VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Mnazi huzaa nazi;mahindi hayatoi maharage. Halali hutoa halali na haramu huzaa haramu. Batili mwanzo ni hadi mwisho pamoja na matokeo yake. Mchakato wa kumpata Dr. Magufuli,kama mgombea wa CCM,umesemwa na Kingunge kuwa ulikuwa batili. Dr. Magufuli hawezi kuwa halali.
Dr. Magufuli amepatikana katika mchakato batili. Ni kama hakukuwa na chochote Dodoma na hakuchaguliwa yeyote. Batili hubatilisha. Huchafua. Dr. Magufuli hawezi kubaki salama. Amechafuka na hachaguliki. Ni batili toka kwenye ubatili. Watanzania wawe macho.
Dr. Magufuli amepatikana kwa kukiuka kanuni. Yeye atazifuata? Amechaguliwa palipovunjwa sheria na taratibu. Yeye atazilinda za kinchi. Dr. Magufuli,tukimuamini Kingunge,amechafuka hasa. Hachaguliki!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam