Imekuwa ni jadi sasa kwa Watanzania kuwa na tatizo la kusahau namna siasa za CCM zilivyo hapa nchini. Mwaka 2005 Rais wa sasa Kupitia C CM Kikwete alionekana kuwa chaguo sahihi na baadhi ya watu na viongozi wa kidini walisema alikuwa ni chaguo la Mungu!
Lakini utendaji wake na hasa katika kushughulikia matatizo ya wananchi ya moja kwa moja haukuwaridhisha wananchi wengi na baadhi wanasema kheri aondoke mapema. Leo naona amekuja Dr. Magufuli
ghafla Watanzania naona wamesahau taabu na suluba zilizosababishwa na uongozi wa chama kile kile cha CCM. Sasa watu wameanza tena kuweka matumaini ya ukombozi mpya wa kiuchumi na tofauti za kitabaka utakaoletwa na Dr.Magufuli.
Ni muhimu tukajiuliza ni njia zipi mpya ambazo Dr.Magufuli atatokea ambazo wenzake hawakuzipitia? Wakati wananchi tukiendelea kupigika ndani ya utawala wa CCM, Dr.Magufuli alikuwa ni sehemu ya uongozi uliotufikisha hapa. CCM ina sera ambazo kwa sasa wanahitaji mfumo mpya wa uongozi na lazima wajifunze wakiwa nje ya uongozi ndipo wanaweza kuelewa haya tunayoyazungumza.
Ni vema watanzania tukawa na fikra za kimapinduzi ili kifanya maamuzi magumu dhidi utawala wa kimazoea na kuingiza utawala wa kisasa unaojali mahitaji na mawazo ya wananchi wa hali ya chini kuliko ilivyo sasa!
Mimi nilidhani Magufuli anachagulika lakini kwa sasa unasema hachaguliki!
Kwa hiyo wewe unadhani nani anachagulika?
Kuniambia fulani hachaguliki bila kunipa alternative ni sawa sawa na kutoa ushauri wa kijinga!
Mzee Tupa Tupa wa Ufipa Dar es Salaam.
Hoja hapa ni Magufuli anachagulika au hachaguliki.Kutokuwepo kwa alternative au mwingine anayechagulika, hakumfanyi Magufuli achagulike. Kwa maneno mengine, huhitaji kutoa alternative ili kupata uhalali wa kutoa hoja kuwa Magufuli hachaguliki. Hoja kuwa Magufuli hachaguliki inajitosheleza provided it is based on a sound premise. Uhalali wa kukosoa jambo hautokani na uwepo wa alternative. Kama jambo limekosewa, limekosewa tu bila kujali kuwa matokeo ya kukosewa huko yana mbadala au la. This is Learning How to Think and Argue 101.
Hoja hapa ni Magufuli anachagulika au hachaguliki.
Huwezi kunieleza alichofanya ni sound premise bila kutoa solution.
Watanzania tuko njiani kwenda kupiga kura halafu unatuambia tunakwenda kumpigia kura mtu ambaye hachaguliki na ametuambia sababu inayomfanya Magufuli asichagulike.
Kwa hiyo nimemuuliza yeye anadhani nani anachagulika?.
Hili ni swali ambalo kwa mtu anayedai anajenga hoja yenye sound premise nadhani angelifahamu kabla ya kutuambia Magufuli hachaguliki.[
Yeye amesema magufuli hachaguliki amemaliza. Swala nani anachagulika ni juu yako wewe kutafuta anayechagulika, mbona wapo wengi tu hata dovutwa ameshatangaza, hata yule mama wa lile tawi lenu.
Mimi nilidhani Magufuli anachagulika lakini kwa sasa unasema hachaguliki!
Kwa hiyo wewe unadhani nani anachagulika?
Kuniambia fulani hachaguliki bila kunipa alternative ni sawa sawa na kutoa ushauri wa kijinga!
Mkuu,..ni kwasababu ya kashfa ya kuuza nyumba za serikali kwa bei ya hasara.
..mdhibiti na mkaguzi wa mahesabu ya serikali, prof.assad, umesema ule ulikuwa ni wizi wa wanasiasa.
..magufuli ameiingiza serikali na taifa hasara kubwa kuliko hasara iliyosababishwa na mramba na yona na kupelekea kufungwa miaka 3.
..magufuli hapaswi kujitetea kwamba ulikuwa uamuzi wa cabinet. Yeye binafsi alijitwalia nyumba. Ni wapi cabinet ilimuelekeza achukue nyumba kwa bei ya kizushi-zushi??
@Ngw'amapalala, Bukyanagandi
Nyerere huyo huyo pia alisema CCM sio mama yangu. Na tena akasema Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata wasipoyaona ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM. CCM aliyosema Nyerere ni ile CCM madhubuti sio hii ya leo ambayo imejaa wezi, wahuni, matapeli na walaghai kama nyinyi
Mtu akikuambia barabara ile unayotaka kupita ina simba, na wewe hufahamu barabara nyingine zaidi ya hiyo na una akili timamu, lazima utamuuliza kama anafahamu barabara nyingine ambayo haina hatari.Hii si mantiki sahii; mtu akikuambia barabara ile ina simba ni lazima akuoneshe barabara isiyo na simba ili uende unakotaka? Wakati mwingine mambo mengine inabidi wewe mwenyewe uyatafutie majibu.
Ona unavyojichanganya,kama Nyerere alikuwa safi huku akiitumia CCM hiyohiyo na unasema CCM ya Nyerere ilikuwa safi basi maana yake tatizo sio mfumo,hili ndilo tatizo la kukariri bila kuelewa ndio maana mnajichanganya kama hivi.
Mkuu,Lazima tuseme ukweli hata kama ni mchungu. Mwl.Nyerere hakuacha CCM ya wezi, majizi, walaghai na mafisadi kama nyinyi. Huu ndio umadhubuti unaousema mkuu? Nawashauri muache kutapeli Wananchi kwa kauli za Nyerere bila kuangalia muktadha wake. CCM ya leo imejaa majizi, matepeli na walaghai. Huu sio umadhubuti, bali ni ulegelege. Kama alivyowahi kusema Nyerere mwenyewe, chama legelege huzaa serikali legelege. Na siku zenu zinahesabika wahuni nyie. Tafakari
Mkuu,
Kwani huyu Nyerere alikuwa kwenye mfumo gani ambao ni tofauti na huu unaodai kwa sasa haufai?
Nielimishe!