Dr. Magufuli amechafuka, hachaguliki

Dr. Magufuli amechafuka, hachaguliki

Nikuulize swali, Nyerere mnayemsifia kila siku aliongoza kupitia chama gani?
aliishia kusema Bila CCM Madhubuti Nchi itayumba,hatimaye tingatinga linaingia kurekebisha paliposinyaa.

Endelea kumzoea Magufuli kama Rais wako wa awamu ya tano,hauna namna nyingine.

Huo ndio ukasuku na undorobo. Kiongozi mzuri atatoka ccm kama watakuwepo wasafi. Ni ni kilichomfanya Nyerere huyo huyo aliposema ccm sio baba wala mama yake? Hilo lilikupita au hukulikariri?
 
Mnazi huzaa nazi;mahindi hayatoi maharage. Halali hutoa halali na haramu huzaa haramu. Batili mwanzo ni hadi mwisho pamoja na matokeo yake. Mchakato wa kumpata Dr. Magufuli,kama mgombea wa CCM,umesemwa na Kingunge kuwa ulikuwa batili. Dr. Magufuli hawezi kuwa halali.

Dr. Magufuli amepatikana katika mchakato batili. Ni kama hakukuwa na chochote Dodoma na hakuchaguliwa yeyote. Batili hubatilisha. Huchafua. Dr. Magufuli hawezi kubaki salama. Amechafuka na hachaguliki. Ni batili toka kwenye ubatili. Watanzania wawe macho.

Dr. Magufuli amepatikana kwa kukiuka kanuni. Yeye atazifuata? Amechaguliwa palipovunjwa sheria na taratibu. Yeye atazilinda za kinchi. Dr. Magufuli,tukimuamini Kingunge,amechafuka hasa. Hachaguliki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

UKAWA mbona hamueleweki. Fanyeni yenu. Magufuli si wenu.
 
UKAWA mbona hamueleweki. Fanyeni yenu. Magufuli si wenu.

Huyo ni COMRADE aliyelelewa enzi za muasisi wa chama chetu.kitukutu cha mafisadi.Anajua zile sheria za ccm in out.Anajua kuwa Fitina ni mwiko kwa mwana ccm.

Anasema cha moyoni mwacheni.Anajua yaliyotokea yalipangwa kunusuru Last Family.Kama ndivo asi Makufuli hawezi kulinda sheria za nchi kama za chama ameshindwa kuzilinda na kuzitetea...

Na amesema atakilinda chama na si Taifa tunahitaji kiongozi atakaye linda Taifa na chama baadaye...
 
Watanzania wanafiki sana. Hata wale unaodhani
wamesoma na kuelimika nao wanafiki kama wakulima
wa darasa la nne. Leo hii ndio Magufuri anapendwa?
Mlimjua kuwa anapendwa na watanzania? Mbona
mliimpigia debe Lowassa na kutuaminisha anapendwa
sana na watanzania. Leo yuko wapi? Opportunists tu
nyie. Hata angepitishwa Membe kwa unafiki wenu
mngesema atashinda ana uzoefu wa kimataifa.
Mtaacha lini unafiki? Kwanini hamkwenda kumshawishi
Magufuri agombee na Kikwete aliwaambia
muwashawishi watu kugombea? Mkaleta maagizo ya
kumshawishi Lowassa akiwa ameshaandaa hema la
kukaa. Acheni unafiki. Mnatafuta vyeo tu hapa kwa
Magufuri hamna lolote. Eti Magufuri anakubalika na
watanzania. Angewaambia mpige mbizi? Acheni
unafiki. Mtaungua na moto nyie. Stand where you
believe to be correct.

Afadhali uwaambie ukweli.Maana leo wako busy kumnanga waliyempapatikia.Ningekuwa Makufuli ningejifikiria mara mbili mbili kuhusu wanaCCM.
 
11223903_400888460107744_3272321365580687833_n.jpg
 
JK ameshamaliza kazi yake ya kusimamia uteuzi na kama waliona ni batili wangezuia hatua ya kuchagua wale watatu wa Kupigiwa kura mkutano mkuu
Upinzani tunafurahi kwa maana hakutakuwa na nguvu kubwa ya kuchakachua kura kwa kuwa Makufuli si mteule wa wenye chama.Uchakachuaji utabaki kwa majimbo machache yatakayowaniwa na watoto we
 
Hoja hapa ni Magufuli anachagulika au hachaguliki.

Huwezi kunieleza alichofanya ni sound premise bila kutoa solution.

Watanzania tuko njiani kwenda kupiga kura halafu unatuambia tunakwenda kumpigia kura mtu ambaye hachaguliki na ametuambia sababu inayomfanya Magufuli asichagulike.

Kwa hiyo nimemuuliza yeye anadhani nani anachagulika?.

Hili ni swali ambalo kwa mtu anayedai anajenga hoja yenye sound premise nadhani angelifahamu kabla ya kutuambia Magufuli hachaguliki.

Hahitaji kukutajia ni nani anayechagulika ili kujenga hoja kuwa Magufuli hachaguliki. Is that too difficult to grasp?
 
Back
Top Bottom