Apologise lady
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 5,980
- 3,115
ukisema alimalizia ya mwakipesile napingana naww. Kat ya wabunge mizigo au bogus iliyowahi kutokea hapa tz basi mwakipesile ni namba moja.
Lile lilikuwa zigo.
Mkuu unajua kwann mwakyembe aliingia kwenye mgogoro wa chinichini na mwakipesile?
Unajua kwann baada ya mwakyembe kuwa mbunge na kikwete alimpa mwakipesile ukuu wa mko?
Hapo kulikuwa na roadblock ambayo ilikuwepo lakn sasa tutaona mengi.
Kipindi mwakipesile anaondoka kwenye ubunge kyela kulikuwa na kampuni moja tu la cocoa nalo ni METL na bei ya cocoa ilikuwa sh 800 tu tena kwa mkopo.
Lakn baada ya mwakyembe kuingia kayaleta makampuni mengne na bei ikapanda.
Mnyonge mnyongen na haki yake mpeni..
Leo mnasema wakisi wakuvua samaki waje bungen watasaidia nn?
Tukianza na majimbo ambayo ya chadema kama mbeya mjin Sugu kafanya nn zaidi ya kurap tu bungne?, msigwa kafanya nn jimbon kwake? Mnyika kafanya nn jimbon kwake mpaka ameamua kulikimbia kwasababu ya hasira ya wananchi?
Mdee kafanya nn zaidi ya mchezo mchafu na ester bulaya.
Tumwache mwakyembe aendelee kufanya kaz pamoja na tingatinga
Kaka huwezi kusema Mwakyembe kafanya kazi kwa kupandisha bei ya cocoa tu,
Bado nakubali jitihada za mwakipesile, hasa kwa kua ni mbuge anaeishi na wana kyela muda wote,
Barabara kuu iliyounga hadi boda ni kazi ya mwakipesile, shule za sekondari kazi ya mwakipesile nafahamu mwakipesile alivyokua karibu kuhuziangalia hzo shule hasa kwa kua nimesoma hapo, maji na umeme wakati wa mwakipesile hatukupata shida, mwanyembe alipokuja alimfanyia fitina mwakipesile akagawa watu katika makundi na kueneza chuki.
Suala la kupanda kwa cocoa limechangiwa na ushindani baina ya makampuni pia hasa baada ya kampuni kama Olam, Baoland n.k kuja kununua cocoa hii ilipelekea bei kupanda. mchango wake ulikuwa mdogo sana.
Turudi kwenye mpunga yako wapi yale makonte na makontena ya wapemba yaliyokuwa yakinunua mpunga kyela???? Yamepaki mbalali yanabeba mchele yanauita super toka kyela wakati mkulima wa mpunga wa kyela akiuza bei ya kawaida ambayo haimlipi kulingana na gharama za kilimo alizotumia, matokeo yake ni kilimo cha mpunga kufa taratibu maana hakilipi watu wanakimbilia kulima cocoa.
Mchagueni kama mnaona anawafaa, mim binafsi mmmh!!!!