Dr. Mwakyembe: Sikumhoji Lowassa kwa sababu ushahidi dhidi yake ulikuwa unajitosheleza!

Dk Mwakyembe, Nassari wapimana






Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari
IN SUMMARY
  • Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.


Nilitafuta sana jinsi ya kuuliza maswali yangu KUNTU juu ya mada hii naamini leo nimepata sehemu husika;
Mosi, nisikitike kwa kauli ya mwalimu wangu Mwakyembe kwa hiki alichokisema bungeni, nimeshangazwa sana sana.
Pili. Mwalimu Mwakyembe baada ya sakata la Richmond alialikwa na mwalimu wangu marehemu Dr. Mvungi kuja chuo kutupigia kidogo mambo ya Ministerial, individual responsibility katika serikali.. Hizi ni principles katika Constitutional law.
Katika lecture yake ambayo naikumbuka ilikuwa na mbwebwe nyingi alisema Waziri mkuu ni mteule wa rais na kwamba amethibitishwa na Bunge hivyo kwa kamati yake iliyokuwa imeundwa TU na BUNGE haikuwa na mamlaka ya kumwita na kumhoji Lowassa kwa sababu alikuwa mkubwa kwa uwezo wa kamati ya Bunge. Alitupia vifungu kadhaa kutoka kwenye Katiba. Kwa kuwa nilikuwa bado kinda nikamwelewa nami nikaridhika Lowassa kweli FISADI na atakiwi kuhurumiwa. LOOH! Hakuwa na kifungu chochote cha ku back up argument hii ila tukaendelea maana ufisadi ndo ulikuwa wimbo kipindi hicho.

Baadae nimekuja kujifunza na kusoma issues za NATURAL JUSTICE nikapata maswali mengi sana juu ya kilichomkuta Lowassa! Principles za natural justice za Right to be heard,nRule against biasness ni vitu vya dhamani kubwa katika sheria na kesi nyingi nimeshuhudia mahakamani waajiri wakishindwa kwa kosa tu dogo...denied right to be heard or biasness or kushindwa kumpa mtu sababu za termination. Ila nikajiuliza Lowassa shida yake nini?

Juzi tena Mwalimu Mwakyembe anaibuka anasema walikuwa na ushahidi LUNDO kwa hiyo hawakuwa na sababu ya kumhoji Lowassa! My goodness. Bora umeenda michezo kwa bongo movie nadhan panakustahili maana ungeweza kuleta sheria polisi wakiwa na ushahidi lundo kwenye kesi basi huyo mtuhumiwa HASISIKILIZWE apigwe mvua ya miaka gerezani.
Mwalimu inakuwaje basi umefundisha watoto pale chuo leo ni mahakimu wengine majaji na wengi mawakili kuhusu natural justice na rule against bianess na right to be heard na fair hearing na evidence na mambo ya cross examination za evidence halafu leo unasema ulikuwa na ushahidi mwingi ambao hakukuwa na sababu za kumwita Lowassa, kweli?

swali langu kwa Mwalimu Mwakyembe
Je Wazir mkuu hapaswi kusikilizwa kwa sheria ipi? Naomba majibu please.
 
Mzee ametuingiza Gizani mpaka TANESCO wameshindwa kuwasha Umeme KARIMJEEE. KARMA is real
 
Back
Top Bottom