Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

.

Mkuu.mbona unaongea pumba.Ninaishangaza JF?Wewe ni kiongozi wa JF?.Umejuaje kama kila mwana Jf anashangaa?.upeo wako mdogo mzee rudia tena kusoma post zangu.

Kiongozi wa JF yeye anawezaje kujua kuna walioshangaa wangapi? kama hawataamua kuchangia. Wewe umefahamu je kuwa upeo wangu mdogo. Nini kipimo chako cha upeo wa mtu? Mchango wangu ni wa hii post moja husika sijajumuisha post zako zote! Heshima mbele mkuu. Hilo neno halikuwa tusi ungelisoma tena ungeliona kuwa ungeweza kujibu kistaarabu tu ili tuendelee kuchangia mada. Pole sana kwa hilo kama limekulemea sana.
 
.

Mkuu wangu Mpenda tz.
Heshima mbele.Unashangaza sana mzee wangu.kama posho mbili zimeenea serikalini kwa hiyo dawa ni kuzihalalisha?hehehe.Kwa mtaji huu kweli tutafika?
Mkuu simaanishi zihalalishwe, ila zifanyiwe uchambuzi wa kina zilianza anza je na zimeenea kiasi gani na zaidi ya hapo Taifa linayo haki ya kufahamu ni kiasi gani zimeigharimu serikali yaani walipa kodi. Ningelifurahi kusikia kuwa hata hao wanaozilipa wakijua wazi kuwa wanakosea kumlipa Mbunge ambaye analipwa posho nyingine na Bunge nao wameitwa wakahojiwe. That is what i mean, kwa sababu kila mtu anafahamu sasa kwanini hao wabunge wamekuwa targeted. Ndiyo maana mwsiho nimesema wakitoka kuhojiwa wakaishia hapo basi tutakuwa na maswali ya kujiuliza.
 
Kiongozi wa JF yeye anawezaje kujua kuna walioshangaa wangapi? kama hawataamua kuchangia. Wewe umefahamu je kuwa upeo wangu mdogo. Nini kipimo chako cha upeo wa mtu? Mchango wangu ni wa hii post moja husika sijajumuisha post zako zote! Heshima mbele mkuu. Hilo neno halikuwa tusi ungelisoma tena ungeliona kuwa ungeweza kujibu kistaarabu tu ili tuendelee kuchangia mada. Pole sana kwa hilo kama limekulemea sana.
.
Kwanini tuendelee kuwaamini wakati hawatoi matumaini yeyote.Watuambie kuwa tukiwachagua wao basi wataondoa mfumo wa ufisadi.Kelele zote ni Lowasa ni fisadi,RA ni fisadi,sasa hayo ni matumaini?. Sawa Lowasa ni fisadi,swali je akiondoka na RA naye aondoke ufisadi utakwisha ndani ya serikali ya ccm?.Kwann tuwaamini watu hawa?.Jibu ni kwamba ugomvi wao ni kikundi cha watu kukosa kufisadi.
 
Mwakyembe muda wote upo Dar, je lini utaweka kambi Kyela ili ujuwe matatizo ya wapiga kura wako na jinsi ya kuyatatua. Mwaka 2010 huwezi kuwambia wananchi kuwa sikuweza kuja kyela mara kwa mara kwa sababu nilikuwa nawapinga mafisadi.
 
Mwakyembe kahojiwa Jana na TBC1 na kukataa kutoa jibu kama amehojiwa au la badala yake anasema mbona mnaniuliza peke yangu, je mpendazowe kaulizwa?

Naona mwakyembe ameanza kupata kigugumizi.
.

Jana kwenye Kongamano,anasema kuna wabunge zaidi ya 300 na magazeti yanaandika habari yake yeye tu kama amehojiwa au hapana, kwa nini?Jibu analo yeye mwenyewe kuwa kwasababu alikahidi kuhojiwa.
 
Mwakyembe ni kweli hayo unayoyasema?

Mwakyembe atema cheche Takukuru
MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameibuka tena na kusisitiza uamuzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru) kuhoji wabunge ni mkono wa mafisadi.

Madai ya Dk Mwakyembe yanakuja wakati mjadala wa kutaka wabunge wa Jamhuri kuhojiwa kwa madai ya kupokea posho mbili ukiwa umeanza kupoa.

Dk Mwakyembe alitoa tuhuma hizo kwenye Kongamano la Maadili lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana.

Alisema kuwa mpango huo unafadhiliwa na mafisadi ambao wanataka kuwavuruga wabunge ili wasiwe na umoja wa kuwabana kutokana na tuhuma mbalimbali za kupora mali za nchi zinazowakabili.

"Kitendo hicho hakipo katika nchi yoyote ile duniani, huo ni mpango wa kifisadi wenye lengo la kudhoofisha mapambano ya ufisadi," alisema Mwakyembe ambaye ni mmoja wa wabunge waliopo mstari wa mbele kupambana na ufisadi nchini.

Aliongeza kuwa katika taaluma yake ya sheria aliyosoma kwa msaada wa fedha za walipa kodi, hajawahi kuona wabunge wakihojiwa kwa kuchukua posho mbili.

"Mimi ni mwanasheria niliyebobea na niliyefundishwa kwa fedha za wananchi wa Tanzania enzi za Mwalimu Julius Nyerere, sijawahi kuona wabunge wakihojiwa kwa kuchukua posho mbili," alisisitiza mbunge huyo.

Akihojiwa na kituo cha Televisheni cha TBC, baada ya kongamano hilo kama Takukuru imesha mhoji kwa madai hayo ya kupokea posho mara mbili, Dk Mwakyemba hakukubali wala kukataa badala yake alisema anayetaka kujua awaulize Takukuru wenyewe.

"Kuhojiwa wala si 'issue' kubwa, kama mtu anataka majibu sahihi yako Takukuru kwenyewe,"alisema.

Mwakyembe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ambayo ilichunguza kashfa ya Richmond, na kumsababisha waziri mkuu , Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili kujiuzulu, alishawahi kuweka wazi msimamo wake kuwa hayuko tayari kuhojiwa na taasisi hiyo kuhusiana suala hilo.

Mbunge huyo pamoja na wabunge kadhaa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwamo, Mbunge wa Same mashariki, Anne Kilango, Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii na Mbunge wa Kahama , James Lembeli wamejitoa mhanga kupambana na vitendo vya ufisadi. Hata hivyo, mara kwa mara wamekuwa wakilalamika kuwa kuna njama za kuwahujumu katika majimbo yao ili wasirejee katika uchaguzi mkuu ujao.
 
Date::12/12/2009

Mwakyembe atema cheche Takukuru
Na waandishi wetu
Mwananchi

MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameibuka tena na kusisitiza uamuzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru) kuhoji wabunge ni mkono wa mafisadi.

Madai ya Dk Mwakyembe yanakuja wakati mjadala wa kutaka wabunge wa Jamhuri kuhojiwa kwa madai ya kupokea posho mbili ukiwa umeanza kupoa.

Dk Mwakyembe alitoa tuhuma hizo kwenye Kongamano la Maadili lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana.

Alisema kuwa mpango huo unafadhiliwa na mafisadi ambao wanataka kuwavuruga wabunge ili wasiwe na umoja wa kuwabana kutokana na tuhuma mbalimbali za kupora mali za nchi zinazowakabili.

"Kitendo hicho hakipo katika nchi yoyote ile duniani, huo ni mpango wa kifisadi wenye lengo la kudhoofisha mapambano ya ufisadi," alisema Mwakyembe ambaye ni mmoja wa wabunge waliopo mstari wa mbele kupambana na ufisadi nchini.

Aliongeza kuwa katika taaluma yake ya sheria aliyosoma kwa msaada wa fedha za walipa kodi, hajawahi kuona wabunge wakihojiwa kwa kuchukua posho mbili.

"Mimi ni mwanasheria niliyebobea na niliyefundishwa kwa fedha za wananchi wa Tanzania enzi za Mwalimu Julius Nyerere, sijawahi kuona wabunge wakihojiwa kwa kuchukua posho mbili," alisisitiza mbunge huyo.

Akihojiwa na kituo cha Televisheni cha TBC, baada ya kongamano hilo kama Takukuru imesha mhoji kwa madai hayo ya kupokea posho mara mbili, Dk Mwakyemba hakukubali wala kukataa badala yake alisema anayetaka kujua awaulize Takukuru wenyewe.

"Kuhojiwa wala si 'issue' kubwa, kama mtu anataka majibu sahihi yako Takukuru kwenyewe,"alisema.

Mwakyembe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ambayo ilichunguza kashfa ya Richmond, na kumsababisha waziri mkuu , Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili kujiuzulu, alishawahi kuweka wazi msimamo wake kuwa hayuko tayari kuhojiwa na taasisi hiyo kuhusiana suala hilo.

Mbunge huyo pamoja na wabunge kadhaa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwamo, Mbunge wa Same mashariki, Anne Kilango, Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii na Mbunge wa Kahama , James Lembeli wamejitoa mhanga kupambana na vitendo vya ufisadi.

Hata hivyo, mara kwa mara wamekuwa wakilalamika kuwa kuna njama za kuwahujumu katika majimbo yao ili wasirejee katika uchaguzi mkuu ujao. Habari hii imeandaliwa na sadick Mtulya na Claud Mshana
 
Kimsingi simwelewi Mwakyembe. Kipindi kile alipokataa kuhojiwa alikuwa anaongea hadi povu linamtoka mdomoni kuwa hata wamsulubishe msalabani hatakubali kuhojiwa. Sasa kama alikubali kuhojiwa ndo nashangaa.

Haki ya nani siasa ni unafiki tu
 
Hawa wanasiasa wa bongo sometime huwa hawaeleweki...
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4833

MBUNGE wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe amesema Rais Jakaya Kikwete ndiye anayefaa kuongoza nchi na ni mhimili mkubwa katika vitaya ufisadi ila baadhi ya wasaidizi wake wanamrudisha nyuma katika vita hiyo.
Alisema hayo jana katika kongamano la miaka 10 Bila ya Baba wa Taifa lililoandaliwa na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchinina kufanyika katika Chuo cha Ustawi Jamii (ISW).
Mwakyembe alikuwa akijibu swali la mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesoma shahada yaelimu, Chagona Deogratias aliyetaka kufahamu iwapo hoja alizokuwa akitoa Dk. Mwakyembe katika kongamano hilo alikuwa akiogopa kumsema Rais.
0‰9E0”2Mimi kwangu namuona Rais anafaa kuongoza0‰9E0„7bali tunapaswa tumuondolee baadhi ya watu wanaomchafua,0‰9E0•2 alisema Dk. Mwakyembe huku akiwataka watu wasimfikirie vibaya anapotoa hoja zake kuwa ni mbwembe bali anajiamini kutokana na elimu aliyonayo na hivyo anajivuna.
Alisema kuwa wananchi kwa ujumla wanapaswa kumsaidia Rais Kikwete katika mapambano ya ufisadi na vitendo vingine viovu katika jamii ili nchi ipige hatua za maendeleo.
Akizungumzia suala la mikataba mibovu, Mwakyembe alidai imekuwa ikisababishwa na ushamba wa wataalamu wetu katika masuala ya mikataba hali ambayo inaigharimu nchi na kuchangia kurudi nyuma kimaendeleo.
Kwa upande wake kada wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) aliyeshiriki katika mkutano huo Nape Nnauye, alisema kuwa kelele za ufisadi zinazopigwa nchini na baadhi ya watu hazimaanishi kwamba nchi nzima imeoza, bali kuna baadhi ya matatizo yanayotakiwa kushughulikiwa ili yasizidi na kuenea na hatimaye kuidhoofisha nchi.
Alisisitiza umuhimu wa kukomesha rushwa wakati wa kugombea nafasi katika uchaguzi mbalimbali la sivyo taratibu za uchaguzi zitaendelea kuharibika na kuwaasa wenye tabia hizo waache.
Mbunge wa Kishapu kupitia CCM Fred Mpendazoe, alisema kuwa umasikini unasababishwa na uongozi mbovu na kushauri miiko ya uongoziipewe kipaumbele.
Katika hatua nyingine alisisitiza umuhimu wa kuongezeka kwa viwanda vingi vya usindikaji wa vyakula na matunda kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ili falsafa ya Kilimo Kwanza itekelezwe kwa vitendo.
 
Inashangaza wala haiingii akilini kuwa Dr. mzima, anasema JK ni muhimili wa vita ya ufisadi. Ndiyo huyohuyo anasema kuwa kuhojiwa kwakwe na Takukuru kuna mkono wa mafisadi.

Sasa hawa mafisadi wanatoka wapi wakati JK amewafagia?

Hivi hawa mafisadi wangekuwa jela, leo hii Mwakyembe angeongea hayo? haoni kuwa ,mafisadi kuwa free ni failure ya yeye mwenyewe na serikali yake ya JK anayoisifia.

Huwa nasema hakuna msafi CCM watu mnatoana povu humu kutetea akina Mwakyembe!!!!!!1
 
Back
Top Bottom