Kuna uwezekano Dkt. Tulia akafanya mazungumzo na Rais wa Marekani Joe Biden

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Kulingana na namna dkt Tulia alivyoongea kwa uchungu hisia kali na maumivu makali juu ya kile kinachoendelea kule mashariki ya kati,na kupelekea vifo vya watu na mateso kwa wengi hasa watoto na akina mama wasio na hatia .kuna uwezekano mkubwa baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na mamlaka ya Palestine ,akatafuta pia nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani Joe Biden katika kutafuta amani ya kudumu mashariki ya kati.

Hii ni kwa kutambua kuwa Marekani ni mshirika wa karibu sana na Taifa la Israel aliyeapa kwa kiapo cha Damu kuilinda na kulipigania Taifa la Israel mpaka tone la mwisho na katika mazingira ya aina yoyote ile ni lazima Marekani awe upande wa Israel. hivyo Marekani hakwepeki katika kumshirikisha katika namna ya kusaidia kudumisha amani mashariki ya kati.

Kwa hiyo namuona Dr Tulia ambaye ameweka wazi kuwa mwakati katika mijadala yao ndani ya umoja wa mabunge Duniani watatoa kipaombele na kujikita zaidi katika kujadili Masuala ya amani na usalama Duniani kwote ,ili kuifanya Dunia kuwa sehemu salama kwa Binadamu ,kwa kulinda na kuthamini maisha na uhai wa binadamu wote bila kujali itikadi,dini,rangi,kabila , utaifa n.k.

Kwa mwendo na kasi aliyoanza nayo Dr Tulia naiona Dunia pakiwa mahali salama na tulivu kwa maisha ya watu wote na mahali pasipo na milio ya risasi kama majangili,naona mwisho wa mateso na vifo vya watoto na akina mama na wazee wasio na hatia vikifika tamati.naona Dunia ya kistaarabu isiyo na migogoro ikizaliwa upya ,nauona upendo ukitamalaki mioyoni mwa walimwengu.

Namuona Dr Tulia akienda kuweka historia ya kuileta pamoja Dunia na Kuiunganisha,naona Dr Tulia akienda kuwa mpatanishi wa Dunia nzima,namuona Dr Tulia akiwa kiungo cha amani Duniani kwote,namuona Dr Tulia akiwa tegemeo la kuleta na kudumisha amani Duniani,namuona Dr Tulia akiwa nyota iangazayo na kuleta matumaini Duniani kwote.

Naona kuinuliwa kwa Dr Tulia ni mpango wa Mungu Mwenyewe kuiponya Dunia na kuifanya kuwa na amani na kutamalaki kwa upendo,naona ni mpango wa Mungu kumtumia Dr Tulia kuhakikisha kuwa silaha za maangamizi na viwanda vyake vikipunguza uzalishaji wa silaha kwa kukosa mahali kwa kwenda kupeleka na kuuza silaha zao.

naona ni mpango wa Mungu Mwenyewe kumuinua Dr Tulia ili kuwafuta machozi na kuwapa matumaini na Tabasamu watoto ,akina mama na wazee ambao wamekuwa wahanga wa mauaji ,ubakaji na mateso ya kila aina. Dr Tulia ameinuliwa kama Tumaini jipya kwa walimwengu kama Rais wa umoja wa mabunge Duniani .jiulize hata wewe mwenyewe namna alivyopanda haraka haraka kufikia nafasi hiyo aliyoshinda kwa kishindoo na aliyonayo kwa sasa ambayo sasa sauti yake inasikika Dunia nzima.

Huo ni mpango wa Mungu,ni kusudi la Mungu kumpa kibali Dr Tulia mbele za watu ili kuleta amani ulimwenguni baina ya mataifa na mataifa na baini ya wananchi kwa wananchi.ni mpango wa Mungu kumaliza utesaji kwa akina mama,wazee na watoto kupitia ulimi wa Dr Tulia ambao umeanza kunena juu ya kuhitaji amani na suluhu kwa njia ya amani ,na kusitisha umwagaji Damu za watu wasio na hatia na kulinda maisha ya watu wote pasipo kupoteza Binadamu hata mmoja kwa risasi .

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Dogo unataka Ukatibu Mkuu CCM??
Mkuu,
hujawahi kuhisi kwamba huyu jamaa kazi yake ni kuona kiwango gani wananchi wana maoni gani kuhusu serikali iljyopo madarakani?

Watu wanapokuwa tempered ni rahisi sana kuropoka chochote kuhusu utawala uliopo, huyu jamaa kazi yake ni kuangalia majority inasema nini kuhusu serikali.

Hakuna kiongozi duniani akosei, yeye huwa ni kusifia tu. Anatia shaka sana.
 
😅😅😅😅 nacheka kwa nguvu.kiukwel Hana mchango wowote mbele ya mtu yeyote ambaye anamkubali myahudi.
Hamas waliyataka wenyewe,na bado.kuua watu 1200+na kuteka wengine!.
Labda sio wale viumbe🤔🤔!
Kiufupi hakuna inshu,south A wameuthata
 
Tulia uwezo anao anaamika sijui kama lissu ataweza pata nafasi ya kuweza kukutana na joe kwenda israel na kutoa maoni yake yeye nafasi ni huko tabata matumbi!
Yaani jizi la kura kukutana na Joe Bidden mnaona ni bonge la deal! Walikuja hapa Marais wa Marekani wawili tena wakiwa madarakani, na hakuna impact yoyote ya maana, itakuwa huyo kiongozi wa taasisi ya uchochoroni?
 
Uchawa unafanya mtu awe hana akili, we jamaa, ipo siku utauza utu wako kwa fedha ama hivyo vyeo.

Siamini kuwa huna akili kiasi hiki, ila unajitoa akili sababu ya malengo fulani, lakini huenda ukawa akili hizo pia huna maana kuna viongozi wapo madarakani unaona kabisa huyu chenga, yupo hapa sababu ni mwana CCM na ana KONEKSHENI
 
Tulia uwezo anao anaamika sijui kama lissu ataweza pata nafasi ya kuweza kukutana na joe kwenda israel na kutoa maoni yake yeye nafasi ni huko tabata matumbi!
Yaani jizi la kura kukutana na Joe Bidden mnaona ni bonge la deal! Walikuja hapa Marais wa Marekani wawili tena wakiwa madarakani, na hakuna impact yoyote ya maana, itakuwa huyo kiongozi wa taasisi ya uchochoroni?
 
Tulia uwezo anao anaamika sijui kama lissu ataweza pata nafasi ya kuweza kukutana na joe kwenda israel na kutoa maoni yake yeye nafasi ni huko tabata matumbi!
Labda Biden awe amepandwa na malaria kichwani. Lakini Biden kama Biden hana mda mchafu wa kuongea na wajingawajinga.
 
Back
Top Bottom