuwa na project/mradi ambao ana ujuzi nao.

  Cha msingi, tuje na hoja nzito ya ku-prove kuwa huenda anatumia cheo chake au hospital ya Ocean road vibaya kwa ajili ya maendeleao ya hospital yake. Hapo kama tuta-prove hilo itakuwa vema zaidi.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna tuhuma zozote wanazopewa madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali binafsi; hapa tunajadili specically juu ya hospitali ya Ocean road ambayo in spite of fedha nyingi za wafadhili na serikali huduma zake haziridhishi. Wala kwamba Dr. Ngoma alianzisha hospitali yake zamani sio issue; watu wanajiuliza je uduni wa maendeleo wa Ocean Road hospitali vinaweza kuwa na uhusiano gani na mkurugenzi wake Dr. Ngoma kuwa na hospitali yake binafsi inayoshindana na ya Ocean road katika kutibu saratani? Je inawezekana kuwa Dr. Ngoma anakuwa mbunifu zaidi akiwa hospitali kwake Mwenge kuliko akiwa ocean Road na ndio maana huduma za hospitali yake binafsi ni bora? Nchi hii inautamaduni wa viongozi kuwa mafisadi je kuwa mkurugenzi Ocean Road hakuwezi kufanikisha madawa na vifaa vya wagonjwa wa ocean Road vikaishia hospitalini kwa mkurgenzi? Bila kuoneana aibu hapa Dr. ngoma ana conflict of interest ambayo ni lazima irekebishwe haraka ili wananchi wapate huduma wanayostahili. Hata wabunge nao ili kutokuwa na conflict of interest inabidi wachague biashsra au Siasa!!
   
 17. M

  Mchili JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hili ni tatizo la kukosa ethics sehemu za kazi. Hata viongozi walioruhusu madaktari wa hospitali za serikali kuendesha hospitali zao binafsi ni wavivu kufikiri. Walitakiwa wajue kwamba lazima kutakua na conflict of interest, hata jinsi ya kugawa muda wa kazi.

  Ilitakiwa daktari akifungua hospitali yake ajiuzulu kwenye hospital ya serikali ili aendeshe biashara yake kwa ufanisi.

  Na serikali ilitakiwa kubuni njia ya kuboresha maslahi ya watumishi wake na sio kukimbilia kuwaruhusu kufanya part time.
   
 18. s

  shabanimzungu Senior Member

  #18
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jealousy- typical tanzanian disease.............
   
 19. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ushaambiw kifaa kimepotea katika mazingira ya kutatanisha, ushaambiwa kunautata kuhusu watu anaowa recommend kwenda hospitali yake, ushaambiwa akienda nje anatumia hela za serikali kwa shughuli zake binafsi, unataka nini zaidi?
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Umenifanya nicheke, kwani siamini kama Watanzania wengine bado tuna mawazo ya ajabu kama hayo yako!

  Hata kama serikali iliruhusu watu kuwa na kazi zaidi ya moja ikiwa ni pamoja na madaktari kuwa na hospitali au kliniki zao bado hiyo haiufanyi uamuzi huo uonekane hauana kasoro. Siyo kila kitu inachoruhusu serikali hakitakiwi kuhojiwa au kujadiliwa. Uamuzi huo nadhani ulifikiwa kipindi cha Mzee Ruksa (Mwinyi) ambaye pia aliruhusu mambo mengine ya ajabu. Mbona suala la kulipia sikukuu iliyoangukia Jmosi au Jpili lilifutwa?

  Hapa kuna tatizo jingine. Kama Daktari kaajiriwa na serikali tena anayo nafasi nzuri na anaendesha hospitali yake, atawezaje kushindana na madaktari walioamua kujiajiri? Hapo kutakuwa na ushindani usio na usawa (unfair competition). Nadhani hili suala la madakari bingwa kuendesha hospitali zao (tena wakati mwingine muda wa kawaida wa kazi) inabidi lipitiwe upya. Kama ni mishahara midogo siyo wao tu bali ni tatizo wafanyakazi wote.
   
Loading...