Dr. Magufuli amechafuka, hachaguliki

Dr. Magufuli amechafuka, hachaguliki

Usijitie ujuha kiasi hicho cha kujifanya hujui tofauti kubwa iliyopo wakati Mwalimu alipokuwa kiongozi wa Tanzania na hawa wahuni, wezi, wapokea rushwa n.k. Unadhani jina la Baba wa Taifa lilidondoka toka mbinguni? Unadhani kwanini Watanzania walio wengi bado wanampenda sana na kumuenzi pamoja na kuwa aling'atuka miaka 30 iliyopita?
Mkuu,
Mimi ninaongelea mfumo wewe unaleta masuala ya kudondoka kutoka mbinguni.

Kwani Mwl. Nyerere alichimbuliwa kutoka ardhini?

Nani amesema Mwl. Nyerere amedondoka kutoka mbinguni?

Kama suala ni utendaji, sasa hizi hoja za mfumo zinatoka wapi wakati mfumo ni ule ule.

Nadhani umedandia hoja bila hata kufahamu msingi wake!
 
Ndio maana nasema lowassa bado anayo nafasi kubwa sana kumaliza magufuli ndani ya chama na kufanya propaganda nje ya chama wakose wote. Kuhama chama atakosea.
 
Kumbe hata kusoma hujui! ndio matatizo ya kupitia shule za kata uelewa wako ni mdogo mno.

Mkuu,
Mimi ninaongelea mfumo wewe unaleta masuala ya kudondoka kutoka mbinguni.

Kwani Mwl. Nyerere alichimbuliwa kutoka ardhini?

Nani amesema Mwl. Nyerere amedondoka kutoka mbinguni?

Kama suala ni utendaji, sasa hizi hoja za mfumo zinatoka wapi wakati mfumo ni ule ule.

Nadhani umedandia hoja bila hata kufahamu msingi wake!
 
kingunge ni nani tz hii,mbona kamati ya maadili haikumjali na lowasa wake?afe salama mzee yule
 
Mm na wasiwasi sana na huyu Mteuliwa kama kweli ataleta maendeleoya kweli kwa sababu nyingi tu ikiwemo hiyo ya kupindishwa utaratibu wa kumteua.Wtu wana matumaini nae kwa sababu ya anavyotoa takwimu kichwani bila kunua kwamba TANROADS kuna watu wanajua umbali achia mbali wa trunks roads bali hata umbali wa district roads ambao Mteuliwa hawezi jua.Tatizo kubwa bongo ni system na bahati mbaya ili haliwezi kubadilishwa hiki.Babati mbaya zaidi hakuna strong opposition kama nchi za jiran zetu ambao wengi wamesonga mbele kimaendeleo.Atatisha tisha watu na kuleta mambo kama ya Mrema lkn kunyanyuka kiuchumi sidhani.Tuombe uzima tu na uwepo wa forumn hii manake huyu jamaa tunamjua sisi tuliowahi kufanya naye kazi
 
VUTA-NKUVUTE

Wachawi kila kona, hata angechaguliwa malaika bado wanga na wachawi hawakosi!!
 
Last edited by a moderator:
VUTA-NKUVUTE

Sio hoja, na hata haina mvuto, kwani hajatoa altenative B baada ya A kufeli na kusema nani anafaa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Hizo hoja za nyumba za serikali zimeishajibiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Frederick Sumaye.

Kwa maelezo zaidi, angalia hii video

[video]https://youtu.be/LofQGOS0bCM[/video]

Kuhusu yeye kuchukua nyumba, ingekuwa ni vizuri ukaleta documents hapa badala ya kuanza kujadili scuttlebutt lakini vile vile, kwani yeye hakuruhusiwa kisheria au kikanuni kununua nyumba zilizokuwa za serikali.

..ndiyo ufisadi wenyewe huo.

..mramba na yona walikuwa na utetezi kama huo lakini mahakama ikawafunga miaka 3.

..hivi kwa hesabu za haraka unafikiri taifa limeingia hasara ya trilioni ngapi ktk ufisadi huu wa magufuli?
 
Mzee kasema kweli mbona mnamsakama kwa maneno ya chuki kingunge bado ni ccm na ataendelea kuwa ccm lazima mkubali kukosolewa pale mnapokosea, kuna msemo unasema heli ya kijana maskini mwelevu kuliko mfalume tajiri mpumbavu asiyekuwa na maono.
 
Mnazi huzaa nazi;mahindi hayatoi maharage. Halali hutoa halali na haramu huzaa haramu. Batili mwanzo ni hadi mwisho pamoja na matokeo yake. Mchakato wa kumpata Dr. Magufuli,kama mgombea wa CCM,umesemwa na Kingunge kuwa ulikuwa batili. Dr. Magufuli hawezi kuwa halali.

Dr. Magufuli amepatikana katika mchakato batili. Ni kama hakukuwa na chochote Dodoma na hakuchaguliwa yeyote. Batili hubatilisha. Huchafua. Dr. Magufuli hawezi kubaki salama. Amechafuka na hachaguliki. Ni batili toka kwenye ubatili. Watanzania wawe macho.

Dr. Magufuli amepatikana kwa kukiuka kanuni. Yeye atazifuata? Amechaguliwa palipovunjwa sheria na taratibu. Yeye atazilinda za kinchi. Dr. Magufuli,tukimuamini Kingunge,amechafuka hasa. Hachaguliki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Heshima kwako mzee wng!! Mjukuu wako ntakutembelea hivi karibuni, ila nina tatizo na ramani/mitaa ta Dar , nikutafute mitaa ya Lumumba au ufipani Mzee wng!?
 
Ccm imeshateua mgombea wake haya wengine leten wenu sis tupime unga na maji tupate ugali mzuri
 
Wanaochagulika CCM hawajai mkononi. Kama kweli Kingunge ni mkweli na aliyajua yote haya alipaswa kujiengua na kuyatamka wakati yalipotokea. Huo ndio ungekuwa uzalendo. Sio uzandiki wa sasa baada ya mteule wa CCM kupatikana.

Lakini silalamiki kwa usaliti wake kwa chama chake. Tungejuaje kanuni zilikuiukwa?

CCM ife tu.

Asante Mzee Kingunge
 
Watanzania ni walewale wooote
Sio ccm Sio ukawa
 
Ukawa Wasafi.JPG
Huyu jamaa amenihuzunisha kweli.
Eti UKAWA ni sehemu ya watu safi...!!!!!!!!!
Ukawa ni wasafi?
Hivi haya mambo wanayoyafanya viongozi wa Ukawa mngekuwa mnayajua kinagaubaga mngesema bora CCM.
Basi wacha tuangalie sakata la usafishaji vyama linavyoenda.
Ukishakubali kujishughulisha na siasa kubali kuchafushwa.
Muwe mnaangalia siasa katika mapana yake aisee. Msikurupuke
 
Mimi nilidhani Magufuli anachagulika lakini kwa sasa unasema hachaguliki!

Kwa hiyo wewe unadhani nani anachagulika?

Kuniambia fulani hachaguliki bila kunipa alternative ni sawa sawa na kutoa ushauri wa kijinga!
Nadhani sa hvi utakuwa umeamka freeeshhhh,
Irudie kusoma na uelewe mkuu
 
kingunge ni nani tz hii,mbona kamati ya maadili haikumjali na lowasa wake?afe salama mzee yule

Watanzania wanafiki sana. Hata wale unaodhani
wamesoma na kuelimika nao wanafiki kama wakulima
wa darasa la nne. Leo hii ndio Magufuri anapendwa?
Mlimjua kuwa anapendwa na watanzania? Mbona
mliimpigia debe Lowassa na kutuaminisha anapendwa
sana na watanzania. Leo yuko wapi? Opportunists tu
nyie. Hata angepitishwa Membe kwa unafiki wenu
mngesema atashinda ana uzoefu wa kimataifa.
Mtaacha lini unafiki? Kwanini hamkwenda kumshawishi
Magufuri agombee na Kikwete aliwaambia
muwashawishi watu kugombea? Mkaleta maagizo ya
kumshawishi Lowassa akiwa ameshaandaa hema la
kukaa. Acheni unafiki. Mnatafuta vyeo tu hapa kwa
Magufuri hamna lolote. Eti Magufuri anakubalika na
watanzania. Angewaambia mpige mbizi? Acheni
unafiki. Mtaungua na moto nyie. Stand where you
believe to be correct.
 
...

....tunakuja na UFUNGUO WA MOTO

Nikuulize swali, Nyerere mnayemsifia kila siku aliongoza kupitia chama gani?
aliishia kusema Bila CCM Madhubuti Nchi itayumba,hatimaye tingatinga linaingia kurekebisha paliposinyaa.

Endelea kumzoea Magufuli kama Rais wako wa awamu ya tano,hauna namna nyingine.

Kwa sababu kuna goli la mkono nakuelewa kabisa
 
Back
Top Bottom