Nimeguswa kuamsha topic hii hapa JF ili kuomba wahusika kupitia JF watupe ukweli.
Nimeguswa na mwandishi Mwambo wa Raia Mwema pale anaposema "Serikali iseme ( iueleze umma) ugonjwa unaomsibu Dr. Mwakyembe Ama ikishindwa kuueleza umma sasa (akiwa hai , na tunamuombea maisha marefu)BASI endapo ikatokea Mpendwa wetu huyu Mungu akampenda zaidi, chochote Serikali itakachosema kuhusu afya yake Watanzania ha watakiamini", it's either NOW or NEVER!
Kwa ujasiri wa dokta nitumie fursa hii kumuomba atujulishe nini kinachomsibu endapo Serikali itakaa kimya.
Kwa nini tunataka ukweli wa hili?
Ni kwa sababu moja tu, inaelezwa kwamba kuna mchezo ulichezwa, kwamba kuna ka kitu alipewa kakapelekea ugonjwa huo. Ni nani aliyemchezea kamchezo hako?, Ni kwa nini alifanya hivyo?, Nini chanzo cha chuki iliyopelekea ukatili huo?
Kama jamii mambo ya hovyo kama hayo ya kuzimishana kwa sumu( kama tetesi zilizopo ni za kweli) tunapaswa kuyakomesha, kama ni kweli basi kwa aliyefanya hivyo katukosea watanzania wote.
Wanaomjua wamtaje, naye akisha tajwa aombe toba kwa Mungu, kwa watanzania na kwa ndugu yetu pendwa, Dr. Mwakyembe.
Kwa Dr. Mwakyembe niseme tu, usikate tamaa, pambana, Mungu yuko upande wako!
Atakuponya.
Atakulinda.
potokaz