Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Hamsumbui vichwa vyenu kufikiria swali la Kitila Mkumbo (Kama kweli aliuliza). Kama Thabo Mbeki alisema UKIMWI ni ugonjwa unaotokana na umaskini inakuaje mtoto wake (ambaye si maskini) afe kwa UKIMWI? Hili ni swali lenye mantiki sana maana kauli hiyo ya Mbeki ilizua mjadala sasa ukipata fursa ya kumuuliza lazima ujue kama bado ana msimamo huo au ameubadili. Sioni sababu ya Mbeki kujaa povu angekuwa muungwana tu na kujibu maswali.
 
Hakuuliza mtoto wa mbeki kufa kwa ukimwi..aliuliza impact ya ile kauli yake(ukimwi ni impact ya umasikini) aliyoitoa akiwa rais
Alipokuwa Rais hakusema habari ya umaskini na ukimwi, yeye alisema straight up kwamba HIV haiambukizi AIDS, period!

Halafu wengine wanasema Mbeki alimsahihisha Kitila kuhusu data zake, wengine wanasema Mbeki alikataa kujibu swali.

Sasa hapa inaonekana hatujui Kitila aliuliza nini, wala hatujui Mbeki alijibu nini, au whether Mbeki alijibu at all! And that's assuming Kitila aliuliza swali at all!

 

Mbona usiyesumbua kichwa kweli hili ni wewe?

Watu weshasumbua vichwa na kwenda kwenye msingi wa swali hadi kufuatilia kama ni kweli mtoto wa Mbeki alikufa kwa UKIMWI au la, itakuwa wewe unaemeza swali na kutoa pongezi kwa swali lililoulizwa bila ya kujua ukweli wa kilichomo kwenye swali hilo?
 
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.

Hapana. Kitila alionyesha jinsi gani ana ufinyu wa kufikiri, kuuliza swali ambalo linahusu familia binafsi, juu ya jambo ambalo halikuwa topic ya mazungumzo. Angesubiri siku Mbeki yuko kwenye vikao kuhusu Ukimwi ndio aulize swali kama hilo. Na unapouliza swali usiingize mambo binafsi ya familia. Alitaka nini hapa, kumkumbusha Mbeki uchungu wa kufiwa mwanae? Nani anaependa kifo cha mwanae kiwe mjadala wa hadhara? Nimefanya kazi na Kitila, nilimheshimu hadi niliposikia kafanya upuuzi huu wa kujitafutia umaarufu binafsi.

Kwanza sijawahi kusikia popote kuwa kuna mtoto wa Mbeki alikufa kwa ukimwi. Najua mtoto wa Mandela alikufa kwa ukimwi. Sasa Kitla alitaka kujionyesha yeye ni CIA sana au nini?
 

Mbeki alitoa tathimini yake kuhusu ukimwi na kugusa familia nyingi hapa barani Africa(Je tathimini ya mbeki ilikusudia kukomoa familia ziliziothirika kwa UKIMWI?)
Dr.Kitila mkumbo kamuuliza swali kutokana na tahthimini yake mwenyewe tena kwa kumtajia familia yake na kuunganisha familia yake ili ku-prove hypothesis ya kauli ya Mbeki.
Mtazamo wako una prejudice kuwa Dr.Mkumbo alikusudia eti kumkomoa.
Hivi swala la ukimwi kwenu ni swala la kificho kiasi hichi????
Mbeki ni public figure na anapaswa kuulizwa jambo lolote linalomuhusu liwe linamfurahisha au liwe linamkera.
Watanzania wengi ni waoga sana kiasi cha kusababisha kuacha baadhi ya mambo yakienda ovyo kwa kuogopa kuuliza viongozi wao just because ni viongozi tu.
 
Aliyekufa kwa Ukimwi ninavyojuwa mimi ni mtoto wa Nelson Mandela.
 

Kwani kauli ya mbeki kusema umaskini ndo chanzo cha ukimwi unadhani ilizigusa familia ngapi za kiafrika?
unadhani iliwakumbusha watu wangapi juu ya ndugu zao waliofariki kwa ugonjwa huo??
Je Mbeki alivyotoa kauli hiyo alikusudia kuwakumbusha wanandugu wa marehemu juu ya wapendwa wao waliokufa kwa ukimwi??
Msipende kuwa-pet viongozi kwa maswali ya kuwafurahisha tu.
 

Dr.Kitila mkumbo kamuuliza swali kutokana na tahthimini yake mwenyewe tena kwa kumtajia familia yake na kuunganisha familia yake ili ku-prove hypothesis ya kauli ya Mbeki.

Kwa maana hiyo, Kitila ni muongo mwizi, maana hakuna mtoto wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI
 
Kwani kauli ya mbeki kusema umaskini ndo chanzo cha ukimwi
Hapana, usimsafishe Mbeki, Mbeki hakusema hivyo, Mbeki alipingana na nadharia za sayansi kwa kudai kwamba HIV haisababishi UKIMWI.

Kwa maana hiyo, Kitila ni muongo mwizi, maana hakuna mtoto wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI
Hapana, hiyo itakuwa ni hitimisho kutokana na anachoripoti "Daudi Mchambuzi," ambacho hatuna uhakika nacho kwa sababu kuna wengine wanashuhudi swali tofauti na hilo.

Tunataka kuona swali la Kitila mstari kwa mstari!


 
Mbeki ana mtoto mmoja tu, alikufa (alipotea?) mwanzoni mwa miaka ya 80 katika mazingira ya kutatanisha.
 
Kwa maana hiyo, Kitila ni muongo mwizi, maana hakuna mtoto wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI
Dr.Kitila sio mwizi hjaiba chochote, Mbeki alipaswa kumjibu kuwa mtoto wake hajafa kwa ukimwi.
Kwa nini waliokuwepo kwenye mkutano huo wanaleta habari nusu nusu??
 
Mimi nakubaliana na Mbeki kuwa Ukimwi ni ugonjwa wa watu maskini. Wagonjwa wengi wa HIV wapo nchi maskini. Pia mwanamke maskini hana uwezo wa kuamua afanye mapenzi na mtu wa aina gani, maana yeye hafanyi tendo la mapenzi kwa kupata raha ila kwa kupata kipato cha kuishi kwa siku hiyo nia ikiwa kupata hela. Kwa hiyo umaskini unachangia sana uwepo wa ukimwa kwa nchi zete hizi maskini.
 

Ni watu wangapi wamewahi kumuuliza Mbeki maana ya kauli yake kwamba umasikini ndio chanzo cha ukimwi akawafafanulia? Watu mna-rukia kwenye conclusion bila hata kujua Mbeki alimaanisha nini. Unataka kuniambia Mbeki hakujua kuna watu matajiri wa fedha walikuwa wanakufa kwa ukimwi hadi mfikiri alikuwa akimaanisha umasikini wa kuwa na fedha?

Basi hata kama swali la Kitila lilistahili kuulizwa katika kikao kile ambacho hakikuwa juu ya suala ukimwi, alipaswa kumuuliza alimaanisha nini, sio kama amebadili msimamo.

Tatizo la waswahili ndio hili, kukosa focus. Ndio maana hatuendelei. Tukitaka kujadili ukimwi basi tufanye kongamano la ukimwi. Tukitaka kujadili "uongozi wenye malengo kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika" basi tuongee juu ya uongozi, sio kuleta mambo ya mtoto wako alikufa kwa ukimwi. Ulimwambukiza wewe?
 
 
Dr.Kitila sio mwizi hjaiba chochote, Mbeki alipaswa kumjibu kuwa mtoto wake hajafa kwa ukimwi.

Huwezi kutumia dhana ya uongo kujenga swali lako ikisha ukatarajia mtu mzima na shughuli zake akusahihishe, hasa ikiwa dhana hiyo inachembe chembe za kukusuta unaeulizwa. Hilo ni moja.

Swali linalobeba dhana ya uongo linamvunjia heshima muulizwa na taasisi anayoihudumia huyo muuliza. Unajua kaabisha Chuo Kikuu na Chadema kwa kiasi gani kwa swali lake hilo?

Kwa nini waliokuwepo kwenye mkutano huo wanaleta habari nusu nusu??

Wewe kama hujui kama Kitila aliuliza swali hilo au la, kwa nini unamtetea kuwa alifanya jambo jema kuuliza swali hilo? Au ndio unafata mkumbo wa Mkumbo?
 

hakuliza?ndo nini hebu kakojoe ulale hujui kitu ! we unadhani udokta wa kitila ni kama degree zenu za Chupi....i know him toka anakuja mkwawa kufundisha biology kama intern..so usiongee lolote kuhusu huyu dokta ntakupakaza mitusi ushangae
 

nani kakuambia kuwa sijui kama Dr. Kitila kama kauliza swali hili au la?
Mkuu mbona kama umeshikwa na jazba hivi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…