Kyela wamekwisha kwelikweli. Kumbe kelele zote hizi za kumsulubu Mwakyembe, mtu aliyewanyua juu kwenye chati ni fedha za Lowassa na Rostam! Duh ama kweli EPA na RICHMOND ni kiboko! Hata hivyo huyu mgombea wa Kyela kutoka London, asiwaumbue BANYAMBALA wa Kyela kwa kumfuatafuata Lowassa mpaka nyumbani kwake. Hajasikia yaliyomkuta yule Mbunge wa Kigoma, nanihii.... nanihii ......?
Tumehabarishwa yuko Arusha kukutana na Mh Edward Lowasa!
Mwakalinga ameisha shindwa kabla hata ya uchaguzi! Hana sera zaidi ya kuwa na kajihoteli huko, kuweni makini wana Kyela hawa mamluki watakuja na njia nyingi, usiache kusoma ulw mwongozo ulotolewa na Kanisa!
.....Engineer wa majungu upo wapi teh teh teh teh teh.....
Bana eeee.... kwanini watu mnakuwa waongo namna hii?!!! Dayyym! George wala hajafika huko Kyela. Bado yuko safarini, na kwa taarifa yako tu, George yuko Ngorongoro leo hii, alikuwa Dar, akazuka Manyara na baadae kujionea maendeleo anayofanya Dr. Slaa kule Karatu, maana ndiko aliko lala.
Kyela wamekwisha kwelikweli. Kumbe kelele zote hizi za kumsulubu Mwakyembe, mtu aliyewanyua juu kwenye chati ni fedha za Lowassa na Rostam! Duh ama kweli EPA na RICHMOND ni kiboko! Hata hivyo huyu mgombea wa Kyela kutoka London, asiwaumbue BANYAMBALA wa Kyela kwa kumfuatafuata Lowassa mpaka nyumbani kwake. Hajasikia yaliyomkuta yule Mbunge wa Kigoma, nanihii.... nanihii ......?
Masa,
Heshima mbele kwa mbele. Jana ulipoona kuwa George Mwakalinga kaanzisha kampeni ulikuja na hii makala:
Baadaye ukaongeza na makala hii hapa chini:
SteveD akakujibu:
Juu ya shule ya Mwakalinga, ni kweli alimaliza shule huko Europe na hata hakurudi Tanzania. Alianza kazi kama Mhandisi na hata alivyojenga KAJIHOTELI ni kuwa hela zote hizo HAKUFISADI hata senti moja ya Mtanzania. Na kama aliiba basi aliwaibia wa Wamarekani. Kama aliaminiwa na hao watu na kumpa kazi UK kwa miaka yote hiyo, wewe wamwita Mhandisi wa majungu, huoni kuwa watu hapa JF wana akili ya kuchambua Pumba na mchele.
Sasa tungelitegemea huo MPANGO wenu umekwama basi MJIPANGE upya lakini somo halijaingia. Mlipoona katoka Dar mkajua kuwa kaenda Kyela kumbe kaenda kwa Dr. Slaa. Loo, what a chenga ya WILAYA. Hii itabidi wachezaji kama Ronaldo waje wapate shule ya chenga. Wanaume mmeenda chali PWAAAA!!! Aibu aibu watu wazima.
Kama hiyo haitoshi, pamoja na kuandikwa alikuwa kwa Dr. Slaa, sasa tayari imeshakuwa alikuwa kwa Edward Lowassa. Kama angelikuwa na shida ya kumuona Lowassa, si angelichukua KIPIPA hapo UK na kujimwaga German kumuona Lowassa siku moja ya weekend? Bei ni nafuu, ni karibu, hahitaji VIZA, hata kwa matrain (via France) ni karibu tu. Amesubiri hadi aje Tanzania ndiyo aende Arusha ili MAPAPARAZI mumuone. Kama ni kuchukua pesa basi angelimtuma hata nduguye. Kwani ni lazima uonekane la Lowassa wakati akiwa Tanzania? Lowassa pia wanaweza hata kuonana Dar.
Hao Moravian wetu hao jimbo la Mbeya/Kyela nao wameanza kujiingiza kwenye VITA ya UDINI ya kumpendelea Mwakyembe. Waambie habari zao tunazo. Siku ikifika na wao madhambi yao yanaweza kupatikana na kuanikwa hadharani na wao ndiyo watakuwa na kulia na kusaga meno maana tofauti na Mwakalinga/Mwakyembe, wenzao ni kama paka - wana miguu minne. Hao viongozi wa Moravian wakiumbuliwa, wataenda kuwa wakulima, na pesa ya sadaka waisahau. Sidhani kama Mwakyembe atawapa hela nzito kiasi kwamba waumini wakiwafukuza, basi wataenda KUPUMZIKA kama Mkapa. Hivyo fikisha habari kwa hao WALA VYA BURE kuwa habari zao zimefika hapa JF na watachambuliwa muda ukifika.
Vinginevyo, wapambe kuweni na SUBIRA. Haya mambo ya kuhaha kuandika barua na kupeleka watu hadi nje ya nchi na mchoke bin mlegee kwa jina la JF, AMINI!!
Sikonge
Mbona wajichanganya na unadisclose Id ya Mwakalinga ndiye Engineer ambaye mimi namwona ni mdaku zaidi, hili huhutaji kuwa mnajimu fatilia post zake, najua wewe ni Pro Mwakalinga aka....sina maslahi na yeyote. Sipendi kuchukuliwa na upepo kama unavyotaka nilazimisha hapa! Wananchi wa Kyela watachagua anayewafaa kwa utashi wao .....
Masa,
Kama ungeliandika hivi kama mawazo yako, nisingepinga. Ila kusema alikuwa Arusha (ni kweli yupo) kwa Lowassa (je umemuona?). Kama uliisoma hapa basi pia ningelikuelewa. Ila hizo zote zimeshasemwa kuwa ni UONGO. Na aliyeandika tayari anafahamika.
Wakuu wote hapa heshima mbele,
- Tafadhalini sana tunahitaji kuwa wastaarabu na waangalifu kwa sababu kwa mwendo ninauona hapa, kuna hatari ya kuwaharibu viongozi imara sana hapa yaani DK na George, ninasema wote ni watu makini sasa tuache tabia zilizokataliwa na Obama juzi kule Accra, za ku-invest kwenye majina badala ya institutions na sound policies, Obama amesema wazi kwamba Africa hatuhitaji majina makubwa au dictators na that is exactly kuna mnaokifanya na hizi kampeni chafu.
- Hakuna mahali popote ambapo George ametangaza kwamba anagombea ubunge wowote ule, sasa hata wale mnaomuongelea hamumsaidii hata kidogo, na wale mnaomuongelea DK ndio kabisa mnanishangaza sana, shujaa wa taifa kama yeye kweli anahitaji hizi cheap kampeni namna hii? Ukweli ni kwamba mnamshusha hadhi na hizi nyepesi nyepesi.
- Tufike mahali tuwajali wananchi wa Kyela kwanza, badala ya ubinafsi wetu wao ndio waamuzi kwamba nani anawafaa, na besides hivi sio vita wala ugomvi kwa sababu DK alimngóa Mwakipesile na hakukuwa na tatizo, kwamba amemuonea jimbo lake sasa kwa nini mnataka kuligeuza hili jimbo kuwa ni la DK badala ya wananchi wa Kyela? Ninamheshimu sana DK na kazi yake kwa taifa, lakini sijui sana huko jimboni, na pia ninamheshimu sana George na idea zake iwapo ataamua kugombea kama inavyotabiriwa hakuna ubaya wowote, na yes niko in contact naye kila siku ya Mungu,
- Anaendelea na likizo yake, najua leo yuko Arusha sasa tuache majungu na wewe unayechochea sana kwamba ametumwa ni vyema ukaacha hayo majungu mkuu, kwa sababu huna ushahidi wala dataz ya hizo sumu unazozitema sana, Rostam aliamua kuacha ubunge lakini mafisadi wenziwe wamemwambia kwenye kikao cha siri kuwa akiacha tu ajue anatinga Segerea kwa hiyo anagombea na ameshaanza kampeni za chini chini, Lowassa anajua sana kwamba akitoka tu jimboni mwake anaondoka na maji, Nchimbi naye anajua maji ni ya shingo kwa hiyo hakuna wa kuacha jimbo lake kwenda la mwingine au kumsaidia mwingine,
- George akiamua kugombea ni sawa kabisa kwa sababu itakuwa vichwa viwili vinapiganishwa na matokeo tutapata ukweli mtupu na itakuwa kampeni of the Century, watakaofaidika ni wananchi wa Kyela na vita hivyo kama vitatokea, na Mungu awajalie wote yaani DK na George, ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi Kyela, maana hata bila ubunge George atawasaidia sana wananchi wa huko Kyela pamoja na umasikini wake kwa sababu ni mkweli na ni committed kwa maendeleo ya Kyela.
Otherwise, ninamtakia heri DK kwa kupona na arudi haraka bungeni na kuendeleza libeneke, na pia ninamtakia George likizo njema na hasa safari nyingi alizonazo, sijui hata kama atapumzika kabla ya kurudi nyumbani.
Respect na Likizoni, tuache uzushi tuwajali wananchi wa Kyela.
FMES! Ni Wazee wa sauti ya umeme!
Wazee wote lazima wang'oke mimi nitagombea igunga
Mkuu, kama ni suala la uzee, mbona Rostam Aziz bado kijana sana!
-umesikika baba!hata hivyo naomba umsamehe MASA BURE!unajua hili jukwaa la siasa hana uzoefu nalo.yeye ni mutu ya kule-kwingine kwa wale jamaa wa ule mlengo mwingine!wamejipa jina la mtandao wa simu za mkononi!alipitiwa tu,msamehe
Fataki..lowassa ni mojawapo ya kampeni za dr. lakini ninawasiwasi kama inaweza kusaidia kule kijijini..Kijijini uko watu wamemchoka ile mbaya sijuhi kwanini.Siku moja nilichukua taxi..Jamaaa akawa anamponda tumemfanyia kampeni anaenda kumpa kazi shemeji yake mchagga inamaana hatuamini wadogo wake kumwendesha? Ila na mimi nikajiuliza hii ni siasa na yeye imekuwaje ameshindwa kutafuta kijana uko uko kwao?Kweli siasa ngumu
Makubwa haya! Hivi Msuya ni Mchagga?
[I][Habari nilizozinasa hapa ni kwamba kuna mpango unasukwa kwa kushirikiana na spika Sitta. Mbunge Mwakyembe ataenda bungeni mara moja na kupokewa na wabunge na kisha ataaga na kwenda Kyela kupokewa na wananchi kwa maandamano; muda wote ataongozana na waandishi habari wa Mengi. Hapa wanasema maandamano yatakuwa ya kumpongeza kwa kuwazidi kete mafisadi waliotaka kumwua kwa ajali ya lori.
Ila kuna tatizo moja maana sasa wananchi wa Kyela wameshaanza kuelewa usanii wa mbunge wao. Kuna watu wana wasiwasi hilo zoezi linaweza kuishia kwenye kuzomewa kwake.
Kila siku kuna vikao jioni kujadili namna ya kufanikisha maandamano hayo. Wacha watuletee pesa na sisi tutaenda na mabango yetu![QUOTE]
Wewe Engineer una lako jambo, inaelekea wewe ni sauti ya mafisadi wanaotumwa kumwandama huyu Mh. Mwakyembe mtumishi w2a watu. Huna point hata moja katika mchango wako.[/B][/B][/B]
Ijabu huo ndo uelewa wa watu wengi tanzania..ukitoka mbeya basi wewe ni mnyakyusa,msoma wewe ni mkurya,kilimanjaro wewe mchagga.Mi mwenyewe mke wangu mjita, kule kwetu wananiambia nimeoa mkurya.
Tukija kwenye point nafikiri dr. katika hilo kachemsha,kumbuka hii ni siasa..WHY MSUYA NOT MWAKATUNDU? mathematical.Mwakatundu mzaliwa na mkazi wa kyela angeweza kulisha watu kumi uko kyela kama driver wa dr.na kwahilo dr kama mbunge angekuwa amewapa maisha bora watu kumi na moja jimboni kwake, Hizo ni hesabu za kujumlisha na kutoa na wala sio hesabu kubwa sana.Nyie mmekalia tu nitajenga shule ,sijuhi nini, wakati kuna mambo madogo kwa kuyaona lakini yanaleta faida kubwa kwa jamii.
Ndugu yangu Msauzi, pamoja na nia yako nzuri, mawazo yako ni ya kikabila ambayo mtu msomi na mwenye utaifa kama Dk. Mwakyembe hawezi kuwa nayo. Ndiyo maana hata dereva wa Prof. Mwandosya ambaye yuko naye miaka mingi, ni Msukuma na siyo Mnyakyusa. Mwacheni Mwakyembe na visheni yake kubwa.
JF sasa inaanza kuharibika, si uwanja wa kubadilishana hoja za msingi tena! Nimemsoma jamaa mmoja humu anajiita Engineer anasema Mwakyembe ni mwizi kwa kuwa kwenye kampuni aliyoianzisha na wenzake ana mabilioni ya pesa! Mimi najiuliza, huyu kaenda shule kweli? Yaani kuna wanaJF wanaoamini kuwa mtu akijaza fomu za BRELA na kutamka kusubscribe kwa mfano for 100 shares za bilioni mbili, basi mtu huyo ana bilioni mbili? Mwanzoni niliamini kuwa hayo ni makosa ya uelewa wa baadhi ya waandishi wa habari, Kumbe hata JF kuna watu wanaamini hivyo? Kama ni hivyo, wote sisi ni mabilionea maana tuna fomu zinazotaja mamilioni na mabilioni ya fedha huko BRELA. Akina Engineer wa JF tafadhali uliza uelezwe kabla hujajianika hadharani kuwa hujui, unaropoka tu!