Dr. Mwakyembe, muda wako umefika

Dr. Mwakyembe, muda wako umefika

Mzee Tupatupa wa Lumumba,

Inaonekani Viongozi wakuu ccm na vibaraka wao wanamchukia Lowassa kwa mengine si ufisadi, Lowassa kajiudhulu 2008 na toka kujiuzulu kwake kumetokea wizi mwingi na wa kutisha kama Escrow, kashfa ya Mwakyembe ya Mabehewa na sasa report ya CAG ya upotevu wa Bil.600, ambao hatulaumu na wala hatuongelei kama richmond na hasa jinsi familia kuu ilivyonufaika na Escrow. Tupo kimya kwa sababu tumejaa unafki na woga na kupenda kujipendekeza.

Inashangaza waliopo serikalini na waliohusika moja kwa moja na uchafu huu ndiyo wa kwanza kuita wengine fisadi:shock: hakyanani Nyani haoni kundule! Mbona sioni mtu akimsema wazi Kikwete kwa uchafu kwa mapungufu yake na kashifa zake, si ni yeye mkuu wa nchi!!!! Wenye akili tunajua kuunganisha doti na kupata majibu juu ya yaliyotokea kwenye richmond na escrow na tunajua ni nani hasa mnufaikaji mkuu.

Viongozi wakuu wa ccm wamejaa unafiki, wivu na chuki dhidi ya Lowassa. Sasa limewafika, Inashangaza JK na Kinana nao wanamuita Lowassa fisadi na wenye akili kushangilia:angry: ni aibu na kuonesha ni namna gani tulivyo wanafki, waongo, wenye kujipendekeza, wajinga na wenye mtindio wa Ubongo. Eti amechafuka! wao ni wasafi? nani kati yao hana kashfa!!! hata ya Hosea hatujasahau na yale ya suti pia.

Laigwani kasema hakubali kufa na mzigo wa mtu; liwelo na liwe na ngoma inogile:tonguez: Tupatupa jiandae kuhama magogoni
 
Ndio maana nasubiri kuamua nampigia kura nani nikiwa ndani ya chumba cha kupigia kura.

Nchi yangu ya ajabu ya hakunaga kwa majanga na binadamu wengi wanasomea shule za chuki na matu.si

Huyu nae aliachia ngazi mara...hakuhusika haya ni wale wale wanalengwa na kujisafisha huku ili apite kugombania uraisi.

Kumekucha maana wa TZ hata hawajaona makosa yake wanataka aingie nao waibe kama yeye atakuwa raisi huruma kama kawa.
 
KUTUBANDUA ? tumegua gogo la mti?

kama wewe ni mtoto wa mjini au mzaliwa wa mjini basi huwezi kusema hujui maana ya hilo neno ila kama ndiyo kwanza umetoka kijijini kwenu mbwinde lazima utalishangaa tu hilo neno
 
Ni kweli alisingiziwa jamani..maananzile documents na madokezo kama katibu mkuu wa baraza la mawaziri alizokuwa anashauri Richmond ipewe mkataba akijua kabisaa ni kampuni hewa pia amesahau ni moja ya hujumaa. Sasa kama unashuri serikali na hasa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri hutakuwa na maslahi nalo. Alafu baadae inafahamika kuwa mshirika wake mmoja ndio msimamizi wa Dowans bongo hapa. Duuh Lowasa angekubali yaishe akae kimya. Suala la Richmond lisijibiwe kisiasa sababu limeshaiumiza nchi mnoo. Mwakyembe ajinyamazie maana ndani ya miaka sita hii amechafuka vibaya.
 
Mzee Tupatupa wa Lumumba,

Inaonekani Viongozi wakuu ccm na vibaraka wao wanamchukia Lowassa kwa mengine si ufisadi, Lowassa kajiudhulu 2008 na toka kujiuzulu kwake kumetokea wizi mwingi na wa kutisha kama Escrow, kashfa ya Mwakyembe ya Mabehewa na sasa report ya CAG ya upotevu wa Bil.600, ambao hatulaumu na wala hatuongelei kama richmond na hasa jinsi familia kuu ilivyonufaika na Escrow. Tupo kimya kwa sababu tumejaa unafki na woga na kupenda kujipendekeza.

Inashangaza waliopo serikalini na waliohusika moja kwa moja na uchafu huu ndiyo wa kwanza kuita wengine fisadi:shock: hakyanani Nyani haoni kundule! Mbona sioni mtu akimsema wazi Kikwete kwa uchafu kwa mapungufu yake na kashifa zake, si ni yeye mkuu wa nchi!!!! Wenye akili tunajua kuunganisha doti na kupata majibu juu ya yaliyotokea kwenye richmond na escrow na tunajua ni nani hasa mnufaikaji mkuu.

Viongozi wakuu wa ccm wamejaa unafiki, wivu na chuki dhidi ya Lowassa. Sasa limewafika, Inashangaza JK na Kinana nao wanamuita Lowassa fisadi na wenye akili kushangilia:angry: ni aibu na kuonesha ni namna gani tulivyo wanafki, waongo, wenye kujipendekeza, wajinga na wenye mtindio wa Ubongo. Eti amechafuka! wao ni wasafi? nani kati yao hana kashfa!!! hata ya Hosea hatujasahau na yale ya suti pia.

Laigwani kasema hakubali kufa na mzigo wa mtu; liwelo na liwe na ngoma inogile:tonguez: Tupatupa jiandae kuhama magogoni

Ulimuuliza Laigwani sijui kwa nini hapendi kuzungumzia UFISADI hata kulaani japo kidogo kama wanavyofanya hao wenzake japo nao wanafisadi..eti nakuuliza tu. Maana tunahitaji raisi anayechukia ufisadi kwa vitendo na sio kwa nadharia tuu.
 
Anaanzia wapi kujibu mapigo ya Lowassa? Alipokwenda kumuomba Lowassa Msamaha alirekodiwa vizuri sana! Ndo maana mwenyewe ametamka kuwa hana visasi nao tena!!! Huyo aliefura amekuwa CHURA? kufura bila kuongea kuna maana gani?.. Ukweli ndo huo kuwa baada ya Lowassa kutoka madarakani kwa Zengwe la Sitta, Mwakyembe na Membe; Serikali ya Jakaya imekuwa kama imekosa msimamizi katika kila Nyanja!!! Waalimu walifaulisha watoto zaidi ya 5000 wasiojua kusoma wala kuandika! Wamejitengenezea uhasama ambao unawafanya watibiwe nje ya nchi kwa kuwaogopa Madaktari waliowang'oa meno na kucha, Wanafunzi hawana mikopo ya elimu ya juu, Biashara ya Sembe imeshamiri, UJANGILI umeshika hatamu, UFISADI umetamalaki si kwenye mikataba ya kishenzi bali hata kwenye ESCROW, Bandari, Mabehewa ya Trani hadi kwenye BVR ... Albino wanaendelea kuangamia!!! Wasaidizi wa JK wanaendelea kung'ang'ania madaraka pamoja na kushindwa ku-deliver huku wakigeuka PANYA RD ... Fedha za Misaada ya Ghadaffi plus Change ya Rader imegeuzwa kuwa ya kampeni za kumuingiza JOKA la MDIMU madarakani ...
MAJIBU YA MWAKYEMBE HAYA HAPA....

Akihojiwa na mwandishi wa vyombo vya habari vya UHURU waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki ameonekana kufura kutokana na madai yaliyotolewa na Edward Lowassa leo kutokana na sakata la Richmond.

Dr. Mwakyembe amemfananisha Edward Lowassa na 'mshenzi' huku akidai kuwa anateswa na mzimu wa urais!

Hali halisi inaonyesha kuwa sasa CCM kumeibuka vita ya aina yake na inaweza kuisambaratisha vibaya CCM!

Lowassa leo ameonekana kuishambulia vilivyo serikali ya Kikwete kwa kudai kuwa yapo makosa yaliyofanywa katika serikali hiyo!

Hali sasa imefika pabaya!
 
Mwakyembe aanze na lile la mabehewa feki kwanza.. Atuambie ushiriki wake,

Nilishamfuta kwenye orodha ya watu wa maana baada ya kupingana na maandishi yake mwenyewe kwenye Bunge Maalum la katiba!!!
 
Hao ccm tumewazoea ni mabwana mipango hao,hapo labda walishajadir jinsi ya kusafishana sisi wananchi tunachezeshwa maboya tu.Ccm si mchezo wanamaigizo mengi sana Jamaa hawa.
 
ccm nimekuwa ninaitumikia,wazazi wangu wote wameipigania ccm mpaka umauti wao,Leo mtu mmoja aliyeichafulia ccm ndio tena awe raisi?Hakika chama kikimpitisha sisi hatutapiga kura.

Sera na siasa kai wa wazazi wako ni toauti na hali ilivyo leo hii. CCM ya leo inabariki na kukumbatia ufisadi na mafisadi. CCM ya wakati wa Wazazi wako haikuwa hivyo. Jitambue
 
mwakyembe Sitta Lowassa , Kikwete ni kati ya wana CCM wenye rekodi mbaya hawana uadilifu ni majambazi wa fedha za umma, wabadhirifu, walanguzi , walewa madaraka na mafisadi , hakuna wakumsafisha mwenziwe wananchi tunawajua hayupo msafi CCM lowassa hafai kama hao wasivyofaa
 
Mabehewa machakvu tutayajadili yatakapojengewa hoja na kuletwa mezani. Hata kama yatafunikwa lakini tutafanya liwezekkanalo tupate namna gani yameathiri taifa na wahusika wa athari zile wawajibishwe.

Lakini kuwepo kwa suala la mabehewa chakavu, halifuti ukweli na uhalisia wa ufisadi wa Richmond. Kinachonisikitisha ni watu waliozowea kula vilivyooza hata hawaoni kinyaa. Wanaona kwao ni halali. Lowasa alimwambia Kikwete kwamba yote aliyoyafanya yeye Lowasa Kikwete alikuwa anajua. Tena akasema isingekuwa busara (Usaliti wanaita busara) ya mzee Mkapa, hata Kikwete aasingekuwa raisi. Kwa kumaanisha kwamba si lowasa wala Kikwete mwenye usafi wa kusema uchafu wa mwenziye. Na kwa vile wote wachafu ila Kikwete alifichiwa uchafu wake na Mkapa, wanyamaze wafichiane siri, maisha yaendelee.......!

Leo wewe unaleta nadharia ile ile kwamba kwa kuwa Mwakyembe naye kachafuka kwa mabehewa, anyamaze kimya, amlinde fisadi lowasa wa Richmond, asiseme lolote ili maisha ya kubebana na kulindana ndani ya ccm yaendelee.!!!.
Huko ni kuzowea kuishi kwa kula mizoga na kuiona ni halali!.

Ukweli ni kwamba, Mwakyembe sasa aweke mambo yote hadharani hata aliyosema yeye Mwakyembe, na Lowasa juzi kayamung'unya kwamba yakisemwa itakuwa shida. Kama ni shida Watanzania tumepata shida ambayo haijawahi kuwepo Tanzania kwa sababu ya ccm na hakuna shida itakayokuwa kubwa na ya kuuimiza kuliko maisha tuliyonayo itakayotokea kwa ajili y akusemwa ukweli wa Richmond.

Kuendelea kuficha ficha kwa kuwa eti wote ni wachafu walindane, ni kuzidisha hasira za Watanzania na kuwazidishia maumivu ya kudharauliwa, kuibiwa, kusalitiwa na kudhalilishwa!.

Na kama wataendelea kulindana, kwa kuwafanya Watanzania wote wapumba.vu, watakuja kuelewa ninalolisema!. Tanzania si mali y accm wala si mali ya mafisadi. Kulilndana kwenu hakuwasaidii kwalolote.




Hana hoja mzee wa mabehewa na vichwa chakavu
 
MIMI NISHAURI TU mwakyembe ni waziri Lowasa ni mbunge tu na wote tunajua amepunic na mbio za urais so haitakuwa busara kwa mwakyembe kumjibu huyo msaka madaraka tujiulize ilikuaje ameondolewa kwenye Uwaziri mkuu tokea miaka hiyo aje aseme leo hizi ni mbinu za kutaka kutafuta pa kutokea na hatolewi mtu as long as ameanza na mbio hizo basi aendelee kusudi aje aone mwisho wake hatuwezi kuongozwa na rais kama lowassa asifikirie kabisa.
 
Lowassa fisadi aliyekubuhu yaani rostam ndio wakutupangia nani awe raisi wetu haikubaliki
 
Watanzani tusaidiane kukumbushana mambo na kupeana elimu ya uraia katika kipindi hichi ili kufifisha ujinga katika vichwa vya walio wengi. Kumbuka ujinga sio tusi, kila mtu ni mjinga, na tafsiri ya ujinga ni hali ya kutojua suala au jambo fulani. Hivyo ujinga una ukombo, lakini upumbavu hauna ukoma sababu umezaliwa nao.

Sijui neno gani litumike kwa wasahaulifu sijui "poyoyo" au ni gani?
Dr.Harrison Mwakyembe katika BUNGE LA KATIBA alisanda, alijificha na kukana maandiko yake. Kama Tundu Lissu alivyotawala hadhira kudadafua jinsi wanaCCM walivyozoea kuishi kwa uwongo uwongo, undumila kuwili na unafiki.

Dr.Mwakyembe alipata udaktari baada ya kuitimisha kwa utafiti kwa andiko aliloamini kwa akili yake yote, kwa moyo wake wote SERIKALI YA SHIRIKISHO ndio dawa ya MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibari. Lakini hakupanua mdomo wake kueleza lolote katika lile bunge.

Ikiwa safari hii atajipiga kifua na kujitokeza mbele kuongea kuhusu RICHMOND, atakuwa ametumwa kwa maslahi ya na mabwana wakubwa lakini sio dhamira yake, sio uzalendo wake, sio kwa kuguswa na msukumo wa nafsi yake.
Watanzania Tusibadilishe Matairi, Tubadilishe Gari. Tuachane na CCM safari hii UKAWA
 
Muda wako umewadia. Muda wako wa kusema ukweli zaidi. Lowassa amekuchokoza leo mjini Dodoma. Amedai kuwa yeye hakuhusika na Richmond. Sakata la Richmond, I mean. Amedai kuwa sakata hilo lilitungwa na kulenga Uwaziri Mkuu wake tu.Hakukuwa na zaidi. Kwa maana nyingine, Dr. Mwakyembe na Kamati yako teule ya Bunge mlitunga kashfa ya Richmond. Yaani,Dr.Harrison Mwakyembe na Kamati yake ni wazushi na waongo!

Dr. Mwakyembe, umepata nafasi adhimu na adimu isiyo na msimu. Nafasi ya kusema hata yale ambayo hukusema Bungeni Dodoma ulipokuwa ukiwasilisha Ripoti ya Kamati yako. Ukweli juu ya sakata la Richmond. Kama Lowassa ameruhusiwa na chama na Serikali kusemea kashfa hiyo, wewe na iliyokuwa Kamati yako hamzuiwi. Mkinyamaza,mtasadifu ukweli wa jina la waongo na wazushi mlilopewa leo hii Dodoma.

Ukiwa nguli wa tasnia ya Sheria, Dr. Mwakyembe panga hoja zako nawe uzungumze na watanzania. Kama huna pesa ya kukodi ukumbi,waite waandishi hata nyumbani kwako. Watakuja na kukusikiliza. Muda wa kulinda heshima yako huu.Kama Lowassa kamwaga mboga, wewe Dr. Mwakyembe mwaga ugali.

Liwalo na liwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Naam; "PANAPOFUKA MOSHI; PANAFICHA MOTO"; Dr Mwakyembe; maneno yanaumba!! Usipozijibu hizi tuhuma nzito kutoka kwa Edward basi tutakuwa hatuna jinsi bali kusadiki kwamba wewe na kamati yako kuhusu kashfa ya richMonduli; mliiasisi; mkaitengeneza na kumlipua mwenzenu kwa nia Chafu ya kumkosesha U-PM!! funguka baba!
 
Kama anawajua si angewashitaki.usiwe mvivu kufikiri

Je kuhusiana na habari hii polisi walimuhoji kama walivyoahidi? mimi na wewe nani mvivu wa kufikiri?

Jeshi la Polisi limejipanga kumhoji Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya ameibua tuhuma nzito dhidi ya Polisi, Usalama wa Taifa, wanasiasa, wafanyabiashara na waganga wa kinyeji, akidai kwamba wamepanga kumuua. Katika orodha hiyo, pia amewahusisha watu kadhaa anaodai kuwa ni Wasomali kutoka katika kundi la Al Shabaab.

Kuhojiwa kwa mwanasiasa huyo kunatokana na taarifa yake ya maandishi aliyoipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Februari 9, mwaka huu.

Mwanasiasa huyo ameeleza mlolongo mrefu wa kishirikina ambao anadai kwamba umefanywa ili "kuwapumbaza Watanzania wote" baada ya yeye kuuawa ili wasiwe na akili ya kuhoji mauaji hayo.

Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini kuwa Februari 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi.

Siku moja baadaye, Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. MTANZANIA imefanikiwa kuipata taarifa hiyo kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wizarani ambako iliandaliwa. Ina nembo ya Serikali na anuani ya Wizara ya Ujenzi. Baadhi ya watu wanaotajwa kwenye taarifa hiyo tumehifadhi majina yao kwa sababu za kitaalum kwa kuwa bado MTANZANIA inaendelea kuwasiliana nao ili kupata ukweli.

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, "Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe


"Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

"Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha "abiria" hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.

"Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a "Master", Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

"Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda "kulogwa" safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

"Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

"Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga' Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni' hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa'. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

"Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

"Kufuatana na ‘mganga' Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza "waliohukumiwa kifo" (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

"Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu' hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028&#8230😉 na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Ushiriki wa Al Shabaab

"Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).
Aelezea
"Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati' wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

"Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. "Utabiri" huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.

"Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu' yamefanywa:

"(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa "maandalizi" hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
"(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

"Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a "Master" na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

"Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.

"Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

"Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.

"Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).

"Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH."

Dk. Mwakyembe anaongeza, "Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

"Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

"Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

"Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi' niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji."

 
Je kuhusiana na habari hii polisi walimuhoji kama walivyoahidi? mimi na wewe nani mvivu wa kufikiri?

Jeshi la Polisi limejipanga kumhoji Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya ameibua tuhuma nzito dhidi ya Polisi, Usalama wa Taifa, wanasiasa, wafanyabiashara na waganga wa kinyeji, akidai kwamba wamepanga kumuua. Katika orodha hiyo, pia amewahusisha watu kadhaa anaodai kuwa ni Wasomali kutoka katika kundi la Al Shabaab.

Kuhojiwa kwa mwanasiasa huyo kunatokana na taarifa yake ya maandishi aliyoipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Februari 9, mwaka huu.

Mwanasiasa huyo ameeleza mlolongo mrefu wa kishirikina ambao anadai kwamba umefanywa ili “kuwapumbaza Watanzania wote” baada ya yeye kuuawa ili wasiwe na akili ya kuhoji mauaji hayo.

Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini kuwa Februari 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi.

Siku moja baadaye, Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. MTANZANIA imefanikiwa kuipata taarifa hiyo kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wizarani ambako iliandaliwa. Ina nembo ya Serikali na anuani ya Wizara ya Ujenzi. Baadhi ya watu wanaotajwa kwenye taarifa hiyo tumehifadhi majina yao kwa sababu za kitaalum kwa kuwa bado MTANZANIA inaendelea kuwasiliana nao ili kupata ukweli.

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe


“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.

“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).
Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.

“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.

“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.

“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).

“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

Habari zote hizi alizo kuwa akizitoa mwakyembe polisi walizichukua na kuwapa gazeti la mtanzania ili kuzichapisha magazetini,hakuna kitu hata kimoja alichokieleza mwakyembe ambacho ni uzushi,nafikiri wote mnajua mmiliki wa gazeti la mtanzania ni nani,baada ya polisi kuzarau kwa makusudi maelezo yote ya dk mwakyembe ,maana walikua wanajua mchezo mzima haikupita muda mrefu dk mwakyembe aliwekewa sumu...nafikiri kun haja ya kueleza namna dk mwakyembe alivyo wekewa sumu na mafisadi ambao wanajulikana mpaka leo.MUNGU akijalia ntafungua uzi mpya kueleza japo kiasi mpango ulivyo kuwa,ntaeleza jinsi wanaume wawili walivyo ondoka tanzania na kuelekea urusi kwa ajili ha mpango mzima
 
Back
Top Bottom