Dr. Mwakyembe unaheshimika lakini kwenye hili umeteleza vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe unaheshimika lakini kwenye hili umeteleza vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kavulata, Aug 3, 2012.

 1. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,165
  Likes Received: 1,532
  Trophy Points: 280
  Dr. Mwakyembe ni kati ya watu wachache nchini wanaoheshika nchini lakini kwa hili amejipunguzia maksi.

  Nilikusikia mwenyewe Waziri wa Usafirishaji bungeni ukisema kuanzia septemba madereva na abiria hakuna kuchimba dawa njiani. Hivi umefanya utafiti wa kutosha kuhusu hili? Sababu ulizotoa za kusitisha uchimbaji dawa sio sahihi kwa sababu hata kule kwenye vyoo mabasi yanakosimamaga kwa chakula bado watoto na watu wazima wanachanganyika wakati wa kujisaidia kitu ambacho sio maadili yetu. Hali kama hii pia inapatikana sehemu zenye mikusanyiko mingi kama kwenye viwanja vya mipira, sabasaba, n.k. tofauti inakuwa huku kuna vyoo vya wanawake na wanaume lakinini pia hakuna vyoo vya watoto na watu wazima wa jinsia tofauti.

  Lakini pia lazima ujuwe kuwa kutokana na sababu za kiafya ama hali ya hewa dereva na abiria wanaweza kushikwa na haja ndogo ama kubwa wakati wowote na popote. Hali hii ikimtokea dereva anapaswa kusimama achimbe dawa vinginevyo umakini wa kuendesha chombo cha usafiri utapungua na ajali zitaongezeka. Mfano, abiria mwenye ukonjwa wa kisukari huwa anahitaji kukojoa kila mara sawa na yule aliyepatwa na mchafuko wa tumbo anavyohitaji kwenda kuharisha kila mara. Pia watoto na mama wajawazito huwa wana vibofu vinavyojaa mkojo mapema hivyo kuhitaji kujisaidia mara kwa mara.

  Hivyo basi, ili amri yako ya kutochimba dawa iheshimike lazima yafuatayo yatimizwe kwanza:
  1. Vyoo vya njiani vijengwe kila baada ya umbali mfupi
  2. Wagonjwa, watoto na mama wajawazito wasisafiri kwenye mabasi
  3.Dereva mwenye kisukari asiendeshe gari la abiria, maana akichimba dawa zake njiani na abiria watashuka kuchimba za kwao
  4. Gari likiharibika njiani litasababisha abiria wachimbe dawa hapohapo, hivyo basi, vyanzo vya kuharibika magari njiani kama vile uingizwaji matairi feki nchini, rushwa za matrafiki njiani, kujaza abiria na mizigo kupita kiasi, injini za malori, n.k vishughulikiwe kwanza
  5. Uboreshwaji wa huduma za chakula njiani ili kuzuia abiria wasipate michafuko ya tumbo njiani
  6. Mabasi yawe na vyombo vya kujisaidia njia (urinal bottles and bed/bus pans) ama yawe na vyoo

  Vinginevyo shughulikia kwanza vyanzo vya ajari barabarani na majini, fufua usafiri wa treni, ongeza ndege badala ya kurukia mambo madogomadogo yasiyofanyiwa utafiti wa kina. tatizo la wananchi sio kuchimba dawa njiani bali.......
   
 2. k

  kachwamayebe Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si dhani kama aliwahi kusafiri kutoka DSM hadi mz,mara au kagera akijionea pori lililopo kama kweli linasubiri kuchimba dawa ktk vituo maalum
   
 3. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Duuh, kweli jamaa kakurupuka. Kwenye Richmond alifyatuka hivyo hivyo, kwani ile hoja yake utekelezaji uko wapi?
  Mimi nilisafiri siku moja, kumbe chakula nilichokula Pale ubungo kikaniletea mchafuko wa tumbo, jamaa yangu acha wewe tabu niliyopata. Huwa naona aibu lakini siku hiyo sikuwa na aibu kumwambia konda gari likasimamishwa kwa ajili yangu.

  Wanasiasa wetu wanakurupuka tuu.
   
 4. S

  SEBM JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mleta mada,

  Nakupongeza sana kwa kuwa umeibua upya mada hii ambayo haiwezi kupita bila kuchangiwa. Kauli ya Mh. Mwakyembe imenipa mashaka sana kuhusan juu ya washauri wa viongozi wetu na namna viongozi wetu wanaopokea huo ushauri.

  Nimewahi kusafiri, kwa mfano, na basi la Dar Express kutoka Karatu hadi Dar Es Salaam. Siku hiyo ilikuwa ya kihistoria sana, kwani nami pia nilikuwa nimeambatana na mtoto wa miaka 6. Kijana wangu alikojoa Karatu wakati tunajiandaa kuanza safari, lakini kwa kujibana sana, alivyofika Arusha aliomba tena kuchimba dawa. Bahati mbaya tulipoondoka Arusha, alipanda dada mmoja ambaye alikuwa anasumbuliwa na tumbo...basi kwa uchache tulisimama vituo vifuatavyo kwa ajili ya kumsaidia aweje kujisetiri 1. Maji ya Chai 2. Moshi 3. Mwanga 3. Same 4. Hedaru 5. Bwiko 6. Mombo 7. Korogwe 8. Kabuku 9. Manga 10. Msata 11. Vigwaza 12. Kibaha.

  Tunamshukuru sana yule dereva wetu - Askofu - kwa msaada wa dawa za miti shamba ambazo zilipunguza adha kidogo kwa yule mlengwa. Sasa namshangaa Mh waziri kwa kauli yake hii (bahati mbaya sikubahatika kuisikiliza hotuba yake yote; niliishia pale alipokuwa anawapa big up masela zake akina Mwandosya, Mh. Rais anayetekeleza Ilani ya uchaguzi)
   
 5. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,949
  Likes Received: 6,706
  Trophy Points: 280
  Jamaa siyo siri kachemka, kwa kuwa anajua yy anaendeshwa kwenye V8 kwa hiyo hajui kuwa hiyo mikweche tunayopanda huwa inaharabika anywhere, hivi basi likiharibika kichakani, bado abiria watatakiwa wajizuie hizo haja zao hadi wafike kwenye kituo chenye choo cha kulipia! hivi keshafanya utafiti kwa mfano toka Dar hadi Mbeya, kuna vyoo vingapi vya kulipia? Jambo la msingi ni madereva kumpuuza huyo mheshemiwa kwa kuwa upo uwezekano kale kataulo alikojifutia pale ofisini kwake hadi kumsababishia aende Apolo-India kutibiwa, huenda vile vilivyonyunyizwa kwenye hako kataulo bado vinamuaffect!
   
 6. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Alikuwa anatafuta umaarifu wa bei rahisi, hata wabunge wenzie hawakumpigia makofi kwa ujinga wake, Shughulika na maswala yanayowasumbua wananchi, daladala zinakatiza root dsm cjawahi kusikia kauli yako....heshima imekushuka mwakyembe, kila mwananchi anakucheka...halafu vp wale walikuwekea sumu uliwshawasemehe au ndo ulikuwa upepo?
   
 7. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe anataka kubadiri methali msafiri kafiri, sasa itakuwa msafiri mstaarabu! inamaana kutajengwa toilet za watoto
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  mwakyembe unaheshimika?speak for yourself dude!!!don't countme in..i despise this man
   
 9. l

  lubaga Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu wanapenda kutizama kinyesi ,hakuna jambo lisilo weza kutafutiwa ufumbuzi ,watanzania tusiwa wavivu wa kufikiri na kuthubutu kukabiliana na changamoto
   
 10. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Msameheni bure jamani, mbado kupona sawasawa
   
 11. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Kwanza uwatoe barabarani hawa pilisi ambao wanasubiri gari imetoka bus stand tu wanaisimamisha si wangeifuata huko?? Au mmetoka tu hotel kula wanaisimamisha! Haya mengine mungu atatusaidia.
   
 12. k

  kamandamakini Senior Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii ni ajabu kabisa eti Mwakyembe analaumiwa kwa hilo,yani mnataka kuendelea kujisaidia porini, aibu sana kwa mleta mada, acheni ushamba wenu,

  Swala la kujadiliwa hapa ni kuongeza kasi ya kujenga vyoo na kuhimiza watu wajenge utamaduni wakujisaidia pale kwenye vituo wanapokuwa wanakula chakula,

  Kwa mfano iwekwe utaratibu kuwa kutoka Iringa mpaka dar gari litasimama labda Mara mbili kwa nusu saa na watu watapata fursa ya kujisaidia ,duniani Kote wanafanya hivyo.

  Ni watu wasiostarabuka wanajisaidia porini, tubadilike Jamari.
   
 13. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60
  Mi nafananisha na speed governor ambayo mpaka kesho hifanyiwi kazi au ile sheria ya kukonyeza ....eti umebaka hahaha....nji hiiii hahahaha

  ...This is not practical...!!!
   
 14. T

  Temboric Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe ana hoja ya msingi kabisa, kwa wale waliowahi safiri kwa Green Star Dsm-Mby wamejionea ustaarabu wa kutojisaidia maporini Gari inasimama sehemu yenye vyoo tu.

  Sehemu za kuchimbia dawa ni zile zile zimekuwa chafu hakuna anayejali, vinyesi vimetapakaa hovyo inakera sana...nenda nchi zinazotuzunguka kuna vyoo na pembezon mwa barabara kuna hata vifaa vya kutunzia taka.

  Bongo watu wanatupa taka hovyo.
   
 15. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mimi mwanzoni nilidhani kuwa Mwakyembe ni mtu makini kumbe wapi! Sikutegemea kama angekurupuka bila ya kufanya utafiti kwanza ili kujua kinachowafanya wananchi kuchimba dawa. Je mabasi ya vyoo? Je baada ya km ngapi barabarani kuna vyoo?Mwakyembe umakini umepotelea wapi? Appolo nchini India?
   
 16. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Je hapa TZ hayo mazingira ya kuwezesha watu kujisaidia kwenye vyoo tu yapo? Ndiyo kukurupuka kwa Mwakyembe tunakokusema.
   
 17. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anza na mzizi wa tatizo siyo matawi. Huwezi kukurupuka kupiga marufuku watu kuchimba dawa kabla hujawatengenezea mazingira kwanza ya kuacha kuchimba dawa. Mimi ningemwelewa kama angeanza ni kujenga miundombinu kwanza ili watu wasichimbe dawa porini badala ya kukurupuka kupiga marufuku kabla ya kuandaa mazingira kwanza.
   
 18. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kavulata, kwa uchambuzi wako huu ningekuwa dhaifu(jk) kesho ningepiga chini Mwakyembe then ungelamba nafasi yake ya uwaziri! Well Done!
   
 19. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Serikali Imeshindwa kujenga vyoo mijini itaweza kujenga vya maporini?
   
 20. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Miminikotofauti kabisa na wewe, Swala la kusimamasimama njia ili kumsaidia mgonjwa wa tumbo sio tatito la waziri wa uchukuzi. Hilo ni tatizo la wizara ya afya.

  Mgojwa kama huyu hakutakiwa kusafiri kabisa siku hiyo badala yake alitakiwa aelekee hospitali.. Na kama Uginjwa ulimuanza njiani basi alitakiwa apelekwe kituo cha afya kinachofuata tangu ameanza kuumwa.

  Pia kwa jinsi hii kazi kubwa inabidi ifanyike ya kuwaelimisha watu umuhimu wa uhai dhidi ya safari, je huyo mgonjwa angefia kwenye gari mgefanyaje?
  Pia nyie mnaopenda kulakula kila kinachouzwa njiani nawashauri muache. Jitahidini sana kula vitu vikavuvikavu sio kwa ajiri ya kushiba bali ili kutuliza njaa na kurudisha nguvu mwilini, vitu kama Snacks na juices au maji kdogo.
   
Loading...