Nawapenda sana makamanda wa CDM, ni wazalendo halisi. Hebu fikiria Waziri(!?) mzima ana wasaidizi na maandalizi ya kila aina ameitisha press conference akijagamba kuwa kaunda Tume. Hata alipoulizwa kwama atajuzulu akadai eti "akijiuzulu mtapata wapi waziri (kilaza?) kama yeye..." Then anasimama mwananchi mmoja, msomi kitaaluma, mzalendo wa ukweli anakosoa na kukataa ***** wa Waziri (special).
Ndani ya saa 24, Wizara bila kuomba radhi inakubaliana na hoja ya Mh. Lissu, na kwa unafiki na aibu wanaamua kubadili usemi. Bila kujuliza kama imekuwa Kamati je hadidu za rejea bado ni zile zile?
Je Wajumbe ni wale wale
na mwisho
Je kuna haja ya hiyo Kamati kuundwa?
Jamani wana JF ni kwa nini tusisimame popote tulipo tumpigie makofi ya asante Mh. Lissu kwa dakika moja?