Dr. Mwakyembe aweka hadharani ugonjwa wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe aweka hadharani ugonjwa wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by buckreef, Mar 20, 2012.

 1. b

  buckreef JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Wetu | Gazeti la Mwananchi

  BAADA ya utata wa muda mrefu wa ama Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amelishwa sumu au la, jana Mbunge huyo wa Kyela, aliweka hadharani ugonjwa wake akisema unafahamika kitaalamu kwa jina la Popular Scleroderma huku akisisitiza: "Sasa nimepona kabisa."

  Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo mwaka jana yalizidi kumtikisa na Oktoba 9, Serikali iliamua kumpeleka Hospitali ya Appolo, India kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe akiwa amevalia kofia ya pama alisema: "Si kwamba sijambo, bali nimepona kabisa baada ya kugundulika na maradhi hayo na kutibiwa."

  "Nimerudi juzi kutoka India na daktari wangu ameniambia nimepona, nilikuwa nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Scleroderma' iliyosababisha ‘skin disorder' (ngozi kutokuwa katika hali ya kawaida), lakini kwa nguvu za Mungu nimepona, namshukuru Mungu."

  Kuhusu sumu
  Alipoulizwa kuhusu tuhuma za kulishwa sumu, Dk Mwakyembe alikataa kuzungumzia hilo akisema anasubiri uchunguzi ulioagizwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.

  Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema angependa kuona uchunguzi huo unakamilika haraka na ripoti yake inatangazwa kwa umma.

  Alisema yuko tayari na anasubiri tume hiyo ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nahodha imhoji ili atoa kile kilichomo katika ripoti ya daktari wake.

  Dk Mwakyembe alisema anachoshukuru hadi sasa ni kwamba afya yake imeimarika kutokana na shinikizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza Serikali kumpa kipaumbele wakati wote akiwa nchini na India hatua ambayo imemwezesha kufika hapo alipo.

  Kutokana na hali hiyo, Dk Mwakyembe aliwataka wananchi wote wakiwemo wa jimboni kwake Kyela kuondoa wasiwasi akisema sasa yupo imara kwa ajili ya ujenzi wa majukumu ya taifa.

  "Ninaomba wapiga kura wangu wa Kyela waache jazba, wawe na subira juu ya matatizo yangu. Wiki ijayo nitakwenda kuzungumza nao ili niweze kuwaeleza matatizo yaliyokuwa yananisumbua, lakini sasa hivi niko fit," alisema.

  Mtaalamu auzungumzia
  Mtaalamu wa afya ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ugonjwa huo wa ‘Popular Scleroderma' unasababishwa na chembechembe hai nyeupe kushambulia kitu kigeni kilichoingia kwenye mwili na kusababisha magonjwa ya ngozi.

  Alisema chembechembe hizo zinaweza kusababisha ngozi ya mwili kuharibika... "Ni magonjwa yanayosababishwa na chembechembe hai nyeupe kujikataa zenyewe na kusababisha ugonjwa wa ngozi na mifupa."

  Kauli hiyo ya Dk Mwakyembe kuhusu ugonjwa wake imefungua ukurasa mpya hasa baada ya baadhi ya wanasiasa kuamini kuwa hakuwa na tatizo jingine bali, amelishwa sumu. Tayari Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba ambaye alitoa ripoti akisema Naibu Waziri huyo hakulishwa sumu kama inavyodaiwa, amefanyia uchunguzi madai hayo na kukabidhi jalada lake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, DPP ili afungue kesi.

  Kauli ya Sitta

  Mmoja wa wanasiasa waliodai kuwa Dk Mwakyembe amelishwa sumu, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta alipoulizwa jana juu ya kauli hiyo mpya ya Dk Mwakyembe alisema hana cha kuzungumza.

  Januari 28, mwaka huu akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Dar es Salaam Sitta alisema Dk Mwakyembe amelishwa sumu.

  Akizungumza kwa utaratibu, Sitta alisema hana mengi ya kuzungumza kuhusu ugonjwa unaomsumbua Dk Mwakyembe na kusisitiza kuwa isubiriwe ripoti kutoka India ambako alikuwa akitibiwa.

  "Dk Mwakyembe si anatibiwa India?," alihoji na kuendelea, "Nadhani umeshapata jibu, tusubiri… acha huko India waendelee na uchunguzi wao, siwezi kusema lolote zaidi ya hilo nililokuambia."

  Dk Mwakyembe alianza kuugua Oktoba 9, mwaka jana na alitibiwa Apollo hadi aliporejea Desemba 11, mwaka jana. Alirejea tena India kuendelea na matibabu hadi Ijumaa iliyopita aliporudi na kusema kuwa amepona.

  Matatizo yake ya kiafya yamesababisha mvutano baina ya viongozi wa Serikali. Wakati Manumba akisema ripoti kutoka Wizara ya Afya ilionyesha hakupewa sumu, waziri mwenye dhamana na afya Dk Haji Mponda alimkana.

  Pia Waziri Nahodha ambaye ana dhamana na jeshi hilo la polisi, alikana ripoti hiyo ya DCI Manumba na kutaka aulizwe mwenyewe alikoitoa huku akisema uchunguzi alioagiza bado unaendelea.

  Ugonjwa wa Scleroderma

  Kwa mujibu wa mtandao wa Johns Hopkins wa
  www.hopkinsscleroderma.org, Scleroderma ni ugonjwa unaohusisha mfumo wa kinga ambao wakati mwingine dalili zake zinaweza kuwa mtu kuwa na baridi yabisi na sugu. Ni ugonjwa unaoathiri mwili, hasa muunganiko wa tishu na kuufanya kuwa mgumu.

  Mfumo wa Kinga

  Scleroderma iko katika kundi la ugonjwa wa mfumo wa kinga. Hii ina maana kwamba mfumo wa kinga wa mtu hufanya kazi kwa kujitegemea. Hulinda mwili dhidi ya maadui mbalimbali kama virusi na maambukizi.

  Kuwa na ugonjwa huo wa mfumo wa kinga maana yake ni tishu au kinga kuvamiwa na wageni, ama virusi au maambukizi mengine na hivyo kusababisha matatizo.Mtu anapokuwa na scleroderma, seli huathirika kwa sababu katika hali ya kawaida seli haipaswi kuwa na kitu kingine cha ziada katika mfumo wake wa utendaji kazi na kama ikitokea hivyo, mtu huyo hujikuta katika matatizo yanayosababisha mfumo wa mwili wake kutokuwa kama ulivyo kawaida.

  Unawezaje kuupata?
  Watu wachache hupata ugonjwa huu na hakuna anayejua unatokana na nini. Scleroderma ni ugonjwa nadra. Chini ya watu 500,000 Marekani wanasumbuliwa nao na hakuna anayejua kwa uhakika chanzo chake.

  Baadhi ya wataalamu wanabainisha kuwa watu kati ya saba wenye kusumbuliwa na ugonjwa huo ni wanawake. Wenye kusumbuliwa zaidi na ugonjwa huo ni wale wenye umri wa kati ya miaka 35 na 50. Hata hivyo, watoto wadogo na watu wazima zaidi wanaweza kuupata.

  Baadhi ya familia zimekuwa zikiathirika zaidi na ugonjwa huu kuliko zingine. Ingawa scleroderma hauonekani kuathiri kifamilia, lakini mara nyingi hutokea katika familia ambayo imewahi kuwa na mtu mwenye magonjwa yanayokaribiana nao kama vile tezi au mengine yanayofahamika kitaalamu kama arthritis rheumatoid au lupus ambayo msingi wake ni kuathirika kwa mfumo wa kinga.

  Dalili za awali
  Kwa baadhi ya watu kuna dalili mbili za kwanza:
  • Vidole kuwa vya baridi na wakati mwingine kubadilika rangi au mtu kuonekana mwenye msongo wa mawazo.
  • Vidole na mikono kuwa migumu na kutoa magamba au unga
  Mabadiliko ya rangi ya kidole husababishwa na kupungua kwa uwezo wa mishipa ya damu kupitisha damu ipasavyo. Hii hutokea kwa sababu ya madhara yaliyotokea dhidi ya mishipa ya damu iliyoharibiwa kutokana na ugonjwa huo.
  Hali ya ubaridi na mabadiliko ya rangi huitwa raynaud's (hutamkwa ray-knowds). Watu wengi wenye hali hii wanaweza kudumu nayo bila kuwa na ugonjwa wa scleroderma.

  Athari tofauti
  Athari ya scleroderma inatofautiana sana kati ya watu. Wengi huanza kuona dalili za vidole kubana na hata kuvimba. Kisha kwa baadhi ya watu huchukua miezi sita wakati wengine hata zaidi ya mwaka ugonjwa kujitokeza rasmi.
   
 2. b

  buckreef JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  The UnfoldingMystery of Scleroderma
  By LESLIE BERGER

  Likemany autoimmune ailments, scleroderma remains a great unknown. Despite decadesof research, the cause of this rare and complicated disease has yet to bediscovered. But the good news is that doctors have a pretty clear understandingof how scleroderma progresses - a natural history, they call it - and arebetter than ever at extending and easing their patients' lives.


  "Lots of patients and lots of doctors used to considerit a ‘black box' disease, a complete mystery, with little that could be done,"said Dr. Philip J. Clements of the University of California, Los Angeles, whois a scleroderma specialist. "Now there's a body of evidence that tells us whatto watch out for, and when."
  Experts now know, for example, that the gradualhardening of tissues and blood vessels that is a hallmark of sclerodermausually starts on the hands and face, with skin thickening, pitted scars andcool, pale fingertips among the earliest symptoms. Damage can then progressinward to internal organs, though the course varies widely from patient topatient. Of the 10,000 cases diagnosed among Americans each year, mainly women,a small subset will die quickly. But many others are able to manage theircondition with a variety of treatments and have normal life expectancies.
  Doctors also now know that if a patient's internalorgans are going to be affected as well as the skin, that is likely to happenin the first four or five years of the disease. So early diagnosis and closemonitoring of the heart, lungs and kidneys are vitally important.
  They have also learned that steroids, once viewed as a cure-all for immune disorders,can worsen the effects of scleroderma, especially in the kidneys, and should beused with caution.

  "Learning which drugs to avoid was itself a big step,"said Dr. John Varga, the Gallagher Professor of Medicine at NorthwesternUniversity and chairman of the Medical Advisory Board for the SclerodermaFoundation, a nonprofit group that sponsors research and support forpatients and families.
  Kidney disease used to cause 90 percent ofscleroderma-related deaths until the advent of a class of blood pressure drugs calledangiotensin-converting enzyme, or ACE, inhibitors in the 1980s. ACE inhibitorsprevent kidney damage by slowing down the chemicalsthat cause the muscles surrounding blood vessels to contract. Complications inthe kidneys now account for only 14 percent of scleroderma deaths, Dr. Steensaid.

  The lungs are still a challenge. About 80 percent ofscleroderma patients develop some form of lung problem - either pulmonary hypertension, due to hardening ofthe veins and arteries in the lung, or pulmonary fibrosis, in which the lung tissuebecomes inflamed and then thickened with scarring. Some patients develop both.Either way, breathing becomes more difficult as the lungs become less pliable.

  "If you die of a scleroderma-related problem, half ofthose deaths are from lung disease," said Dr. Virginia Steen, a professor at GeorgetownUniversity and director of the Rheumatology Fellowship Programthere. She wrote a seminal 2007 article that documented theshift from kidney disease to pulmonary disease as the biggest cause of deathamong scleroderma patients.

  One successful remedy called Revatio, routinelyprescribed since 2005, came from an unexpected source: Viagra.Repackaged from a little blue diamond to a round white tablet and renamed formarketing, dosage and insurance purposes, the drug works by relaxing the bloodvessels and improving blood flow, whether for erectile or lung dysfunction.

  "No one could understand why all these women weretaking it four times a day," said Frannie Waldron, chief executive of theScleroderma Foundation.
  Doctors also have a growing arsenal of experimentaltreatments and potential cures, some of which are risky.

  Among them is cyclophosphamide, or Cytoxan, a powerfulbut highly toxic cancer drug that acts on the immune system. The drug decreasesthe inflammation that causes pulmonary fibrosis and has been used onscleroderma patients for the last 10 years.
  But cytoxan has dangerous side effects, including anincreased risk of bladder cancer, and usually is not given formore than a year. Moreover, the fibrosis seems to start again once drugtreatments stop. Several studies involving the medication are under way, as wellas efforts to find alternative treatments, many of them sponsored by drugcompanies.

  Another big push involves stem cell transplant, anextremely risky process in which doctors try to reset the patient's immunesystem and bypass the glitch that causes scleroderma. The procedure is thesubject of a National Institutes of Health study called the SCOT trial, for Scleroderma:Cyclophosphamides or Transplantation?
  Similar to a bone marrow transplant, doctors first draw thepatient's blood and extract the stem cells, the highly malleable buildingblocks that are thought to be free of the seeds of scleroderma. The patient isthen subjected to high doses of radiation or chemotherapy with Cytoxan to kill the bonemarrow. The last step is to reinfuse the stem cells, in the hopes that theyreplicate themselves in a healthy form free of disease.

  The study will compare the benefits of the stem celltransplant with giving patients just monthly doses, but high ones, of Cytoxan.Preliminary results have been promising, several experts said.
  "You'dthink you'd have trouble recruiting for this," said Dr. Arthur C. Theodore of BostonUniversity, one of the investigators in the project. "Butscleroderma patients are desperate."
  ****************************************************
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sina imani na huo uchunguzi utakaofanywa.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mami NN, heri yako huna imani na uchunguzi.

  Mkapa yeye ana imani kubwa kwa Serikali na Chama cha CCM.......

  Mie nina imani zaidi na Wassira......

  [​IMG]
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi serikalini??ile ile iliyokuwa inatuhumiwa? Something is wrong somewhere!!!Yangu macho ya kuona,na masikio ya kusikiliza!!!
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Naona imekuwa kama hadithi ya "The Sky is Falling."

  Ugonjwa wa ngozi tukaambiwa sumu
   
 7. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kwahiyo haikua sumu....... Pambaff zake
   
 8. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni bora DPP sasa awaburuze Sitta na Wenzie waliowazushia mafisadi kuwa Mwakyembe amelishwa sumu. Nimepitia kwenye google kuhusu huo ugonjwa wa "popular scleroderma" kwanza hakifahamiki chanzo cha ugonjwa vile vile katika aina za scleroderma hakuna popular sclerodema bali kuna Limited na vivus sclorederma. Mwakyembe ni muongo na mzushi kuwa alilishwa au kugusishwa sumu. Big up Manumba.
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwani na huyu Wassira naye ana ugonjwa wa ngozi?..........
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jamani, acheni. Mbavu zangu!
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  heshima yako mkuu. Mbona mnanyamaza vicent akitukanwa hadharani? Na anayoyasema ndo yaliyopo kwenye vichwa vya familia? Mlijiuliza kwa nini nkapa aliomba uraia wa butiama baada ya jkn kufariki? BTT ni jambo la kutegemea hasa kwa wakati huwa ambapo madaktari wana shinikizo la mgonjwa na wanasiasa kukimbilia kwenye idiopathic diseases. Apolo wanaogopa wakisema ni sumu watakosa wagonjwa kutoka jmt kwani ni serikali iliyohusika katika mpango huo na wao wanategemea pato kutoka huku maana kuna miezi huwa wanalipwa hata kuja kutalii chini ya ufadhili wa wizara ya afya. Sikutegemea ripoti ya apolo iitundike serikali ya jmt inayoongozwa na genge la majambazi wa mali za umma.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Si tulisema humu, huo ni upungufu wa kinga mwilini unaosababisha hayo! kiko wapi.

  Kimya!
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sumu unaijuwa wewe au unaisikia tu?
   
 14. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mtaalamu auzungumzia
  Mtaalamu wa afya ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ugonjwa huo wa ‘Popular Scleroderma' unasababishwa na chembechembe hai nyeupe kushambulia kitu kigeni kilichoingia kwenye mwili na kusababisha magonjwa ya ngozi.

  Hata sumu yaweza kuwa ni kitu kigeni... (read between the lines)
   
 15. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyu mwakyembe nadhani anatuzingua tu. Kwa jinsi alivyowajibu waandishi jana sikutegemea nadhani hakuna lolote ni kutafuata tu umaarufu na huruma ya watu ...nimefuatilia picha nzima na kauli zinzotolewa naye pamoja na washirika wake ......kuna kujichanganya mno and i am fade up bora nikajadili mambo yenye maana.
   
 16. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Jana nilisema humu ndani kuwa hakuna kitu kigeni kinaweza kutoka kinywani mwa mwakyembe.........hawezi kupingana nao maana ni mmoja wao....naomba niwambie hivi baada ya mda huyu mtu atarudi huko india
   
 17. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
 18. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  usiamini haraka ....siku zote ugonjwa huu hitokana na kitu kigeni kuingia mwilini na kushambulia hasa seli za mwili.....lakini pia kumbuka kwamba huyu mwakyembe ni mzuri wa kupindisha taarifa....
   
 19. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwani ugunduzi wa magonjwa umefikia mwisho? maana hata leo kuna aina nyingi za virus vya HIV na vinazidi kubadilika. Unachotuambia hapa ni kwamba waliomtibu wamemdanganya aina ya ugonjwa.
   
 20. Manjagata

  Manjagata JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 1,750
  Trophy Points: 280
  Jamani sasa kile kitaulo na sabuni zimeishia wapi? Big up Manumba! Port jamaa walitaka kukusulubu bure, itabidi tukuombe radhi kwa yote!
   
Loading...