MAJIBU YA MWAKYEMBE HAYA HAPA....Hahahahaha Kozi mwana mandanda kulala na njaa kupenda... Mzee Tupatupa; Mwakyembe hana ubavu wa kujibu mapigo ya Lowassa! Yeye wakati uli alibainika kuwa alikuwa na Kampuni ya kufua Umeme wa upepo Singida ambayo alitaka waingie Mkataba na TANESCO!!! Nani asiejua kuwa Kamati ya Mwakyembe walikwenda Marekani eti kuchunguza Kampuni ya Richmond! Walipofika wakaambiwa kuwa ile ilikuwa Deal la USA kupitia MNCs zake! Jamaa wakapewa Mshiko! Mwisho wa siku wakaja kumtuhumu PM ... Tambua kuwa Lowassa aliwahi kukatiza mkataba wa City Water ambayo nayo ilikuwa ya wakubwa wa USA!!! ... Clinton, Obama wamefika Ubungo kuzindua miradi yao na sasa watu kimyaa!! Wameumbuka hawana la kusema ...
Mwakyembe aliyeikana tafiti yake ya Phd kwenye maoni ya Katiba mpya,ndo nguli wa sheria unayemtaja? Yule Mwakyembe kwanini uamini report yake ya Kamati teuli ilihali aliisaliti research yake ya taaluma? Mwakyembe naye ni opportunist tu. Mwakyembe na Sitta wote #Wasaka tonge tu hao!
Nashauri Lowasa amwage Mboga na Ugali vyote,
...
....saa nne asubuhi UKAWA iko ikulu[/QU
Register and vote kama tunataka changes
Mwakyembe alikuwa ni mzushi kwenye kashfa ya Richmond kama alivyo Zitto Kabwe kwenye hii ya Eskrow. Tatizo la Mzee Lowassa ilikuwa ni kujiuzuru kirahisirahisi kwa kelele za Mwakyembe na genge lake la wazushi.
...
....saa nne asubuhi UKAWA iko ikulu[/QU
Register and vote kama tunataka changes
YES! It begins with you
ni Dr kitaaluma aisee, acha kabisa kulinganisha na JKHivi mwakyembe dr??????????? Naomba kujuzwa au ndio kama Dr Mrema....na KJ
Kwa Hiyo Chama Mbele Utaifa nyuma? Kwa hiyo anaipenda sana CCM kuliko Tanzania yetu?Alikaa kimya kukinusuru chama!!
Muhusika mkuu wa Richmond anajulikana ndo mama kila wakati watu wanamnukuu akisema kuwa tukimpitisha Lowassa atalipiza kisasi.
MAJIBU YA MWAKYEMBE HAYA HAPA....Muda wako umewadia. Muda wako wa kusema ukweli zaidi. Lowassa amekuchokoza leo mjini Dodoma. Amedai kuwa yeye hakuhusika na Richmond. Sakata la Richmond, I mean. Amedai kuwa sakata hilo lilitungwa na kulenga Uwaziri Mkuu wake tu.Hakukuwa na zaidi. Kwa maana nyingine, Dr. Mwakyembe na Kamati yako teule ya Bunge mlitunga kashfa ya Richmond. Yaani,Dr.Harrison Mwakyembe na Kamati yake ni wazushi na waongo!
Dr. Mwakyembe, umepata nafasi adhimu na adimu isiyo na msimu. Nafasi ya kusema hata yale ambayo hukusema Bungeni Dodoma ulipokuwa ukiwasilisha Ripoti ya Kamati yako. Ukweli juu ya sakata la Richmond. Kama Lowassa ameruhusiwa na chama na Serikali kusemea kashfa hiyo, wewe na iliyokuwa Kamati yako hamzuiwi. Mkinyamaza,mtasadifu ukweli wa jina la waongo na wazushi mlilopewa leo hii Dodoma.
Ukiwa nguli wa tasnia ya Sheria, Dr. Mwakyembe panga hoja zako nawe uzungumze na watanzania. Kama huna pesa ya kukodi ukumbi,waite waandishi hata nyumbani kwako. Watakuja na kukusikiliza. Muda wa kulinda heshima yako huu.Kama Lowassa kamwaga mboga, wewe Dr. Mwakyembe mwaga ugali.
Liwalo na liwe!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)