Dr Nchimbi ameunda Kamati sio Tume

ni vizuri viongozi wa serikali kabla ya kutoa matamshi nyeti wakapata ushauri wa kisheria kwanza kwani sheria ya commission of inquiry Act iko wazi kabisa kuhusu tume kuundwa na raisi na si mwingine.Pili kamati ile mbona haijaweka wataalamu wa makosa ya kijinai wa kutosha ili kubaini kama tukio lile lina jinai yoyote au la? hapa nina maana kwamba kwa mtazamo wangu wajumbe hawa wanawakilisha sehemu fulani tu ya watu.

Mkuu hii nchi ingekuwa inafuata kweli utawala wa sheria na uwajibikaji (kama wanavyojiadai) huyu waziri ilitakiwa hadi muda huu awe amejiuzulu.

Miongoni mwa makosa makubwa ni kuingilia mamlaka na madaraka ya Rais. Hili ni kosa kubwa ajabu pengine sawa sawa na mauwaji. Huu ni almost uhaini kwa waziri kusimama hadharani na kutangaza ambacho ni Rais peke yake alitakiwa afanye hivyo.

Lakini lol, serikali inacheka cheka tu.
 
Typical of the Tanzanian Swiss cheese legal framework.From the constitution down to the intricacies of the proclivities disposed to the politburo and its apparatchik.

What is strictly prohibited by one decree, is easily loopholed into legality by another.

Sasa in effect hapa, de facto, tofauti ya Tume na Kamati ni nini?
 
Ndugu zangu, when you critcise you give suggestion this is what Tundu Lisu (Honourable) has done and CCM has copied and paste and this is the type of PHD holder we have in this nation. Tumekwisha ni mpaka CDM iseme ndio wafanye masahihisho na marekebisho humohumo. Mimi sikuwa na chama na sasa nimeshajua where is the right direction and destiny.
Tunaendeshwa kama hatuna baba wala mama utafikiri kuku wa kienyeji?? Tanzania kama hatuamka sasa basi upepo huu ukipita hata Mungu hatutamlaumu kwa sababu yeye yuko tayari ni sisi tu kuamua. Asanteni.
 
Ni jina la hicho kikundi.
 
Wizara imekiri wazir nchimbi ameunda kamati ya uchunguzi na sio tume kama ilivyoelezwa na mh TUNDU LISU hapo jana.

Source Itv habari 8:00pm

my take kama waziri anatuwekea kamati ya nini? Inakuwaje waziri ambaye ndio mwenye mapolisi ateuwe kamati imchunguze ufanisi wake? Tehe tehe tehe! Kazi ipo
 
Ndugu zangu, when you critcise you give suggestion this is what Tundu Lisu (Honourable) has done and CCM has copied and paste and this is the type of PHD holder we have in this nation. Tumekwisha ni mpaka CDM iseme ndio wafanye masahihisho na marekebisho humohumo. Mimi sikuwa na chama na sasa nimeshajua where is the right direction and destiny.
Tunaendeshwa kama hatuna baba wala mama utafikiri kuku wa kienyeji?? Tanzania kama hatuamka sasa basi upepo huu ukipita hata Mungu hatutamlaumu kwa sababu yeye yuko tayari ni sisi tu kuamua. Asanteni.

Hapo kwenye
red; na ndicho CCM wanachotaka eti badala ya kukosoa tu TOA USHAURI kwa Serikali ili iwe rahisi kwao ku-copy and paste kama alivyofanya waziri na timu yake. Ujinga mtupu! Kama hawajui wanachopaswa kufanya wana-hold maofisi ya nini?
 
Tangu jana nilisema humu kuwa Tundu amechemka vibaya sasa muamini kuwa chadema ni wachemfu bangi mbaya sana yaone
 
Typical of the Tanzanian Swiss cheese legal framework.From the constitution down to the intricacies of the proclivities disposed to the politburo and its apparatchik.

What is strictly prohibited by one decree, is easily loopholed into legality by another.

Sasa in effect hapa, de facto, tofauti ya Tume na Kamati ni nini?
Nakupa tu mfano,kamati ni kama zile za maandalizi ya harusi,sherehe tofauti ama hata misiba.Jamaa katolewa nishai na Lissu,sasa kajifungia sijui wapi huko,katoa hii taarifa kuwa si tume ni kamati.Akibinywa tena sijui atasema kitu gani,maana sasa kamati ya nini?kwa pesa za walipa kodi?kwanza kilichokuwa kikiitwa "tume",ni kwasababu ya kupata majibu ya kisiasa,na si prosecutiion,mashitaka yanahitaji tume toka lini na ushahidi nje nje?hata kama kusingekuwa na ushahidi wa wazi,bado mashitaka ya mauwaji hayaundiwi tume au kamati.Only in Tanzania.

Kama walivyosema wachangiaji wengine,tukishazipata hadidu za rejea za kamati hiyo,then tutajuwa malengo yake.
 
Typical of the Tanzanian Swiss cheese legal framework.From the constitution down to the intricacies of the proclivities disposed to the politburo and its apparatchik.

What is strictly prohibited by one decree, is easily loopholed into legality by another.

Sasa in effect hapa, de facto, tofauti ya Tume na Kamati ni nini?
Duh Mr. Kiranga, you dangerous of saying english. it is of you very very tough of the language. me look of the dictionary but, mh, i go empty ofcouse. you study your english of where? tell and me please!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ALIUNDA KAMATI SIO TUME

Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa katika kikao chake na Waandishi wa Habari cha tarehe 4 Septemba, 2012, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alitoa taarifa ya kuunda Kamati kuhusiana na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, tarehe 2 Septemba, 2012 ambapo katika vurugu hizo mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi alipoteza maisha.

Waziri Nchimbi alisema aliunda Kamati hiyo, (na siyo Tume), ili kumsaidia kupata majibu ya maswali yafuatayo, ambayo alisema hakuwa na majibu yake:

  1. Nini kilikuwa chanzo cha kifo cha mwandishi wa habari, Bw. Daudi Mwangosi,
  2. Kama upo uhasama kati ya waandishi wa habari wa Iringa na Polisi,
  3. Kama ipo orodha ya waandishi watatu (3) waliopangwa kushughulikiwa na Polisi,
  4. Kama ukubwa wa nguvu za Polisi zilizotumika ulikuwa sahihi,
  5. Kama zipo taratibu zinazoruhusu Vyama vya Siasa kukata rufaa visiporidhika na maamuzi ya Polisi,
  6. Kama kuna tatizo la mahusiano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa.

Taarifa hii inatolewa ili kuweka sawa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tindu Lissu akisema Chama chake hakiungi mkono Tume ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten, kwa madai kwamba imeundwa kinyume cha Sheria ya Tume za Uchunguzi ya Mwaka 1962 Sura ya 29, ambayo alisema kwa mujibu wa Sheria hiyo, tume zote za uchunguzi huundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupitia taarifa hii, tunapenda kuuarifu Umma kuwa Waziri Nchimbi hakuunda Tume ila aliunda Kamati hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kama Waziri na uundaji wa Kamati hii hauhusiani kwa vyovyote na matakwa ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Marejeo ya Mwaka 2002.

Utaratibu wa kutumia Kamati kutafiti jambo kwa kina kwa ajili ya kumshauri Waziri au kiongozi mwingine yoyote ni wa kawaida katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ya umma.

Imetolewa na Isaac J. Nantanga
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
06 Sepemba, 2012

8926605.png

9386909_orig.png

Source: wavuti - wavuti
 
Nakupa tu mfano,kamati ni kama zile za maandalizi ya harusi,sherehe tofauti ama hata misiba.Jamaa katolewa nishai na Lissu,sasa kajifungia sijui wapi huko,katoa hii taarifa kuwa si tume ni kamati.Akijibinywa tena sijui atasema kitu gani,maana sasa kamati ya nini?kwa pesa za walipa kodi?kwanza kilichokuwa kikiitwa "tume",ni kwasababu ya kupata majibu ya kisiasa,na si prosecutiion,mashitaka yanahitaji tume toka lini na ushahidi nje nje?hata kama kusingekuwa na ushahidi wa wazi,bado mashitaka ya mauwaji hayaundiwi tume.Only in Tanzania.
Kama walivyosema wachangiaji wengine,tukishazipata hadidu za rejea za kamati hiyo,then tutajuwa malengo yake.

Governance by task forces and commitees.

Baba Moi kazitumia sana hizi tactics.
 
Jamani nisaidieni je hii kamati ina uwezo gani wa kisheria katika kupata undani wa tukio la Iringa. Wamesema ni kamati ya kumshauri Waziri Mchimbi na siyo tume eti. Sasa kamati ya kumshauri kitu gani si angeunda alipoingia tu kazini mbona inahusisha wataalam wa milipuko, waandishi na jaji? Nimemdharau kabisa kumbe hatuna watu serikalini; ameniudhi sana
 
Tume huwa inaundwa na raisi kwa mujibu wa sheria ya Commission of Inquiry Act, na tume inakuwa na madaraka kama mahakama kuu.Inaweza kumwita yoyote na kumhoji kwa kupewa summons na akikataa anaweza hata kufungwa kwa kuzarau tume. Kamati ya waziri haina madaraka yoyote.Na kwamba haiwezi kumhoji Waziri wala IGP hata kama itaonekana nao wanahusika. Kmati yenye nguvu za kisheria ni Kamata ya bunge na hii inaundwa na bunge.

Kwa maana hiyo na zile zinazoundwa na Bunge ni magumashi??
 
Back
Top Bottom