Dr Nchimbi ameunda Kamati sio Tume

Dr Nchimbi ameunda Kamati sio Tume

mgomba101

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
1,822
Reaction score
711
Wizara ya mambo ya ndani imetoa statement kwamba waziri Dr Emmanuel Nchimbi ameunda Kamati ya kuchunguza tukio la kifo cha Daudi Mwangosi na sio Tume.

source: habari za saa{ITV}

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ALIUNDA KAMATI SIO TUME
Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa katika kikao chake na Waandishi wa Habari cha tarehe 4 Septemba, 2012, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alitoa taarifa ya kuunda Kamati kuhusiana na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, tarehe 2 Septemba, 2012 ambapo katika vurugu hizo mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi alipoteza maisha.
Waziri Nchimbi alisema aliunda Kamati hiyo, (na siyo Tume), ili kumsaidia kupata majibu ya maswali yafuatayo, ambayo alisema hakuwa na majibu yake:
1. Nini kilikuwa chanzo cha kifo cha mwandishi wa habari, Bw. Daudi Mwangosi,
2. Kama upo uhasama kati ya waandishi wa habari wa Iringa na Polisi,
3. Kama ipo orodha ya waandishi watatu (3) waliopangwa kushughulikiwa na Polisi,
4. Kama ukubwa wa nguvu za Polisi zilizotumika ulikuwa sahihi,
5. Kama zipo taratibu zinazoruhusu Vyama vya Siasa kukata rufaa visiporidhika na maamuzi ya Polisi,
6. Kama kuna tatizo la mahusiano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa.
Taarifa hii inatolewa ili kuweka sawa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tindu Lissu akisema Chama chake hakiungi mkono Tume ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten, kwa madai kwamba imeundwa kinyume cha Sheria ya Tume za Uchunguzi ya Mwaka 1962 Sura ya 29, ambayo alisema kwa mujibu wa Sheria hiyo, tume zote za uchunguzi huundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kupitia taarifa hii, tunapenda kuuarifu Umma kuwa Waziri Nchimbi hakuunda Tume ila aliunda Kamati hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kama Waziri na uundaji wa Kamati hii hauhusiani kwa vyovyote na matakwa ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Marejeo ya Mwaka 2002.
Utaratibu wa kutumia Kamati kutafiti jambo kwa kina kwa ajili ya kumshauri Waziri au kiongozi mwingine yoyote ni wa kawaida katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ya umma.
Imetolewa na Isaac J. Nantanga
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
06 Sepemba, 2012

Leo nimesikia ambacho bado masikio yangu hajaamini ,imetangazwa kuwa ile iliyoundwa kuchunguza mkasa mzima wa matukio ya mauaji ya Daud Mwangosi(R.I.P) sio tume bali ni Kamati, hiki nikichekesho cha machana kweupe kama viongozi tulionao tena wenye hadhi ya Udaktari basi tunakazi kubwa sana .Zamani kabla ya Uhuru wa vyombo vya habari tulidanganywa sana, jamani hata leo kwenye utandawazi kila taarifa watu wanazo bado tunadanganywa?Hivi hamtaki kukiri kama mlikosea .Waziri wa Mambo ya Ndani tuombe radhi kwa kudanganya kuwa imeundwa tume kumbe huna Mamlaka nayo.
 
kama ile 'kuna bomu lilirushwa' ya kamuhanda
 
Ha ha ha unacheza na Lissu na CDM wewe wamevurumisha sasa wanaanza kuuma maneno ni kamati tena sasa kamati huwa zinafanya uchunguzi au ndio wanataka kujiadhirisha tena
 
ha ha ha sasa iweze ameunda tume ya kuchunguza kifo cha daud mwangosi? Lissu kawaumbua kwel kwel ha ha ha wakishikwa pabaya huwa wanachanganyikiwa akili zinaruka
 
Tayari kuchanganyikiwa ndio kumeanza, CDM tafuteni namna ya kupelaka the Hague mashitaka ya mauaji yote wanayofanya hawa polisi na kutoa visingizio ambavyo havina msingi, mauaji hay sasa ni TOOOOOOOOOOOOOOO MUCH. Lazima kupata njia ya kuhakikisha yanasimama na yasiwepo tena
 
Tume huwa inaundwa na raisi kwa mujibu wa sheria ya Commission of Inquiry Act, na tume inakuwa na madaraka kama mahakama kuu.Inaweza kumwita yoyote na kumhoji kwa kupewa summons na akikataa anaweza hata kufungwa kwa kuzarau tume. Kamati ya waziri haina madaraka yoyote.Na kwamba haiwezi kumhoji Waziri wala IGP hata kama itaonekana nao wanahusika. Kmati yenye nguvu za kisheria ni Kamata ya bunge na hii inaundwa na bunge.
 
kwahiyo hii ni kama guru ya uchunguzi .... haa haaa haaaaa

T.A Lissu atawachezesha kwata mpaka muwe maselule
 
Tume huwa inaundwa na raisi kwa mujibu wa sheria ya Commission of Inquiry Act, na tume inakuwa na madaraka kama mahakama kuu.Inaweza kumwita yoyote na kumhoji kwa kupewa summons na akikataa anaweza hata kufungwa kwa kuzarau tume. Kamati ya waziri haina madaraka yoyote.Na kwamba haiwezi kumhoji Waziri wala IGP hata kama itaonekana nao wanahusika. Kmati yenye nguvu za kisheria ni Kamata ya bunge na hii inaundwa na bunge.

Mdizi says thank you for this useful post
 
Tundu Lissu kweli wewe ni toto tundu, yaani unamuumbua Dr, Prof. Nchimbi mchana kweupeeeee!!! Niliwahi kusikia kuna watu wanaohudhuria shule na watu wanaenda shule kusoma.Wanaohudhuria shule ni wale wanaotumia kichwa kuotesha nywele.
 
Back
Top Bottom