Vyoo vya migahawa ya barabarani ni vichafu vina hali mbaya

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Habari waungwana,

Nalileta kwenu hili na kwa wahusika wa migahawa yote nchini ambayo inapatikana kwenye barabarani kubwa za mikoani na za kwenda nje ya nchi.

Ni jambo la kawaida tunaposafiri kwenda haja (kuchimba dawa) na kununua vyakula katika migahawa hii iliyopo pembezoni mwa barabara kuu.

Hata hivyo jambo kuu linalotusimamisha kutoendelea na safari ni suala la kwenda kuchimba dawa (haja), hivyo dereva husimamisha bus katika migahawa husika na kutangaziwa kupewa dakika tano mpaka kumi za kwenda haja na kula.

Mara nyingi tunaposhuka kwenye bus abiria wa mabasi mbalimbali huenda moja kwa moja chooni kwenda kuchimba dawa ila tukifika huko vyooni tunavikuta vyoo viko kwenye hali mbaya.

Yaani huwa kuna harufu kali ya mikojo, maji hamna, nzi wamezagaa, mtu hauwezi kwenda haja kubwa, mlindikano wa watu hali hii si nzuri kiafya kwa sisi watumiaji na wasafiri wa mara kwa mara kwa haya mabasi.

Madereva wa mabasi wanatakiwa watupeleke kwenye migahawa yenye hali ya usafi wa vyoo na mazingira. Mabwana afya hii hali hawaioni au kuna namna inaendelea?

Migahawa ilioko Msamvu, Gairo na ile ya barabara ya Morogoro - Iringa kwa wanaoenda Mbeya hali ndio ni mbaya sana.

Wahusika wa migahwa na serikali wasimamie hii hali tusijepata Magonjwa ya mlipuko.
 
Inatakiwa vyoo visimamiwe na watu wa usafi kila nusu saa
Ila sasa, unakuta mtu kasimama nje ya Choo anakusanya hela tu na zingine ni bure lakini ni pachafu mpaka kero

Ila na watu wachafu sana
 
Back
Top Bottom