Dr Nchimbi ameunda Kamati sio Tume

Katibu Uenezi CCM taifa Nape Mnauye ktk clip hapa chini anakurupuka na kurudia rudia '' Tuiachie Tume ifanye kazi yake'' tizama alivyopotea stepu Katibu Uenezi Taifa CCM na pia Mh. Tundu Lissu akitoa somo la elimu ya uraia kwa wote ikiwemo Nchimbi na Nape


source: Tangibovu wa youtube


Mkuu hivi unadhani Nape alikuwa anafahamu alichokuwa anakisema kweli? Unaonaje uelewa wa yule dogo? Ha ha ha ha!

Hebu msameheni bure, huu mziki mnene kwake - hii issue ni sheria tena level ya Katiba ya nchi na sio ilani au sera za magamba.
 
Last edited by a moderator:
Mbona Nape Mnauye, Katibu Uenezi wa CCM ktk video hapa chini pia anarudia rudia kwa kutamka ' Tuiachie Tume ifanye uchunguzi..........''? na CCM ndiyo yenye serikali na Polisi



Hata Ma RPC wakiulizwa maswali na waandishi wa habari wanasema "iacheni tume ifanye kazi yake siwezi kulisemea jambo ambalo liko kwenye uchunguzi wa tume" Wamechemka wakubali tu!
 
Last edited by a moderator:
Leo nimesikia ambacho bado masikio yangu hajaamini ,imetangazwa kuwa ile iliyoundwa kuchunguza mkasa mzima wa matukio ya mauaji ya Daud Mwangosi(R.I.P) sio tume bali ni Kamati, hiki nikichekesho cha machana kweupe kama viongozi tulionao tena wenye hadhi ya Udaktari basi tunakazi kubwa sana .Zamani kabla ya Uhuru wa vyombo vya habari tulidanganywa sana, jamani hata leo kwenye utandawazi kila taarifa watu wanazo bado tunadanganywa?Hivi hamtaki kukiri kama mlikosea .Waziri wa Mambo ya Ndani tuombe radhi kwa kudanganya kuwa imeundwa tume kumbe huna Mamlaka nayo.

Akiongea profesa au mtu mwenye masters hana tofauti na darasa la pili; "Rev. Msigwa" sasa ndo hii ya huyu Dr. Kilaza. Mpaka 2015, CCM mtakuwa mmehitimu kozi nyingi mnazofundishwa na Chadema hususan Tundu Lissu tena bila ada.
 
ccm wameshikwa pambaya yaani wanahaha kama kuku atafutapo pa kuatangia lakini imeshakula kwao
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ALIUNDA KAMATI SIO TUME

Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa katika kikao chake na Waandishi wa Habari cha tarehe 4 Septemba, 2012, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alitoa taarifa ya kuunda Kamati kuhusiana na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, tarehe 2 Septemba, 2012 ambapo katika vurugu hizo mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi alipoteza maisha.

Waziri Nchimbi alisema aliunda Kamati hiyo, (na siyo Tume), ili kumsaidia kupata majibu ya maswali yafuatayo, ambayo alisema hakuwa na majibu yake:


  1. Nini kilikuwa chanzo cha kifo cha mwandishi wa habari, Bw. Daudi Mwangosi,
  2. Kama upo uhasama kati ya waandishi wa habari wa Iringa na Polisi,
  3. Kama ipo orodha ya waandishi watatu (3) waliopangwa kushughulikiwa na Polisi,
  4. Kama ukubwa wa nguvu za Polisi zilizotumika ulikuwa sahihi,
  5. Kama zipo taratibu zinazoruhusu Vyama vya Siasa kukata rufaa visiporidhika na maamuzi ya Polisi,
  6. Kama kuna tatizo la mahusiano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa.

Taarifa hii inatolewa ili kuweka sawa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tindu Lissu akisema Chama chake hakiungi mkono Tume ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten, kwa madai kwamba imeundwa kinyume cha Sheria ya Tume za Uchunguzi ya Mwaka 1962 Sura ya 29, ambayo alisema kwa mujibu wa Sheria hiyo, tume zote za uchunguzi huundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupitia taarifa hii, tunapenda kuuarifu Umma kuwa Waziri Nchimbi hakuunda Tume ila aliunda Kamati hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kama Waziri na uundaji wa Kamati hii hauhusiani kwa vyovyote na matakwa ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Marejeo ya Mwaka 2002.

Utaratibu wa kutumia Kamati kutafiti jambo kwa kina kwa ajili ya kumshauri Waziri au kiongozi mwingine yoyote ni wa kawaida katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ya umma.


Imetolewa na Isaac J. Nantanga
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
06 Sepemba, 2012

8926605.png

9386909_orig.png


Source: wavuti - wavuti

Huo "Utaratibu wa kawaida wa kuunda Kamati" anaoudai Dr Nhimbi ni kwa mujibu wa Sheria ipi? Je, hao wajumbe wanaapishwa ili wafanye kazi kwa mujibu wa Sheria na kama ni hivyo Waziri ana uwezo wa Kisheria kuapisha?
 
Kiti na kigoda vyote vinafanya kazi moja. Tofauti ni majina tu.
Kwanza manumba kesha sema mauaji yataendelea kutokea huyo ndie mwenyekiti wa kuchunguza mauwaji ya raia wasio na hatia.
 
Tume huwa inaundwa na raisi kwa mujibu wa sheria ya Commission of Inquiry Act, na tume inakuwa na madaraka kama mahakama kuu.Inaweza kumwita yoyote na kumhoji kwa kupewa summons na akikataa anaweza hata kufungwa kwa kuzarau tume. Kamati ya waziri haina madaraka yoyote.Na kwamba haiwezi kumhoji Waziri wala IGP hata kama itaonekana nao wanahusika. Kmati yenye nguvu za kisheria ni Kamata ya bunge na hii inaundwa na bunge.

Mkuu hapa umenisaidia sana, sikujua nguvu au madaraka za kamati na tume za namana hii.
 
kamati ya bunge ni moja ya muhimili of goverment, kama itaundwa inakuwa na nguvu ya kisheria, lakini kamati ya wizara ni lazima isiathiri the mother law, sasa tuangalie ni sheria gani inampa waziri nguvu ya kisheria itakayohusisha judicial?(check and balance) na hapa ndipo waziri alipokosea, kama ataweza awaombe radhi watz

Kama tatizo ni neno ''TUME'' au ''KAMATI'' Nimemsikiliza tena leo speech yake Ebony fm! Na waliirudia makusudi kujua Waziri alitamka nini.
Kwa kumsikiliza kwangu sikusikia Waziri akitamka neno kuundwa ''TUME'' alichokisema ni kuundwa kwa ''KAMATI''
Nadhani kwa hili Lissu AMECHEMKA, af bado wafuwasi wake wanamsupport kwa KUPOTOKA kwake..
 
Kama tatizo ni neno ''TUME'' au ''KAMATI'' Nimemsikiliza tena leo speech yake Ebony fm! Na waliirudia makusudi kujua Waziri alitamka nini.
Kwa kumsikiliza kwangu sikusikia Waziri akitamka neno kuundwa ''TUME'' alichokisema ni kuundwa kwa ''KAMATI''
Nadhani kwa hili Lissu AMECHEMKA, af bado wafuwasi wake wanamsupport kwa KUPOTOKA kwake..

Ni kifungu gani cha sheria alichotumia waziri kuunda 'Kamati' ya kuchunguza kifo? Na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata inasemaje? Kwamba waziri wa mambo ya ndani ataunda 'kamati? Na kamati ita-report kwa nani?

Kwenye statement iliyotolewa na home affairs, waziri anasema ameunda 'kamati' ili impatie majibu ya maswali sita aliyonayo yeye waziri. Where is the IGP in all this? Kulikuwa na haja gani ya kuunda 'kamati' wakati IGP naye anafanya uchunguzi? Waziri hawezi kupata majibu ya maswali yake sita toka kwa IGP? Au DCI ambaye naye anachunguza?
 
Hiyo waliunda Tume sasa wameumbuliwa ndo wanakumbuka shuka huku kumeisha kucha Chezea Lissu makini huyo jamaa
 
Wanabodi, hapa naweka nukuu kutoka gazeti la Raia Mwema, toleo la 257 la tarehe5 Septemba 2012, kumaliza mzizi wa fitina. Vinginevyo, Waziri Nchimbi atueleze kuwa alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari au siku hiyo ulimi wake uliteleza na kutamka tofauti na alichokusudia

"Tume hii itakuwa huru na ya haki, hakuna kupendelewa wala kushindwa kwa jambo lolote lile, na nimeshawaambia ikiwa watakuwa na tatizo lolote la kitaalamu wasisite kuwasiliana na wizara ili tuombe msaada kutoka nje,
" alisema Dk Nchimbi.
 
Mbona kwenye hiyo rejea ya hiyo kamati ya Nchimbi hakuna kuwatambua wauaji ameongelea mambo mengine tu?
 
Hiyo waliunda Tume sasa wameumbuliwa ndo wanakumbuka shuka huku kumeisha kucha Chezea Lissu makini huyo jamaa
 
Hahaaaa viongozi wetu kwa kupenda kukanusha hawajambo. Watakanusha sana mpaka ukifika muda wa kuondoka madarakani
 
Back
Top Bottom