Apologise lady
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 5,980
- 3,115
Ukitaka kujibu hoja soma na uelewe siyo unakurupuka kama uliyetoka kuvuta bangi
Nieleweshe basi bangi isha isha.
Jazba ndio jani yenu ccm
Ukitaka kujibu hoja soma na uelewe siyo unakurupuka kama uliyetoka kuvuta bangi
Mwakembe hayo unayosema amefanya, alitumia shahara wake??? Hilo daraja lilijengwa baada ya kukati kwa mawasiliano baina pande mbili wakati wa mvua za masika ndipo akapata fungu. Hiyo ilikuwa ni kama ajali tu.
Zaidi amefanikiwa kuifitini kyela fm kufungiwa.
Vile vile halmashauri ipo chini ya ccm na mwakyembe ni ccm hvo, mnaelewa fika kuwa wote mliopo kwenye hiyo system ya chama mna matatizo hapo wilayani, kukaimu kwa wakurugenzi nyie na madiwani wenu ni chanzo.
Rudi wakati wa mwakipesile kama wakurugenzi walikuwa wanakaimu hovyo hovyo.
Umeme gani unazungumzia, umeme ambao unamgao usiokoma?? Wew umezaliwa juzi hapo bila shaka
Msitetee uovu bhana.
ndumbulwe unaandika uongo kwa manufaa ya nani ? unazikumbuka ahadi za mwakyembe alizozitoa mwaka 2010 ? ni ipi aliyoitimiza ?Ukitaka kujibu hoja soma na uelewe siyo unakurupuka kama uliyetoka kuvuta bangi
huyo mwakipesile unayemsema ni yupi?
Huyu ambaye alishindwa kufikisha umeme hata maeneo ya bwato?
Huyu ambaye alishindwa kuleta makampuni ya cocoa mpaka bei ya kokoa ikawa sh800?
Huyu ambaye barabara inayotoka njia panda ya ipinda ilishindwa hata kulima kwa greda ilijaa mafuliko mpaka watu wa kutoka ipinda,matema wakitaka kuja kyela walilazimika kuipitia ntaba kutokea tukuyu ndio warudi kyela?
Huyu ambaye barabara inayoenda kyela mjini hata magari mawili hayakuweza kupishana?
Huyu ambaye daraja la mto lufilyo upande wa lusungo aliweka daraja la mianzi?
Huyu ambaye bei ya debe la mahindi lilikuwa 2500-300?
Unamsema mwakipesile yupi? Ambaye kazi yake bungeni ilikuwa kama wasira kusinzia tu?
Suala la kyela fm hilo ni la TCRA.
ndumbulwe unaandika uongo kwa manufaa ya nani ? unazikumbuka ahadi za mwakyembe alizozitoa mwaka 2010 ? ni ipi aliyoitimiza ?
nakusanya ushahidi na ikiwezekana ntaweka hapa video ili kuthibitisha hoja zangu , kyela hatutaki unafiki .tatzo lako ww bwana unakimbilia kushika uwongo wenzako lakn huelezi ni upi ukweli?
.
nakuhakikishia kwamba kila aliyehusika kuhujumu redio hii iliyokuwa kiunganishi cha wanakyela Mungu hatamuacha , unasikia bhana , matatizo yanapotokea ni vema kusaidia kutatua badala ya kukandamiza , damu ya kyela fm itakwenda na wengi sana .Mmmh!!! Haya uwanja wenu.
Suala la kyela fm anahusika kwa asilimia 120.
nakusanya ushahidi na ikiwezekana ntaweka hapa video ili kuthibitisha hoja zangu , kyela hatutaki unafiki .
Apologise lady unakumbuka kipind mwakipesile anaondoka madarakan kyela kulikuwa na high schoo ngapi?
Lakn mwakyembe amekuja kutetea suala la elimu mpaka sasa kyela day, matema beach hizo ni high school.
Mwakipesile ameacha shule za secondary tatu kama sio nne tena hata yeye alizikuta kipinda chake hamna chochote kilichofanyika
Kaka suala la Elimu ni mpango wa Lowasa na sio mwakyembe hata kidogo, njoo idara ya elimu sekondari tukuthibitishie,
Wakati akiwa waziri mkuu alisimamia kuwepo kwa shule za kata ili angalau kiwango cha chini cha elimu kiwe form 4, pia alihakikisha kila wilaya iwe na japo high school zisizopungua 3. Kati ya mwaka 2006- feb 2008, alifikia sehemu nzuri kiasi lakin yaliyotokea yakatokea.
Baada ya hapo miaka zaidi ya 5 ndio wananchi wanachangishwa pesa ya maabara n,k. hali mbaya, majengo yaliyojengwa miaka ya katikati yana nyufa za kutosha, vitabu wanategemea msaada wa Longman na Oxford, Apparatus shule zinaazimana zaidi 10 loh!!!
Hizo shule, zote hapo tangu itope hadi kajunjumele ni kazi ya mwakipesile na Lowasa, huyo mnaemsema tunamshukuru kwakupigia picha majengo over.
aisee yaan mnamwonea mwakyembe kweli.
Shikamoooooo siasa kuleta utani kwenye maendeleo.
lakn ujue mwakyembe ndio mbunge wako mpaka 2020
kudos brother....
Kuna watu wamejawa na ushabiki usio na maana. Tatzo moja la wanakyela ni uvivu wa kufanya kazi wao wanataka kila kitu mbunge awape.
Japo mm sijatembea wilaya nzima lakn kuna maeneo yalikuwa hayapitiki kwetu tunaita lujingija lakn sasa hvi magar yanapita.
Kulikuwa na barabara inayopita ndobo unapitia lukwego unanyoosha mpaka sehem moja kuna mto unaitwa mabhe unapita kule mpaka kisyosyo pale ilulu unanyoosha mpaka sehem moja panaitwa kwa bwanashamba. Ile njia ilikuwa maji na matope kulijaa mito na mamba na watu wameliwa na mamba kipindi cha mwakipesile lakn alivyoingia mwakyembe ameitengeneza ile njia inapitika mpaka magari ya tani yoyote yanapita. Lakn yote hayo hawayaoni. Kutoka ipinda mpaka mabunga mpaka kanga kule barabara zinapitisha magari mpaka mashamban.
Watu wakimsema mwakyembe kuwa hajafanya lolote itakuwa ni unafki mkubwa.. Jiulize kipind alichokaa mwakyembe madarakan linnganisha na wabunge wengne kama wamemzidi
Hizo barabara ni kodi zetu. Mwakyembe hakuna alilofanya Kyela